Ujenzi wa hidden roof na paa la kawaida

Jenga kawaida tu maana shughuli ya kuweka gutter si mchezo. Zitaenda nondo na cement hapo mpaka utie akili. Hapo bado shughuli ya kupaua upate fundi mzuri.
 
Kama fundi wenyewe ni bora fundi, jiandaye kuwa na miavuli au nylon sheets wakati wa masika mkuu.

Kuna jamaa alifumua na kuweka mapaa ya kawaida. Hana hamu na hataki hata kusikia mtindo huo🤣🤣🤣🤣
Huu mtindo unavutia, sema unachangamoto endelevu zinazoumiza hadi mifukoni.
 
Mimi nimepaua hidden roof ... Haivuji .... But kama unachagua namna ya upauaji kwa ajili ya kupunguza gharama wewe bora upaue paa la kawaida tu. Ukijichanganya kwenye hidden roof eti unapunguza gharama utaimba haleluya
1. Mwaka wa ngapi huu tangu upaue. Hidden roof?
2. Bati za gage ngapi umeezekea?
 
Hidden roof huvuja sababu kwa sababu kuu tatu;
1. Wakati wa kutengeneza gutter haikuzibwa vizuri na kupigwa plasta kwenye kona za ukuta hivyo kusababisha maji kutuama na kuingia kwenye ukuta.

2. Mabomba ya kutolea maji ni finyu au yameziba au gutter hazina slope ya kutosha

3. Fundi bati alizingua aidha hakuziba vizuri sehemu ambazo bati inaingia kwenye ukuta wakati wa kuezeka au alikuwa na pilika nyingi zilizopelekea kukanyanga bati maranyingi. Hii hutokea pale ambapo ushapaua ndio unapandisha tofali za kumalizia juu au kupiga plasta.
 
Back
Top Bottom