SEHEMU YA 39
“ mheshimiwa kwanza nina furaha sana kuona kama kuna watu ambao wana moyo kama wako , kwani jambo uliloongea hapa ni jambo ambalo linagusa moja kwa moja maisha ya kila mtanzania , na niseme kwamba moyo wako wa kipekee na mapenzi yako kwetu sisi watanzania ni hakika kwamba umewazidi hata watanzania wenyewe , lakini mheshimiwa swala hilo linanipa ugumu kidogo kulitolea maamuzi kwani mpaka sasa mimi natafutwa ndani ya nchi yangu na hata maadui zangu bado sijawajua vizuri “
Aliongea damiani na kumfanya mheshimiwa atabasamu
“ najua bwana damiani kuwa unatafutwa , na pia kila hatua uliokuwa ukipita katika maisha yako nilikwa nafatilia kwa ukaribu sana nataka nikwambie tu bwana damiani kwamba you are chosen one for your country , damiani wewe ni special and trust me mambo yote unayopitia sasa hayana budi kutokea , na siku zote kila jambo lina suluhisho lake , je utajisikiaje nikikwambia kwamba kuna njia sahihi ya kuingia nchini kwako bila kujulikana tena ?”
“ mheshimiwa natamani swala hilo liwezekane “
“ ndio bwana damiani hujanijibu swali langu “
“ kama kuna njia ya mimi kuingia nchini kwangu bila kujulikana nitafurahi na itakuwa furaha kwangu kufanya na kutimiza yale yote ambayo mheshimiwa bendera alitaka na alikuwa akiyaota yafanikiwe “
“ hahahha.. nimefurahishwa sana na jibu hilo bwana damiani , na niseme kwamba mpaka sasa njia ya wewe kuingia nchini ipo ,unachotakiwa kwasasa ni kufata taratibu za kubadilisha jina na munekano wako “.
Hapo damiani alijikuta akiwa kwenye mshangao Zaidi , hakuelewa maneno ya mheshimiwa yalikuwa yanamaanisha nini , japo alijua kuwa china kuna maajabu mengi katika maendeleo lakini swala la kubadilisha muonekano wake lilikuwa ni swala gumu sana kulielewa kwa kichwa chake kidogo na exposure yake .
“ naona hujanielewa bwana damiani , lakini kabla maswala hayo hayajachukua nafasi yake naomba unipe jibu kama kweli upotayari kuipigania nchi yako kama bendera alivyokuwa akihitaji na akiota “.
“ nipo tayari mheshimiwa “
‘ good , kama nilivyosema damiani kwamba wewe ni chaguo la mungu kwa ajili ya watanzania swala hilo linatakiwa liwe katika ubongo wako kuanzia sasa , najua moyo wako umejawa na visasi , lakini nataka nikwambie kwamba anaepaswa kutoa hukumu kwa wale wote waliotutendea mabaya sio sisi binadamu bali ni mungu pekee , hivyo basi kisasi kisikufanye kuwa kiwingu kwa kusudio la mungu aliloliandaa kwa ajili yako , yangu ni hayao tu na unapaswa kuyaweka akilini kwanzia sasa .
“ asante sana muheshimiwa kwa maneno yako ya kibusara “.
“maongezi yangu yataishia hapa , kwa sasa nimuachie luang shu atakuongoza na kukuonesha njia zote za kuingia ndani ya taifa la Tanzania bila mtu yoyote kujua “.
Mheshimiwa waziri aliondoka ndani ya hoteli hio akifatishana na baadhi ya walinzi wake huku akimuacha damiani na luang shu .
Siku mbili mbele ndipo bwana damiani alipoingizwa ndani ya kampuni ya TENCET kampuni iliokuwa na makao makuu yake hapo hapo ndani ya jiji la shenzheni , dhumuni la damiani kuingizwa hapo ni kwa ajjili ya kuoneshwa namna ambayo anaweza akaingia nchini Tanzania bila maadui zake kumtambua .
Kwake mwendelezo wa mshango ulikuwa ukiendelea tu , mpaka sasa aliona mambo hayo ni ya kawaida , lakini kadri alivyokuwa akionyeshwa mambo mapya , alikiri hayakuwa yakawaida , alikiri kwamba china ilikuwa imeendelea
“hii ni dreamer T room ni chumba ambacho kimejengwa kwa teknolojia ya hali ya juu sana ambayo bado haijafahamika kwa watu wengi Zaidi ya wachina , ni teknolojia ambayo nimeigunda mimi mwenyewe nikiwa na moja ya mainjinia wengine ndani yakampuni hii .
“ inahusu nini hii dreamer T “
“ hii kazi yake ni kutoa taarifa zote za kila mtu duniani kote , na mambo yote yanayo endelea duniani inauwezo mkubwa wa kutafuta mtu yoyote mahali popote pale na ikamtolea taarifa kuanzia umri wake mpaka group ya damu yake , teknolojia hii kiufupi imewezeshwa na mfumo wa satiliati za kisasa zilizopo juu lakini kuna muunganiko wa teknolojia nyingi sana zimeunganishwa ili kuhakikisha ufanisi wake unakuwa mkubwa “
Damiani alieshangazwa na maneno hayo , huku akizidi kuoneshwa mambo mengi sana ndanni ya kampuni hio ya TENCET mwisho kabisa ndipo alipoelekwa sasa katika teknolojia ambayo ingemuwezesha kuingia nchini Tanzania bila kugundulika.
Hii ni teknolojia inayokwenda kwa jina la FULL BODY MASK(FBM) ni technolojia mpya yenye uwezo wa kubadilisha muonekano wako wote na kuwa muonekano wa mtu mwinigine , ni teknolojia mpya kwa sasa , na majaribio yake yashakwisha kumalizika , bado kuitangza rasmi duniani kote , haina madhara yoyote kwa binadamu lakini pia inakupa faida kuu mbili ya mwili kuwa mwepesi na uwezo wa kuchanganua mambo kuongezeka .
Matengenezo ya mask yanakuwa ni juu ya muhusika na aina ya muoenkano anaoutaka yeye mwenyewe moja ya wagunduzi waliofanikisha swala hilo mmoja wapo ni mtanzania mwenzako “ aliongea luang shhu na kumfanya damiani ashangae
“ yeahi ni mtanzania tena mwanamke , mwenye a PHD yake akiwa na umri mdogo kabida na hii ndio project yake kubwa ambayo kwa kushirikiana na wenzake waliifanikisha na kumfanya atunukiwe PHD “
“ napataje hio mask sasa , na je nikitaka kuitoa mwilini na kutumia uso wangu wa kawaida? “
“ jambo hilo pia linawezekana , hii teknolojia dhumuni lake sio kwa ajili ya watu kuitumia hovyo ila linalenga watu maalumu tu wakiwemo wana usalama na wanasiasa na VIP pale wanapokuwa katika hali ya hatari , hivyo basi inawezakana kuvaliwa na kuvuliwa vile upandavyo , nadhani nimekueleza mengi sana juu ya jambo hilo kesho utarudi hapa kwa ajili ya kutengenezewa mask yako kwani kuna mambo ya kibiashara ambayo tunataka kuzungumze “
“aliongea luang shu na kisha walitoka na kwenda kwenye ofisi nyingine ndani ya jengo hilo la TENCET kuna maswali mengi damiani alikuwa nayo juu ya luang shu lakini hakutaka kuuliza kwa wakati huo .
“ sasa bwana damiani , nadhani kwa sasa sisi ni marafiki nitakuita kwa jina la damiani tu “ .
“ hakuna shaka luang shu “
“ sasa kuna kiwanda kilichopo Tanzania ambacho kipo on hold , na kiwanda hichi kipo chini yangu na lilikuwa ni ombi kutoka kwa bwana bruno kusaini mkataba uliokuwa ukinihusisha mimi kama mmiliki wa kiwanda hicho , lakini dhumuni kubwa ni wewe kupewa kiwanda hicho kwa ajili ya kuendeleza teknolojia kwani , lilikuwa ni jambo ambalo bruno alikuwa akiliota sana kulitimiza “
“ unaamaanisha hakikuwa sehemu ya mauzo kwenda kwa INNOVA “.
“ ndio na huu ni mkataba niliosaini nao bruno , lakini kabla ya kukabidhi kiwanda hichi inabidi niende Tanzania kwa ajili ya kukiidhinisha kuwa mali yangu kisheria na ndipo nitasaini mkataba wa kubadilisha umiliki kwenda kwako “
Aliongea luang shu na damiani alimuelewa vyema , alicho kuwa akimaanisha ,
Basi siku mbili mbele luang shu alisafiri kwenda Tanzania , ilikuwa ni mara yake ya kwanza , huku mgeni wake mkubwa akiwa ni Rebecca .
Upande wa damiani na yeye alishangazwa na teknolojia ya FULL BODY MASK , kwani siku mbili chache alipewa sanduku lake la plastic kama la kubebea nguo na maelekezo yote .
“ hili sanduku litakuwa ni kwa ajili ya kuhifadhi mask yako pale utakapo taka kuivua , na pia hili hili litakupa uwezo wa kuivaa tena , unachotakiwa ni kusimama ndani ya hili begi na kisha unatumia hii rimoti kuvaa na kuvua mask hio , na swala hili lazima lifanyike ukiwa huna nguo yoyote mwilini “
“ mwisho kwa maagizo uliopewa na muheshimiwa , kwasasa utaitwa stpehano lamberk , na taarifa zako zote zishawekwa mtandaoni , na kwa sasa kila kikao cha bodi ya wakurugenzi katika kampuni ya HUAWEI unatakiwa kutumia FULL BODY MASK “ aliongea mwanadada huyu ambae alikuwa ni injinia wa kmpuni hio .
Kwanzia siku hio damiani alikuwa ni mwendo wa kuvua na kuvaa mask hio na jina lake rasmi likabadilika kutoka damiani rabani na kwenda stephano lamberk , na halikubadilishwa jina tu kila kitu kilibadilika kwanzia taarifa zake zote , kwa muonekano aliokuwa nao wa kizungu hata yeye alishangaa kabisa technolojia .
“ ogopa sana Mungu na teknolojia “ alijikuta siku hio akiongea wakati akiwa anajiangalia jisi alivyo badilika kimuonekano kwenye kioo .
Maisha yake kama mfanya biashara yalianza rasmi ndani ya jiji la shenzheni , ganzhou m Beijing , chongdong , hongkong , Taiwan , mpaka Singapore , hayo ni baadhi ya maeneo alioyatembelea kwa miezi michache akiibua fursa mbali mbali za kibiashara , huku akitambulika kama tajiri mwenye uraia wa Tanzania anaeisi nchi za nje(DIASPORA ).
******
IKULU –DAR ES SALAAM
Ni siku ambayo suzzane alikuwa ameahidiana kukutana na mheshimiwa raisi kwa ajili ya kutoa taarfa ya sehemu aliofikia katika upelelezi wake wa kujua uwepo wa damiani nchini , lakini siku hio ni siku ambayo mheshimiwa raisi alikuwa na miadi pia ya kuonana na mfanya biashara mkubwa aliengia nchini bwana stephano lamberk ambae kwa wakati huo alikuwa akimfahamu kama mrithi wa bruno .
Suzzane ndio aliekuwa wakwanza kuonana na raisi siku hio , ilikuwa yapata saa sita mchana wakati suzzane akiingia ndani ya ikulu hio .
“ haya suzzane nipe updates za kazi yako “.
“ mheshimiwa kwanza niseme kazi ni ngumu sana , japo uchunguzi una matumaini lakini mpaka sasa bado sijafikia muafaka wa kuthibitisha uwepo wa damiani hapa nchini , jambo nililoligundua mpaka sasa ni mtu anaejiita mzalendo , ambaye japo sijapata ushahidi naamini kwamba ndie aliehusika na shambulio la pale hotelini siku ile. “
“ ni nani huyo suzzane , inapaswa akamatwe mapema sana “
“ mheshimiwa kama nilivyo sema kuwa mtu huyo bado sina ushahidi kuwa ndio yeye ila kwa mambo yaliotokea hivi karibuni naamini atakuwa anahusika kwa namna moja ama ningine , kwani juzi yake nilikutana nae katika mapambano na pia ndie aliehusika na kuiba mzigo bandarini na kwenda kuuchoma katika shamba la kimbona lilopo fukayose “.
“ suzzane anaonekana kuwa hatari sana na anajua kila tunach fanya , lakini bado hujanambia huyu mtu ni nani mpaka sasa “
“ mheshimiwa bado sijapata taarifa zake mpaka sasa , lakini naamini siku mbili zijazo nitakuwa na taarifa kamili juu yake , lakini pia nitatafuta ushahidi kama alikuwa akihusika na shambulio lile , lakini pia mheshimiwa mpaka sasa kuna jambo linalonichanganya ?”
“ unachanganywa na nini suzzane “.
“ kama nilivyokuambia kuhusu huyu mtu anaejiita mzalendo , japo ya kuwa jina linafanana kila mahali tukio linapotokea , lakini sura zinakuwa tofauti tofauti , na pia sura hizo zinakuwa ni za wahusika ambao hawahusiki na matukio ya aina yoyote ile “
“ inawezekana vipi suzzane , unataka kuniambia kuwa mtu huyo anatumia sura zawatu , au watu hao wanajifanya hawahusiki “.
“ mheshimiwa najua swala hili linaweza lisiaminike , lakini watu wote walioonekana katika matukio hawahusiki moja kwa moja , hivyo naamini kabisa kuwa mhalifu anatumia sura za watu ili kutuchanganya na mpaka sasa sijajuia ana kusuidio gani “
“ kama ni hivyo swala hilo litakuwa gumu sana , lakini pia inatupasa kuwa makini na nia ya huyu muhalifu kutumia sura za watu kutuchanganya , lakini vipi kuhusu damiani unaadhani haya yote yanahusiana nay eye , hususanni kwenye waraka wa bendera ?”“.
“ mheshimiwa mpaka sasa sina uhakika kama damiani yupo nchini , lakini swala hilo bado nalifanyia kazi kujua kama yupo nchini au la “.
“ suzzane kama swala hili ni kubwa nikuongezee watu wa kukusaidia , hasa huyu damiani ananinyima akili , kuna hisia zinaniambia kuwa matukio yote ya hivi karibuni atakuwa ameyafanya yeye “.
“ inawezekana mheshimiwa , kwasasa inabidi niendelee na uchunguzi wangu na pale nitakapo pata mwanga nitakuwa na kueleza “.
“ sawa suzzane , hakikisha swala hili unalifanya kwa akili sana na unapata majibu , wewe ni mtu ninae kuamini sana ,isitoshe umefanya kazi zangu nyingi sana na za hatari “
“ hakuna shaka muheshimiwa mimi nadhani niondoke sasa nikaendelee na upelelezi wangu , lakini kama ulivyosema kuna watu nahitaji wanisaidie katika kazi hii , wapo ndani ya kitengo cha TISS nataka ruhusa yako ili kuwachukua kwa muda “
“ hakuna shaka suzzane , hakisha wawe ni watu unaowaamini ambao watakuwa si rahisi kutusaliti , maana swala hili ni nyeti hususani swala la nyaraka alioacha raisi bendera , nafikiri unajua ninacho maanisha hapa suzzane “
“ ndio muheshimiwa “
‘ kuna swala lingine nataka pia ulifanyie kazi “
“swala gani hilo muheshimiwa ?”.
“ kuna mfanya biashara maarufu alieingia hapa nchini nataka umfahamu ni nani na historia yake ya nyuma , kila kitu kinacho muhusu nakitaka , kiufupi nikwambie kuwa ameingia nchini na anatambulika kama mtoto wa bruno aliekuwa akiishi nje ya nchi na amerudi Tanzania kwa ajili ya uwekezaji , lakini nina wasiwasi nae kabisa , naziamini sana hisia zangu , hivyo swala hili nataka ulifanyie upelelezi na unipe majibu , na muda si mfupi ataingia hapa nataka upelelezi wako uanzie hapo
“ sawa muheshimiwa “
Baada ya suzzane kutoka nje ya ofisi ya raisi alikutana na sabi mboneche , mkurugenzi wa mawasiliano ikulu .
‘ vipi suzzane ?”
“ poa sabi “
“ naona unatoka kuonana na mheshimiwa “.
“ ndio kuna mambo nilikuja kuyatolea taarifa “
“ okey sawa , lakini vipi tunaweza kuonana leo jioni kwa chakula , kama unayo nafasi ?”
“ kwa sasa niko bize sana , labda nikipata nafasi nitakuambia “
“basi naomba namba yako , na uchukue yangu ili ukipata nafasi iwe rahisi ya kuambiana “
“ hahaha .. sawa sabi “ alioogea suzzane na kisha alimpa kadi suzzane iliokuwa na namba yake na pia suzzane aliandika namba yake kwenye simu ya sabi “.
Wakati huo suzzane na sabi wakiongea ndio wakati ambao mfanya biashara stephano lamberk alikuwa akiingia hapo ikulu , huku akiwa ameongozana na secretary wa raisi .
Stephano mzungu feki huyu alijikuta akisimama kwa mshangao na hio ni mara baada ya kumuona sabi , kuna muda alidhani amemfananisha , lakini kadri alivyokuwa akiwasogelea ndipo alipo jua kuwa macho yake hayakuwa yakimdanganya , alikuwa ni sabi mwenyewe aliekuwa akiongea na suzzane .
“ sabii “
CONTINUARA
SEHEMU YA 40
“ Bebi mbona upo hivyo leo “ lilikuwa ni swali kutoka kwa patrick kwenda kwa merina , kwani siku hio merina alionekana kutokuwa sawa kabisa , muda huo alikuwa nyumbani kwake anaangalia runinga pembeni akiwepo patrick , lakini japo ya kipindi kinacho oneshwa kuwa moja ya vipindi vyake pendwa lakini siku hio hakuonekana sawa kabisa , na hata mpenzi wake Patrick ambae ndio kaingia nyumbani hapo muda mfupi uliopita alijua mabadiliko aliokuwa nayo merina .
“ niko sawa Patrick , nadhani uchomvu tu , ngoja nikapumzike tutaonana kesho bye “ aliongea huku akimuaga Patrick aliekuwa amesimama akimwangalia mpenzi wake huyo kwa nyuma , Patrick alionekana mwenye huzuni kweli , hakujua hatima ya penzi lake na merina ni nini , kwani ni wiki kadhaa tu tokea warudishe penzi lao upya .
“ broo unawaza nini ?”
“ ilikuwa ni sauti yamdogo wake merina aitwae mage “.
“daaha ! hamna kitu mage , mimi naondoka “
“ bro bhana unamuwaza sista najua , tokea jana alivyorudi hakuonekana sawa kabisa “.
“ jana saa ngapi ?”
“ jana alirudi kazini , harafu akaondoka tena akasema kuna mtu anakwenda kuonana nae “aliongea mage na kumfanya Patrick awaze kidogo na kisha alitabasamu na kuaga kuondoka , na muda huo ilikuwa ni saa moja za jioni .
Patrick wakati akiwa kwenye gari lake alikuwa na mawazo kweli , alimjua merina sana ni mgumu wa kumwambia mambo yake kiasi cha kupelekea muda mwingine kumuona mwanamke huyo kama mbinafsi , lakini kwakuwa anampenda aliamua kumuelewa , lakini jambo hilo halikuwa rahisi kwake , kwani hakupenda kumuona merina akiwa katika hali huzuni .
Alimpigia rafiki yake ahmedi yuko kiwanja gani , na kama alivyotegemea kwani alikuwa akimjua rafiki yake huyo kwa kupenda kula bata , alimwambia kuwa yupo havoc , maeneo hayo hayo ya masaki , Patrick aliingia sellasie road na kuja kutokea havoc club , japo muda huo ilikuwa ni mapema mno lakini sehemu hio ilikuwa imechangamka sana .
Alisalimiana na rafiki yake na kisha akaketi kwenye kiti na muda mfupi tu alikuja mhudumu na kumuuliza kinywaji na akaagiza heneken .
“naona leo mambo swafi “
“ kwanini ?”
“ unajulikana ukiwa na stress kinywaji chako kikubwa ni heinken “.
“hahaha ni kweli , yaani mapenzi yananiendesha , biashara nazo zinaniendesha , ngoja nitoe mawazo “
“ rafiki yangu wewe shida yako ni moja tu umependa mshikaji wangu , yaani Patrick sio Patrick wa miaka ile saivi umebadilika “.
“ miaka inaenda ahmedi unajua , itafikia kipindi hata wewe utataka kuanzisha ffamilia”
“ familia gani ! unamaanisha kwamba nioe , hilo sahau mpaka sasa naitwa baba kuna haja gani ya mimi kuoa tena “.
“nakujua wewe kwa ubishi lakini trust me kuna muda lazima utataka kuoa “.
“ haiwezi kutokea bhana , vipi na huko kwenye biashara kunasemaje “
“acha tu mpaka sasa kuna hati hati ya kufunga ile kampuni ya maswala ya mawasiliano”
“ kwanini “
“unakumbuka nilikuambia kuhusu kile kiwanda cha marehemu bruno kule kurasini nilitaka nikinunue ?”
“ ndio nakumbuka “.
“ sasa kumbe kilikuwa kimeuzwa na mwenyewe kabla hajafariki na nilikuwa na kitegemea sana “
“sasa hilo linakupaje stress si unatafuta eneo lingine , pesa si unayo ?”
“ ndio pesa ninayo , lakini ushindani wa soko utakuwa mkubwa na naweza kupata hasara kama nitaanza upya na ndio maana nilitaka kile kiwanda niendeleze alipoishia bruno “
” yeah ni kweli usemayo , lakini mimi naona bora uachane na huo uwekezaji ufokasi kwenye fursa nyingine “
“ahmedi ndoto yangu kubwa ilikuwa ni kuona namiliki kiwanda cha electronics “.
“ najua Patrick ndio maana naona kama hutaki kuanzisha sehemu yako bora uachane a huo uwekezaji “.
“na wazee nina bahati nimewaona mabosi wenyewe “ aliongea jamaa mmoja mrefu mweusi alievalia tisheti na jinsi akiwa mbele ya Patrick na ahmedi na alionekana kuwajua vyema .
“ hahaha wewe mzee wa bata umefika “.
“ nimefika mpenda bata mwenzangu “.
“ huyu jamaa naona leo na heinken “
“ hahaha.. nikajua mimi tu ninaemjua pat kumbe hata wewe “.
“achenp zenu nyie , vipi kamote mambo yako poa “
“ fresh pat , unajua leo nimefurah kukuona maana siku hizi umepunguza sana kuja sehemu hizi ,tokea umpate yule mrembo maana sio poa jana nilikutana nae pale serena mh !”
“naunga mkono hoja mtoto mkali , ndio maana pat kadata “. Aliongea ahmedi na wote wakacheka .
Saa tatu kamili ndio muda Patrick alipotoka club hapo kwa ajili ya kuelekea nyumbani kwake , muda huo alikuwa akipita feri , jjapo alikuwa amekunywa lakini akili yake ilikuwa sawa kabisa .
“ jana merina alikuwa akifanya nini serena ‘ ni swali lililoibuka kwenye kichwa chake na pia alijaribu kuunganisha na maneno ya mdogo wake merina kuna jambo lilimjia ila aliamua kupotezea , lakini alishituliwa pia na mlio wa simu na alipo angalia aliona ni jina la baba yake walisalimiana na kisha aliambiwa kuwa aende ikulu siku inayofauta .
Upande wa merina alikuwa kwenye mawazo , muda huo alikuwa amelala lakini usingizi ulikuwa hauji kabisa mambo kadhaa yalikuwa yakizunguka kweye kichwa chake , japo mwanamke huyu kuwa na urembo wa kipekee lakini hakuwa ni mwenye furaha kabisa .
“hivi damiani ananipenda kweli kama ninavyoteseka kwa ajili yake ,na ukute saivi kakumbatiwa na mwanamke wake inabidi nimsahau sasa ” yalikuwa mawazo ya merina .
“ hivi mama yake Patrick mbona simuelewi ana maana gani kuniambia vile “
“ siijui wamefikia wapi kwenye huo uchunguzi wao” yote hayo ni mawaz mchanganyiko kwenye kichwa cha merina
*****
Ni siku moja nyuma merina alieonekana akiingia ndani ya hoteli ya serena , muda huo ilikuwa yapata saa tisa na madakika kadhaa mchana , alikuwa mahali hapo kwa ajili ya kutiii wito wa kuonana na mke wa raisi , baada ya kufika mapokezi alipokelewa na mwanadada mmoja alievalia suti na merina alikuwa akimjua vyema huyo mwanadada kama moja ya wasaidizi wa mke wa raisi .
“ karibu merina “ aliongea mke wa raisi na merina na yeye aliachia tabasamu na kumsalimia huku wakikaa .
“ vipi maendeleo yako merina ?”.
‘ naendelea vizuri namshukuru mungu “
“nafrahi kusikia hivyo , nadhani umeshangaa kukuomba tuonane “.
“ ndio mama lakini pia nimefurahi kuonana na wewe “
“ Nashukuru hata mimi pia nimefurahi kuonana na mwanamke mchakarikaji kama wewe unanikumbusha mbali sana enzi zangu nayasaka maisha “
“ asante mama “
“sasa merina nataka niende moja kwa moja kwenye jambo lililonileta nataka kujua mahusiano yako wewe na patrick “ merina alijikuta akishangaa kidogo huku ni kama mtu aliekuwa akiwaza ajibu nini
“Patrick ni Zaidi ya rafiiki yangu mama “
“ nadhani umeshangaa kwanini nimeuliza hivyo lakini nina maana yangu , vipi unampenda Patrick naomba uniambie ukweli wako merina kuwa huru “
“ kwakweli mama nipo kwenye hatua ya kujifunza kumpenda Patrick kwani ni muda sasa kuna mtu nampenda lakini hatujaonana muda mrefu mpaka nimejikatia tamaa ya kuonana nae tena ”.aliongea merina , japo alionekana na wasiwasi .
“ sikia merina naomba usinifikirie vibaya , ila naomba usiwe karibu na Patrick hususani kimapenzi , najua wewe ni mwanamke mrembo sana , unatabia njema na mwanaume yoyote anaweza kukupenda , lakini kwa faida yako na ya Patrick naomba msiwe na ukaribu wa kimapenzi “ aliongea huku akionekana kumaanisha kile anacho kiongea na pia kilimshangaza merina .
“ labda naweza kujua sababu mama “.
“utanisamehe merina , lakini siwezi kukuambia , lakini naomba uzingatie nilichosema , hii ni kwa ajili yenu wote wawili , si rahisi kwangu kuja kukuambia haya lakini zingatia hayo merina , na naomba usimwambie Patrick kama tumeonana leo maana sipendi kuingilia maisha ya Patrick lakini inanipasa “ aliongea mke wa raisi na hakukua na maneno mengi aliaga na kuondoka akimuacha merina kwenye mawazo , hakujua ni kwasababu gani mwanamama huyo anamwambia mambo hayo .
****
Ni siku nyingine kabisa siku ya alhamisi muda wa saa tatu kamili , alionekana mzungu feki yaani stephano lamberk akiingia ofisini kwake siku hio ndani ya kampuni mpya kampuni ijulikanayo kwa jina la NLT (NEXT LEVEL TECH)
Alisalimiana na lissa , mwanadada aliekuwa akikaa mapokezi na kisha moja kwa moja alienda mpaka kwenye ofisi yake , mara baada ya kuingia ndani ya ofisi hio alivua koti lake na kulining`iniza na kisha alisogelea kiti chake na kukaa huku akiwasha tarakishi yake , na muda huo huo aliingia secretary na kumletea ratiba yake ya siku hio .
Siku hio ratiba yake kubwa ilikuwa ni kuoanana na mainjinia ambao wangekuwa wafanyakazi rasmi ambao watakwenda kufanya kazi katika kampuni yake hio , kwani mpaka muda huo injinia hao walikuwa tayari nchini dar es salaam wakitokea china na ni moja ya ahadi ambayo alikuwa ameahidiwa na waziri wa mambo ya ndani ya uchina .
Ni muda wa saa nne ndio muda ambao alikuja kuitwa na secretary akitaarifiwa kuwa watu wote washafika kwenye ukumbi wa mikutano kwa ajili ya kikao ambacho kilikuwa kwa ajjili ya utambusliho wa wafanyakazi wapya na nafasi zao za kazi kwenye kampuni hio .
Alivaa koti lake na kuchukua tablet yake na kuelekekea ndani ya ukumbi huo na kuingia ndani , ilikuwa ni timu ya watu kumi waliokuwa ndani ya ukumbi huo .
“kuna mmoja hajafika bado naomba tumsubirie “ ilikuwa ni sauti ya mwanamama Rebecca akimwambia damiani ama stephano na damiani alitabasamu na kukubaliana nae kwa kutingisha kichwa.
Zikiwa zimepita dakika kama tatu hivi ndio mlango ulipofunguliwa , macho yote yalikuwa mlangoni kuangalia ni nani aliekuwa anaingia , na hata kwa stephano ilikuwa ivyo hivyo kwani hata yeye mainjinia waliokuwa hapo ndani alikuwa hawajui .
Alikuwa ni mrembo mno , alievalia suti yake nyeusi lakini iliokuwa imemkaa vizuri , alionekana kujiamini sana wakati anaingia , macho yote yalikuwa kwa mwanadada huyo , Rebecca alimuonesha kiti na kukaa .
Upande wa damiani alikuwa na mawazo ni wapi mwanadada huyo alimuona , anaikumbuka vyema sura hio lakini hakuwa akikumbuka ni wapi alishawahi kumuona mlimbwende huyo , aliangalia karatasi la majina alillokuwa ameshikilia , lakini alijikuta akipigwa na mshangao .
Damiani aliweka karatasi ile pembeni na kisha alirushu kikao kianze na jambo la kwanza ilikuwa ni utambulisho , damiani alijitambulisha , Rebecca nae alijitambulisha kama afisa masoko na zamu kwa wageni , damiani alikuwa na hamu kubwa ya kuwatambua wageni waliokuwa mebele yake kwani hao ndio aliokuwa akiamini wangekwenda kuibadilisha Tanzania .
Mtu wa kwanza kuinuka alikuwa ni yule mwanadada ambae hakuwa akimfahamu jina ila alikuwa akiikumbuka sura yake .
“ naitwa janeth bendera elimu yangu ni phd katka maswala ya software and electronics engeneering “kila mtu alishangazwa na utambulisho huo ‘ janeth bendera ‘ ,phd ndio moja ya sehemu kubwa zilizowavutia watu na kuwashangaza .
Damiani na yeye alikuwa kwenye mashangao , kilichomshangaza ni kwamba mwana dada huyo ni kweli karatasi yake ilikuwa ikionesha kabisa kuwa ana phd na hakuwa akidanganya hata kidogo , lakini kilicho mshangaza yeye ni umri wake na mwonekano wake vyote ni vitu vilivyokuwa vikimshangaza , hakujua kuwa duniani kuna watu mpaka wa miaka kumi na nane ambao tayari washapata phd kwenye maisha yao .
Kwakuwa kikao hakikuwa cha kuhoji sana walijitambulsiha wengine , damiani alijikuta akitabasamu mno , na kuona kweli ni moja ya zawadi kubwa mheshimiwa raisi bendera aliacha nyuma , kwani kila aliekuwa amejitambusliaha alionekana kuwa na elimu nzuri sana ambayo ikitumika vizuri kwenye taifa la Tanzania basi teknolojia kwa ujumla wake itafika mbali sana na hata pia maendeleo ya watu yangeongezeka .
“ kwanza nashukuru sana kwa wote kufika katika kampuni hii , niseme jamb dogo tu kwamba kampuni hii sio ya kwangu mwenyewe , kampuni hii ni ya kwetu sote nikimanisha sisi tuliopo hapa na watanzania kwa ujumla , ni moja ya zawadi kubwa mno ambayo mheshimiwa bendera ametuachia , na ili kuenzi juhudi zake za kulikomboa taifa hili katika umasikini ni kuhakikisha mipango yake tunaiendeleza , nimefurahi kuwafahamu na Imani yangu inaniambia nyie ni watu sahihi kwa taifa hili lakini pia kwangu pia katika katika kazi hii , hivyo basi kesho nimeaamua kutoa asilimia ishirini ya hisa ziende kwa wananchi wanaotaka kununua hisa katika kampuuni yetu na asilimia 30 nimeitoa kwenu kwa kila mtu na ratio yake ., kesho ni siku ambayo tutakutana na bodi nzima ya wana hisa kwa ajili ya kupanga siku ya kufungua kiwanda chetu rasmi , lakini kabla ya jambo hilo naamini kuwa mnayo mapendekezo mengi ya kipi tuanze nacho kwenye kampuni yetu ili kuingia sokoni “
Aliongea damiani na kila mtu alifurahishwa na maneno yake na baada ya hapo kikao kilifungwa na kila mtu alitoka na kuendelea na majukumu , damiani yeye alirudi kwenye ofisi yake huku mawazo ya janeth yakiwa bado yanamuandama , alikuwa akijaribu kumkumbuka msichana huyo alimuona wapi , lakini akili yake ilikuwa haikumbukii kabisa ni wapi aliwahi kumuona .
“ boss miss janeth anataka kuongea na wewe “ ilikuwa ni sauti ya secretary ndio iliomshitua damiani na kuinua uso na kumuangalia secretary huyo na hakuwa na ubishi alimwamba kuwa amruhusu aingie kuongea nae
Dakika chache mbele mlango ulifunguliwa na aliingia mrembo huyo , alikuwa ni mrembo haswa na hata yeye mwenyewe alikiri kuwa mwanadada huyo alikuwa mrembo alionekana kuwa mbichi kabisa jambo ambalo hata kwa damiani alikuwa akijiuliza inakuwaje mrembo huyo akawa na phd kwa muonekano huo .
“bwana CEO “ ilikuwa ni sauti ya kwanza ya janeth mara baada ya kuingia ofisi hio akimwangalia damiani kwa mapozii kama kawaida yake .
“ karibu sana “ aliongea damiani kwa heshima zote maana alijua mtu aliekuwa mbele yake alikuwa ni mtu mwenye PHD .
“ asante mister steohano lamberk aka damiani rabani kutoka lushoto Tanga “ aliongea janeth huku akiweka mapozi ya kike huku akiwa amekunja nne , lakini kwa damiani alikuwa kwenye mshangao na mshituko wa aina yake kiasi kwamba hata mapigo yake ya moyo yalikuwa yakidunda kwa kasi sana , kwani mpaka hapo aliaminni kuwa siri yake ya kuwa na muonekano feki ishajulikana kwa mlimbwende huyo ..
*****
Kitendo cha kontena lao lililokuwa limejaa madawa ya kulevya kuharibiwa kilimkasirsisha sana kimbona , hakuamini akama amepoteza mabilioni ya pesa kwa siku moja , jambo hilo kwake lilimuuma sana , alijiapiza lazima amfundishe adabu mtu ambae kahusika kwenye swala hilo , lakini swala hilo halikuwa kwake tu pia hata kwa sam kwakuwa alikuwa moja ya washirika wa mzigo huo uliopotea jambo hilo liliwauma sana , walikaa wakajadiliana ni kwa namna gani wanaweza kumdaka mtu ambae amehusika katika jambo hilo .
“ mimi nishampa kazi hio carlos cardosso aifanyie kazi “.
‘ unaamini ataliweza hilo swala ?”
“ lazima ataliweza , kumbuka yule ni mtu hatari na mpaka sasa ashagundua baadhi ya watu waliohusika katika hilo na yupo kwenye hatua za mwisho kulikamilisha “
“ ni watu gani ?”
“ huwezi kuamini kama watu waliohusika ni panya wadogo wadogo tu ndio waliosababisha sisi kupoteza kiasi chote hicho cha pesa “
“ unamaanisha nini kusema panya wadogo wadogo “.
Wakati huo walikuwa wakifanyamaongezi yao ndani ya ofisi ya kimbona iliokuwa ndani ya kampuni yake ndani ya jengo la LAPF commercial tower , kimbona alivuta droo yake na kisha alitoa picha na kumpa sam .picha hizo zilikuwa zikimuonesha abasi pamoja na janeth .
“unamaanisha hawa ndio waliohusika kuteketeza mzigo wetu ?”
“ ndio hao ndio waliohusika na kiongozi wao ni huyo mwanadada , anafahamika kwa jina la janeth bendera “
“ janeth bendera ?”
“ ndio janeth bendera , inaonesha hata wewe umeshitushwa na jina hilo , na hata mimi pia limenishitusha pia “
“ huyu janeth ni nani na kwanini ahusike na swala la kuchoma bidhaa yetu “.
“ hilo ni swala ambalo mpaka sasa carlos analifanyia kazi muda mfupi atakuwa na majibu kamili , kwni kuna hisia zinaniambia kuwa huyo ni mtoto wa bendera , swala hilo linanichanganya kidogo bendera hana mtoto mzuri kama huyo “
“ ni kweli , pia watoto wake wote si wanajulikana , lakini nadhani ni swala la kusubiria majibu kutoka kwa carloos tuone anatuambia nini “
“ kweli kabisa , lakini kuna lingine kubwa “
“ lipi hilo “
“ elimu yake imenishangaza “
“ kwanini elimu yake ikushangaze kimbona “
“huyo mwanadada ni phd holder “
“ acha utani kimbona , inawezekana vipi mtu awe na phd mdogo hivi “
“ ndio nakwambia sasa tena ya mambo ya teknolojia “
“ acha utani kasomea chuo gani ?”
“ kasomea boston university shahada yake ya kwanza na masters , phd kapatia chuo kikuu cha Tsinghua kilichopo Beijing china “ aliongea kimbona na kumkabidhi karatasi iliokuwa ikionesha taarifa ya mwanadada janeth , lilikuwa jambo ambalo kwa sam lilimshangaza mno, hakuamini kabisa.
“naiskia leo katambusihwa kama mfanya kazi ndani ya kampuni ya NLT “
“ unamaanisha ile kampuni ambayo ni ya bwana stephano lamberk “
“ ndio “
“ sasa kwanini mtu mkubwa kama huyu na phd yake akafanye kazi katika kampuni ndogo ambayo inaanza ?”
“ hilo ndio swali ambalo pia mpaka sasa linanishangaza , jana nimejaribu kuongea na mheshimiwa raisi , kaniambia swala la stephano lamberk lipo chini ya usalama wa taifa wanalifatilia kwa ukaribu ili wapate kuujhua undani wa bwana huyo “.
“ kimbona nadhani sasa ni wakati wakuwa makini sana kwani mpaka sasa mambo yanayo endelea hapa nchini yanaanza kuniogopesha “
“ kwanini unangea hivyo “.
“ hebu jaribu kufikiria matukio yaliotokea hivi karibuni , kuanzia mheshimiwa raisi ashambuliwe kule hotelini mpaka sasa , kuna mambo ambayo yaendelea hapa nchini ambayo sisi wenyewe hatujui”
“unayoyasema ni kweli sam , hata mimi nikijaribu kuunganisha matukio naona kabisa ni kweli kabisa kuna mambo ambayo yanaendelea hapa nchini ambayo hatuna ufahamu nayo , lakini hujaniambia swala la damiani limeishia wapi “
“ hilo ndio swala ambalo nalifanyia kazi , na mpaka sasa ndani ya U-97 kuna mpelelezi wa kimataifa analifanyia kazi “.
“unaamini anaiweza kazi ?”
“ kimbona ulifikiri nawapa kazi kama hao vijana wako , huyu kwa taarifa nilizo nazo ni kwamba ni jasusi wa CIA ambae yupo chini ya U-97”
“kwa sasa yupo wapi “
“ alikuwa nchini china akiendelea kufatilia hatua kwa hatua kuhakikisha anajua sehemu aliopo damiani , lakini ninavyo zungumza sasa yupo kwenye ndege anakuja Tanzania kwa ajili ya kuendelea na uchunguzi , na nataka pia nimpe na kazi ya kujua ni nini kinaendelea hapa nchini “ aliongea sam
“ ni nani huyo lakini ?”
“ anaitwa marie , ndio niliempa kazi kwa mara ya kwanza na akampata damiani nchini thailland “
“kama ataiweza kazi mimi naunga mkono hoja , ila kwa sasa nataka nimkamate huyu janeth , kwani naamini kuna mtu yupo nyyuma yake nikishampata nitampa mateso mpaka ataje ni nani anamfanyia kazi “
“ hata mimi naona kabisa kuna watu wanafanya kazi na yeye na huwenda ni kazi aliopewa kuifanya , inaidi tumkamate “
“lakini kazi hio atafanya nani”
“ carlos naamini anaiweza hio kazi , ngoja kwanza aniletee taarifa kamil ndio nimpe kazi “ aliongea kimbona na kisha aliagana na sam .
ITAENDELEA
SEHEMU YA 41
Suzzane hakutaka kukurupuka katika kufanya kazi yake , alikuwa na kazi mbili za kufanya kwa wakati huo ili kujua ukweli anaotaka kuujua , mtu wa kwanza aliekuwa akimfatilia , alikuwa ni janeth , na wa pili alikuwa ni stephano lamberk alikuwa makini kweli na kazi yake hakutaka kabisa kuwapa nafasi watu anaowafatilia wajue kama wanafatiliwa , na ndio maana alikuwa akitumia akili sana katika kuwafatiilia , hata ile alipogundua kuwa kuna uhusiano kati ya mke wa raisi na janeth hakutaka kumwambia mheshimiwa raisi , kwani aliona kabisa anapaswa kujua kabisa kile kinacho endelea na ndipo atoe taarfa hio kwa mkuu wake .
Siku hio ilikuwa ulikuwa ni muda wa saa mbili kamili akiwa ametoka kwenye mihangaiko yake ya kiuchunguzi , alikuwa amekaa mezani akijaribu kuunganisha matukio.
Jina la janeth bendera na jina la stephano lamberk ni majina ambayo yalikuwa kwenye akili yake .alikuwa na picha zilizokuwa zikiwaonesha wawili hao kuchekeana kabisa , picha alizochukua siku hio mchana ndani ya makao makuu ya kampuni ya NLT .
Alikuwa akiangalia picha ya stephano akiwa ameshikana mkono na janeth , na muda huo walionekana walikuwa wakiagana , tabasamu lililokuwepo kwenye uso wa janeth na pia kwenye uso wa bwana stephano lamberk vilimfanya aje na hitimisho kuwa wawili hao walikuwa wanafahamiana .
Lakini jambo la pili lililomchanganya ni jina la janeth “janeth bendera ‘ ni jina ambalo lilimchangaya sana , kilicho mchanganya Zaidi ni mwanadada huyo kuwa na elimu kubwa mno tena akiwa na umri mdogo , hakuamini kwamba mwanadada huyo ni kweli alikuwa na PHD kwa umri aliokuwa nao , jambo hilo kwake pia lilikuwa likimpa maswali mengi ambayo kuna muda yalikuwa yakigongana .
“ kama janeth ana PHD inawezekana pia alienda kwenye kampuni ya NLT kwa ajili ya biashara kwani wote wapo kwenye fani moja , lakini pia nina hisia wawili hawa wanaonekana kufahamiana kwa muda mrefu japo ni hisia zangu lakini naamini uwezekano huo upo , na kama watakuwa washakutana kabla kuna uwezekano pia wakawa wanashirikiana pia katika maswala mengine , ikiwemo la janeth kuchoma madawa ya kimbona , lakini bado kuna jambo linanichanganya na natakiwa kulifania uchunguzi , inawezekanaje huyu anae jiita mzalendo kutumia sura za watu wengine katika matukio yake ya nyuma , inatakiwa ni ujue ukweli lakini ukweli nitaujua vipi ?” hayo yote yalikuwa ni mawazo ya mwanadada suzzane , jasusi mbobezi aliekuwa akimtii sana mheshimiwa raisi katika kazi zake nyingi .
*****
Ni siku ambayo ndani ya kampuni ya NLT kulikuwa na kikao cha wakurugenzi wa bodi , yaani wale wamiliki wate wa kampuni walikuwa wapo kwa ajili ya kujadiliana mustakabali wa kampuni hio mpya tanzania katika maswala ya teknolojia kwa ujumla wake.
Kwa damiani hata yeye pia alifurahishwa sana na muamko wa watanzania , kwani kitendo cha kutangaza kuuza hisa asilimia ishirini na hisa hizo kununuliwa zote , aliamini sana watanzania wanaipenda teknolojia na wapo tayari kwa ajili ya kuona taifa lao likiwa linaendelea katika swala zima la teknolojia
Siku hio mda wa asubuhi ndio muda ya watu mbali mbali waliokuwa ni wamiliki wa hisa za kampuni ya NLT waliingia ndani ya ukumbi wa mikutano ndani ya jengo hilo la NLT , moja ya watu waliongia eneo hilo alikuwa ni Patrick mtoto wa mheshimiwa raisi .
Patrick alikuwa ni mmoja ya mmiliki wa hisa katika kampuni hio na haikueleweka kwanini alivutiwa na kampuni hio mpaka kununua hisa , kwani hata yeye pia alikuwa ni moja ya watu waliokuwa wamkimiliki kampuni inayo endana na hio ya NLT lakini pia alikuwa ni adui mkubwa wa kampuni hio .
Kilichomshangaza Patrick ni mara baada ya kuingia ndani ya ukumbi wa mikutano ni kumuona merina , hakujua kuwa na merina alikuwa ni mmiliki wa asilimia kadhaa ndani ya kampuni hio sio kwake tu lakini pia kwa merina pia alishangazwa na uwepo wa Patrick ndani ya ukumbi huo kwani pia hata yeye hakujua kuwa patrick alikuwa mmiliki wa hisa ndani ya kampuni hio .
Nusu saa baada ya watu wote kuingia ndani ya ukumbi huo , akiwemo janeth , na mainjinia wengine , rebbecca , luang shu hakuwepo kwani alikuwa tayari amekwisha rudi nchi kwao china .
Basi damiani aliingia huku akiwa amevalia suti yake safi kabisa ya bei mbaya , alikwenda moja kwa moja kuketi katika kiti chake maaulumu kama kurugenzi wa kampuni hio , lakini pia kama mmiliki wa kampuni kwani yeye ndie aliekuwa anahisia nyingi katika kampuni hio ( major share holder ).
Damianni ama stephano na yeye pia alijikuta akishangazwa na uwepo wa merina ndani ya eneo hilo , alikuwa akimjua merina kama mteja wake , lakini hakujua kuwa mwanadada huyo alikuwa amekwisha kununua hisa katika kampuni yake , alijikuta moyo wake ukifurahi , hali ambayo hata yeye hakujua kwanini alikuwa akifurahi , aligeuza upande wa janeth na wakagongana macho na kila mmoja alitabasamu .
Basi kikao icho kilianza kwa kutambulisha watu mbali mbali waliokuwa wakimiliki hisa zao kwa asilimia zao na Patrick alikuwa akimiliki asilimia kumi na merina pia alikuwa akimiliki asilimia kumi , pia kikao kiliambatana na moja ya malengo ya kampuni siku za usoni .
MASAA MACHACHE NYUMA .
Kitendo cha stephano kuitwa jina lake halisi na mrembo janeth kilimchanganya na kumshitua kwa wakati mmoja , hakujua ni kwa namna gani mrembo huyo alimjua , japo alikuwa akikumbuka kuwa mrembo huyo kuna sehemu ashawahi kukutana nae , lakini swala la kumjua kuwa amevaa ngozi feki lilimchanganya .
“ usiwe na waswasi siri yako ipo salama “ aliongea janeth kwa mapozi .
“ wewe ni nani ?”
“ mimi ni janeth mfanyakazi wako “ aliongea janeth kwa mapozi huku akizunguka ndani ya ofisi hio kama mtu aliekuwa akiichunguza na alionekana alikuwa akijiamiani sana mbele ya damiani .
Stephano japo mwanadada huyo alikuwa ameonesha kujua siri yake lakini hakutaka kabisa kuwa mwepesi aliweka ngumu
“ sijui unacho ongea kuhusu siri “
“ hahahaha… kwa hio unamaanisha ninayo ongea hapa ni uongo “
“ ndio ni uongo , inakuwaje unaniita jina ambalo sio la kwangu na huyo damiani ni nani ?”
“ damiani ni jina lako halisi nakujua A to Z najua unaweza ukawa umenisahau , au unataka nikukumbushe tulipokutana mara ya kwanza “.
“ sijawahi kukutana na wewe mimi “ aliongea stephano kwa kujiamini huku akiangalia tarakishi yake “
“ naona umesahau siku ile ulivyogongana na mimi ndani ya hoteli ya four season china wakati unaenda kuonana na waziri wa china “
Hapo ndipo stephano alipokumbuka sehemu aliokutana na mwanadada huyo , alijikuta akijilaumu kwa kutomkumbuka mapema , alimkumbuka mwanadada huo alipogongana nae wakati anaingia kwenye lift .
“ naona umenikumbuka sasa “
“ janeth nina kazi kwasasa naomba tuishie hapa kwa leo “ aliongea stephano kwa sauti ambayo ilionesha kuwa na waswasi ndani yake .
“ usijali damiani , kwanza unaelewa kuwa hio ngozi ndio mimi nilioitengeneza , au luang shu hajakwambia “
Kauli hio ndio iliomfanya stephano kushangaa Zaidi , na hapo hakuwa na ujanja kabisa , mpaka hapo alijikuta akikumbuka kauli ya luang shu kumwambia kuwa mtu alieitengeneza FULL BODY MASK alikuwa ni mtanzania mwenye phd yake , mpaka hapo alijua kuwa mtu aliekuwa akiongea nae alikuwa akimjua vyema .
“ wewe ndio uliotengeneza full body mask “.
“ ndio ni mimi damiani “ aliongea janeth huku akikaa kwenye sofa huku akimwangalia damiani akiwa ameachia tabasamu
“ ila sikujua kuwa unatumia jina la stephano lamberk mpaka nilipo kuona , nikajua umevaa ngozi bandia “
“ sina hoja , ila nasema hongera sana “
“ asante damiani , ila nilikuwa nikikutafuta sana tokea siku ile ulionigonga “
“ ulikuwa ukinitafuta!! , kwa ajili ya nini ulikua ukinitafuta ?”
“ nitakuambia siku nyingine damiani , kwasasa kuna majukumu yangu nataka kwenda kuyashughulikia lakini nisindikize basi “ aliongea mrembo huyo na kisha damiani alinyanyuka na kutoka na janeth mpaka eneo la kupark magari na walipeana mkono kwa bashasha kubwa , na wakati wanapeana mkono ndio wakati ambao suzzane alikuwa akiwapiga picha .
*****
Mheshimiwa raisi japo swala la uwekezaji wa Stephano lamberk lilikuwa swala lenye tija kwa nchi , lakini kwake aliliona wala hilo kama mwiba katika maendeleo yake mwenyewe , alijua kuwa kampuni ya INNOVA na kampuni ya NLT kuingia nchini na kuwekeza inamaanisha yeye kampuni yake kufa kabisa , kwani aliamini asingeweza kabisa kushindana na INNOVA na NLT, alikuwa akiwaza mambo kadha wa kadha ni kwa namna gani angeishi pasipo kupata hasara Zaidi . mchaga huyu japo ya kuwa raisi lakini alikuwa akipenda pesa pia , na ndio maana alikuwa tayari kufanya lolote kwa ajili ya kujiingizia pesa .
Siku hio ni baada ya kuonana na bwana stephano na kufanya mazungumzo nae , alikuwa ameshikilia karatasi ya asilimia za hisa ambazo zilikuwa zikiuzwa na kampuni hio ya NLT alikuwa amekaa chini akiwaza ni maamuzi gani afanye , lakini pia upande wa pili pia alikuwa akiwazia uwekezaji wa kampuni ya INNOVA ambayo pia ilikuwa ikiuza asilimia za hisa zao .
Baada ya kuwaza muda wa masaa kadhaa , ndipo alipokuja kufanya maamuzi ya kununua hisa katika makampuni hayo yote mawili kwa wakati mmoja , alitoa simu yake na kupiga mahali .
“ nataka kununua hisa zote za kampuni ya NLT na INNOVA “ aliongea mheshimiwa .
“ mheshimiwa hisa zilizobaki ni asilimia kumi tu kwa kampuni zote mbili “”
“ hizo zingine zimeenda wapi “
“ zimekwisha kununuliwa na SWIFT TRANSIT “
“ okey sawa nitanunua hizo zilizobaki nafanya muamala sasa “ aliongea na kisha alikata simu .
“ huyu ni merina mchumba wake Patrick huyu , mwanamke anaakili sana huyu sijui Patrick anakwama wapi kumuoa huyu mwanamke , inabidi nimuite nifanye nae mazungumzo “ alijifikiria huku akiendelea kuchezesha simu yake , na dakika kadhaa alikuwa ashanunua hisa zote .
Mara baada ya kufanikisha hilo ndipo alipoendelea na majukumu yake , mpaka muda wa kutoka ofisini.
Lakini kabla ya kutoka aliingia kijana wake ambae alikuwa akimfanyia baadhi ya shughuli zake binafsi , kijana huyu aikuwa akijulikana kwa jina la talimba , alikuwa ni kijana msomi mno aliekuwa ni mwanausalama kitengo cha ikulu , na moja ya kazi kubwa ambayo alikuwa amempa kijana huyu kuifanya ni kumfatilia mke wake , kwani mheshimiwa raisi japo alikuwa akimpenda sana mke wake lakini hakuwa akimuamini hata kidogo , haikujulikana ni sababu gani hakuwa akimuamini mke wake
“ vipi talimba kuna habari yoyote “
“ ndio muheshimiwa na ndio maana niko hapa “ aliongea talimba , alikuwa ni kijana mojamfupi maji ya kunde mwenye macho makubwa hivi na mwili wake mnene kiasi .
Muda huo mheshimiwa alikuwa amesimama nje ya ofisi na alikuwa akitaka kuelekea upande wa familia yake , lakini ilibidi aghaili na kurudi ndani ya ofisi kuongea na talimba , kwani alijua kabisa kila talimba anapofika anayo taarifa , basi jua ni taarifa ya siri ambayo hakutaka mtu oyote yule ndani ya ikulu aifahamu
“ mheshimiwa madam siku mbili zilizopita kakutana na mwanadada anaefahamika kwa jina la janeth bendera muda wa jioni maeneo ya ununio ndani ya nyumba moja ambayo kwa kufatilia niligundua kuwa inamilikiwa na msichana huyo , pia siku ya jana yake alikutana na mwanadada merina muda wa saa kumi kamili ndani ya hoteli ya serena “
‘’umesema janeth , huyo janeth ni nani “
“ janeth kwa taarifa nilizo nazo ni mwanasayansi aliengia nchini miezi kadhaa iliopita akitokea china , kiwango cha elimu yake ni PHD “”alijjibu talimba na kumfanya bendera ashangae na awaze kidogo na majina hayo mawili yalipita ndani ya kichwa chake yaani ‘merina na janeth’.
“ safi endelea kuwafatiilia na unipe taarifa Zaidi “
“ sawa muheshimiwa “
Baada ya mheshimiwa kupewa taarifa hio na talimba alitoka ofisini na kwenda upande wa familia yake na kuonana na mke wake aliekuwepo sebleni akiangalia tamthilia , wema mara baada ya kumuona mme wake , aliinuka na kumkumbatia
Mheshimiwa alioga na kisha alimua kupumzika huku akijaribu kuwaza jambo la mke wake kukutana na merina na janeth hakujua ni kwanini wamekutana ila aliamini kama kuna mpango unaendelea ambao yeye haujui basi angeujua tu , muda wa saa mbili kwenda tatu ndipo alipo mkumbuka patrick na kumpigia simu na kumpa maagizo ya kufika ikulu siku inayo fata .
Ilikuwa siku nyingine siku ya asubuhi na mapema ndio siku Patrick alifika kwa ajili ya kuonana na baba yake na walianza mazungumzo
“ kesho nataka ukahudhurie kikao cha wana hisa ndani ya kampuni ya NLT , nimenunua hisa asilimia kumi ndani ya kampuni ile japo nilihitaji kununua zote ila inaonekana mkwe kanizidi ujanja “
“ mkwe gani baba “
“ si merina au kuna mwingine ?”
“ inamaana merina kanunua hisa kwenye kampuni ya NLT “
“ ndio , inakuwaje merina ni mpenzi wako na hujui hilo “
“ baba mimi na merina hatuzungumzi sana maswala ya kazi “
“ anhaa sawa .. ila patrIck kuna kitu sikielewi , hivi unaamini kweli yule mwanamke anakupenda ?”
“ baba hata mimi mpaka wakati huu nachanganyikiwa kabisa , nampenda sana merina , lakini merina kuna mtu anampenda “
“ kuna mtu anampenda , unamaanisha sio wewe “
“ ndio baba kuna kijana mmoja anafahamika kwa jina la damiani , ndio merina anampenda lakini mpaka sasa kijana huyo hajawahi kuonekana tokea atekwe”
“ unasema damiani?? “
“ ndio mbona umeshituka unamfahamu ??“
“ hapana lakini ni kama nishawahi kulisikia hilo jina “
‘ yawezekana baba kwani ni moja ya watu waliokuwa wakihusiana na bruno , kwani mama yake alipigwa risasi na mahasimu wa bruno “
“ kwa hio unamaanisha merina na damiani wanafahamiana , na walifahamiana vipi ?”
“ hata mimi swala hilo linanichanganya , sijui wapi walikutana ila najua wanafahamiana kwani merina alilia sana siku ambayo alitekwa “ aliongea Patrick huku akimuhadithia baba yake tukio la damiani kutekwa ndani ya hosputali ya lushoto “
“kweli inaonekana wanafahamiana , sasa unamaamuzi gani juu ya merina maana hata mimi nimetokea kumpenda yule mwanamke , ana akili sana za kimaisha na kama atakuwa mke wako atakusaidia sana “
“ baba hata mimi mpaka sasa sijui nifanyeje kumteka merina kihisia kwani nampenda sana “
“ hahaha kijana wangu wanawake ni viumbe dhaifu sana , hakikisha merina anakuwa mke wako , usikubali mtu mwingine akimchukua kutoka kwako “ aliongea raisi na kumfanya Patrick atabasamu .
“ baba umenitia nguvu sana , na mimi lazima merina awe mke wangu sitoruhusu mtu yoyote amchukue “
“ safi sana kijana wangu , pia hakikisha bishara zinaenda vizuri “
‘ sawa baba “
Itaendelea