Hidden roof/Paa la kuficha: Naweza kuezua na kuweka paa la kawaida au ndo imekula kwangu?

Shabikia

Member
Aug 21, 2023
18
21
Habari za usiku huu wana wa JF,

Nimekuja kuomba ushauri maana nimewaza peke angu bila kupata majibu. Nimejenga kajumba kangu wa style hii ya sasa la bati la kuficha ila sasa kiukweli nakosa usingizi maana si kwa kuvuja huku.

Hivi naweza kuezuwa na kuweka paa la kawaida au ndo imekula kwangu? Msaada please Natanguliza shukurani zangu za dhati.
 
Kama umeshajenga hidden roof na inavuja inawezekana kabisa ukaezua na kujenga paa la kawaida ila garama ya marekebisho no kubwa zaidi. Ningeshauri utafute mtaalamu akurekebishie tu hiyo hidden roof isivuje kuliko kupaua upya.

Jamani tuwe tunatafuta wataalamu wa hivi vitu ukipenda kitonga hasara zake ni kubwa zaidi. Unajenga nyumba itakayo dumu zaidi ya miaka 50 kwa nini utafute mafundi wakuunga unga na usitafute mtaalamu mzur.

Tukitaka vitu vizur tukubali kugaramika sababu kubwa ya watu kujengewa vitu vibovu ni kupenda mteremko zaidi
 
Hivi naweza kuezuwa na kuweka paa la kawaida au ndo imekula kwangu?
Unaweza kuezua na kuweka paa la kawaida.

Kabla ya kufanya hivyo jaribu kutafuta fundi mzuri wa kuezeka akushauri, huenda nyumba ilipojengwa haikuandaliwa mifereji ya kukinga maji.
 
Unaweza kuezua na kuweka paa la kawaida...

Kabla ya kufanya hivyo jaribu kutafuta fundi mzuri wa kuezeka akushauri, huenda nyumba ilipojengwa haikuandaliwa mifereji ya kukinga maji...
Yes kabisa ndio sababu kuu za hizi nyumba kuvuja.

Jamani tuelewe hidden roof si ya kupunguza garama za ujenzi km unajenga kwa kupenda muonekano sawa ila asikidanganye mtu utakuwa unakwepa garama.

Inatakiwa ugaramike ijengwe mifereji imara ya zege zuri na juu iwekwe water proofing material hizi zote ni garama.

Sasa ww unataka kujenga ukaweka kamfereji Cha hovyo hovyo slope yenyew haieleweki lazma ikuvujie mpaka uitike abeee
 
Habari za usiku huu wana wa JF,

Nimekuja kuomba ushauri maana nimewaza peke angu bila kupata majibu. Nimejenga kajumba kangu wa style hii ya sasa la bati la kuficha ila sasa kiukweli nakosa usingizi maana si kwa kuvuja huku.

Hivi naweza kuezuwa na kuweka paa la kawaida au ndo imekula kwangu? Msaada please Natanguliza shukurani zangu za dhati.

Unaweza hata bomoa nyumba yote ukaanza upya, issue ni maokoto tu.
 
Habari za usiku huu wana wa JF,

Nimekuja kuomba ushauri maana nimewaza peke angu bila kupata majibu. Nimejenga kajumba kangu wa style hii ya sasa la bati la kuficha ila sasa kiukweli nakosa usingizi maana si kwa kuvuja huku.

Hivi naweza kuezuwa na kuweka paa la kawaida au ndo imekula kwangu? Msaada please Natanguliza shukurani zangu za dhati.
Jitahidi kupata mafundi wazuri hasa kampuni zilizosajiliwa na kulipa kodi, nenda ERB NA crb KUPATA wajenzi wa hizo paa, hutojuta.
Usibadilishe gharama ni kubwa sana ,.
 
Kama umeshajenga hidden roof na inavuja inawezekana kabisa ukaezua na kujenga paa la kawaida ila garama ya marekebisho no kubwa zaidi. Ningeshauri utafute mtaalamu akurekebishie tu hiyo hidden roof isivuje kuliko kupaua upya.

Jamani tuwe tunatafuta wataalamu wa hivi vitu ukipenda kitonga hasara zake ni kubwa zaidi. Unajenga nyumba itakayo dumu zaidi ya miaka 50 kwa nini utafute mafundi wakuunga unga na usitafute mtaalamu mzur.

Tukitaka vitu vizur tukubali kugaramika sababu kubwa ya watu kujengewa vitu vibovu ni kupenda mteremko zaidi
Hata aje fundi kutoka wapi, itazidi kuvuja tu
 
Unajua kaz ya fundi ni kujenga kile kilicho designiwa tatzo mnataka kuruka stage ya design ndo shida inapokuja hapo na ubaya ni kuwa hiyo stage hairukiki ukiruka utarudi tu either kwa kuvuja au makosa mengine mengine
 
Back
Top Bottom