Mbeya: Mwanafunzi wa Form 4 akamatwa kwa tuhuma za kuchoma moto vyumba viwili vya madarasa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,813
11,991
Kuzaga111.JPG

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia mwanafunzi wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Serikali Iyela ya Jijini Mbeya aitwaye YESSE CHARLES [17] kwa tuhuma za kuchoma moto vyumba viwili vya madarasa vya Shule hiyo.

Ni kwamba, Septamba 13, 2023 huko katika Shule ya Sekondari Iyela, Mwanafunzi YESSE CHARLES [17] kidato cha nne alichoma moto vyumba viwili vya madarasa katika Shule hiyo kwa kutumia mabua na karatasi ambapo chumba kimoja kati ya hivyo kilikuwa kikitumika kama bweni kipindi hiki cha likizo kwa baadhi ya wanafunzi wa kidato cha nne walioweka kambi kujisomea kwa ajili ya maandalizi ya mitihani ya kitaifa ya kidato cha nne.

Kamanda wa Polisi Mbeya, Benjami Kuzaga amesema chanzo cha tukio ni chuki ya mwanafunzi huyo mtukutu baada ya kuadhibiwa na Mkuu wa Shule hiyo kwa kosa la utovu wa nidhamu na kutokuhudhuria vipindi shuleni hapo.

Moto huo uliteketeza vyumba viwili vya madarasa, nguo, magodoro na madaftari ya wanafunzi. Upelelezi unaendelea.
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia mwanafunzi wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Serikali Iyela ya Jijini Mbeya aitwaye YESSE CHARLES [17] kwa tuhuma za kuchoma moto vyumba viwili vya madarasa vya Shule hiyo.

Ni kwamba, Septamba 13, 2023 huko katika Shule ya Sekondari Iyela, Mwanafunzi YESSE CHARLES [17] kidato cha nne alichoma moto vyumba viwili vya madarasa katika Shule hiyo kwa kutumia mabua na karatasi ambapo chumba kimoja kati ya hivyo kilikuwa kikitumika kama bweni kipindi hiki cha likizo kwa baadhi ya wanafunzi wa kidato cha nne walioweka kambi kujisomea kwa ajili ya maandalizi ya mitihani ya kitaifa ya kidato cha nne.

Chanzo cha tukio ni chuki ya mwanafunzi huyo mtukutu baada ya kuadhibiwa na Mkuu wa Shule hiyo kwa kosa la utovu wa nidhamu na kutokuhudhuria vipindi shuleni hapo.

Moto huo uliteketeza vyumba viwili vya madarasa, nguo, magodoro na madaftari ya wanafunzi. Upelelezi unaendelea.
Huko mbeya kuna nini? Wanafunzi wanatrend negatively sana.Nawapongeza walimu muda wote naona hawawi chanzo wala sehemu ya matukio hayo .Mwanafunzi huyo segerea moja kwa moja ni muhujumu uchumi kwa kuchoma moto Mali za wananchi/serikari.
 
Na sheria inasema kuchoma jengo kwa makusudi hukumu yake ni kifo, sasa haya ngoja tuone unafiki unavyofanya kazi
 
Back
Top Bottom