Mbona malalamiko mengi kwenye nyumba za kuficha Bati (Hidden Roof), Mafundi wanakosea nini hadi zinavuja?

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,119
1709544320233.png

Kumekuwa na malalamiko mengi kuwa nyumba za kuficha Bati maarufu kama Contemporary au Hidden Roof zina shida ya kuvuja sana, sasa wataalamu au mliofanikiwa kujenga hizo nyumba hebu tushauriane hapa mafundi maiko wetu hawa wanakosea wapi?

Maana nataka kubadili paa langu liwe Hidden ila kila nikiona malalamiko ya wadau na picha za baadhi ya nyumba zinavyotia balaa nakosa ujasiri wa kufanya hizo changes.
 
Nyumba hizo ni hatari sn. Sitarudia tena. Zimenipa HASARA KUBWA SANA. Nimeamua kuezeka kawaidi. Sasa nafurahia kuwa nyumbani kwangu kwa raha hata kama mvua inanyesha. Zamani inapokuja mvua ROHO JUU! Maana imewahishusha Gypsam board yote chini. Ikavunja vitu vingi ndani pale. Aise sitakaa nisahau.
 
Hatari sana
 
View attachment 2924216
Kumekuwa na malalamiko mengi kuwa nyumba za kuficha Bati maarufu kama Contemporary au Hidden Roof zina shida ya kuvuja sana, sasa wataalamu au mliofanikiwa kujenga hizo nyumba hebu tushauriane hapa mafundi maiko wetu hawa wanakosea wapi?

Maana nataka kubadili paa langu liwe Hidden ila kila nikiona malalamiko ya wadau na picha za baadhi ya nyumba zinavyotia balaa nakosa ujasiri wa kufanya hizo changes.
Yaani hujui tu ubabaishaji wa Tanzania? Mafundi wenye sifa ya ufundi ni wachache sana. Wengi vishoka. Nchi nzima.
 
Nyumba nying za namna hiyo kwanza zinatakiwa mtu anaaza msingi akijuwa anataka kujenga paa la ndani hivyo luanzia vipimo vya urefu na upana nguzo nk lazima vianze chini ili kuzalisha zege upana wa gata pamoja na kujua ukubwa wa bomba na wapi utayapeleka maji
 
Contemporary roofing style ina mahesabu fulani ambayo kama yakikosewa mfumo mzima wa paa hautakuwa wa ufanisi ..will fail during rains. 'span' ..slope, overlapping, joints ..canopy, proofing etc ..ni mfumo ambao unasave material ( mbao na mabati) una muonekano mzuri ..ila unahitaji ujuzi wa ziada, sio kila fundi wa kupaua anaweza.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom