KUNA MAKOSA KIDOGO YA KIUANDISHI KWENYE SCRIPT NA MAJINA NADHANI TUTAVUMILIANA NIMEKOSA MUDA WA KU EDIT. BUT INASOMEKA VIZURI TU
SEHEMU YA 35
Ni ndani ya jumba moja la kifahari lililokuwa ndani ya ununio jijini dar es salaam , alionekana mwanamke mmoja mrembo sana akiwa ndani ya jumba hilo huku akiwa amevalia kijigauni kilichomuacha maungio yake kuwa nje kabisa na wala hakuwa akijali kabisa japo ya kwamba ndani hapo alikuwa amezungukwa na walinzi ( mabodigadi) waliokuwa wakimlinda , lakini yeye hakuwa akijali , muda huo mlimbwende huyu mwenye umbo lake matata sana linaloweza kumdatisha kila mwanaume aliekuwa akimwangalia , alikuwa ameshikilia glass iliokuwa na mvinyo huku akiangalia maji yaliokuwa kwenye swimming pool kama mtu aliekuwa akiyashangaa , huku akionekana alikuwa akiwaza jambo.
Wakati huo upande wa getini ilionekana gari aina ya Subaru ikiingia ndani hapo na kwenda moja kwa moja kupark .
“ janeth yuko wapi “ ni mwanaume mmoja mtanashati mwenye mwili wa kimazoezi ndie alietoka kwenye gari hio na kisha kumuulizia janeth .
“ yupo garden “ alijibiwa kisha moja kwa moja alitoka na kuelekea mpaka upande wa garden na kweli alimkuta mrembo huyo akiwa hana habari na uwepo wake alisimama kisha akatabasamu na kumsogelea .
“ boss” aliita mwanaume huyo na kumfanya mlimbwende huyo ageuze shingo yake kimadaha na kumwangalia mwanume huyo .
“Abasi karibu “ aliongea mlimbwende huyo akimuonesha abasi sehemu ya kukaa .
“ vipi kazi imefanikiwa ?”
“ imefanikiwa kwa asilimia mia na kama ulivyoagiza tumechukua kontena na kulipeleka chimbo ,vijana kwa sasa wanasubiria maagizo yako tu “.
“safi sana nadhani kimbona sasa anababaika huko “ aliongea mlimbwende huyo huku akikunja nne na kumfanya kijana abasi amwangalie kwa uchu wa kimatamanio .
“ tunafanyaje na hayo madawa “.
“ nataka niyachome moto , siwezi kuyaruhusu yaingie mtaani ilihali yanaharibu vijana wa taifa hili , nina mipango mikubwa na Tanzania , hivyo nataka uyachome moto “.
“ sawa bosi ngoja niwape vijana maagizo “.
“ hapana nitaenda mwenyewe kushuhudia yakiteketea kwa moto “ aliongea mlimbwende huyo na kisha alinyanyuka na kuingia ndani ya jumba hilo la kifahari huku akimuacha kijana abasi akiwa anamwangalia kwa uchu kwa nyuma jinsi makalio ya mwanadada huyo yalivyokuwa yakienda kushoto kulia .
Alikuwa ni mwanadada wa miaka kati ya ishirini na saba kwenda therathini , mrefu saizi ya kati mweye rangi nyeupe na uso wake ulioumbwa vizuri , alikuwa amejaaliwa moja ya shepu moja nzuri sana , shepu ambayo kwa mwanaume rijali angemuona angemmezea mate huyu ndio mlimbwende janeth .
Dakika kumi mbele mlimbwende huyo alitoka huku akiwa amevalia suti ya zambarau na kiatu cheusi cha high heels na kisha alilisogelea gari aina ya mercedez benz wagon , gari moja ya kifahari na kisha abasi na yeye alifatia kwenye gari hio na gari ikatolewa ndani ya jengo hilo .
Masaa kadhaa mbele walikuwa wakipita bagamoyo , na walikuwa wakielekea njia ya kwenda msata baada ya kufika eneo moja lililokuwa likifahamika kwa jina la kidomole relini walikunja kushoto na kuingia kwenye barabara ya vumbi iliokuwa ikielekea kanisa la katoliki na baada ya kufika hapo walikunja kulia na kwa mbele kulionekana karakana moja imejengwa , waliendesha mpaka eneo hilo na kisha walipaki gari , na kuingia ndani na hapo ndipo walipokutana na kontena likiwa ndani ya gari bado.
“ litoeni hapa tunaenda fukayose ‘ aliongea janeth na kisha gari lile lililobeba kontena lilitolewa na kwenda mpaka fukayose , baada ya kufika eneo hilo nyuma kidogo gari ile ilikunja kushoto na kuingia kwenye moja ya shamba kubwa .
“ hili shamba la nani ?” aliuliza abasi .
“ la kimbona “ aliongea mwanadada yule huku akionekana kwenye sura ya kazi , baada ya kufika ndani ya shamba hilo walifanya utaratibu wa kushusha lile kontena na walifanikiwa kisha janeth aliwaamrisha vijana walifungue , na kweli lilifunguliwa na madawa ya kulevya yaliokuwa kwenye mfumo wa unga unga yalitolewa na kisha kubwaga chini na kumwagiwa mafuta ya petroli na janeth alitoa kiberiti cha gesi na kisha alitupia kwenye madawa hayo yalioanza kuteketea .
“ nyie mnaweza kuondoka “ aliamrisha vijana wake na wakapanda kwenye gari na kuondoka , huku janeth akiangalia mpaka alipohakikisha kila kitu kimebaki majivu alipanda kwenye gari akiwa na abasi na kisha walisepa .
*****
Kimbona mara baada ya lutoka moja kwa moja alienda mpaka chimbo ambako vijana wake ndio walipokuwepo , alisimamisha gari yake na muda huo kigiza kilikuwa kishaanza kuingia , alisogea kwenye karakana hio na kuingia ndani na kukutana na vijana wake waliokuwa wakimsubiri .
” derick ni nini kimetokea ?”
“ boss tumefika bandarini na kuonesha nyaraka ya kuhitaji mzigo na tukapewa , lakini baada ya kufika hapa na kuufungua tumekutana na chumvi “ aliongea derick na kumfanya kimbona asogelee lle kontena na kuhakiki na kweli iilikuwa ni chumvi kutoka kenya .
“ *** ! kuna mchezo hapa tumefanyiwa ila nitajua .aliongea kimbona na wakati huo simu yake ilitoa mlio na aliitoa na kuangalia kwani ulikua ni ujumbe wa meseji “.
“ MZIGO WAKO UMEFIKA SALAMA , UPO SHAMBANI KWAKO FUKAYOSE , BY MZALENDO “ ilikuwa ni meseji ambayo ilimshangaza lakini hakutaka kupoteza muda alitaka kujaribu kupiga ile namba ila ilikuwa ni private namba .
“ derick chukua vijana twende fukayose “ aliongea kimbona na derick alichukua vijana na safari ya kwenda fukayose ikaanza , na hapakuwa mbali sana kwani sehemu walikuwepo kwene chimbo lao ilikuwa ni bunju .
Nusu saa tu walikuwa wameshafika na jambo la kwanza kimbona kuona ni moshi mzito , walisogea mpaka eneo hilo na hapo ndipo walipopigwa butwaa kwani kontena walilikuta likiwa tupu lakini pia walijua kuwa mzigo wote uliteketezwa kwa moto , kimbona alijikuta akikaa chini kwani hakuamini kama tani nzima ya madawa ya kulevya iliokuwa ikiingia nchini ndio hio imeteketezwa yote , ilikuwa ni hasara kubwa kwake kupata , kwani ni mzigo ambalo ulikuwa umemgharimu pesa nyingi mno .
Wakati akiwa kwenye majuto simu yake ilitoa mlio kuwa kuna mtu aliekuwa akipiga , aliichukua na kuona ni sam aliekuwa akipiga simu
“vipi umefanikiwa ?”
“ hapana ni majanga mzigo wote umeteketezwa “”
“unamaanisha mzigo wote “
“ ndio na mtu aliefanya hivyo naonekana kutujua kwani ndio kanitumia ujjumbe kuwa mzigo upo huku shambani na ndipo nilipoukuta umeunguzwa wote “.
“ kimbona hio ni hatari kubwa sana na hasara kwa ujumla , nimehangaika mwezi mzima kuusubiria huo mzigo ufike nchini , inaonekana hakuwa makini na vijana wako “.
‘ nilikuwa makini sana sam , huu sio mzigo wa kwanza kupokea”
“ unafikiri nani katufanyia hivyo “
“ kuna ujumbe ambao kaniachia ngoja ni kufowadie “
“ sawa “.
“ derick huyu mtu inabidi akamatwe haraka wasiliana na carlos tumpe kazi ya kumfatilia “ aliongea kimbona na derick aliwasiliana na carlos Cardoso na kumpa maelekezo .
*****
Suzzane alikuwa ni mwenye hasira sana juu ya mtu aliekuwa anajiita mzalendo , aliapia kumuonyesha siku akimtia kwenye mikono yake , upelelezi wake ulikuwa ukifanyika kwa kina kweli , hakutaka kukurupuka kwani aliamini kuwa mtu ambae alikuwa akideal nae alikuwa ni mtu mwenye akili na hivyo hata yeye alipaswa kutumia akili vile vile , alijiapiza kumkamata mtu anaejiita mzaelndo , hakujua mtu huyu ni nani japo kuna muda hisia zake zilimwambia kuwa mtu huyo alikuwa ni damiani lakini hakutaka kuamini kabisa , wakati kontena la madawa ya kulevya linashushwa bandarini alikuwepo na hata vijana wa kimbona walivyochezewa mchezo wa kubadilishiwa kontena pia aliliona jambo hilo , ila kwakuwa halikuwa likimuhusu aliona sio kazi yake , Zaidi ya yote yeye alitaka kujua ni mtu gani yupo nyuma ya vijana waliofanya mchezo wa kubadilisha kontena , kwanza mwanzoni zilikuwa ni hisia zake tu ambazo zilimpeleka bandarini mara baada ya kupata taarifa hio ya kushushwa kwa mzigo wa madawa kutoka kwa mtu wake aliekuwa ndani ya TISS kuna hisia zilimwambia lazima kuna jambo lingetokea na ndio maana aliingia ndani ya eneo hilo tokea muda wa saa kumi akiangalia kila mtu aliekuwa akiiaangia bandarini hapo na kutoka na alijikuta akitabasamu mara baada ya kubaini mchezo uliokuwa ukifanyika bandarini mpaka vijana wa kimbona ambao alikuwa akiwajua vyema kubadilishiwa kontena , na hata kontena hilo la madawa lilivyotolewa hapo bandarini , hakuwa nyuma na gari yake aina ya brevis nyeupe , alifatilia mpaka linafika kidomole na kuingizwa kwenye karakana hakutaka kuwa na papara kwani alirudi barabarani na kisha alipaki gari lake kwenye duka moja la jumla na kununua soda na kukaa huku akinywa akiangalia upande wa barabara ambao gari lile lililokuwa na kontena lililoambatana na vijana wale ambao hakuwajua , alikuwa ameweka umakinni wa hali ya juu , alikaa hapo Zaidi ya lisaa na ndipo alipo ona gari moja la kifahari likipita na kukunja upande ule ule , alijikuta akichanua kwa tabasamu pana mara baada ya kuona gari hio kwani aliamini kabisa aliekuwa ndani ya gari hio alikuwa ni mtu anaemtaka , alitulia kama nusu saa na akanyanyuka na kisha alilisogelea gari lake na kuingia ndani na kuliwasha , lakini ile anakanyaga mafuta alishuhudia ile benz ikitoka na safari hii ikikunja kuelekea kiwangwa msata , alijikuta akisubiria kama dakika moja , na gari iliokuwa imebeba kontena ile aliona na yenyewe ikifuatia , aliacha imuache mbali mita kadhaa na ndipo alipowasha gari yake na kufatilia kwa nyuma mpaka gari ile ilipokunja kwenye shamba yeye alipitisha gari na kwenda kupaki mbele na kisha alirudi kwa miguu na hapo ndipo aliposhuhudia madawa yale yakiteketezwa , jambo hilo kidogo lilimshangaza , kwani aliamiani mtu ambae alifanya mchezo hu huenda alikuwa akiwazunguka wenzake na kutaka kuyauza madawa hayo lakini alichoshangazwa ni kuteketezwa kwa madawa yale .
“ hawa watu ni wakina nani ?” lilikuwa ni swali ambalo lilizunguka ndani ya kichwa chake huku akimwangalia mwanamke ambae alionekana kuwa ndio kiongozi wa kuchoma madawa hayo mpaka pale walipomaliza na kuondoka , na yeye haraka haraka alikimbilia gari lake na kuingia kwenye gari na kulifatilia lile benz.
“Nataka tuingie mapinga kwanza kwenye nyumba yangu ‘aliongea janeth .
“ kuna mishe gani ?”
“ kuna mtu nataka kuoanana nae “
“ poa “ .
Gari waliopanda janeth na abasi mara baada ya kufika mapinga ilikunja kushoto na kuchukua barabara ya zamani na kuja kupita kituo cha polisi mwisho zahanati ya mapinga na ikaja kutokea kwa mbele kabisa kwenye shule ya msingi mapinga , ilienda mbele kidogo na kusimama nje ya nyumba iliokuwa na ukuta , na abasi alishuka na kisha alifungua geti na gari ile ikaingia ndani.
Suzzane yeye hakutaka kabisa kuwapoteza watu hao , alidhamiria kabisa kuwajua na mpango wake ilikuwa ni kuwavamia usiku na ndio maana mara baada kuona gari ile imeingia ndani ya geti lile , alirudi na kwenda kupark kwenye moja ya duka la madawa huku akiangalia nyumba ile , muda huo giza lilikuwa limeingia kwani ilikwa ni kama muda wa saa moja hivi , wakati akiwa amesimama simu yake ilitoa mlio kuwa inaita , aliitoa mfukoni na na kuangalia mpigaji na aliona alikuwa ni mheshimiwa raisi .
“ hellow mheshimiwa “
“ ndio suzzane , uko wapi ?”
“ nipo bagamaoyo , kuna nini mheshimiwa ?”
“ kuna mzigo wetu umeibiwa bandarini na mtu anaejiita mzalendo , na mpaka sasa tumefatilia na tumegundua umechomwa moto ‘ aliongea mheshimiwa na kumfanya suzzane abenue midomo kwa dharau .
“ kwahio unataka nifanye nini muheshimiwa “
“ nataka uwakamate hao watu inawezekana akawa damiani “
“ sawa muheshimiwa “ aliongea suzzane na kukata simu na kisha hakutaka kuchelewa , kwani hisia zake zilimwambia kabisa kuwa watu walioingia kwenye nyumba ile mmoja wapo ni yule anae muwinda kwa udi na uvumba .
Alilisogelea geti kama mtu anaepita , huku akiangalia kama kuna kamera lakini hakuona hata moja na hapo aliona jambo lake lingeweza kuwa rahisi , alizunguka upande wa nyuma na kuangalia urefu wa ukuta huo na kisha aliangalia kushoto na kulia na kama paka aliparamia ukuta hu na kwenda kutua ndani ya nyumba hio nyuma kabisa ya tank la maji .
Alishika kiuno kuangalia bastora yake na kuitoa kisha akaangalia risasi zilizokuwemo na baada ya kuona anazo zakutosha alitembea kwa kuinama na kwenda kujibanza kwenye kona ya ukuta karibu na mlango , aliangalia usalama na kisha alitembea kwa kasi ya ajabu na kwenda kutua kwenye kibaraza karibu kabisa na mlango wa kuingilia , aliusogelea mlango i kama mtu aliekuwa akisikilizia sauti kutoka ndani lakini hakuna sauti iliosikika japo taa zilikuwa zikiwaka , akili yake ilikuwa ikifanya kazi kwa kasi mno , hakutaka kuingia kizembe zembe , alitaka ajihakikishie kuwa yupo salama .
Alishika kitasa cha mlango na kukinyonga kwa utaaramu wa hali ya juu pasipo kelele na akafungua mlango kidogo na alitumia mwanya huo kuangalia eneo la ndani , aligudnua kuwa ene hilo lilikuwa na sable lakini ambayo haikuwa na mtu .
Aliamua kuingia ndani kabisa kwa tahadhari kubwa mpaka kwenye sable kubwa pana iliojaa masofa huku TV ikiwa inawaka .
“ karibu , nilikuwa nakusubiri “ ilikuwa ni sauti nyororo ilimshitua suzzane kwa nyuma na kugeuka kwa kasi lakini ile anageuka bastora ilipigwa teke na kwenda kudondokea mbali. .
ITAENDELEA
SEHEMU YA 36
Suzzane baada ya kuona bastora yake imeenda mbali , hakutaka kuzembea , japo mbele yake alionekana mwanamke mrembo lakini jinsi bastora yake ilivyopigwa teke alijua kuwa mtu anaepambana nae sio mtu wa kawaida kabisa .
“wewe ndio mzalendo wa nchi hii “ aliongea suzzane kwa dharau akimwangalia janeth uson
“ wewe unanionaje , unafikiri mimi ni kama wewe unaowasaidia waharifu , mpaka kumuua mpenzi wako danieli ‘ aliongea janeth na kumfanya suzzane apandwe na hasira na kumfata janeth huku akidhamiria kumpiga pigo , lakini na janeth ni kama na yeye alikuwa akimsubiria kwani ile suzzane anarusha ngumi janeth aliikwepa , kushoto , lakini suzzane alikuwa mwepesi kweli kwani ile anahepa kushoto tayari alikuwa amechia teke la mbavu lililompata kisawasawa janeth na kuugumia maumivu , huku suzzane akimfata kwa kasi yake , lakini hilo lilikuwa kosa kwa suzzane kwani ni kama janeth alikuwa akimtegea kwani ile anafika alipigwa bonge la mtama na kwenda chini na hapo hapo janetha akaachia front kick , lakini suzzane aliona hilo kwani alibiringita kushoto na kwenda kutua kwenye friji huku akijinyanyua , ulikuwa ni mtanange , janeth alijnekana mtaalamu na pia suzzane alikuwa ni komandoo mbobezi , zilianza kupigwa ngumi hapo huku kila mtu akijaribu kuwekpa na kupangua za mwenzake , kiufupi japo janeth alikuwa yuko vizuri lakini kwa suzzane alikuwa mtoto tu , kwani kadri muda unavyoenda ndio alipokua anachoka na alianza kuchezea mapigo na moja kubwa lilimpeleka chini ni teke la roundhouse lililimpiga tumboni na kwenda kutua kwenye sofa , suzzane alikuwa na hasira kama mbogo kwani alimfata huku akidhamiria kumzimisha , lakini alijikuta akutulizwa na sauti nyuma ikumuarisha asimame hivyo hivyo kabla hajachanguliwa ubongo , lakini abasi alikuwa amechelewa kwani suzzane kama chui alikuwa asharukia mlango na kuchomoka nje kabisa na hakutaka kubaki ndani hapo kwani aliona si salama kwake , aliruka ukuta na kutoa nje kabisa kisha alienda mpaka barabarani na kupanda gari yake huku akijifuta jasho , alionekana alikuwa akisikiliza baadhi ya maumivu .
“ pumbavu nitawakamata tu , walikuwa wakinisubiria , kama nisingekuwa mweepesi wangenikamata “ aliongea suzzane huku akijikuta akitoa machozi mara baada ya kukumbuka kauli ya mwanadada jaenth iliokuwa ikumuhusu Daniel
Jinsi alivyokuwa abaendesha gari alikuwa ni kama mwehu maana alikuwa kwenye spidi kali mno , madakika kadhaa tu alikuwa ndani ya jogoo na kukunja kushoto na kupeleka gari mpaka nje ya nyumba kubwa iliokuwa na geti kisha alifungua kwa rimoti na kuingiza gari ndani .
“angeniua mshenzi yule “ aliongea janeth huku akionekana kuwa kwenye maumivu makali
‘”suzzane ni komandoo yule anambinu nyingi za kivita si rahisi kushindana nae kwenye ulingo ukashinda “
“ ni kweli lakini lazima tumpate lasivyo kazi zetu zitakuwa ngumu sana “.
*******
KIA ( KILIMANJARO INTERNATIONA AIRPORT )
Ilikuwa ni ndani ya uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro ilionekana ndege ya shirika la KLM ikisimama eneo lake kwa ajili ya kushusha abiria mara baada tu ya kutua ndani a uwanja huo wa ndege , dakika kadhaa mbele alionekana mwanaume mmoja wa kizungu mwenye mwili wa mazoezi alievalia tisheti ilimbana vyema na kufanya mwili wake kujichora , mwanaume huyu alikuwa amevalia miwani .
“naweza pata ndege ya kunipeleka dar asubuhi hii “ aliuliza mwanaume huyu .
“ ndio ipo inayotoka saa nne ya shirika la ATCL”
“ nipe ticket ya daraja la kwanza “ aliongea bwana huyu na kisha mwanadada aliekuwa hapo uwanjani alifanya kama alivyoambiwa na kumpatia ticket mara baada ya malipo kufanyika kwa njia ya kadi .”
Saa tano na nusu bwana huyu alionekana akitoka ndani ya uwanja wa kimataifa wa mwalimu nyerere mara baada tu ya kutoka alionana na mwanamama aliekuwa anamjua vyema na kumsoggelea .
“ Rebecca ‘
“ za siku nyingi ?” mwanaume huyu japo ya kuwa na rangi ya kizungu lakini alionekana kukijua vizuri Kiswahili .
“ nzuri kabisa bwana stephano lamberk “ aliongea Rebecca na kumfanya bwana stephano lamberk kutabasamu huku wakilisogelea gari aina ya ford na bwana stephano aliingiza begi lake ndani na kisha alifungua mlango wa mbele na gari liliondoshwa .
Ni mwendo kama wa lisaa hivi gari ile ilikuwa ikipita maeneo ya kawe na kuja kutokezea lugalo na kuingia taki bovu na iliendeshwa na kukunja kushoto barabara ya kwenda makongo juu na kwenda kusimama kwenye moja ya jumba la kifahari kabisa ndani ya eneo hilo lililokuwa limezungukwa na ukuta mrefu .
Baada ya kuingia ndani ya jumba hili gari ilikweda kupark na stephano alitoka kwenye gari na hap ndipo alijikuta akichanua tabasamu na hio ni mara baada ya kuonana na mtu aliesimama mbele yake .
“luang shu “ aliongea Stephan na kumfanya luang shu atabasamu na kisha walikumbatia .
“ ni muda wa miezi sasa tokea uniache china “
“ ni kweli karibu tena Tanzania “ aliongea
“ asante sana nimefika kwa mara nyingine baada ya miaka miwili sasa tokea niondoke “ aliongea bwana stephano huku akitabasamu na waliongozana mpaka ndani huku wakifatiwa na Rebecca nyuma .
“china umeionaje ?”
“ nchi yenu ni endelevu sana katika mambo mengi huamini nimeingia nchini bila mtu kunijua kabisa hahaha “
“yeah kwa staili hio hakuna mtu wa kukufahamu kabisa “ aliongea stephano huku akichukua begi lake na kuelekea chumbani akiwa ameongozana na luangshu huku Rebecca akibaki sebleni , baada ya kufika ndani , walitoa nguo zote kwenye lile begi na kuzibwaga kitandani na kisha stephano alitoa kijidude kama chaja na ukichomeka ukutani kwenye soketi ya umeme na baada ya hapo alifungua lile begi na kuingiza miguu ndani na kusimama , kilikuwa ni kitendo cha sekunde kadhaa tu kulitokea kama moto uliokuwa unatokea kwenye lile begi na ni kama ulikuwa ukimuunguza bwana Stephano na hapo hapo ngozi yake ikabadililka na kuwa ya kiafrika kabisa na wala sio ya kizungu tena
‘ karibu damiani Tanzania kwa mara nyingine “ aliongea luangshu na kumfanya damiani atabasamu na kisha alivaa nguo na kutoka mpaka sebleni na hapo ndipo rebeka alishangaa.
“ rebbecca ogopa sana Mungu na teknolojia hahaha “ aliongea damiani na umfanya Rebecca kushangaa tu kwani mtu alieingia hapo akiwa na ngozi ya kizungu sasa anatoka akiwa na ngozi ya kiafrika .
“ kweli kabisa inapaswa tuogope mungu na teknolojia “ .
*****
Ni siku ambayo damiani anaingia nchini katika geti la ikulu kulionekana magari mawili ya aina ya range yakitoka na kuingia barabarani na kuchukua barabara salenda , na nusu saa mbele gari zile mbili zilionekana zikipita mwenge hatimae zilipita mbezi beach , tegeta na kuingia barabara iliokuwa ikielekea ununio dyanstry beach . dakika kadhaa gari zile zilikuwja kusimama kwenye jumba la kifahari la mrembo janeth , geti lilifunguliwa na gari ziliingizwa ndani kabisa na mwanadada aliekuwa mkakamavu alitoka na kumfungulia mke wa raisi , huku na gari ya nyuma wakitoka wadada wawili waliokuwa wamevalia suti na walikuwa mhali hapo kwa ajili yakuimarisha ulinzi .
Mara baada ya mke wa raisi kutoka kwenye magari hayo moja kwa moja aliingia ndani ya jumba hilo , mpaka sebleni na hapo ndipo alipomuana janeth na janeth mara baada ya kumuaona mke wa riais alimkimbilia n kwenda kumhug.
“mom nimekumis sana “ aliongea janeth akijidekeza kwa wema .
“ ni mekumis pia mwanangu “
“ lakini mama haya maisha mpaka lini ya kujificha ficha “
“sikia janeth najua unateseka sana , lakini vumilia mambo yakiwa sawa utanichoka mwenyewe “
“ mhmh mom kila siku unaniambia mambo yakiwa sawa , nimekuwa mtu wa kufichwa tokea nimezaliwa mpaka sasa “
“ ni kwa usalama wako mwanangu sina jinsi “.
“sawa mama lakini nakumiss sana “
“ nakumiss pia mwanangu mmefikia wapi ?”
“ jana tulifanikiwa kukamata kontena ya madawa ya kulevya na tumeyachoma yote “
“ safi sana , nataka kila madawa yanayoingia hapa nchini yachomwe , sipo tayari kuona taifa ambalo raisi bendera alilipigania kwa nguvu zake zote likiharibiwa tena “
“ nitapambana mama “
“ haya niambie kuna lingine limetokea ?”
“ ndio mama jana suzzane nilipambana nae “
“nini , ilikuwaje ukapambana na suzzane “
“ nadhani jana alikuwa akitufatilia kwa muda mrefu kwani gari yake niliiona kidomole na hata wakati wakurudi pia niliona nikajua tu kuna mtu anatufatilia japo sikujua ni nani na ndipo nilipomuambia abasi tuingie mapinga kumsubiri , na kweli saa moja kama na nusu aliingia ndani hapo kwa lengo la kutukamata , ndipo tulipo pambana nae mpaka akakimbia “
“ kuwa makini sana na suzzane , anaroho mbaya sana yule mwanamke , hashindwi kukuoa duniani , kama ameweza kumuua danny sembuse wewe na isitoshe ni mtiifu sana kwa mheshimiwa raisi “
“ ni kweli sema nimegundua jambo hilo linamuuma sana “
“ hahaha hana lolote huyo namjua sana tu kwa usaliti wake “ aliongea mke wa raisi huku akionesha kufurahishwa sana na uwepo wa mahali hapo kwani meno yote nje
“ mimi naondoka janeth kabla mheshimiwa hajaanza kuchezwa na machale , maana namjua sana mambo yake “ aliongea mke wa raisi .
“ sawa mama nitakuwa nawasiliana na wewe kwa kupita sabi “.
“ sawa hakuna shaka, shika hiki kiboksi kitunze sana , ndio kilichonifanya leo nije hapa , usikifungue mpaka pale nitakapokuambia na kukupa ufunguo wake “
‘ kina nini mama? “
“ wewe kitunze utajua baadae kina nini “ aliongea mke wa raisi na kisha aliagana na mtoto wake
Dakika chache mbele gari za mke wa raisi zilitoka ndani ya jumba hilo na kuingia barabarani , lakini wakati huo huo gari ya brevis nyeupe ya suzzane ilionekana ikiwa nyuma ya gari hizo .
“ hizi gari mbona ni za ikulu zinafanya nini hapa “ ni swali alililojiuliza suzzane na aliona majibu yake ni kumpigia raisi simu
ITAENDELEA
SEHEMU YA 37
Wazo namba moja ambalo alikuwa nalo agent z ni kumjua kwa undani bruno lamberk ,aliamini kwa kumjua bwana huyo angeweza kufahamu baadhi ya mambo ambayo yangemsaidia kujua baadhi ya mambo katika misheni yake , alikuwa akimjua kimbona na mheshimiwa raisi kama watu waliokuwa wakimtafuta kijana damiani lakini alikuwa akiamini kabisa kwamba kuna mengi ya kuyajua yaliokuwa yakihusiana kati ya damiani na bruno , ambayo kidogo yangemletea mwanga wa kazi yake , kazi hii ilionekana ngumu kwake kutokana na mpangilio wake , maana alijua kama damiani angekuwa nchini thailland kama uchunguzi wake wa mara ya kwanza, basi kazi ingekuwa ngumu kidogo kupata ukweli , lakini kwakuwa wakuu wake wa kazi walikuwa wamempatia kazi ya kufahamu tu kama kijana huyo bado yuko huru au yupo kwenye mikono ya mheshimiwa , aliona pia kuna urahisi wa kazi hio .
Siku hio alikuwa ndani ya jumba lake la kifahari lililokuwepo ndani ya eneo la kigamboni , alikuwa amekaa chini akijaribu kufatilia habari zinazomuhusu bwana bruno lamberk , aliangalia kwanzia mali zake mpaka makampuni yake , na hapo alijikuta akipata wazo la kufanya siku ya kesho , kwani muda huo ilikuwa tayari ni jioni kabisa .
“ kesho inanibidi kwenda kwenye moja ya kampuni zake , naamini kuna kitu naweza kukipata pale “ aliongeaa huku akigagua baadhi ya makaratasi yake , mpaka pale alipokuja kushituliwa na honi ya gari getini , alifata kamera na kuangalia ni nani aliekuwa akipiga honi na alitabasamu mara baada ya kuona ni mpenzi wake mellisa .
Siku iliofata bwana zakayo hakutaka kabisa kuchelewesha kazi kwani huo ndio uliokuwa moto wake wa kazi , aliamini kumaliza kazi haraka ndio kupata kazi nyingine na kutengeneza pesa Zaidi , siku hio asubuhi alikuwa amevalia kinadhifu sana kama kawaida yake , huku akiwa kwenye gari yake aina ya roll Royce , muda huo alikuwa akikatiza mtaa wa magomeni akiiendea morocco na moja ya nia yake kubwa ilikuwa ni kwenda mpaka mikocheni , dakika chache mbele alikuwa mbele kidogo ya jengo la airtel alikunja kushoto kwa mbele na kuingia kwenye jengo ambalo ndani yake kulikuwa na makao makuu ya kampuni ya bruno enterprises .
Baada ya kuegesha gari yake alitoka na moja kwa moja alieelekea mpaka ndani ya jengo hilo , aliangalia kwenye screen kujua flour ambayo kampuni ya bruno ilipokuuwa ikifanya kazi, aliipata ilikuwa ni ghorofa ya 10 , aliingia kwenye lift na moja kwa moja alienda mpaka ndani ya flour hio na hapo ndipo alipopigwa na mshangao kwani alikuta wafanya kazi wakifanya usafi na hali iliiokuwepo humo ndani iliashiria kabisa kampuni imefungwa , alimsogelea mdada mmoja aliekuwa akikusanya baadhi ya maboksi na kumsalimia .
“samahani naulizia nini kinaendelea hapa , maana nilikuja kwajili ya kuonana na meneja wa kampuni ya bruno “.
“ pole kaka kumbe huna taarifa , kampuni ya bruno saivi imefungwa rasmi , na kubashilishwa jina , kwa sasa inajulikana kwa INNOVA “
“ INNOVA ?””
“ ndio kaka , kwa taarifa ni kwamba kampuni imeuzwa kwa kampuni ya INNOVA ya Italy na sasa wamehamia jengo la PSPF posta “ aliongea mwanadada huyo huku akiendelea na kazi .
Zakayo alitoka ndani ya jengo hilo huku akiwa na mawazo ya hapa na pale , alikuwa akiwaza ni nani alieuza kampuni hii ilihali mhusika mkuu alikuwa hana ndugu hapa nchini , hio ilikuwa ni kazi nyingine kwake ambayo aliona anapaswa kuitafutia jibu asubuhi hio .
Jambo hilo aliona ni ngumu kulipatia majibu na hapo ndipo jina la rafiki yake irene aliekuwa ni moja ya wana usalama ndani ya kitengo cha TISS liliibuka kwenye kichwa chake , alitoa simu yake wakati huo akiwa ndani ya gari yake na kuanza kupiga , na sekunde chache tu simu hio ilipokelewa .
“ nambie mwana mitindo”
“ safi za masiku Irene ?“
“ poa umenisusa kweli zakayo “
“ sio kweli mambo ni mengi tu “
“ mhmh haya , niambie lakini “
“ fresh , kuna jambo nataka unisaidie Irene “
“ jambo gani hilo ?”
“ kuna taarifa naihitaji , naamini lazima mtakuwa nayo kitengoni hapo “
“taarifa gani “
“ bruno interprises nafikiri hii taarifa mnayo juu ya hii kampuni kuuzwa “
“hahaha zakayo sisi tunahusikaje na maswala ya mauzo ya kampuni “
“ come on Irene , kuna mambo ya kiusalama yanaendelea ndani ya ile kampuni , na naamini lazima kuna mambo mnayajua , mimi nataka unisaidie kujua ni nani alierithi mali za bruno “.
“mhmh , inaonekana upo kazini kama kawaida yako “
“ yeah kuna kazi naifanya na ndio maana nahitaji hio taarifa “
“ sawa ngoja niangalie kama kweli kutakuwa na taarifa nitakupatia “
“ hayo ndio maneno “
“ ukifanikisha hilo uje mjengoni ni kupe gauni la bure “
‘ hahaha … haya bwana na nitakuja kweli “.
Zakayo baada ya kuona ashapata sehemu ya kupatia taarifa yake , hakuona haja ya kuzunguka jiji hilo kwa siku hio na moja kwa moja alienda mpaka kwenye kampuni yake mtaa wa mlimani city ili kumsubiria Irene afanye kazi yake .
“kuna mtu lazima hapa nchini alimsaidia damiani kufika nchini thailland , nikimpta huyu nitajua wapi alipo damiani na kama yupo hai au hayupo hai “ aliongea zakayo huku akiingia kwenye lift akiingia ndani ya jengo lake la biashara la PSSSF commercial tower .
Baada ya kufika ndani hakukaa sana , aliingia secretary wake akimtaarifu kuna mgeni anashida naye , kwani alikuwa akihitaji vazi .
“sasha mruhusu aingie , si unajua utaratibu “
“ ndio lakini kagoma anasema uende upande wa maduka anataka ukamchagulie nguo “ aliongea sasha na kumfanya zakayo ainuke kwenye kiti chake na kutoka ofisini ili kwenda kuonana na mteja jeuri , alisogea mpaka kwenye maduka yake maduka yake ya nguo na hapo ndipo alipojikuta jicho likimtoka .
“ janeth !” aliongea zakayo kwa mshangao akimwangalia mlimbwende aliekuwa mbele yake ,
“ zakayoo “ aliongea janeth na kisha walikumbatiana kwa furaha .
“ nimekumis sana bro “. Aliongea janeth kwa mapozi na kumfanya zakayo atabasamu kwani alikuwa akimjua vyema huyo mwanamke aliekuwa mbele yake .
“ umerudi lini ?”
“ nina miezi sasa tokea nirudi “
“ ndio ukashindwa hata kuniambia kama umerudi “.
“ mambo mengi , ila jana baada ya kujua jina la kampuni yako nikaona ni vyema leo nije hapa unichagulie nguo “.
Aliongea janeth kimapozi , maana janeth na yeye alikuwa mzuri mno , na ni kwa kipindi kirefu sana zakayo alikuwa akimpenda huyo mwanamke tokea siku ya kwanza kukutana nae nchini indonesia katika mashindano ya mitindo , na siku alipokuja kugundua kuwa mwanamke huyo alikuwa ni mtanzania ndio alipojenga nae urafiki , lakini bahati mbaya kwake ni kwamba mrembo huyo hakuwa mwepesi kabisa , kwani hata baada ya kurusha ndoano , aliishia kuambiwa kuwa wawe marafiki na huku janeth akipigilia msumari kwa kumuita zakayo kaka jambo ambalo kwa zakayo aliona kama tusi . .
Baada ya kumchagulia gauni , waliongozana na kurudi ofisini , zakayo alimkaribisha na kisha waliketi , na muda huo huo simu yake ilitoa mlio wa sauti kuashiria ilikuwa ikiita , aliitoa mfukoni na kisha aliangalia jina la mpigaji na kukutana alikuwa ni Irene , alimwangalia janeth na kisha alipokea simu hio
“ niambie irene”
“ poa, nishafanikisha kazi yako “
“ enhe niambie “
“ mmiliki wa mali za bruno mpaka sasa ni bwana stephano lamberk “
‘ stephano lamberk ?”
“ ndio inasemekana ni mtoto wake na kwa taarifa nilizo nazo ni kwamba tayari yupo hapa jijini dar es salaam “
“ sawa asante Irene nashukuru kwa msaada wako “
“ naja kuchukua gauni langu nikitoka kazini ndio nitapokea asante yako “
“ hahaha .. wewe njoo tu “
Alikata simu na kumwangalia janeth aliekuwa bize na simu .
“ sasa bro mimi naondoka “
“ hivi janeth utaacha lini kuniita bro “
“ hahahah.. basi zakayo mimi naondoka “
“ aliongea janeth na kisha alinyanyuka na kuaga na kuondoka huku akimuacha zakayo akimwangalia kwa nyuma kwa masikikitiko “
“ abasi kuna jina nakutumia hebu jaribu kufatilia taarifa zake “ aliongea janeth mara baada ya kufika kwenye gari yake .
“ jina gani ?”
“ stephano lamberk”
“ sawa “
Aliingia kwenye gari na kisha kusepa bila kujulikana alikuwa akielekea wapi muda huo
******
Ilikuwa ni siku nyingine muda wa asubuhi kabisa mwanadada merina siku hio kazini aliletwa na Patrick , walikumbatiana mara baada ya kufika kwenye maegesho na kisha Patrick aliwasha gari yake na kuondoka , wakati huo Patrick anaondoka kwenye mapokezi ya magari , kuna gari nyingine ilio onekana kumfatilia , kwani Patrick alivyo ondoka tu na gari ile iliondoka .
Ni gari iliokuwa ikiendeshwa na mwanume mmoja wa makamo miaka si chini ya ishirini na nne mrefu mweupe , mara baada ya kusogea umbali wa mita kadhaa kutoka kwenye jengo la SWIFT TRANSIT , alitoa simu yake na ,kupiga mahali .
“ vipi hassani “
“ madam kama ulivyo niagiza nimewaona wako pamoja , asubuhi hii Patrick kamleta hadi kazini kwake “
“ sawa , endelea kuwafatilia “
“ sawa madam “ aliongea bwana yule na kisha alitoka eneo lile kwa spidi
Upande wa ofisini mara baada ya kuingia tu na kuketi kwenye kiti chake , aliingia afisa masoko .
“Madam kuna tenda hapa imetufikia “
“ inatoka wapi? “
“ kampuni ya NEXT LEVEL TECH (NLT )”
“ ni kampuni gani? “
“ ni kampuni ya maswala ya utengenezaji vifaa vya simu na innovation (uvumbuzi )
Aliongea mwanaume huyo wa makamo alikuewa akifahamika kwa jina la sogone wambura , ambaye alikuwa ni afisa masoko , alimpatia merina tenda hio na kuanza kuipitia kwa umakini mkubwa .
“ kuna maelezo mengine ?“
“ ndio kasema atakuja CEO kusaini mwenyewe hio tenda , pia anasema kuna mambo mengine ya kibiashara ya kuzungumza “.
“ sawa hakuna shaka mpe maelekezo secretary wangu amuwekee appointment “ aliongea merina huku akionekana kuangalia baadhi ya makabrasha yaliokuwa hapo ndani , lakini dakika chache tu simu yake ya mezani iliita .
“ kuna nini monica ?” alikwa ni secretary .
“ kuna mgeni wako anasema anamaswala binafsi ya kuzungumza na wewe “
Merina alijikuta akiwasha kamera ya mapokezi kumuangalia mgeni mwenyewe , alijikuta akifikiria kidogo na kisha alimwambia amruhusu .
Alikuwa ni mwanaume mrefu mweusi alievalia suti iliomkaa vyema , miaka yake si chini ya therathini mwenye ndevu za kiuchebe .
“ karibu “
“ asante sana merina , mimi sio mkaaji lakini kuna ujumbe wako hapa nimekuletea kutoka ikulu “.
“ ujumbe gani?? “.
“ madam wema anataka kuonana na wewe siku ya leo saa kumi kamili jioni hoteli ya serena “
Merina alijikuta akishangaa , hakuelewa kuna sababu gani ya yeye kukutana na mke wa raisi alijifikiria kwa dakika chache .
“ sawa nitaonana nae “ aliongea merina
“ hakuna shaka , lingine amesema usimwambie Patrick swala hili “
Jambo hilo pia lilimshangaza merina , lakini alijikuta akishangaa Zaidi , na pia waswasi ulichukua nafasi yake , kwani hakujua ni kwanini kuonana na mwanamama huyo kulikuwa na masharti kama ni mambo ya kawaida tu , aliamini kuna jambo , lakini hakutaka Zaidi kuweka mambo mabaya katka kichwa chake aliona ni bora atii wito kwanza .
Siku yake ilikuwa ni bize siku nzima kwani alikuwa akikutana na watu mbali mbali ambao siku hiio , muda kama wa saa saba muda ambao alikuwa ndio anataka kutoka kwa ajili ya kwenda kupata chakula ndio muda ambao secretary aliingia ndani ya ofisi yake akimtaarifu kuwa kuna mgeni anataka kuonana nae
“ anaitwa nani “
“ kajjitambulisha kwa jina la stephano lamberk kutoka kampuni ya NLT “
“ okey sawa mruhusu “
Alijiweka sawa kumsubiria bwana huyo kwani kwa tenda ambayo aliacha asubuhi , ilikuwa ni moja ya tenda yenye pesa nyingi mno ambazo angeingia nae mkataba , kampuni yake ingeneemeka .
“ karibu “ aliongea merina akimkaribisha bwana stephano lamberk ambae aliachia tabasamu mwanana baada ya kumuona mwanamke huyo mbele yake.
“ kitendo cha merina na yeye kukutanisha macho na mwanaume huyo alievalia kinadhifu kabisa suti yake na tai alijikuta akiganda kwa dakika “
“ asante “ ilikuwa ni sauti iliomshitua sana merina , ni sauti ambayo alikuwa akiijua vyema , japo mtu aliekuwa mbele yake hakuwa na sura ya mtu mwenye sauti hio kwani aliekuwa mbele yake alikuwa ni mzungu .
CNTINUARA .
SEHEMU YA 38
Japo mwanaume aliekuwa mbele yake alikuwa mzungu lakini sauti yake iliendana vyema na ya damiani , hakujua ni kwanini anamawazo hayo lakini ukweli ni kwamba alikuwa akiikumbuka vyema sauti ya damiani, sauti ambayo alikuwa akitamani sana kuisikia katika maisikio yake kwa mara nyingine .
Upande wa bwana stephano alikuwa akimwangalia mlimbwende huyo huku akitamani hata kusema neno tofauti na jambo lililomleta , lakini kwake aliona ni jambo la hatari sana kufanya hivyo japo mara kwa mara alikuwa hamkumbuki mlimbwende huyo lakini siku hio alivyopata kuonana nae alijikuta akishangaa , kwanza kilichomshangaza ni juu ya mrembo huyo kuwa CEO wa kampuni hio , kwani mara ya kwanza kwake kuonana na mrembo huyo ni siku ambayo alikuwa ndani ya kampuni hio kwa ajili ya kuomba kazi na merina na yeye akiwa mmoja ya waombaji kazi , jambo hilo lilimshangaza kidogo , fikra zake hazikumuacha kwenye jambo hilo tu , lakini alikumbuka vyema siku walipo kuwa ndani ya wilaya ya lushoto hospitalini , siku alipofungua macho yake na kuonana na merembo huyo , fikra hizo zilimfanya aanze kuvuta hata picha ya kupigwa busu kwenye paji la uso wake , japo tukio hili alikuwa amelisahau kwa miaka kadhaa , lakini kulikumbuka jambo hilo tena , aliona ni kama lilitokea jana yake , alijikuta akitabasamu huku akishindwa kuzuia mshangao wake mpaka pale alipo karibshwa kiti ndani ya ofisi hio .
“ naitwa stephano lamberk ni kurugenzi mtendaji wa kamouni ya NLT “ alijitambusha huku akipeana mkono na merina .
“ karibu bwana stephano , kwa majina naitwa merina sosteness ni mkurugenzi mtendaji wa kamuni ya SWIFT TRANSIT LIMITED “.
“ nashukuru kukufahamu merina , nipo hapa kwa ajili ya business proposal , nimejaribu kuangalia baadhi ya makampuni ya usafirishaji hapa nchini yene mafanikio na nimeona kampuni hii imefanya vizuri Zaidi , hongera sana “
Aliongea bwana stephano na kumfanya merina atabasamu , huku akipenda sauti ya bwana stephano , alitamani aendelee kuongea .
“ asante sana karibu SWIFT TRANSIT”
“ nashukuru sana , labda niende moja kwa moja ili nisichukue muda mrefu , nadhani nishatanguliza tenda kwenye kampuni hii “
“ ndio nimeiangalia , na niseme asante sana kwa kuchagua kampuni yetu “
“kama nilivysema mwanzo sikuchagua kampuni hii kwa sababu za kiupendeleo ni kutokana na vigezo vya kupokea tenda kama hii “ aliongea huku akitoa karatasi baadhi na kumpatia merina .
“ kampuni yangu kwa sasa inahitaji malighafi nyingi kutoka nje ya nchi ,kwa ajili ya maswala ya kiteknolojia , hivyo nimeona mizigo yangu yote ya kampuni yapitie kwenye kampuni yenu , huo ni mkataba ambao utakuwa ni wa miaka miwili ya mwanzo , na utaongezeka kutokana na ufanisi wa huduma kutoka kwenye kampuni yako “.
“ nashukuru bwana stephano kwa kuchagua kampuni yetu , na nimeangalia vipengele vya mkataba huu viko vizuri na vinaendana na utendaji wa kampuni yetu hivyo nakubali mkataba huu “. Aliongea na kisha alisaini mkataba huo na kupeana mikono na kisha stephano aliaga na kuondoka huku akionekana kuwa na tabasamu pana usoni .
Alienda moja kwa moja mpaka kwenye gari yake aina ya benz new model na kuwasha gari na kuondoka .
“ she is beutifull as always” stephano alijikuta akitamka hayo maneno huku akiwasha gari yake na muda huo nia yake ni kwenda kurasini
Upande wa merina , alijikuta kumbukumbu zake zikimrudisha nyuma , siku aliokuwa akiongea na damiani nje ya kampuni yake , kuna vitu alikiri anaweza kuvisahau katika maisha yake lakini sio sauti ya kijana damiani , sauti hio hakuweza kuisahao kabisa katika , kwani kwake ni kama kumbukmbu aliokuwa nayo juu ya damiani , na hata mwanaume aliengia hapo na kusaini nae mkataba alikiri kwamba alikuwa na sauti iliokuwa ikiendana kwa kila kitu na ya damiani , alijikuta akiinuka na kuangalia upande wa nje wa jengo hilo akimwangalia mwanaume huyo akiingia kwenye gari yake na kuondoka , alirudi kwenye kiti chake mara baada ya kuvuta pumzi ndefu mno , na kukaa kwenye kiti chake lakini bado sauti haikumtoka , alijikuta akichukua simu yake na kuanza kutafuta jina la stephano lamberk kwenye mitandao .
“stephano lamberk ni mtoto wa marehemu bruno lamberk amezaliwa mwaka 1996 ni mmiliki wa kampuni changa ya teknojia ijulikanayo kwa jina la NEXT LEVEL TECH yenye makazi yake nchini Tanzania ana utajiri wa dollar millioni 400 zinazotokana na umiliki wa hisa wa asilimia 23 ndani ya kampuni ya HUAWEI “
Ilikuwa ni taarifa ambayo ilimuacha mdomo wazi merlina , mambo mawili yalimfanya ashangae , jambo la kwanza ni kuwa mtoto wa bruno , jambo la pili ni utajiri aliokuwa nao , mambo hayo mawili kwa wakati mmoja yalimfikirisha kwa wakati mmoja , kumbukumbu za mama yake damiani kuuliwa kikatili na watu waliokuwa maadui wa bruno lamberk ziliijaza fikra yake mara moja .
“ this is serious “ ni nenno aliloongea merina akimaanisha jambo hilo sio la kawaida.
Upande wa stephano na yeye alikuwa kwenye mawazo ya aina moja na merina alikuwa akimuwazia mrembo huyo tokea anatoka ndani ya kampuni hio mpaka anafika kurasini , jambo lililompa fikra fikirishi ni juu ya mrembo huyo mara yake ya kwanza kukutana nae kujitambulisha kwake kama mtu ambae alikuwa akifanya interview kama yeye.
“ who is merina ?” ni moja ya swali lililokuwa ndani ya kichwa chake , alienda moja kwa moja mpaka ndani ya kiwanda , mtu wa kwanza kukutana nae alikuwa ni Rebecca , mwanamama ambae anaishi maisha ya kifahari jijini lakini haikujulikana alikuwa akifanya kazi gani .
“ luang shu yupo wapi ?” lilikuwa ni swali la kwanza kutoka kwa damiani ama stephano .
“ yupo ofisini “..
Damiani aliaenda moja kwa moja mpaka upande wa jengo moja refu lilikuwa limejengwa kwa usanifu wa hali ya juu ambapo pembeni kulikuwa na kiwanda cha uzalishaji , aliingia moja kwa moja kwenye lift ambayo ilimpeleka mpaka ghorofa ya nane .
Baada ya kufika alisalimiana na dada mmoja hivi mweusi sio mrembo sana lakini alionekana kuwa mrembo kutokana na mavazi yake na pia na miwani yake ya macho aliovalia ilimfanya apendeze .
“damiani karibu boss mkubwa “
“ vipi maendeleo “.
“ bado tupo kwenye mwanzo wa kudraft mapendekezo na idea mbalimbali “
“ namaanisha DREAMER T
“ twende ukajionee mwenywe kila kitu kipo sawa kwa sasa “.
Walitokana kuingia kwenye lift iliokuwa na vibonyeze kumi na moja yaani kuanzia ground flour mpaka gorfa ya kumi , baada ya kuingia ndani ya hii lift , luangshu alibonyeza namba moja mara mbili na lift ilianza kushuka kwenda chini na walikuja kutokea kwenye vyumba vya chini ya Ardhi lakini huwezi jua kama walikuwa kwenye ardhi kwani ndani yake hakukuwa kukitofautiana sana na vyumba vya juu tofauti mkubwa ndani ya flour hii ya chini ya ardhi ni mwanga, mwanga wake ulikuwa ni wa rangi ya blue tupu , na pia ilionekana sehemu kama maabara flani hivi , lakini pia ili uweze kuingia ndani ya flour hii baada ya kutoka kwenye lift lazima uvuke four layers of protection (deterrence , access control ,detection and identification aka four layers )hivi ni vizuizi vya kiulinzi kwa mtu kuingia ndani ya eneo hilo .
Basi baada ya kupita kwenye vizuizi hivyo vyote moja kwa moja waliingia kwenye chumba ambacho kilikuwa na maandishi makubwa ya DREAMER T ROOM .
“ ding!!! WELCOME MISTER DAMIANI RABANI AND LUANG SHU IN DREAMER T ROOM “.
Ilikuwa ni sauti flani ya kike ya kuvutia iliosikika kwenye sauti zamasikio ya damiani , alijikuta akishangaa , japo alikuwa muwezeshaji wa project nzima ya ujenzi wa chumba hicho lakini hakuamini kutakuwa na mafanikio ya aina hio , kwa mtu wa kawaida usingejua chumba hicho kinahusu nini , kwani hakikuwa na kiti chochote Zaidi ya mwanga wa blue na taa flani za mfano wa projector rangi ya blue .
“ unaweza kuuliza chohote “ aliongea luang shu na damiani alijjifikiria na likaja jambo kwenye kichwa chake .
“DREAMER T who is merina sosteness CEO of swift transit limited ?“(dreamer t nataka kumjua merina sosteness ni nani )
“Dingg !!!” MERINA SOSTNESS IS THE FOUNDER AND CEO OF SWIFT TRANSIT LIMITED, BORN IN 1996 IN SINGIDA , HAS STUDIED AT HARVARD UNIVERSITY TAKING A COURSE IN ECONOMICS HER MOTHER AND FATHER ARE OWNERS OF ATPAY , A CANADIAN BASED COMPANY , HER FORTUNE IS US$10 MILLION. MANY LIKE TO TEASE HER BY CALLING HER A RICH BEUTY .
ARE YOU SATISFIED OR NEED MORE INFORMATION ABOUT MERINA MISTER DAMIANI ?”
(merina sosteness ni mwanzilishi na mmiliki wa kampuni ya SWIFT TRANSIT Limited , amezaliwa mwaka 1996 ndani ya mkoa wa singida amesomea maswala ya uchumi ndani ya chuo cha Harvard , mama yake na baba yake ni wamiliki wa kampuni ya ATPAY lampuni yenye makao yake makuu ndani ya canada , utajiri wake ni dolla milioni kumi (bilioni ishirini na tatu za kitanzania ) wengi wanapenda kumtania kwa kumuita mrembo tajiri . , vipi unahitaji taarifa Zaidi kumuhusu merina au umeridhika bwana damiani rabani )
“ No thank you ( hapana asante )
“ WELCOME AGAIN”(karibu tena )
Damiani alijikuta akitabasamu na kuamuangalia luang shu , aliona hela zake alizotoa kwajili ya kujengewa DREAMER T hazikwenda bure kabisa .
*******
MIEZI KADHAA NYUMA
SHENZHEN –CHINA
Ilikuwa sku ya kipekee sana kwa bwana damiani rabani kutambulishwa kama moja ya wamiliki wa kampuni ya HUAWEI jambo kwake lilikuwa ni kama ndoto , hakuamini katika maisha yake angekuja kukaa na watu wakubwa na wenye pesa zao kama ilivyokuwa siku hio , hata CEO wa kampuni ya HUAWEI alipomtaka kunyanyuka kwa ajili ya kusalimiana na wakurugenzi wa bodi ,kwake aliona ni kama alikuwa ndotoni , makofi aliopigiwa na watu hao kuonyesha ishara ya kumkaribisha katika familia hio, kwake aliona akiamka asubuhi atakuta ni ndoto , lakini haikuwa ndoto , kila kitu kilichokuwa mbele yake kilikuwa ni uhalisia , damiani alikuwa sio damiani wa miaka ya nyuma huyu alikuwa ni damiani mwingine , damiani tajiri, damiani anaye miliki hisa ndani ya kampunni kubwa nchini china katika maswala ya teknolojia .
Hata baada ya kikao hicho cha wakurugenzi kuisha na kuanza kuonyeshwa mazingira ya hapo ndani , alizidi kushangaa , alikiri kwamba kampuni hio ilikuwa ni kampuni iliokuwa imeendelea sana katika swala zima la kiteknolojia .
Alizungushwa kwenye baadhi ya sehemu ndani ya jengo hizo , sehemu ambazo ilikuwa ni baadhi tu ya viwanda vilivyokuwemo vikitengeneza baadi ya bidhaa ikiwemo simu alishangaa mno , lakini ulikuwa ni mshangao ulioambatana na mafunzo ndani yake , alitamani sana mambo kama hayo yangekuwepo ndani ya taifa lake la Tanzania , japo taifa lake lilikuwa masikini , lakini alijivunia sana kuwa mtanzania na aliona maendeleo waliokua nayo wachina hata Tanzania wanaweza pia kuwa nayo kama tu wakiwa na uongozi thabiti na sera imara .
Wakati akiongozwa na CEO wa kampuni hio akielezwa jinsi ya utendaji wa kampuni hio ,ndio alikuja bwana mmoja wa kichina na kuongea maneno machache na CEO wa kampuni hio aliekuwa akijulikana kwa jina la shang lee .
“ mister damiani , huyu ni luang shu ni mtoto wa waziri wa mambo ya ndani ya uchina “ alitambulishwa kwa bwana luang shu na damiani alitabasamu huku wakiongea kimombo na bwana luang shu .
“damiani nimefika hapa kukupa mwaliko maalumu wa kukutana na baba yangu kwa ajili ya chakula cha jioni “ aliongea bwana luang shu na kumfanya damieni aendelee kushagaa , kila jambo kwake lililokuwa likiendelea ndani ya nchi hio mengi yalikuwa ni ya mshangao , kualikwa na waziri wa nchi hio lilikuwa ni jambo kubwa mno na sio kubwa tu , ni heshima kubwa sana , japo alikuwa na mawazo kwanini anataka kuonana na waziri huyo lakini aliona kuna sababu ya kutii wito .
Damiani alikubaliana na bwana luang shu kwa ajili ya kuonana na baba yake , muda wa saa mbili kamili za jioni , ndio muda ambao damiani alikuja kuchukuliwa ndani ya hoteli ilioko ganzhou na kwenda kwenye miadi yake , na mtu aliekuja kumchuku alikuwa ameagizwa na waziri huyo .
Gari iliyoyoma mpaka ndani ya hoteli kubwa ya kimataifa iliokuwa ndani ya jiji la Shenzhen iliokuwa ikifahamika kwa jina la four season , ni hoteli kubwa sana iliokuwa na mazingira ya kuvutia .
Mara baada ya kufika ndani ya hoteli hii alipelekwa moja kwa moja mpaka kwenye vyumba vya VIP kwa ajili ya kuonana na mheshimiwa , kwake yeye aliendelea kushagaa mandhari ya hoteli hio kama kawaida yake , lakini wakati anaingia ndani ya flour hio ndefu yenye mazingira ya kuvutia ndipo kidogo tu apigane kikumbo na mwanamke mmoa mrembo wa kiafrika , mpaka mwanadada ambae alikuwa amemtangulia damiani alitabasamu .
Damiani aliangalia na mwanadada huyo kisha aliomba msamaha na akapishana nae na kuendelea na safari
Waziri wa mambo ya ndani ya uchina alikuwa ndani ya eneo hilo tayari kwa ajili ya kuonana na damiani rabani , hakuwa peke yake kwani pia alikuwa na mwanae luang shu , damiani aliasalimiana na mheshimiwa huyo kwa heshima zote na kisha alikaribishwa .
“ bwana rabani kwa jina naitwa shu liang lee ni waziri wa mambo ya ndani ya uchina , nadhani unamaswali mengi unayo jiuliza kwanini ghafra tu nimekuita kwa ajili ya kuonana na wewe “ aliongea waziri wa mambo ya ndani , aliekuwa amevalia suti yake , alikuwa ni bwana mmoja mwenye kipara cha umri , alionekana tayari alikwisha uvuka ujana mpaka wakati huo .
“ ni kweli mheshimiwa , kwanza kwangu imekuwa heshima kubwa sana , japo wito wako niliupkea kwa mshangao , kwani sikuwahi tegemea katika maisha yangu kuja kuonana na kiongozi mkubwa kama wewe ndani ya taifa hili “
“ haha ni kweli uyazungumzayo , lakini kila jambo linatokea kwa sababu maalumu , labda nijitambulishe kuwa mimi ni moja ya watu wa karibbu na marafiki wakubwa wa marehemu raisi bendera lakini pia kupitia bendera nimefahamiana na mfanya biahsara bruno lamberk “ .
“nashukuru sana mheshimiwa kwa kujua kuwa wewe ni moja ya marafiki wa raisi bendera , kiufupi mimi pia ni mmoja ya watu ambao nilikuwa nikimpenda sana raisi bendera na kifo chake kilinigusa sana “.
Walikuwa wakiongea huku chakula tayari kikiwa kishaletwa , kilikuwa ni chakula cha ki VIP kweli kwa rabani alikuwa mshamba lakini hakutaka kuonekana mzembe kabisa , alijitahidi kuendana na mazingira .
“ bwana rabani kama nilivyojitambulisha kwako juu ya uhusiano wangu na bendera pamoja na bruno , nataka niseme kwamba kabla ya raisi bendera hajafariki aliniomba kuisaidia Tanzania katika maswala ya kiteknolojia , na mpaka sasa ninapo zungumza kuna vijana ambao wamemaliza kusoma hapa china Katika maswala mbali mbali ya kiteknolojia na kwa sasa wapo kwenye moja ya kampuni baadhi kwa ajili ya kupata uzoefu , lakini kwa bahati mbya ni kwamba mpango huu tuliufanya kuwa binafsi mimi na bendera mpaka pale vijana hao watakapo maliza masomo yao , lakini ndio hivyo mheshimiwa amekwisha tangulia mbele za haki , na ni jukumu langu kuangalia ni namna gani vijana hawa kama ilivokuwa nia ya mheshimiwa kuhakikisha wanarudi na kuendeleza teknolojia ndani ya taifa la Tanzania , kwani naamini hio itakuwa ni moja ya jambo ambalo kwangu mimi ndio nitalifanya kuenzi kifo chake “ alinyamaza kisha akaendelea na wakati huo damiani hakuwa na jambo la kuongea Zaidi ya kushangazwa na maneno ya waziri .
“ hivyo bwana rabani kwakua sasa ushajulikana kama mfanya biashara rasmi na mrithi wa mali zote za bruno , wewe kama mfanya biashara nataka tuambizane katika kuhakikisha teknolojia ndani ya Tanzania inakuwa , kwa kunzisha kampuni ya kiteknolojia nchini Tanzania , na vijana wote wa kitanzania walio chini yangu nitawaweka chini yako , naamini wewe ni mzalendo wa kweli kwa taifa lako hivyo swala hili sio gumu lako kulifanyia maamuzi “
Swala hilo kwa damiani lilimpa furaha , na furaha aliopata ni kuona kwamba kuna watu waliokuwa wakiitakia mema nchi yake kama ilivyokuwa kwa waziri wa viwanda , lakini jambo moja ambalo lilikuwa likimpa mashaka mpaka kwa wakati wake ni watu wanaomtafuta , pia kisasi alichokuwa akitaka kukikamilisha juu ya wote waliohusika na kifo cha mama yake .
itaendelea ......
USISITE KUWASILIANA NAMI WATSAPP KWA NAMBA 0687151346
AU UNAWEZA GUSA LINK HIO HAPO CHINI CHINI ITAKULETA MOJA KWA MOJA WATSAPP
WhatsApp Messenger: More than 2 billion people in over 180 countries use WhatsApp to stay in touch with friends and family, anytime and anywhere. WhatsApp is free and offers simple, secure, reliable messaging and calling, available on phones all over the world.
wa.link