mayenga
JF-Expert Member
- Sep 6, 2009
- 4,118
- 1,966
Nipo nimepumzika nasikiliza kipindi cha Jahazi Clouds FM ambapo kama kawaida Ephraem Kibonde akiwa na Partiner wake Gadna Habash wanasherehesha.
Katika Habari waliyoisoma wamekataa kata kata kuwa Mpendazoe kuwa ni kigogo wa CCM. Wamewataja vigogo kuwa ni Jakaya, Mkapa, Msekwa, Kingunge na wengine wenye rank zinazofanana na za hao.
Walichonishangaza na kunisononesha ni kuwa Mpendazoe ametajwa na Kibonde kuwa hana hadhi ya kuwa Kigogo ndani ya CCM badala yake ana hadhi ya TOOTH PICK na katu asijidanganye kuwa ni KIGOGO.
Pia amemponda kuwa asijifanye kigogo kwa kuhama chama kwakuwa hata yeye alihama kutoka CTN kwenda Clouds (kama concept ya kigogo ni kuhama kutoka point moja kwenda nyingine) basi na yeye ni KIGOGO.
Mwenyekiti wa CCJ ameibiwa nyaraka zake Kariakoo leo na katika nyaraka hizo yalikuwepo majina ya wanachama wao. Kibonde amemkejeli sana na pamoja na mambo mengine amekikejeli CCJ kuwa eti " chama gani wanachama wanajaa kwenye handbag(nadhani anamaanisha wanachama ni wachache) na akatoa mfano CCM ambacho kina wanachama kuanzia chipukizi, shule za sekondari hadi vyuo vikuu.
Great thinkers mnaonaje hili? Sio kama ni mpango umeandaliwa na wahuni fulani wa kisiasa kufifisha vuguvugu hili la mabadiliko linaloendelea sasa kwa kuwatumia wanahabari pamoja na vyombo vya habari?
Mzi
Mh.