Victor Mlaki
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 3,542
- 3,451
Habarini wanajamvi!..
Tunafahamu kinachoendelea juu ya ujenzi wa madarasa kote nchini chini ya ufadhili wa IMF lakini kinachofanyika kimenisukuma kuandika haya.
Mosi, wakuu wa shule wamejikuta katika wakati mgumu sana kutokana na kuwepo kwa wimbi kubwa la wakaguzi na wafuatiliaji ambao kila mmoja amekuwa akitoa mapendekezo yake juu ya ujenzi licha ya kuwepo kwa muongozo katika Bill of Quantity (BOQ)
Pili, kumeibuka wimbi la watu wa kati wanaovuruga biashara ya vifaa vya ujenzi, jambo linalosababisha vifaa hivyo kuuzwa kwa bei kubwa kuliko kawaida yake.
Tatu, muda uliopangwa ili kukamilisha ujenzi wa madarasa hayo ni mfupi kiasi cha kutia mashaka juu ya ubora, mathalani hakuna muda wa kutosha ili kumwagilia maji majengo hayo licha ya kutumia saruji nyingi.
Nne, Bill of Quantity haijaonesha gharama zote mfano gharama za maji, umwagiliaji na usafiri.
Tano, licha ya ukweli kuwa kazi hii inahitaji usimamaizi wa karibu katika muda wote wa kazi, hakuna kiasi kilichotengwa kwa ajili ya chakula au maji ya wasimamizi.