Ni Sahihi Kutumia Nondo za 10mm Kwenye Mifereji ya Paa la "Hidden Roof"?

Shakir

JF-Expert Member
Jul 31, 2012
1,602
1,819
Kwema Wakuu?
Nimeanza Ujenzi wa Nyumba yenye Hidden Roof, na nishapiga kozi 10 nataka sasa nianze kwenye Linta kwenda juu kozi 6 pamoja na kibaraza na mifereji yake ya maji.

Katika "quotations" nilizopata kutoka kwa mafundi kama watatu hivi kuna mmoja ameniambia kua lile zege za mifereji ya maji yanayotoka kwenye bati tutatumia nondo milimita 10 sababu ni maji tu yatakayopita mule, sio zege la kuweka kitu juu yake.

Amesema kuweka nondo za milimita 12 ni sawa lakini sio lazima so long as hilo zege ni la kupitishia maji tu so kwa ajili ya bajeti minimization of cost basi nichukue tu za 10mm.

Naombeni ushauri wenu wakuu, mnaonaje huu ushauri wa huyu fundi? Bado sija conclude ndio niko kwenye kuchanganua hizi quotations nione niende na yupi.
 
Kwa mifereji pekee ya roof less, nashauri utumie hiyo 10mm round bar kwasababu hakuna mzigo utakao kaa juu ya hiyo mifereji. Kikubwa nashauri utumie kokoto ndogondogo zisizo zidi 12-14mm, pia hakikisha resho ya cement inakua imechangamka.
 
Nondo za mm 10 zinafaa sana hata za mm 8 pia zinafaa kwa mfereji chief
Ila angalizo muhimu ni namna ya kuzifunga na zege ishindiliwe vizuri
Nakukumbusha ukumbuke kuweka njia za ukubwa wa kutosha kutoa maji juu na kuyapeleka chini ni muhimu sana
 
Hii kitu nilikuwa sijaona inavyofanywa; lst week nilikuwa nafanya roofing ya servant quarter yangu (self contained) ya 2 rooms Chuga ndo fundi wakaja na hizo habari za kutengeneza mifereji ya kupokea maji.... sema inataka pia kujiandaa hasa kwenye cement na nondo siyo ya kukurupuka sanaaa; kwa case yangu nilitumia nondo za mm 12 kwa sababu ndizo zilizokuwepozilibaki wakati natengeneza structure ya gate na masalia wakati wa ujenzi wa nyumba kubwa!!
 
Nondo za mm 10 zinafaa sana hata za mm 8 pia zinafaa kwa mfereji chief
Ila angalizo muhimu ni namna ya kuzifunga na zege ishindiliwe vizuri
Nakukumbusha ukumbuke kuweka njia za ukubwa wa kutosha kutoa maji juu na kuyapeleka chini ni muhimu sana
Ahsante sana Mkuu,
Katika mafundi wa3 walionipa quotations ni mmoja tu ndio kataja hizi za 10mm, wengine wawili wametaja 12mm nkaona niulize wadau hapa
 
Kwema Wakuu?
Nimeanza Ujenzi wa Nyumba yenye Hidden Roof, na nishapiga kozi 10 nataka sasa nianze kwenye Linta kwenda juu kozi 6 pamoja na kibaraza na mifereji yake ya maji.

Katika "quotations" nilizopata kutoka kwa mafundi kama watatu hivi kuna mmoja ameniambia kua lile zege za mifereji ya maji yanayotoka kwenye bati tutatumia nondo milimita 10 sababu ni maji tu yatakayopita mule, sio zege la kuweka kitu juu yake.

Amesema kuweka nondo za milimita 12 ni sawa lakini sio lazima so long as hilo zege ni la kupitishia maji tu so kwa ajili ya bajeti minimization of cost basi nichukue tu za 10mm.

Naombeni ushauri wenu wakuu, mnaonaje huu ushauri wa huyu fundi? Bado sija conclude ndio niko kwenye kuchanganua hizi quotations nione niende na yupi.
Funga hata hizo za 10milm, cement tumia ile kali. Ukibania na hapo unakaribisha kuvuja. Muhimu upate fundi mzuri tu.
 
Hivi watanzania tumerogwa na nani!! Mara nyingi tunaonywa kuwa hidden roof nikujiweka kwenye hati hati ya kurudia kupaua lakini bado tunaendelea. Haya kila la heri.
 
Ongea technically, shida iko wwpi?
Ni kila hidden roof itarudiwa kupauliwa?
Mtu akija humu kuuliza namna ya kujenga ina maanisha hana uwezo wa kumuweka mwandisi majengo. Hii inaashiria kuwa uwezo wa mtu huyo kwenye contemporary roofing ni mdogo. Teknolojia hii ya ujenzi ndiyo imeingia nchini na mafundi wengi wa mtaani hawana mafunzo ya mfumo huu. Wengi wao wanafanya kwa kuiga namna walivyojenga na wachina hivyo kujikuta wakiwaharibia watu wengi nyumba.

Contemporary roofing/housing inahitaji msanifu majengo (Architect) na mwandisi majengo (Civil Engineer) waliyosomea au wenye uzoefu wa mfumo huu mpya wa ujenzi. Kuwatumia hawa wataalamu kunahitaji fedha.

Hivyo ninashauri kujenga kawaida kama uwezo wako ni kutaka ushauri kwa watu wa humu ndani, ambao utaupata bure lakini siyo kutoka kwa mtaalamu, ili usije ukajuta na kujenga uadui na fundi wako.
 
Mimi nakushauri upaue kawaida, yaani hilo paa exposure to sunlight iko so close and direct, angalau hilo paa la kawaida kuna space kabla ya boards (gypsum). Kingine huwezi kuzuia maji yasishike kwenye kuta, so utahangaika sana
 
Kwema Wakuu?
Nimeanza Ujenzi wa Nyumba yenye Hidden Roof, na nishapiga kozi 10 nataka sasa nianze kwenye Linta kwenda juu kozi 6 pamoja na kibaraza na mifereji yake ya maji.

Katika "quotations" nilizopata kutoka kwa mafundi kama watatu hivi kuna mmoja ameniambia kua lile zege za mifereji ya maji yanayotoka kwenye bati tutatumia nondo milimita 10 sababu ni maji tu yatakayopita mule, sio zege la kuweka kitu juu yake.

Amesema kuweka nondo za milimita 12 ni sawa lakini sio lazima so long as hilo zege ni la kupitishia maji tu so kwa ajili ya bajeti minimization of cost basi nichukue tu za 10mm.

Naombeni ushauri wenu wakuu, mnaonaje huu ushauri wa huyu fundi? Bado sija conclude ndio niko kwenye kuchanganua hizi quotations nione niende na yupi.
Tumia, Haina shida
 
Contemporary building ukijenga kimasikini inakula kwako

Turudi kwenye mada: hapo nondo mm8, 10 hata 12 ila ratio iwe nzuri na kokoto ziwe zile ndogo za ½ inch au hata ndogo yake sio mbaya
 
Mtu akija humu kuuliza namna ya kujenga ina maanisha hana uwezo wa kumuweka mwandisi majengo. Hii inaashiria kuwa uwezo wa mtu huyo kwenye contemporary roofing ni mdogo. Teknolojia hii ya ujenzi ndiyo imeingia nchini na mafundi wengi wa mtaani hawana mafunzo ya mfumo huu. Wengi wao wanafanya kwa kuiga namna walivyojenga na wachina hivyo kujikuta wakiwaharibia watu wengi nyumba.

Contemporary roofing/housing inahitaji msanifu majengo (Architect) na mwandisi majengo (Civil Engineer) waliyosomea au wenye uzoefu wa mfumo huu mpya wa ujenzi. Kuwatumia hawa wataalamu kunahitaji fedha.

Hivyo ninashauri kujenga kawaida kama uwezo wako ni kutaka ushauri kwa watu wa humu ndani, ambao utaupata bure lakini siyo kutoka kwa mtaalamu, ili usije ukajuta na kujenga uadui na fundi wako.
Ahsante Mkuu kwa ushauri
 
Back
Top Bottom