Ujenzi wa vyumba vya madarasa sekondari kwa fedha za mkopo ni matumizi mabaya ya fedha zetu

U-fresh

Member
Aug 4, 2022
21
19
Tatizo kubwa linalosumbua nchi yetu ni viongozi kuamini wanahakili nyingi kuliko wasio viongozi, awamu hii ya sita imekuwa ikipeleka fedha nyingi kwenye miradi ya shule sekondari bila kufanya tathmini kuwa je bado kuna uhitaji mkubwa wa vyumba hivyo? Mbaya zaidi fedha inayopelekea huko ni ya mkopo wenye riba.

1. Uhitaji vyumba vya madarasa ni mkubwa zaidi s|misingi na sio sekondari,shule za msingi ndiko kuna idadi kubwa sana ya watoto mathalani chumba kimoja wanawekwa watoto zaidi ya 200.

2. Kuna drop out kubwa sana sekondari,wanafunzi wengi wanaacha shule sekondari kuliko hata shule ya msingi,hii inapelekea baadhi ya shule kuwa free room nyingi sana,mathalani kwa taarifa shule x, 2021 ilipewa fedha ya vyumba vinne, ikasajiri wanafunzi 180 wa kidato cha kwanza 2022 cha kushangaza kufikia desemba wanafunzi wengi wameacha shule na kubakia 60 tu na wameunganishwa darasa moja, kibaya zaidi fedha za mkopo zimepelekwa shule hiyo tena kwa 2022 kujenga madarasa matatu,lkn tayari wanayo free matatu ya last year, huko ni kuchezea fedha zetu.

3. Hakuna uwiano wa idadi ya walimu na wanafunzi kwa sekondari na primary pia.Walimu ni wachache sana kuweza kufundisha wanafunzi waliogawanyika katika mikondo mingi, mfano, mwl. mmoja unamwambia afundishe mikondo mikondo 8 kitu hichohicho sidhani kama atafundisha kwa ufasaha.

4. Morali ya walimu ipo chini sana kutokana na mazingira magumu waliyonayo,walimu wanalipwa kidogo sana, hii imepelekea walimu kujitafutia kipato kwa njia zingine ili kuweza kujikimu hivyo kutelekeza majukumu yao ya ualimu, walimu kazi yao kubwa kwa sasa ni bodaboda,wauza maduka na magenge,wakulima n.k.

5. Serikali iwekeze zaidi kujenga mabweni kwani ndiyo changamoto kubwa sana kwa sasa badala ya madarasa yanayojengwa kisha hayatumiki, wanafunzi wanaosoma shule za kata nyingi wanatoka mbali na shule ilipo hii inawalazimu kupanga vyumba, hii imesababisha utoto na kuacha shule, mimba, uvutaji bangi, ndoa zisizo rasmi, ukweli uwekwe kupanga ovyo mitaani kunachangia sana kuharibu wanafunzi.

Serikali iangalie maeneo mengine ya kuboresha elimu yetu badala ya kila kukicha kujenga madarasa yanayozidi mahitaji yetu, pia uelekeze nguvu shule za msingi ambapo kuna tatizo kubwa sana.
 
Unaijua hali halisi ya hizi shule za sekondari za kata?. Achilia mbali miundo mbinu chakavu katika shule kongwe za sekondari.

Sekondari hizi za kata zilizo nyingi zimejengwa kwa nguvu za wananchi. Na majengo yake kwa sasa hayapo katika hali rafiki.

Na kwa miaka ya hivi karibuni kumekuwa na utitiri wa wanafunzi wanaofaulu elimu ya msingi na kujiunga na elimu ya sekondari. Je, umepata wasaa wakwenda kuchungulia kwenye vyumba vya madarasa uone vijana wanakaaje humo?. Kidato cha kwanza chenye mikondo mitatu, kina jumla ya wanafunzi 400.

Je, Serikali inakosea kuwajengea vyumba vya madarasa?.
 
Back
Top Bottom