Upinzani Tanzania ni dhaifu na Kibogoyo

Tlaatlaah

JF-Expert Member
May 18, 2023
8,179
11,600
wasalam,

Natafakari juu ya mbadala wa Serikali Tanzania, yaani upinzani sipati majibu. Kuna umuhimu wa kua na upinzani kweli? Umuhimu wake uko wapi? Ikiwa kila Jambo linakuja na linapita kama lilivyo bila pingamizi lolote popote, si ndani ya Bunge au nje ya Bunge. Je, kuna Serikali mbadala kweli Tanzania?

Wenye mawazo tofauti na ya serikali wakapate wapi matumaini? Haya yote yanayotokea na yanayoendelea kutokea kungekua na upinzani makini na imara, mpaka sasa kungekua na mgogoro wa kikatiba ambao ungepelekea masahihisho na mabadiliko mengi sana ndani ya serikali na pengine kungekua hata na serikali ya Umoja wa kitaifa ya JMT.

Kwa mfano:
1. Kuna wabunge wanaitwa covid 19 wamefutwa uanachama kwenye vyama vyao lakini mpaka leo wanadunda bungeni kwa madaha na mikogo kama yote bila wasiwasi. Je, upinzani umeshindwa na Bunge, Mahakama au serikali? Upinzani makini usingeruhusu muhimili wowote kati ya hii kuwakumbatia hawa COVID-19 ambao wako kinyume na Sheria. Inchi ingesimama whether kuna kesi Mahakamani au hakuna.

2. Kukamatwa na kutiwa nguvuni kwa miongoni mwa wapinzani nchini kwa tuhuma za kubambikiwa. Kungekua na upinzani makini nchi haingekua stable na kazi zote zingesimama.

3. Tozo kwenye miamala, mfumuko wa Bei na kupaa kwa gharama za maisha. Upinzani makini usingeruhusu hali hii ishamiri kiasi hiki. Ungekua aidha umeilazimisha serikali kufanya Jambo au kuhamia Burundi.

4. Ukosefu wa ajira na ongezeko la vitendo vya kihalifi mtaani na mitandaoni, vitendo vya ushoga na ukahaba. Upinzani makini ungerekebisha hali hii kwa kelele mingi za hoja na mapendekezo ya mipango mbadala kutatua tatizo.

5. Tuhuma za Rushwa iliyokithiri kwenye taasisi na mashirika ya umma. Upinzani makini haungekubali watuhumiwa wa Rushwa kuendelea kushika nafasi serikalini.

5. Mradi wa SGR na Behewa zake, Bandari na Dp world ni hoja kubwa sana inayoweza waunganisha wa Tz na kuwawajibisha wahusika na serikali kwa ujumla na hatimae kuongeza uwazi na utawala bora nchini. Upinzani dhaifu na Kibogoyo kimya.

6. Tume huru ya uchaguzi, Sheria za uchaguzi, Daftari la wapiga kura na Katiba mpya, zilitosha kua hoja za kuifanya serikali isitulie wala kulala usingiz bali kuwatumikia wananchi kadiri ya mapendekezo yao kupitia upinzani.

7. Uvunjiwaji nyumba bila fidia kupisha miradi mbalimbali ya kiserikali, kuhamishwa kwa Lazima wananchi kutoka sehemu moja kwenda nyingine wakiwemo wamaasai wa Longido.

8. Utekaji wa watu na upotevu wa watu na watu wasiojulikana.

Kwa maoni yangu hayo yalitosha kuwaunganisha wapinzani na wananchi kuisimamia na kuiwajibisha serikali vilivyo nje ya Bunge na hatimae Taifa lingeweza kupiga hatua za kimaendeleo.

Mapendekezo
1. kuundwe Baraza la upinzani nje ya Bunge, likihusisha vyama vyote vya upinzani. Ili kusudi maoni ya wananchi yasipowasilishwa vema bungeni, Baraza nje ya Bunge lichukue nafasi hiyo.

2. Wapinzani kuepuka kuwatanguliza mbele viongozi hasa vijana wasio na maadili na wasioweza kudhibiti hisia zao dhidi ya hoja tofauti na Mawazo na mitazamo yao. Wawekwe viongozi makini, wastarabu wa kujibu hoja kwa hoja na sio matusi. Wanazuoni wengi wanatamani kujiunga upinzani lakini credibility ya upinzani inaondolewa na frontend youth ambao wanadhani kutukana na kudhihaki viongozi wa serikali ndio ujasiri au ndio aonekane kiongozi hodari kumbe anashusha weledi wa Chama kizima na hivyo wengi kusita kujiunga nao.

3. Kujizuia na Kuepuka kuongea ongea na kujieleza sana hadi inakua kero. Ni vizuri kusamarize kwa kifupi tena kwa lugha nyepesi with clearity sio unaongea hadi wasikilizaji wanasahau unaongelea nini, na ulianzia wapi na waulize maswali gani.

4. Kuepuka Kudandia dandia kila hoja hata zisizo na maana na baada ya muda mfupi inakua haina maana tena na wewe unakosa maana vilevile. Inafanya uchoke na jamii ikuchoke vilevile.

5. Kuonekana onekana mara kwa mara, yaani kiongozi hata jamii haikumisi, yaani we kila siku tunakuona tu leo umezunguzia hili kesho lile, keshokutwa umekubali hili, mtondogoo umekataa lile. Yaani haileweki lipi ni lipi. Hii sio nzuri, potea kidogo then ibuka na detailed info ya kitu ama vitu flani utakua relevant sana politically speaking.

Mwisho
Nadhani upinzani Tz unapaswa kua na Think Tanks ambao wao kazi yao ni kupanga, kubuni na kushauri dira na uelekeo sahihi wa upinzani kwa wakati sahihi. Kwa kufanya hivi Tanzania tunaweza kuendelea mbele na kwa kasi zaidi. Kuwa think tank na vilevile actor kunafanya uchuje na kuishiwa pumzi, mvuto na uelekeo haraka.

Aidha, Ubinafsi, Tamaa na kutokuaminiana kutaendeleza udhaifu na ukibogoyo uliopo na kudumaza maendeleo, haki, usawa na uwajibikaji.

Yapi maoni yako?
 
Magufuli ndio katufikisha hapa kwenye DP-WORLD kwa kutuletea bunge la mburulaz

 
Mabadiliko yanaletwa na wananchi sio upinzani. Sasa wewe keyboard analyst endelea kusubiri mabadiliko huku umekaa nyumbani kwako comfortably. Kuwa mpinzani nchi hii ni kupoteza muda, wananchi wenyewe kila kitu kinapita tu no resistance. Kila mtu ashinde mechi zake
 
Usilaumu wapinzani kwani nguvu ya wapinzani ni wananchi walio na uthubutu. Watanzania kama unavyojua wengi ni wajinga na waoga.

Pia upinzani ndio unapona kutokana majeraha ya ukatili wa Magufuli.

Katiba yetu ni mbaya mno hata watu kuandamana kwa amani hawaruhusiwi.

Hayo yote uliyoandika yanaonesha zaidi ubovu wa serikali na wananchi wake kuliko ubovu wa upinzani.
 
Nchi zote wananchi ndio wanaoleta mabadiliko bila kujali vyama vyao kwa kuwa huko wanajitambua, wewe umekaa unangoja Mbowe na Zito walete mabadiliko! Kama ni hivyo endelea kulala tu.
Odinga wa KENYA alikuwa Frontline. Lakini hawa wakwetu wanatutanguliza walalahoi huku wao wakitutizama kwenye tv online
 
We unafanya nn?
Kwann hicho unachotaka upinzani wakifanye isikifanye wewe?

Watanzania ni rahis sana kuwaongoza leo hata tukiambiwa gb moja utauziwa 16k hawana shida wiki Moja tu wanalia then after wanazoea

Mabadiliko hayaletwi na vyama vya siasa
 
Usilaumu wapinzani kwani nguvu ya wapinzani ni wananchi walio na uthubutu. Watanzania kama unavyojua wengi ni wajinga na waoga.

Pia upinzani ndio unapona kutokana majeraha ya ukatili wa Magufuli.

Katiba yetu ni mbaya mno hata watu kuandamana kwa amani hawaruhusiwi.

Hayo yote uliyoandika yanaonesha zaidi ubovu wa serikali na wananchi wake kuliko ubovu wa upinzani.
Wananchi wa Tz watatoka kwenye usingizi wa pono siku mungu mwenge atakapofutiliwa mbali
 
Tlaah Tlaah wa Tura wewe,

Upinzani sio wa kulaumiwa HATA KIDOGO,dola iliamua ccm ndio chama cha kuongoza,hivi vingine kazi yake ni kuisaidia CCM!!sasa unawalumu upinzani KWA lipi!?wakati imeshaamriwa rasmi na Dola!!!?
 
wewe hujaelewa topic hii, kazi za upinzania ni kutoa possible alternatives kwa serikali, mtoa mada hajaona alternatives za upinzani, and of course nataka wanipiganie fala wewe.
Asant sana Mama kwa kunielewa kwa ufasaha mno 👌. wenye bado kuelewa hii maneno, tuwasaidie taratibu kwa lugha nyepesi na kwa upendo, wakiwa tayari watajua nakuelewa nazungumzia nini.
Thank you very much.
 
Wa kulaumiwa ni wananchi maana úpinzani unapewa nguvu na wananchi kama wananchi maandamano tu tunaandamana mtandaoni ila site hatwendi.

Hivyo, kuna mawili ama wananchi hawaungi mkono upinzani au wananchi ni waoga wanataka akina mbowe ndio wapigani vita dhidi ya ccm yenye majeshi yote
 
Wa kulaumiwa ni wananchi maana úpinzani unapewa nguvu na wananchi kama wananchi maandamano tu tunaandamana mtandaoni ila site hatwendi.
Hivyo, kuna mawili ama wananchi hawaungi mkono upinzani au wananchi ni waoga wanataka akina mbowe ndio wapigani vita dhidi ya ccm yenye majesho yote
very interesting 👍🙏
 
Back
Top Bottom