Kwanini kila Januari lazima Waziri wa TAMISEMI awakaripie Wakuu wa Mikoa kukamilisha ujenzi wa shule? Lini ujenzi wa madarasa utakamilika?

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
876
4,101
Kila mwaka ikifika Januari lazima tangazo la kuwataka wakuu wa mikoa kukamilisha ujenzi wa miundombinu ya shule Litoke.

Tangazo hili uambatana na kuwatumbua wakuu wa mikoa au wilaya kuashiria waziri mwenye dhamana yupo serious. Lakini tujiulize, hayo madarasa yanakamilikaga kila Januari tu?

Kama kila Januari tunasema wakamilishe ujenzi, habari hizi zitaenda hadi lini? Mbona vyuoni hakuna hizi habari za kukamilisha ujenzi? Au wanafunzi wa primary na secondary wanaaribu sana mazingira?

Wakuu wa shule wanakuwa wapi hadi wakuu wa mikoa wapigwe nginja nginja waache kusherekea mwaka mpya?
 
Serikali huwa haitumii takwimu za sensa vizuri
Wanajua kbs mwaka flan kutakua na ongezeko la wanafunzi wa Sekondari na Primary ila ikifika huo muda ndo inaanza kutekeleza miradi ya Ujenzi wa vyumba vya madarasa tena kwa baddhi ya shule.
Wakati huo huo inaendelea kujenga shule Mpya ambazo hazikamiliki , wakati ilikua na uwezo wa kuongeza madarasa shule flan na kuifanya boarding na kupunguza matumizi ya ardhi na gharama za uendeshaji.
 
Kila mwaka ikifika Januari lazima tangazo la kuwataka wakuu wa mikoa kukamilisha ujenzi wa miundombinu ya shule Litoke.

Tangazo hili uambatana na kuwatumbua wakuu wa mikoa au wilaya kuashiria waziri mwenye dhamana yupo serious. Lakini tujiulize, hayo madarasa yanakamilikaga kila Januari tu?

Kama kila Januari tunasema wakamilishe ujenzi, habari hizi zitaenda hadi lini? Mbona vyuoni hakuna hizi habari za kukamilisha ujenzi? Au wanafunzi wa primary na secondary wanaaribu sana mazingira?

Wakuu wa shule wanakuwa wapi hadi wakuu wa mikoa wapigwe nginja nginja waache kusherekea mwaka mpya?
Vipi kuhusu vitendea Kazi/vifaa vya kufundishia
Vipi kuhusu walimu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili ni tatizo kubwa mno ndo maana Walimu wanaamua TU kwenda na mdundo ..Wengine wanajiingiza kwenye kuiba mitihani ya TAIFA Ili TU wasivuliwe madaraka wakati wanajua Hali ni Tete.
Nyumba za Walimu hakuna
Vifaa na zana za kujifunzia ni shida Kila mahali
Wizi mwingine Sasa ni kila Halmashauri au Wilaya kuwa na Shule ya Serikali ambayo inafundiaha kiingereza TU either ya primary au Sekondari, naona saa hizi wameanza na Primary huu ni utapeli na sio sera ya Serikali hapa pia wazazi WANAENDA kupigwa.

Si ajabu Leo Mtoto anamaliza Sekondari hajui vifaa vya maabara hata kama atavijua hajui kazi zake🤔.
 
Hauwezi kamilika kwa sababu kasi ya kuzaliana ipo juu, tuendelee kuongeza cheap labour jamani, changamka....
 
Kila mwaka ikifika Januari lazima tangazo la kuwataka wakuu wa mikoa kukamilisha ujenzi wa miundombinu ya shule Litoke.

Tangazo hili uambatana na kuwatumbua wakuu wa mikoa au wilaya kuashiria waziri mwenye dhamana yupo serious. Lakini tujiulize, hayo madarasa yanakamilikaga kila Januari tu?

Kama kila Januari tunasema wakamilishe ujenzi, habari hizi zitaenda hadi lini? Mbona vyuoni hakuna hizi habari za kukamilisha ujenzi? Au wanafunzi wa primary na secondary wanaaribu sana mazingira?

Wakuu wa shule wanakuwa wapi hadi wakuu wa mikoa wapigwe nginja nginja waache kusherekea mwaka mpya?
Wakuu wa shule kama hajatumiwa hela hapo katikati watajenga na nini?
 
Wazazi na wanakaripia mafundi kumalizia uniform!
Kipindi hiki watu wanakaripiana sana
Waziri wa TAMISEMI anawakaripia Ma-RC
Mzazi anamkaripia fundi amalize haraka uniform za watoto wake.
Wakuu wa Shule wanakaripia wazazi kuleta ada nusu nusu.
Mwanamke anamkaripia mme wake asiguse hela yake ya vikoba.
Mtendaji anamkaripia Mwenyekiti wa kitongoji ahakikishe watoto wa umri wa kwenda shule wanaandikishwa.
Wakuu wa Shule nao wanawakaribia walimu wa Taaluma kupokea pokea wanafunzi wa uhamisho

Ili mradi TU tuingie mwaka Mpya na stress
 
Huku chini watoto wanatakiwa wajiunge Shule zilizopo maeneo Yao na Kila siku uzalianaji unaongezeka.....Huko juu Advance na Vyuoni WANAFUNZI wanakuwa allocated/ wanachaguliwa wapi pa kwenda kulingana na nafasi zilizopo kwenye Shule au chuo husika.
 
Kila mwaka ikifika Januari lazima tangazo la kuwataka wakuu wa mikoa kukamilisha ujenzi wa miundombinu ya shule Litoke.

Tangazo hili uambatana na kuwatumbua wakuu wa mikoa au wilaya kuashiria waziri mwenye dhamana yupo serious. Lakini tujiulize, hayo madarasa yanakamilikaga kila Januari tu?

Kama kila Januari tunasema wakamilishe ujenzi, habari hizi zitaenda hadi lini? Mbona vyuoni hakuna hizi habari za kukamilisha ujenzi? Au wanafunzi wa primary na secondary wanaaribu sana mazingira?

Wakuu wa shule wanakuwa wapi hadi wakuu wa mikoa wapigwe nginja nginja waache kusherekea mwaka mpya?
Na walimu wanaongeza au wanajenga tu madarasa
 
Januari ukimpeleka mwanao kidato cha kwanza shule Serikali utaambiwa kununua kiti na meza.

Usipoambiwa hayo ujue umebahatika tu.

Hii maana yake Serikali inapwaya katika kuboresha miundombinu ya kujifunzia na kufundishia. Ila ni serikali hii hii inanunua ma viete ya milioni 500 kwa ajili ya kiongozi mmoja kutembelea wakati mwingine anatembelea nje ya majukumu ya serikali.

Waafrika tumeumbwa kama sehemu ya kichekesho duniani
 
Kipindi hiki watu wanakaripiana sana
Waziri wa TAMISEMI anawakaripia Ma-RC
Mzazi anamkaripia fundi amalize haraka uniform za watoto wake.
Wakuu wa Shule wanakaripia wazazi kuleta ada nusu nusu.
Mwanamke anamkaripia mme wake asiguse hela yake ya vikoba.
Mtendaji anamkaripia Mwenyekiti wa kitongoji ahakikishe watoto wa umri wa kwenda shule wanaandikishwa.
Wakuu wa Shule nao wanawakaribia walimu wa Taaluma kupokea pokea wanafunzi wa uhamisho

Ili mradi TU tuingie mwaka Mpya na stress
Maombi zaidi yanahitajika kote ni kukosa usimamizi thabiti na mipango endelevu!
 
Kila mwaka ikifika Januari lazima tangazo la kuwataka wakuu wa mikoa kukamilisha ujenzi wa miundombinu ya shule Litoke.

Tangazo hili uambatana na kuwatumbua wakuu wa mikoa au wilaya kuashiria waziri mwenye dhamana yupo serious. Lakini tujiulize, hayo madarasa yanakamilikaga kila Januari tu?

Kama kila Januari tunasema wakamilishe ujenzi, habari hizi zitaenda hadi lini? Mbona vyuoni hakuna hizi habari za kukamilisha ujenzi? Au wanafunzi wa primary na secondary wanaaribu sana mazingira?

Wakuu wa shule wanakuwa wapi hadi wakuu wa mikoa wapigwe nginja nginja waache kusherekea mwaka mpya?
"Socialism hangover" ni mbaya sana kwa watawala na watawaliwa katika nchi nyingi za Afrika, ikiwemo Tanzania. Hii ndiyo inasababisha katika familia maskini watu kuzaliana hovyo, kiholela sana tena bila mpangilio na pasipo kutaka kuwajibika.

Serikali nayo inawaendekeza na kuwadekeza kwa kutaka kuwapa vitu vya bure. Licha ya kutopea katika lindi la ufukara, bado watu wanaendekeza kuishi katika ndoa za mitala, mabinti kuzalishwa hovyo na kutelekeza watoto, matokeo yake ni ongezeko la watoto wengi bila hata ya kuendana mipango ya serikali katika kupanga kutoa huduma bora za kijamii.

Kila mtu anapaswa kutoa matunzo mazuri kwa watoto aliowazaa, hii inajumuisha chakula bora, elimu bora, huduma nzuri za afya kupitia bima za uhakika, malazi bora, mahitaji ya usalama wa mtoto awapo sehemu yotote ile, michezo na burudani, kumrithisha utamaduni wenye mlengo mzuri wa Kiafrika, kumuandaa kuwa na imani thabiti kwa Mola wake, na vitu vingine kama hivyo.

Vyote hivyo hapo juu ni gharama, na mwenye kupaswa kuubeba mzigo huo ni mzazi mwenyewe. Serikali inapaswa kupitia wizara yenye dhamana na ustawi wa jamii kuhakikisha kuwa sehemu kubwa ya uwajibikaji unafanywa na wazazi ama walezi.

Ongezeko la mahitaji ya madarasa kwa elimu ya msingi kila mwaka ni dhahiri kuwa kuna ongezeko kubwa sana la watoto kuzaliwa. Hili ni bomu la wakati, "Yes! It is a time bomb". Serikali ni lazima iwaelimishe watu ili kuepuka "social instabilities" katika siku zijazo. Ni muda sasa serikali kuacha kutoa elimu ya bure.
 
Back
Top Bottom