Ujio wa CCJ: Yote unayotaka kujua

Ujio wa CCJ: Yote unayotaka kujua

Nini maana ya MNF na kundi la mtaa wa sita?

Mimi ninavyotafsiri ni hivi:-

MNF = Mwalimu Nyerere Foundation

Mtaa wa Sita = Spika Samuel Sitta na watu wenye mtizamo unaofanana naye e.g. Seleli, Ole sendeka, Mwakyembe etc.
 
Kati ya propaganda za nguvu zilizowahi kutokea kwenye historia yetu, basi hii CCJ ni mojawapo!

Naona sasa watu watasahau wapinzani waliokuwa msitari wa mbele badala yake tunashabikia vigogo watakaokwenda CCJ ambao majina yao bado ni siri wakati tuna miezi sita kabla ya uchaguzi. Hadi tutakapogundua kuwa CCJ ni 'chui wa karatasi' akina Chadema na Kafu watakuwa wamepoteza ufuasi kwa kiasi kikubwa.

Mie nasema hili nalo ni changa la macho!
 
Upinzani wa kweli na maendeleo ya kweli yatapatikana kwa mtanzania/watanzia thabiti wenye uzalendo na nia ya kweli. Kuunganisha vikundi vya mafisadi ulivyovitaja hapo sio tiba.

Je CCJ wana wazalendo wa kweli??
 
Upinzani wa kweli na maendeleo ya kweli yatapatikana kwa mtanzania/watanzia thabiti wenye uzalendo na nia ya kweli. Kuunganisha vikundi vya mafisadi ulivyovitaja hapo sio tiba.

Nakubaliana kuwa ni kweli tunahitaji hivo lakini hapa mi nazungumzia jinsi na namna ya kushinda uchaguzi. Kuwa na utitiri wa vyama si hoja, Tz ni nchi kubwa na tatizo kubwa la upinzani ni jinsi ya kukampeni nchi nzima. Dar ndio watu wanasoma magazeti na kuangali tv lakini huko vijijini ambako kuna watu wengi zaidi ni lazima uwafuate, na wao wengine hadi leo bado wapo kwenye zama za chama kimoja sasa jinsi ya kuwafikia hao ndio suala gumu.

Jingine ukiangalia historia fupi ya upinzani bongo tangu ianze miaka ya tisini wamepoteza majimbo mengi waliochukua toka CCM ambayo yamerudi CCM, mfano mzuri ni Dar hivi sasa hakuna mbunge wa upinzani ilihali Ubungo, Temeke na Kigamboni yote yalikuwa kwenye mikono ya upinzani yakarudi tena CCM na kote huko ukiangalia wapinzani kwa jumla walikuwa na kura nyingi zaidi ya CCM tatizo ni mgawanyiko.

Mi ushauri wangu uko palepale CCJ ni lazima washirikiana na wapinzani wengine waliopo sasa na kukubaliana namna thabiti ya kushirikiana kwenye uchaguzi vinginevyo hadithi ni ileile

Ukweli unabakia palepale, yaani umoja ni nguvu
 
Ni wazo zuri ndugu but tunarudi pale pale katika umoja lazima watu wajulikane ni akina nani? chadema tunamjua mzee mtei na Mbowe, CUF yuko Lipumba na Seif, NCCR Mageuzi na wengineo wengi. Haya tuambie CCJ ni akina nani? Historia zao zikoje.

Hivi unadhani wewe utaungana na mtu ambae haumjui mtaaminiana? Kama ana nia kuwavuruga vuruga je?
 
- Wakuu kikao kimekwisha hakuna lolote la maana kwa masilahi ya taifa, isipokua ya chama tu labda tusubiri NEC ya tarehe 8, April 2010.

Respect.

FMEs!

- Off course the heat is felt all over, juzi kwenye CC mkulu amelilia sana wazee viongozi wote kuwashawishi viongozi wa dini, maana hao sasa anaamini kwamba huenda ndio wenye trufu za uchaguzi ujao through CCJ!, ndio maana ninasema it is for real!

Respect.

FMEs!

Mzee FMES in CCM damu, tusiwape watu matumaini yasiyokuwepo labda hadi utakapoweka majina ya hao vigogo wanaodaiwa kuwa nyuma ya CCJ.
 
Mie siwajui nawala sina ushabiki nao.

Ila mimi ninachotaka kitokee ni CCJ waimegue CCM kwanza.

MkamaP Tuko pamoja katika hilo ndio maana mie nasema naikalia mbali. Kuna anashauri waungane mie sikubaliani nao kwanza wajulikane ni akina nani ndipo waungane venginevyo huo muungano utazaliwa kwa lengo la kuua upinzani.
 
Mimi naomba CCM ipigwe radi, tutawale ambao tumekuwa tukitawalia siku zote.
 
Nakubaliana kuwa ni kweli tunahitaji hivo lakini hapa mi nazungumzia jinsi na namna ya kushinda uchaguzi. Kuwa na utitiri wa vyama si hoja, Tz ni nchi kubwa na tatizo kubwa la upinzani ni jinsi ya kukampeni nchi nzima. Dar ndio watu wanasoma magazeti na kuangali tv lakini huko vijijini ambako kuna watu wengi zaidi ni lazima uwafuate, na wao wengine hadi leo bado wapo kwenye zama za chama kimoja sasa jinsi ya kuwafikia hao ndio suala gumu.

Jingine ukiangalia historia fupi ya upinzani bongo tangu ianze miaka ya tisini wamepoteza majimbo mengi waliochukua toka CCM ambayo yamerudi CCM, mfano mzuri ni Dar hivi sasa hakuna mbunge wa upinzani ilihali Ubungo, Temeke na Kigamboni yote yalikuwa kwenye mikono ya upinzani yakarudi tena CCM na kote huko ukiangalia wapinzani kwa jumla walikuwa na kura nyingi zaidi ya CCM tatizo ni mgawanyiko.

Mi ushauri wangu uko palepale CCJ ni lazima washirikiana na wapinzani wengine waliopo sasa na kukubaliana namna thabiti ya kushirikiana kwenye uchaguzi vinginevyo hadithi ni ileile

Ukweli unabakia palepale, yaani umoja ni nguvu

Ningependa kukuliza swali.
watu wa mjini wanaosoma magazeti, wa watu wa vijijini wasioona gazeti ni wepi kati yao ambao wana rate nzuri ya kuchagua wapinzani??
 
Ni wazo zuri ndugu but tunarudi pale pale katika umoja lazima watu wajulikane ni akina nani? chadema tunamjua mzee mtei na Mbowe, CUF yuko Lipumba na Seif, NCCR Mageuzi na wengineo wengi. Haya tuambie CCJ ni akina nani? Historia zao zikoje.

Hivi unadhani wewe utaungana na mtu ambae haumjui mtaaminiana? Kama ana nia kuwavuruga vuruga je?

Ni kweli ni lazima wajitokeze tuwajue na uzuri siku hizi hawa wanasiasa wetu zaidi wa CCM wanajulikana wako upande upi, hivo basi kwa mfano ikija julikana kuwa CCJ ni kina EL, RA etc tutajua wanasimama wapi au kama ni kina Mwakyembe, Sitta vilevile tutajua cha msingi tuombe waivuruge kidogo CCM ili upinzani upate kupumua, wasiwasi wangu tu ni kuwa tunaishangilia na kuipa matumaini mengi CCJ na tusije tukawasahau kina Chadema na CUF maana hawa wamefanya kazi ya kusambaza demekrasia bongo yetu na kufichua baadhi ya maovu ya CCM...
Hivo yetu macho tusubiri tuone ni kina nani watatoka CCM kwenda CCJ kisha tutaona kama ni kiini macho au ni wa kweli
 
MkamaP Tuko pamoja katika hilo ndio maana mie nasema naikalia mbali. Kuna anashauri waungane mie sikubaliani nao kwanza wajulikane ni akina nani ndipo waungane venginevyo huo muungano utazaliwa kwa lengo la kuua upinzani.

Unajuwa viongozi wote waliopo watawala na wapinzani wana mtazamo na fikra za kama Mugabe.

Sasa wanamapinduzi wa kweli tumewaweka kando, na kwa mtindo uliopo ni ngumu kuingia ktk uongozi.sasa saizi kinachotakiwa ni kutengeneza equal chansi. Hilo nafikiri ndo kwanza linatakiwa kutokea
 
The Following 71 Users Say Thank You to Field Marshall ES For This Useful Post:911 (Yesterday), Abraham (Today), akilipana (Today), AmaniGK (Yesterday), Andindile (Today), araway (Today), Babuyao (Yesterday), bht (Today), carmelChief (Today), D5 (Today), De Novo (Today), Dingswayo (Today), Dreamliner (Today), EdoEdson (Today), ELNIN0 (Today), fangfangjt (Today), Felixonfellix (Today), FirstLady1Fisherscom (Yesterday), Gamaha (Today), Gashle (Today), housta (Today), Jafar (Today), Jasusi (Yesterday), Jayfour_King (Today), jmushi1 (Yesterday), Junius (Yesterday), KakalendeKiby (Today), Kidatu (Yesterday), kilembwe (Today), Kingi (Today), Kitila Mkumbo (Today), Kyachakiche (Today), Lekanjobe Kubinika (Today), Lusajo (Today), Madabwada (Today), Mauza uzamayenga (Today), Mdondoaji (Today), MpendaTz (Today), Mrimu (Today), Mtu KwaoMugerezi (Today), Mzawa Halisi (Today), Mzee Mwanakijiji (Today), Nanu (Today), Ndahani (Today), Ngala (Today), nguvumali (Today), nyani<abiziani> (Today), Nyunyu (Today), PainKiller (Yesterday), Papizo (Yesterday), Pasco (Today), Pdidy (Yesterday), Renegade (Today), SelousShadow (Today), Shakazulu (Yesterday), Sikonge (Yesterday), SMU (Today), SupermanTiba (Today), Timtim (Today), Tshala (Today), Tusker Bariiiidi (Today), Waberoya (Yesterday), WaMzizima (Today) (Today), (Today), (Today), (Today), (Yesterday), (Today), (Today), (Today),
- Wakuu wote hapo juu, ninaomba kusema hivi I humbled na sasa ninaamini sana kwamba kumbe mcheza kwao hutunzwa, well tupo pamoja sana kwa sasa tayari nipo kwenye post ya dataz tukishapata green light tu tutamwaga some more dataz,

- Na kwa wale the tomasos Thanks guys na nimewasikia sana, isipokuwa basi tujaribu kuwa what we are yaani Great Thinkers, mimi nimethibitisha kwa kutoa dataz basi na wewe jitahidi kutokuthibitisha kwa kutoa japo dataz kidogo, hapo ndipo tutatimiza demokrasia au? I mean otherwise sidaiwi na mtu au member yoyote yule anything, nikiamua kuweka dataz nitaweka na nisipoamua kuweka kwa sababu yoyote, we will just call it a day na kusonga mbele kwenye mijadala mingine!

- Otherwise, wakulu wote heshima mbele na upepo ukikaa sawa tutamwaga more dataz, lakini msimamo bado ni ule ule kwamba ninaamini na kuthibitisha kwamba CCJ is for real!

Respect.

FMEs!
 
Kwa infrastructure ya Tanzania na hali halisi ya Watanzania hakuna uwezekano wa CCJ kuwa chama mdadala, yaani mara tu baada ya uchaguzi wa mwaka huu, hata kama NEC ya sisiemu ikikatika katikat vipande viwili vilivyo sawa.

Mpinzani wa kweli angeshajiunga na CHADEMA long time, wengine wote waganga njaa na vyeo.

Lets wait & see, time will tell
 
chadema haikuanza magazeti yalianza nenda kwenye archives ukaone je hapakuwapo na habari kuhusu epa na tena kabla slaa hajapewa madokumenti ya kuzungumza wacheni kujipa vikrediti kwamba nyie ndio noma! uwiiiiiii! na tena hakuna vitu vilivyoingia mlango wa nyuma soma maelezo ya mwanasheria mkuu wa serikali na taratibu za kuandika kanuni juu ya hoja za wabunge za sheria zinazotakiwa tusiwe tunaimba bila kuwa na breki ya kuangalia kama tunaimba kw atoni inayotakiwa mhhhh shiiii au ndio kusema upepo wa kusi unazuia kaskaz nini
Asante, lakini sijakupata. Naomba uhariri post yako vizuri ndiyo nielewe unataka kusema kitu gani.
 
Wamzizima

Kitu kingine unatakiwa ukumbuke watanzania tunachagua mtu ktk ubunge.

Kwa hiyo sio kweli kabisa unayoongea kwamba jumla ya kura za upinzani zilikuwa nyingi kuliko za ccm. Nafikiri lazima utambue kuna option A B......

Hivyo kuna uwezekano mkubwa kwamba kama mgombea wa TLP asingekuwepo basi ningepigia wa CCM. Kumbe basi kuunganisha vyama hakuna maana kwamba wale wote ambao walipigia wapinzani wengi tofautitofauti ni hao wote wangempigia mpinzani mmoja.

Mfano Mrema asipogombea urais basi kura yake haitaenda kwa lipumba ,bali itaenda ccm.upo??
 
we are getting there.. you know what.. watu wengi wanasahau unabii wenyewe ulikuwa unahusu nini hasa.. Niliandika hivi hapo juu:
Ni maneno hayo hayo ambayo Mpendazoe ameyarudia na mtayaona yakirudiwa na wengi wakuu watakaotoka CCM... Unabii haufanyi haraka wala hauchelewi.. hutimia kwa wakati.
.

- Strong words na dalili za mvua huwa ni mawingu!

Respect.

FMEs!
 
Ningependa kukuliza swali.
watu wa mjini wanaosoma magazeti, wa watu wa vijijini wasioona gazeti ni wepi kati yao ambao wana rate nzuri ya kuchagua wapinzani??

Haya ni maoni yangu, ukiangalia hivi sasa mikoa ambayo ina wapinzani mfano Kilimanjaro, Arusha, Kigoma, Shinyanga na Pemba utaona kuwa wamechagua personality zaidi kuliko sera. Na hata hapa Dar wale wapinzani waliokuwepo kina Mrema walikuwa ni mashuhuri zaidi kuliko vyama vyao. Sina uhakika labda kama kuna analyst mzuri humu ndani atupe ushauri zaidi kuhusu hili.

Ila ni vizuri kuanisha yafuatayo;

Cheyo na UDP wana nguvu kule kwao Shinyanga, Chadema wamejikita kwa kina Slaa, Kabwe na Kilimanjaro, CUF wanapeta Unguja na Pemba. Sasa sijui kama hi ni sababu ya ukabila au watu wa huko wanakubaliana zaidi na sera za hivi vyama kuliko sehemu nyingine bongo.
 
Kwa infrastructure ya Tanzania na hali halisi ya Watanzania hakuna uwezekano wa CCJ kuwa chama mdadala, yaani mara tu baada ya uchaguzi wa mwaka huu, hata kama NEC ya sisiemu ikikatika katikati kati.

Mpinzani wa kweli angeshajiunga na CHADEMA long time, wengine wote waganga njaa na vyeo.

Lets wait & see, time will tell
Kwanini mnawachagulia chama??
Unapofanya kitu unafanya na malengo wenda hao ccj wameshajipanga na kuweka malengo marefu ,wameshachagua waziri wa nishati, rais ,waziri mkuu nk.

Sasa mnataka waende chadema wakaanze kukonvice Mbowe na mkwe wake? Na hata hivyo wangeenda huko mgesema ni akina mrema wanaenda kuvuruga chadema.

Hebu wapeni uhuru wao.
 
Nipo nimepumzika nasikiliza kipindi cha Jahazi Clouds FM ambapo kama kawaida Ephraem Kibonde akiwa na Partiner wake Gadna Habash wanasherehesha.

Katika Habari waliyoisoma wamekataa kata kata kuwa Mpendazoe kuwa ni kigogo wa CCM. Wamewataja vigogo kuwa ni Jakaya, Mkapa, Msekwa, Kingunge na wengine wenye rank zinazofanana na za hao.

Walichonishangaza na kunisononesha ni kuwa Mpendazoe ametajwa na Kibonde kuwa hana hadhi ya kuwa Kigogo ndani ya CCM badala yake ana hadhi ya TOOTH PICK na katu asijidanganye kuwa ni KIGOGO.

Pia amemponda kuwa asijifanye kigogo kwa kuhama chama kwakuwa hata yeye alihama kutoka CTN kwenda Clouds (kama concept ya kigogo ni kuhama kutoka point moja kwenda nyingine) basi na yeye ni KIGOGO.

Mwenyekiti wa CCJ ameibiwa nyaraka zake Kariakoo leo na katika nyaraka hizo yalikuwepo majina ya wanachama wao. Kibonde amemkejeli sana na pamoja na mambo mengine amekikejeli CCJ kuwa eti " chama gani wanachama wanajaa kwenye handbag(nadhani anamaanisha wanachama ni wachache) na akatoa mfano CCM ambacho kina wanachama kuanzia chipukizi, shule za sekondari hadi vyuo vikuu.

Great thinkers mnaonaje hili? Sio kama ni mpango umeandaliwa na wahuni fulani wa kisiasa kufifisha vuguvugu hili la mabadiliko linaloendelea sasa kwa kuwatumia wanahabari pamoja na vyombo vya habari?

Mzi
 
Back
Top Bottom