Haya ni maoni yangu, ukiangalia hivi sasa mikoa ambayo ina wapinzani mfano Kilimanjaro, Arusha, Kigoma, Shinyanga na Pemba utaona kuwa wamechagua personality zaidi kuliko sera. Na hata hapa Dar wale wapinzani waliokuwepo kina Mrema walikuwa ni mashuhuri zaidi kuliko vyama vyao. Sina uhakika labda kama kuna analyst mzuri humu ndani atupe ushauri zaidi kuhusu hili.
Ila ni vizuri kuanisha yafuatayo;
Cheyo na UDP wana nguvu kule kwao Shinyanga, Chadema wamejikita kwa kina Slaa, Kabwe na Kilimanjaro, CUF wanapeta Unguja na Pemba. Sasa sijui kama hi ni sababu ya ukabila au watu wa huko wanakubaliana zaidi na sera za hivi vyama kuliko sehemu nyingine bongo.
Hujanielewa, wanaowachagua hao akina cheyo, marehemu kabuye, maremu chacha na mrithi wa chacha wa leo ,ni watu wa mjini?? yani watu wa dar, mwanza dodoma mjini ndo wanaenda kupiga kura kule???