Ujio wa CCJ: Yote unayotaka kujua

Kaitaba

JF-Expert Member
Jun 30, 2009
916
52
Mwenyekiti na katibu wa CCJ, leo walikuwa wageni wa WAPO redio ktk kipindi cha meza ya busara, nilicho kipata kutoka kwao, zaidi ya kunipotezea muda wa kuwasikiliza, ni kubaini udhaifu mkubwa wa kujieleza na kujibu maswali ya wasikilizaji na mtangazaji,

Baadhi maswali yalikuwa hivi;

-Ni kwa nini umeanzisha hiki chama? akashindwa kujibu,
-Vyama viko 18 umeona dosari gani ktk vyama hivyo? akajibu hakuna dosari ila CCM inafanya vizuri na vyama vingine siwezi kuvisemea
-mmeanzisha ccj mko wangapi, jibu tuko wawili tu,
-ofisi zenu ziko wapi, akajibu ni siri yetu
nk

Kutokana na majibu hayo na udhaifu wa kujieleza, msikilizaji mmoja amesema kuwa hao wametumwa kujitokeza kwa niaba ya wengine ndio maana hata kujieleza wanashindwa, pia vyama vyote majina yao ni ya kiingeleza ispokuwa CCM na CCJ, alipoulizwa kuna siri gani ktk hili hakuweza kutoa jibu la moja kwa moja.

Ktk
haya yote CCJ tunaoinaje sisi?
 
Msajili wa vyama vya Siasa alishasema kwamba CCJ is a hoax na wenyewe wameshathibitisha kwamba chama chao ni cha watu wawili tu. Why waste time discussing chama hewa?
 
chama hewa kingewakosesha usingizi CCM!! kwani chama kinaanzishwaga na watu wangapi?
 
Inaeleweka fika kuwa hawa jamaa[viongozi wa muda ccj] wana front wazee ambao hawataki kujitokeza sasa ila wakati wa mchakato wakitupwa nje wawe na alternative option[opportunists wa siasa
 
Mwenyekiti na katibu wa CCJ, leo walikuwa wageni wa WAPO redio ktk kipindi cha meza ya busara, nilicho kipata kutoka kwao, zaidi ya kunipotezea muda wa kuwasikiliza, ni kubaini udhaifu mkubwa wa kujieleza na kujibu maswali ya wasikilizaji na mtangazaji,

Baadhi maswali yalikuwa hivi;

-Ni kwa nini umeanzisha hiki chama? akashindwa kujibu,
-Vyama viko 18 umeona dosari gani ktk vyama hivyo? akajibu hakuna dosari ila CCM inafanya vizuri na vyama vingine siwezi kuvisemea
-mmeanzisha ccj mko wangapi, jibu tuko wawili tu,
-ofisi zenu ziko wapi, akajibu ni siri yetu
nk

Kutokana na majibu hayo na udhaifu wa kujieleza, msikilizaji mmoja amesema kuwa hao wametumwa kujitokeza kwa niaba ya wengine ndio maana hata kujieleza wanashindwa, pia vyama vyote majina yao ni ya kiingeleza ispokuwa CCM na CCJ, alipoulizwa kuna siri gani ktk hili hakuweza kutoa jibu la moja kwa moja.

Ktk
haya yote CCJ tunaoinaje sisi?

CHADEMA, SAU, Demokrasia Makini ( Late Prof Shayo) n.k
 
Kuna umuhimu wa kukisajili chama hiki?, yaani hawataki hata kutaja sera zao, walipoulizwa hilo wamesema kuwa ni kupanua wigo wa demokrasia tu,
 
Kuna umuhimu wa kukisajili chama hiki?, yaani hawataki hata kutaja sera zao, walipoulizwa hilo wamesema kuwa ni kupanua wigo wa demokrasia tu,

Sera zao zilielezwa kama unafuatilia hata Raia Mwema waliweka kwa ufupi sera zao.
 
Mpaka sasa hivi, naamini CCJ walichopatia ni jina la chama tu... wala hakuna zaidi ya hapo!!! I will remain to be corrected now and 4rever!
 
Kuna umuhimu wa kukisajili chama hiki?, yaani hawataki hata kutaja sera zao, walipoulizwa hilo wamesema kuwa ni kupanua wigo wa demokrasia tu,

Hebu tuambie sera moja tu ya PONA kama unaijua
 
hiki chama ni chama cha mamluki nikweli kuna vigogo ila hawataki kujitokeza kutokana na usalama wao watakapo ng'atuka ccm, kama wanabisha wajitokeze, hii nikutokana na m/kiti wao kujichanganya alipokuwa anahujiwa na stationmoja hivi hapa jiji dar
 
Hivi kuna siri bongo jamani? hao wakubwa akina nani? kama hawajulikani simply hiki chama ni cha freemasons!
 
Itakuwa jambo jema ikiwa wapambanaji wa CCJ baada ya kujiengua kutoka CCM wakashirikiana katika uchaguzi 2010 ili kupata wabunge wengi. Washirikiane katika kampeni nchi nzima. Pia waachiane majimbo pale ambapo upande mmoja unanguvu kuliko mwingine. Kwa hiyo nina wahimiza wabunge wote wa CCM wanaotaka maendeleo katika nchi yetu waondoke CCM, waingie CCJ na kisha waimarishe kambi ya upinzani
 
wasisahau na kuwashirikisha jeshi la polisi na la wananchi litawasaidia sana, wawe huru
 
Kwa hiyo nina wahimiza wabunge wote wa CCM wanaotaka maendeleo katika nchi yetu waondoke CCM, waingie CCJ na kisha waimarishe kambi ya upinzani

Mkuu kuimarisha upinzani si swala la kwenda CCJ peke yake, kwani hata mimi na wewe hatuju hiyo CCJ itakuwaje mbele ya safari, cha msingi ni kwa wanachama wa CCM wenye uchungu na Nchi hii, wenye nia ya kuletea mabadiliko, wenye msimamo Chanya kwenye rasimali za nchi hii wanatakiwa KUONDOKA CCM na kwenda Upinzani ili kuindoa CCM madarakani haraka na upesi iwezekanavyo kwani wamesibitisha kufilisika, Kiitikadi, hawana Uzalendo, hawana uchungu na Nchi hii na rasirimali zake.

Imefikia wakati si swala la kutaka bali ni lazima CCM waondoke.
 
Ndoto za mchana.

Hamna lolote litakalopatikana la maana ikiwa watu wataegemea kwenye hivi vyama vya siasa ambavyo vingi vinasukumwa na kuendeshwa kwa ubinafsi, umafioso, visasi plus many other wrong reasons. It is time to give up the current system people..don't waste ur time on something which has already proved failure.
 
Cha msingi vyama vijitahidi kunadi sera zao na kuonyesha picha nzuri kwa wananchi. Huu ushirikiano wa vyama vyenye sera tofauti ni usanii sawa na wapambanaji walioko ndani ya CCM.
 
Back
Top Bottom