Yafuatayo ni mambo 10 muhimu kuhusu ujenzi wa msingi

greater than

JF-Expert Member
Sep 22, 2018
783
1,215
MAKALA YA 1
Karibu katika Makala uhusio Ujenzi Majengo madogo mfano; Nyumba,maduka,Zahanati,Darsa n.k
Leo tuangazie ujenzi wa msingi(foundation) wa jengo.
Yafuatayo ni mambo 10 muhimu kuhusu msingi
1.Ujenzi wa jengo hujumuisha sehemu kuu tatu.Ambazo ni paa,kuta na Msingi hufanya kazi zifuatazo
-kubeba uzito wote wa jengo na kupotelea kwenye ardhi
-huwezesha jengo kusimama
-hukinga jengo ahidi ya madhira ya mtikisiko/tetemeko,maji na mmomonyoko ardhi

2.Aina za msingi: zipo nyingi.lakini, katika ujenzi wa Majengo madogo,kuna aina kuu tatu za msingi;strip,raft na pile.
uchaguzi wa aina ipi ya msingi kutumika hufanywa kwa kuzingatia ardhi ya eneo husika,uzito wa jengo ,upatikanaji wa matilio na gharama za ujenzi.

3.Msingi wa Raft :Ardhi huchimbwa na eneo lote ambalo litakalokuwa na jengo humwagwa zege.ujenzi wake ni gharama sana ,lakini pia imara na bora kuliko aina nyingine.

4.Msingi wa pile :Hapa ardhi uchimbwa na kuweka nguzo.hutumika katika maeneo ambapo tabaka la udongo lenye kubeba jengo hupatikana kwa kuchimba umbali wa zaidi ya mita 1.2
Mf:maeneo ya Fukwe za bahari,mito na maziwa,lakini pia magorofa mengi kutumia aina hii ya msingi.

5.Msingi wa Strip: Hii ndiyo aina ya msingi inayotumika katika ujenzi wa Majengo mengi zaidi.Aina hii huwa ni gharama nafuu kuliko aina nyingine.
Huwa una sehemu mbili ,sehemu ya chini kabisa ndiyo huwa kitako na Nene kuliko kuliko sehemu ya juu.
Na huu ndiyo tunauelenga.
 
6.Kwa maeneo yenye udongo wa mfinyanzi ni vizuri kitako cha msingi kikiwa cha zege lenye nondo ili kuzuia kukatika kwa msingi.
Maeneo ya Mbezi juu,Changanyikeni,Goba,Kinyerezi,Mbezi (Luis,makabe,msakuzi,msumi)Kimara,Msigati,Kibamba na Kiluvya

7.Kuna maeneo kitako cha strip kinatakiwa kiwe na upana wa angalau 0.45 m ili jengo lisizame,na msingi uwe na kina cha 0.6m
-maeneo yenye mchanga mwingi :Zingiziwa,Buyuni,Majohe,Chanika,Kisarawe II,Kibada,Pembamnazi,Kigogo.
-Maeneo yenye ardhi nyeusi isiyo kauka maji:Mikocheni A,Msasani Bonde la mpunga na Mikoroshini,Kunduchi mtongani,Mbezi Africana,Mwananyamala,Kigogo

8.Maeneo yenye mawe magumu/huwa hayana gharama katika msingi.
Haina haja ya kuchimba zaidi ya 0.10m :maeneo ya Masaki, Oysterbay,Makangira(Namanga),machimbo ya kokoto kunduchi mbuyuni na boko.

9.Matilio : unaweza kujenga msingi kwa kutumia Vyuma tupu,Zege,Mbao, Mawe ,Matofali ya kuchoma na matofali ya block.
Lakini hapa nchini Majengo mengi yamejengwa kwa misingi yenye kutumia blocks: Dar na mikoa ya pwani.
matofali ya kuchoma:Nyanda za juu
mawe: mikoa iliyopitiwa na bonde la ufa

10.Ubora wa jengo lolote ,huanza katika ujenzi wa msingi.
Tumia matilio zenye ubora na fundi/mjenzi mwenye uwezo.Jengo lako litadumu hata miaka 50.

Nakaribisha maoni na maswali
 

Attachments

  • images-24.jpeg
    images-24.jpeg
    52.7 KB · Views: 14
  • images-23.jpeg
    images-23.jpeg
    34.1 KB · Views: 16
  • images-22.jpeg
    images-22.jpeg
    43.6 KB · Views: 16
View attachment 2913076
Naweza kujenga msingi hapo na juu nikaweza rooms? Lengo ni kuepuka gharama za kuweka slab
Kidogo swali lako lina tungo tata...
1.Je,wauliza kama hiyo sehemu ambayo kwasasa ina parking unaweza kugeuza kuwa chumba....kwa ramani ambayo jengo lishajengwa.?
au
2.Je,wauliza unaweza geuza hiyo parking kuwa chumba .....kwa ramani ambayo ujenzi haujaanza.?
 
View attachment 2913076
Naweza kujenga msingi hapo na juu nikaweza rooms? Lengo ni kuepuka gharama za kuweka slab
Kama swali lako linalenga kipengele namba moja.
Hapo hakutokuwa na haja ya kuweka msingi, kwakuwa eneo hilo lazima itakuwa lina beams zinazotoka ukuta mmoja kwenda mwingine (zimezunguka eneo lote la parking),lakini pia kibaraza chake hapo kitakuwa na slab ngumu na imara ili iweze kuhimili uzito wa gari.
Kwahiyo hiyo slab ya parking hapo,ina uwezo wa kubeba uzito wa hizo kuta mpya za chumba.


Kama umelenga swali la pili.
kama ujenzi bado haujaanza, hapo ni kitendo cha kubadili matumizi ya eneo, na fundi wako kipindi cha uchimbaji msingi atachimba mpaka huko.

Ila unaweza fafanua swali lako vizuri ili liweze kujibiwa.
 
Kidogo swali lako lina tungo tata...
1.Je,wauliza kama hiyo sehemu ambayo kwasasa ina parking unaweza kugeuza kuwa chumba....kwa ramani ambayo jengo lishajengwa.?
au
2.Je,wauliza unaweza geuza hiyo parking kuwa chumba .....kwa ramani ambayo ujenzi haujaanza.?
3-38.jpg

Mkuu ujenzi haujaanza. Hitaji langu ni kuepuka gharama za slab na beams. Kwa hiyo, badala ya kuweka hizo nguzo, slab, niweke msingi wa moja kwa moja toka chini mpaka usawa wa slab. Maana yake hiyo parking haitakuwepo, badala yake ni kifusi tu.
Kitaalamu inawezekana?
 
Msingi wa room 3, sebule, jiko, dining unagharimu bei gani
Sasa hapo kuna ugumu wa kufanya makini.Vifuatavyo ni muhimu kwenye kufanya makisio ya gharama.
i) matilio uliyopanga kutumia katika ujenzi. Je ni matofali ya block,kuchoma,mawe au zege.Mana hapo kila moja ina gharama zake.
ii) eneo ulilopanga kujenga;ni wapi umepanga ufanye ujenzi.
Mfano:maeneo mengi ya Goba,Makabe,Luis na Kimara ni gharama sana katika ujenzi wa msingi kwakuwa hayapo tambarare na yana udongo mvunjifu wa mfinyanzi.
iii) Vipimo vya hivyo vyumba vyako ni vikoje.Kwa maana kuna mtu Chumba chake kimoja kina ukubwa sawa na vyumba viwili kwa mwingine.
Hapo ramani ndiyo itakuwa msaada kwenye kukotoa.
 
View attachment 2914205
Mkuu ujenzi haujaanza. Hitaji langu ni kuepuka gharama za slab na beams. Kwa hiyo, badala ya kuweka hizo nguzo, slab, niweke msingi wa moja kwa moja toka chini mpaka usawa wa slab. Maana yake hiyo parking haitakuwepo, badala yake ni kifusi tu.
Kitaalamu inawezekana?
Ndiyo unaweza ukafanya hivyo.
Ila,kuta zakuzunguka hiko kifusi itabidi;
i) Ziwe imara sana,ambapo itakupsa utumie matofali ya changarawe,na uyalaze kutoka usawa wa mikanda wa zege wa chini mpaka juu.Kufanya hivyo itasaidia kuta kuwa na nguvu ya kuhimili presha ya udongo.

ii) Uandae mfumo mzuri wa kuondoa dhahama ya dampness/unyevu ambapo yatakuwa yanapanda kwa ndani kutoka ardhini. Na mfumo huo utasaidia kupunguza presha pia.
 
Ndiyo unaweza ukafanya hivyo.
Ila,kuta zakuzunguka hiko kifusi itabidi;
i) Ziwe imara sana,ambapo itakupsa utumie matofali ya changarawe,na uyalaze kutoka usawa wa mikanda wa zege wa chini mpaka juu.Kufanya hivyo itasaidia kuta kuwa na nguvu ya kuhimili presha ya udongo.

ii) Uandae mfumo mzuri wa kuondoa dhahama ya dampness/unyevu ambapo yatakuwa yanapanda kwa ndani kutoka ardhini. Na mfumo huo utasaidia kupunguza presha pia.
Nimekupata sawia. Lakini kwa maoni nitafanikiwa kupunguza gharama? Au ni yaleyale tu
 
Chaguo la nguzo na slab...
1.Lina kupa nafasi ya chini ya nyongeza.
2.Hatua zake za ujenzi ni nyepesi...
3.Lina gharama kidogo.

Chaguo la kifusi mpaka juu.
1.Gharama nafuu kidogo.
2.Hatua zake za ujenzi ni nyingi
 
Mwezi wa 4 naingia likizo
Kwa mwenye kuhitaji kutembelewa katika eneo lake, kukagua na kutoa ushauri juu ya tatizo lolote, kuwa huru kunijuza.

Gharama : Huduma hii ni bure
Usafiri : ndiyo pekee utagharamia.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom