Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 13,227
- 26,048
Bado nasema na nitasema daima , kati ya jambo ambalo bado serikali imefeli kupambana nalo ni ujinga na ushamba na ukitaka kuona nchi hii wajinga ni wengi sana basi fuatilia mijadala ya humu JF
Leo Mama Samia kafanya kikao na wafanyabiashara wa Oman na ameelezea fursa ya kusafirisha wanyama hai kutoka Tanzania kwenda Oman na nchi za kiarabu
Kwa ujinga tu wa Watanzania wengi wametafsiri statement ya Mama Samia kuwa ni kusafirisha wanyama pori!
Ujinga na ushamba wa watu hawa umesababishwa na kutokujua kuwa kwa mujibu wa dini ya kiislamu ambayo ndo dini kuu ya uarabuni sio vizuri kula kibudu. Waislamu hasa wanaamini nyama anayotakiwa kuila Muislamu safi ni nyama (fresh) iliyochinjwa kwa kufuata taratibu zao na hili ndo limepelekea kukua sana kwa biashara ya usafirishaji wa wanyama hai kutoka nchi mbalimbali kwenda nchi za kiarabu!
Wanyama hao ni mbuzi, kondoo, ng'ombe na hata Ngamia na moja ya nchi zilizokamatia hii fursa mapema kabisa ni nchi ya Australia. Waarabu wa sasa wanataka kumuona mnyama na kumchinja wenyewe ili wamle kwa sababu dini yao inawalazimisha kula nyama inayotokana na mnyama fresh aliyechinjwa kwa kufuata taratibu zao(Halal).
Wafanyabiashara wa Australia walikosa sana masoko uarabuni kwa sababu waarabu walianza kupunguza kununua nyama na kuhitaji wanyama hai jambo lililowafanya wabadili mbinu na kuanza kusafirisha wanyama hai!
Mama Samia ameona hiyo fursa na pia ameona pia fursa ya nchi yetu kuwa na bandari kubwa inayoweza kutumika kusafirisha wanyama hawa hai kiurahisi kwenda nchi za uarabuni maana kijiogrqphia Tanzania tuko karibu sana na nchi za uarabuni na ameamua kuisimamia ifanikiwe.
Kwa ushama na ujinga wa Watanzania wanaponda hadi hili kisa tu chuki zao! Mbaya zaidi wanahusisha na wanyamapori jambo ambalo sio kweli!
Piga kazi Mama Samia! Wenye akili tunakuelewa sana