Ngongo
JF-Expert Member
- Sep 20, 2008
- 18,954
- 31,256
HATIMAYE ujenzi wa jengo jipya la Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, utakaogharimu Sh 30.2 bilioni unatarajiwa kuanza mwezi Septemba mwaka huu mjini hapa.
Akizungumzana waandishi wa habari jana, Afisa mwandamizi wa jumuiya hiyo na msimamizi wa ujenzi huo, Phil Makini Klerruu alisema ujenzi huo unatarajiwa kukamilika mwaka 2011.
Klerruu alisema, fedha za ujenzi wa jengo hilo ambalo litatosheleza idara zote na vitengo vyote vya jumuiya hiyo, zimetolewa na serikali ya Ujerumani.
Alisema katika jengo hilo, kutakuwa na kumbi za mikutano, ukumbi wa kisasa wa Bunge la Afrika Mashariki, ukumbi wa mahakama ya jumuiya hiyo na sehemu ya Secretarieti ya jumuiya hiyo.
"Katika ramani ya ujenzi wa jengo hili kutakuwa na eneo kubwa la kuegesha magari, eneo la chakula na ofisi za wabunge wote"alisema Klerruu.
Alisema tayari michoro yote ya jengo hilo imekamilika na imeridhiwa na jumuiya hiyo na sasa kinachosubiriwa na mkandarasi kupitishwa na kuanza kazi.
Alisema ujenzi wa jengo hilo, utapunguza gharama za matumizi ya kulipia pango jumuiya hiyo katika majengo mbali mbali likiwemo jengo la mkutano wa kimataifa(AICC)
ambapo sasa ndipo yalipo Makao Makuu yake.
Alisema katika jengo la AICC pekee jumuiya hiyo inalipa kwa mwezi dola za Marekani 4,050 kama pango na pia kuna majengo mengine ambayo yanalipwa kwa kukodisha vitengo vya jumuiya hiyo.
Msimamizi huyo wa ujenzi alisema eneo ambalo litajengwa ofisi hizo lina ukubwa wa hekta 9.8 na lipo jirani na jengo la AICC.