Meya na diwani wa zamani wa Kinondoni na Ubungo akiwa na ripoti za CAG mbele yake mezani studio ya Wasafi MEDIA na kuulizwa maswali na jopo la watangazaji na pia wasikilizaji anafafanua sababu za udhaifu wa kiuongozi ktk halmashauri za Dar es Salaam na nchini kwa ujumla.
Meya mstaafu Boniface Jacob aelezea jinsi wakaguzi wa ndani wa Halmashauri jinsi wanavyofanyiwa mizengwe kwa kunyimwa vitendea kazi ikiwemo usafiri na ofisi za Ukaguzi wa Ndani kuwekwa pembeni mbali na mkurugezi wa Halmashauri ili kuwakatisha tamaa na wasifurahie mazingira ya ofisi zao na kutishia ufanisi wa kazi yao nyeti ya ukaguzi .
Kada wa CHADEMA kamanda Boniface Jacob katika mahojiano exclusive na ya wazi ameelezea mapungufu makubwa ya wakurugenzi wa majiji na halmashauri za miji ambao hawana uzoefu lakini walipachikwa ktk nafasi za juu za uongozi na kusababisha CAG kuibua madhaifu mengi
Mfano ni ikiwemo matumizi mabaya ya kodi, kutofuata utaratibu, kulipa fedha za madawa Bohari Kuu ya Madawa MSD kisha Halmashauri hizo kutokwenda kuchukua mabilioni ya madawa na vifaa tiba vilivyolipiwa lakini havikuchukuliwa kupelekwa ktk mahospitali kutibu wananchi ....
Meya mstaafu alipoulizwa chini kuhusu kipindi halmashauri ya Kinondoni na Ubungo zilipokuwa na mameya na madiwani wengi wa CHADEMA hali ilikuwaje?
Meya Mstaafu Boniface Jacob anasema walidhibiti mianya ya upotevu wa Mali na matumizi mabaya ya mapato pia kodi hivyo kuibuka na hati safi kutoka kwa CAG na kusema hii ndiyo faida ya kuwa na sifa za kweli za vyama vingi Mali ya umma inalindwa kwani kuna macho ya vyama ktk baraza la udiwani, bungeni na vyombo huru vya habari kuhoji yaliyomo ktk ripoti ya CAG bila woga kama kipindi cha John Magufuli ambapo mahojiano hayo hayangewezekana na hata kama yangefanyika basi wangekuwa wamezingirwa nje ya ofisi na watu wasiojulikana kuwatisha na kuwatia nguvuni...
Kuhusu nini kifanyike ili halmshauri ziwe na wakurugenzi na wakuu wa idara thabiti walio na uwezo wa kufanya kazi kwa umahiri, meya mstaafu Boniface Jacob anasema wafanyakazi wa Halmashauri na idara za serikali waliofanya kazi kwa muda mrefu ndiyo wanatakiwa kupandishwa vyeo kuwa wakurugenzi au wakuu wa idara badala ya makada wa UVCCM na CCM kupachikwa ktk uongozi wakati hawana uzoefu ktk ofisi za umma.