Ujenzi wa nyumba za kuficha paa/contemporary/ hidden roof

Colgate3

JF-Expert Member
Jun 13, 2020
800
1,424
Habari waungwana na wadau wa ujenzi.
Nawajaribisha tushirikiane kujadiliana aina hii ya ujenzi kwa wataalam na wadau wa ujenzi wa aina hii....karibuni
1.Je una changamoto katika ujenzi wa nyumba tajwa hapo juu?

2. Umejengewa nyumba ukakutana na changamoto ya kuvuja?

3. Wewe ni mjenzi na hujui namna ya kujenga kwa usahihi nyumba za kuficha paa?

4. Una ndoto ya kujenga nyumba za aina hii lkn hujui gharama zake?

Niko hapa kutoa ushauri bure kabisa.

734325105.jpg
111861820.jpg



......................................................................................
Chukua haya yafuatayo;
1. Msingi uinuke
2. Boma liwe na tofali laini 11
3. Baada ya lenta hakikisha unatengeneza sehemu ya kupokelea maji
4. Pawepo na ducts za kupitishia maji na sio bomba
5. Upake bitumen pamoja na mebrane cloth maeneo ya wazi ya kupokelea maji.

6. Epuka slop ndefu za paa bali livunje vunje vipande vipande ili maji yashukie sehemu tofauti

Ukizingatia haya nyumba hii hsivuji na utaifurahia na haina gharama kubwa
 
Kwangu mimi;
1. Nyumba zenye mwonekano bomba sana
2. Gharama za paa ni nafuu sana karibu robo ya nyumba za kawaida
3. Tatizo wengi hawazijui namna ya kuzijenga
Uwe unawaambia pia kwamba zinahitaji kemikali maalumu kuunga paa na kuta zisivuje.

Pia uwaeleze kwamba kwa kuwa hazina roof overhang zinahitaji kupakwa rangi maalumu ambazo zitahimili jua na mvua/unyevu kwa kuwa kutazake zina direct contact na jua na mvua tofauti na traditional houses

La mwisho uwaeleze wateja wako kwamba hizo nyumba mara nyingi zinakuwa na extra costs Ili zipendeze yaani makuta kuta,maurembo mengi na finishing ya nguvu.Kiufupi gharama za ufundi ni kubwa zaidi kuliko nyumba za kawaida.

Mwisho wa siku unakuta ule unafuu wa gharama ya paa ume offset kwenye finishing tena ya nje ambapo on average zina gharama kubwa kuliko nyumba za kawaida.

All in all ni nyumba nzuri kama una pesa ila kama pesa ya kuunga bora ujenge traditional houses
 
Uwe unawaambia pia kwamba zinahitaji kemikali maalumu kuunga paa na kuta zisivuje.

Pia uwaeleze kwamba kwa kuwa hazina roof overhang zinahitaji kupakwa rangi maalumu ambazo zitahimili jua na mvua/unyevu kwa kuwa kutazake zina direct contact na jua na mvua tofauti na traditional houses
Naam, umenena vyema, nitaweka kila kitu hapa
 
Back
Top Bottom