Ujenzi wa nyumba za kuficha paa/contemporary/ hidden roof

Tatizo mafundi wetu wezi sana, ukimuuliza bei ya hizi paa za kuficha gharama unakuta ni mara 2 ya paa za kawaida. Ila ukiangalia hizi paa za kuficha zinatumia bati na mbao kidogo sana kwan muundo wake ni slope. Pili hasara ni nyingi kwa hii design kwa sababu ina space ndogo kati ya bati na ceiling ya ndani hii inaweka ugumu wa service za umeme na vitu vingine vitavyohitaji upande darini.
 
kama vitu gani? kwan wiring lazim ipite juu ? si hata chin
 
Bro umeongea yote;
Iko hivi: nyumba hii inahitaji myaalam ambaye anajua namna ya kuanza hadi kumaliza.
Wengi anampa fundi wa kujenga tofali then analeta mwingine wa kuezeka....

Hii nyumba inajengwa na mtaalam mmoja mwanzo hadi mwisho.

Chukua haya yafuatayo;
1. Msingi uinuke
2. Boma liwe na tofali laini 11
3. Baada ya lenta hakikisha unatengeneza sehemu ya kupokelea maji
4. Pawepo na ducts za kupitishia maji na sio bomba
5. Upake bitumen pamoja na mebrane cloth maeneo ya wazi ya kupokelea maji.

6. Epuka slop ndefu za paa bali livunje vunje vipande vipande ili maji yashukie sehemu tofauti

Ukizingatia haya nyumba hii hsivuji na utaifurahia na haina gharama kubwa
Hii bitumen na membrane cloth inapatikana wapi mkuu??
 
IMG_0569.jpg

IMG_0570.jpg
 
Mbona swali lako hili pia ni la kijinga! Kwani elimu ndo inajenga nyumba au ujuzi wa mtu! Hujifunzi kwa mainjia wale wa majengo wanavoharibu kazi na mavyeti yao!
Ninachokijua mimi ni kwamba ujenzi wa nyumba ni professional kama zilivyo professional nyingine kama vile udaktari,urubani na kadhalika.

Sasa unavyodai kuwa kinachojenga nyumba siyo elimu bali ni ujuzi wa mtu,je ninaweza kumfanyia mtu operesheni ya moyo au operesheni ya ubongo bila elimu?Huo ujuzi wa kufanyia watu operesheni nitaupata wapi kama siyo kwenye elimu?
 
Uwe unawaambia pia kwamba zinahitaji kemikali maalumu kuunga paa na kuta zisivuje.

Pia uwaeleze kwamba kwa kuwa hazina roof overhang zinahitaji kupakwa rangi maalumu ambazo zitahimili jua na mvua/unyevu kwa kuwa kutazake zina direct contact na jua na mvua tofauti na traditional houses

La mwisho uwaeleze wateja wako kwamba hizo nyumba mara nyingi zinakuwa na extra costs Ili zipendeze yaani makuta kuta,maurembo mengi na finishing ya nguvu.Kiufupi gharama za ufundi ni kubwa zaidi kuliko nyumba za kawaida.

Mwisho wa siku unakuta ule unafuu wa gharama ya paa ume offset kwenye finishing tena ya nje ambapo on average zina gharama kubwa kuliko nyumba za kawaida.

All in all ni nyumba nzuri kama una pesa ila kama pesa ya kuunga bora ujenge traditional houses
Umefafanua vizuri sana mkuu asante kwa angalizo
 
Ninachokijua mimi ni kwamba ujenzi wa nyumba ni professional kama zilivyo professional nyingine kama vile udaktari,urubani na kadhalika.

Sasa unavyodai kuwa kinachojenga nyumba siyo elimu bali ni ujuzi wa mtu,je ninaweza kumfanyia mtu operesheni ya moyo au operesheni ya ubongo bila elimu?Huo ujuzi wa kufanyia watu operesheni nitaupata wapi kama siyo kwenye elimu?
Hicho ni kipaji kama vipaji vingine unaweza kuwa daktari kila siku ukawa unauwa watu tu..hata madaktari wanasomea professionalism lakini uwezo wamepishana why! Mkuu usitegemee sana vyeti.
Sisi tulioko makazini tunaona tofauti ya shule na talent ya mtu, japokuwa wwngine wana vyote yaani shule na kipaji
 
Back
Top Bottom