Ujasusi - Umoja namba 97

KAULI YA MWISHO YA RAISI KABLA YA KIFO
U-97
MTUNZI :SIMGANOJR

SEHEMU YA 21
MAWASILIANO 0687151346



ILIPOISHIA
“ luang shu ???,kama ni mtoto wa waziri itakuwa ngumu kumzuia kufanya biashara hapa nchini “.
“ ni kweli kabisa , lakini swala kubwa Zaidi ni kwamba kiwanda anachotaka kutumia na ambacho amepewa ni cha marehemu bruno lamberk kutoka kurasini na kasema ana nyaraka zte zinazomuwezesha kukichukua kiwanda hicho na kukiendeleza kihalali katika kusuka mitambo yake ya 5G.
“unataka kusema nini kiwanda hiki si kilikuwa kipo chini ya mahakama mpaka pale mwenyewe atakapo tokea inakiuwaje akawa na nyaraka hizo ?”.
“ hilo ndio swala ambalo mpaka sasa sijajua , ila kwa taarifa nilionayo nikwamba kapitia vipengele vyte vya sheria na mahakama nidio ilioidhinisha kwa bwana luang shu kutumia kiwanda hicho “.
Patrick alijikuta akitetemeka kwani swala hilo hakulitegemea kabisa , kiwanda hicho alikuwa akikitegemea mno na aliamini katika kukitumia kiwanda hicho angeweza kupata siri zote za kitechnolojia zilizokuwa zikitumiwa na bwana bruno , hivyo alimuomba baba yake amuwezeshe kutumia kiwanda hicho lakini jibu alilopewa ilikuwa ni kusubiri mchakato wa mahakama uishe, sasa leo hii anasikia kuwa kiwanda kishamilikishwa kihalali kwa mtu mwingine .
“f***ckk , ngoja niongee na baba huenda hajui swala hili “ aliongea Patrick huku akionesha kuwa na hasira sana na swala hilo kwani alikuwa ameguswa penyewe

INAENDELEA SEHEMU YA 21.
WIKI MOJA NYUMA
Ndani ya uwanja wa kimataifa wa mwalimu nyerere ilitua ndege ya shirika la ATCL na moja ya abiria alietoka katika ndege hio alikuwa ni bwana mmoja hivi aliekuwa kijana kabisa kwani mwili wake haukuwa mnene wala mwembaba ila bwana huyu alionekana kuwa ni mtu anaefanya mazoezi , bwana huyu baada ya kukaguliwa na kuonyesha passport yake alitoka mpaka sehemu ya kuchukulia mizigo na alichukua begi lake na kutoka kabisa nje ya uwanja , huyu bwana alikuwa ni mchina kabisa kwani rangi yake na hata sura yake na ongea yake ilikuwa ikifanana kabisa za wachina .
Baada ya kutoka kabisa nje ya uwanja aliona mwanamama mmoja mweupe alievalia wigi mweupe, umri wake ulikuwa ni makadirio ya miaka 40 kwenda 5 hivi .
“ miss Rebecca “ alitamka bwana huyu maneno hayo kwa lafudhi yake ya kichina .
“ luang shu you are welcome in Tanzania , I think its your first time in this country “
“ karibu sana Tanzania nafikiri ni mara yako ya kwanza kufika katika taifa hili “
“its true rebbecca and just by looking I can tell Tanzania is a very beutifull nation .”
“ ni kweli Rebecca lakini kwa kuangalia tu naweza sema Tanzania ni moja ya mataifa mazuri sana “. Rebecca alimuongoza bwana huyu mpaka kufikia kwenye gari moja aina ya AUD A3 SEDANI ilioneka imetumika lakini uzuri wake haukupotea .
“ baada ya kutoka pale bwana huyu alipelekwa moja kwa moja mpaka hoteli ya golden tulip iliokuwa ikipatikana msasani pembeni ya barabara ya seokoe toure drive , basi gari ile iliingizwa kwenye moja ya maegesho yaliokuwepo ndani ya hoteli hio na Rebecca alitoa begi la bwana luang shu na kisha waliongozana kuingia ndani ya hoteli hio .
Rebecca alienda mpaka mapokezi na kisha alichukua kadi kwani tayari alikuwa ashabook chumba , na waliongozana na bwana huyo mpaka kwenye chumba chake na wote waliingia ndani .
“ thank you rebbecca “ aliongea luang shu .
“ “ I think now you have to rest , tomorrow I will come with a lawyer for the purpose of reviewing the contract and steps to take to get the factory “.
“ Nafikiri unapaswa kupumzika sasa , kesho nitakuja na mwanasheria kwa ajili ya kupitia mkataba na hatua za kuchukua kupata kiwanda “
“Okey rebbecca”
Kesho yake ilivyofika rebbecca alifika hotelini hapo akiwa ametangilizana na bwana mmoja ambae alikuwa na ndevu nyingi huku mkononi akiwa amebeba briefcase , , walipita mapokezi na moja kwa moja walifika kwenye chumba cha luang shu na kugonga na bwana huyu alionekana alikuwa tayari ashaamka kwani alikuwa amebadilisha mavazi tayari na kuwa nadhifu .
“ hellow Rebecca morning “ aliongea luang shun a kuwakaribisha .
“ luang shu as I saidi yerstarday I wiil bring lawyer , this is mr juma bakari he is lawyer , juma this is luang shu son of the chinese interior minister and he is here for investing in telecommunication business but as I mentioned , years ago they signed a contract with bruno lamberk for the purchase of an existing factory in kurasini .
“ luang shu kama nilivyokuambia jana kwamba nitamleta mwanasheria , huyu ni bwana juma bakari ni mwanasheria , juma huyu ni luang shu mtoto wa waziri wa mambo ya ndani wa china yupo nchini kwa ajili ya kuwekeza katika maswala ya biashara ya mawasiliano , na kama nilivyosema kwamba kampuni ya luang shu nchini china walisaini mkataba na bruno lamberk ili kununua kiwanda kilichopo kurasini .
Basi walisalimiana na kisha bwana juma alipewa ule mkataba na aliupitia kwa umakini kubwa kwa kila kipengele .
“ hati inayo onyesha malipo yamekwisha fanyika iko wapi ?” aliuliza juma na luang shu alitoa hati ile na kumuoesha .
“ okey kwa ushahidi huu ni sawa kabisa kusema wewe ni mmiliki halali wa kiwanda kilichopo kurasini , lakini kwakuwa mali za bwana bruno mpaka sasa zipo chini ya serikali na mahakama basi kuna hatua ambazo nitapitia ili kuhakikisha unapata haki yako “ aliongea juma na kisha waliagana
Siku mbili mbele bwana luang shu alikabidhiwa rasmi kiwanda kilichopo kurasini , kiwanda ambacho kilikuwa kikihusika na utengenezaji wa vifaa vya electronics , na baada ya kupewa kiwanda hichi bwana luang sh alifata taratibu zote za kiwizara pamoja na kubadilisha jina la kiwanda hicho na kuweka wazi anataka kufanya biashara gani .
Mwana mama aziza kibwetere waziri wa viwanda alitia saini karatasi zilizowasilishwa ofisini hapo na luang shu , pamoja na Rebecca .
*****
Mara baada ya suzzane kutoka kituo cha magogoni moja kwa moja alienda mpaka ikulu na kuomba kuonana na muheshimiwa na aliruhusiwa na kuingia .
“vipi suzzane ??.
“ mheshimiwa ridhiwani kwa maelezo yake inaonekana hahusiki kabisa na kile kilichotokea pale serena ,lakini kwa maeneo aliokuwepo yananipa shaka “
“ unamaanisha nini suzzane kusema maeneo aliokuewepo , kwani ni maeneo gani aliokuwepo ?”
“ kwa maelezo ni kwamba muda wa saa moja alikuwa ndani ya U-97 cassino “ aliongea .
“ ndio kama alikuwa kwenye U 97 ulikuwa wataka kumaanisha nini hapo mpaka upatwe na shaka? “.
“ mkuu jambo ninaloliwaza, nataka kwanza kulifanyia uchunguzi nione kama ni kweli hisia zangu zipo sahihi na ndipo nitakuja kuekueleza kwa undani , lakini kama unavyo jua kuwa hatuna mamlaka ya kufanya upekuzi ndani ya U-97 swala hili linakuwa gumu kwangu , hivyo kwa ruhusa yako nataka nipate kibali cha kuingia ndani ya U- 97 CASSINO “ aliongea suzzane
“una uhakika jambo unalotaka kufanya, je litatupeleka mpaka kujua ni nani muhusika ?”
“ ndio muheshmiwa I m positive about it “
“ okey unaweza kwenda nitawasiliana na meneja wa casino na akuruhusu lakini hakikisha hakuna kibaya kinacho tokea kwenye ile casino kwani its beyond my reach “.
“ sawa mheshimiwa “ aliongea suzzane na kisha aliingia kwenye gari yake aina ya brevis na kisha alitoweka ikulu na kuelekea upanga ambako U-97 cassino ilikuwa ikipatikana , muda huo ilikuwa ni saa nane mchaana wakati akiingia eneo la casino hio , alienda mpaka mlangoni na kujitambulisha kisha aliruhusiwa kuingia .
Ebwana eeh kuna watu walikuwa wanafanya dhambi , kilichokuwa kinafanyika ndani ya casino hio ilikuwa sio mchezo , kulikuwa na kila aina ya ufuska , wadada mbali mbali walikuwa wakitembea uchi wengine walikuwa wakinyonya ‘rungu’ , kuna waliokuwa wakicheza Kamari , lakini ndani pia ya casino hilii kulikuwa na ofisi na zilionesha hizo ofisi zilikuwa zikitumika kwa ajili ya kazi za kutia mikataba , kwa wale waliokuwa wakicheza Kamari mezani kulikuwa na pakti za madawa ya kulevya , mwanga uliokuwa humo ndani haukuwa tofauti na usiku , kwani ulikuwa na giza na mwanga wa taa za kuvutia za rangi , suzzane hakuwa mgeni sana ndani ya casino hii
“ nahitaji kuonana na muongoza camera wa hapa ndani “ aliongea suzzane akimwambia meneja wa casino bwana mmoja alivalia kipensi huku akiwa ameshhikilai sigara yake kubwa aina vasobranie black russians, ilikuwa ni moja ya sigara ghali sana .
Meneja yule kwa ishara alimruhusu suzzane na kwenda upande wa camera .
“ nahitaji matukio ya jumapili kwanzia muda wa saa kumi na moja jioni “ aliongea suzzane na kuonyeswa na vijana hao wa IT , alianza kuangalia watu waliokuwa wakiingia ndani ya casino hilo , alijikuta akitabasamu baad aya kuona sura aliokuwa akiitafuta , sura hii ilikuwa ni ya ridhiwani na hata miondoko yake ilikuwa ni ya kijana ridhiwani na alionekana aliingia hapo casino saa kumi na mbili kama na nusu hivi , suzzane aliendelea kuangalia baadhi ya picha na hapo kuna sura ilimvutia Zaidi aliomba waikuze , hii ilikuwa ni ya mwanaume aligongana nae ndani ya hoteli ya serena usiku wa jana yake jumapili na hata kumjibu vibaya na mtu huyu alionekana aliingia ndani ya casino hilo kwenye muda wa saa kumi na moja za jioni .
“ rudisha , peleka mbele kidogo , kuza hio picha “ aliongea suzzane na alifanyiwa kama alivyo elekezwa na hapo ndipo alipo tabasamu kwani aliona kuna mwanga., alikuwa ni ridhiwani akitoka , lakini ridhiwani huyu alikuwa akitofautiana na ridhiwani alieingia , alimuona bwana huyu akiingia kwenye gari aina ya crown yenye namba XXX za gari na ikaondoka eneo hilo .
“ alingalia watu waliotoka saa nne kamili usiku , hapo ndipo alipomshuhudia ridhiwani akitoka na mwanadada na kuondoka eneo hilo na huyu alikuwa ni ridhiwani mwenyewe “.
Aliendelea kutafuta karibia camera zote lakini kuna sura aliona mara moja tu ikiingia lakini sura hio haikutoka kabisa , huyu alikuwa ni mwanaume aliekutana nae serena hoteli .
“ okey asanteni nilichokuwa nikikitafuta nimekipata “ aliongea na kisha kuondoka .
“ yule mwanume mweusi aliekuwa akinisemesha ndio kahusika lazima , lakini nawezekanaje akawa na sura ya ridhiwani , nitajua baada ya kumtia mikononi yule “ aliongea suzzane na kisha akawasha gari lake na kwenda mpaka serena , alisimamisha gari na kisha alienda hadi mapokezi na kutaja shida yake
“ kama aliingia ndani ya ile casino na hakuonekana kutoka basi anaweza akawa ni huyo alietoka na sura ya ridhiwani , japo sijui kama jambo hili linawezekana lakini hsia zangu zinaniambia hivyo “ aliwaza muda huo akifika mapokezi .
“ nataka taarifa za mgeni chumba namba 85 aliongea suzzane na kisha bwana mmnoja wa kiume aliekuwa hapo mapokezi alitaka agome , lakini baada ya kuoneshwa kitambulisho alifanya kazi hio .
“ jina lake ni DAMIANI RABANI “.
“ DAMIANI RABANI “ aliongea suzzane na kumfanya apatwe na mshangao ,
“ nataka kwenda kwenye chumba chake, ashaondoka au yupo??”
“ taarifa hapa zinaonesha hajarudisha chumba “ aliongea kijana yule na suzzane aliomba kadi ya ziada na akapewa na kisha alielekea mpaka kwenye kile chumba , baada ya kufika kwenye mlango wa kile chumba alitoa siraha yake na akagonga mlango , lakini hakukua na majibu , alichokifanya ni kuweka ile kadi na kisha akafungua mlango na kwa tahadhari ya hali ya juu alijirusha ndani , alkini alikutana na chumba kikimchekea , kwani hakukuwa na mtu , lakini kwenye kijimeza kulikuwa na box lililotengenezwa na karatasi , aliliangalia , lakini hisia zilimwambia kulikuwa na mtu bafuni , alienda kwa tahadhari ya hali ya juu na kufungua mlango , lakini holla .
Chumba hakikuwa na mtu kabisa . alienda mpaka kwenye meza na kuchukua lile box na kulifungua
GOOD TRY SUZZANE by mzalendo

KESHOOOOOOO........

Kesho ndo inakaribia kwisha Mzee
 
SEHEMU YA 22
Suzzane alijikuta akipagawa aliona sasa ni mchezo ambao alikuwa akichezewa tena makusudi kabisa na mtu ambae alikuwa akifanya hivyo alikuwa akimjua kila hatua anayo pitia , kwani hii ilikuwa ni mara ya pili kwa mtu huyu kumchezea akili , alijikuta akikaa kitandani huku akipumua kwa nguvu kwani kwenye maisha yake ya kazi yake hio , hakuwahi kuchezewa kama anavyo chezewa.
“ inamaana ni damiani , damiani anawezaje kuingia nchini pasipo ya sisi kujua , na inawezekana je akawa na sura tofauti au ni watu wanaotaka kunichezea akili , ila nasema hakuna atakae niweza mimi ndio miss k , watajuta kuingia kwenye himaya yangu “ aliongea huku akinyanyuka kitandani na kutoka eneo hilo , alirudi mpaka chini na kuomba tena kuangalia camera za ulinzi kama anaweza kupata jambo lolote , alikubaliwa na kupelekwa kwenye chumba cha ulinzi aliangalia lakini hakufanikiwa kupata kitu chochote kwani bwana yule ambae amejiandikisha mapokezi kwa jina la damiani rabani hakuwa ameonekana kabisa kwenye camera akitoka , jambo hilo lilimshangaza , ila aliona ni swala linalowezekana maana kama mtu huyo alikuwa na uwezo wa kufanya shambulio sehemu ambayo ilikuwa na ulinzi mkali basi kupita sehemu na camera zisimuone ilikuwa ni swala ambalo linawezekana kabisa .
Upande wa ikulu alionekana patrick akiingia ndani ya ofisi ya baba yake na alimkuta baba yake aliekuwa akitaka kutoka .
“ Patrick my son , tena bora umekuja wakati muafaka , nilikuwa nikijiandaa kwa ajili ya kwenda kumuoana yule rafiki yako alieniokoa nadhani litakuwa jambo jema kama tutaenda wote eneo hilo “ aliongea raisi .
“ baba kabla ya kwenda huko kuna jambo nataka nikueleze kwanza na ni muhimu sana kwani linahusu biashara zetu “
“ ni sawa tunaweza kuongea tukiwa kwenye gari “ aliongea mheshimiwa na Patrick alijifikiria kisha alikubali na wote wakaongozana na kuingia kwenye gari moja pamoja na muheshimiwa . na safari ya kuelekea aghakani hospital kijana sabi alipolazwa ikaanza .
“ ni jambo gani hilo unataka kuniambia ?“
“ baba si unakumbuka nilikuwambia umuhimu wa kupata kile kiwanda cha bruno kilichokuwepo kurasini “.
“ ndio nakumbuka si nilikueleza kiwanda kile kwa sasa kipo chini ya mahakama na mpaka pale tutakapo kuwa na nyaraka za kukimiliki kihalali, kwani siwezi kutoa tu kauli ya wewe kukimiliki ni swala ambalo linaweza kuniletea kashfa “.
“ ndio baba , lakini mpaka sasa ninavyo ongea kiwanda kile kipo chini ya mmiliki mwingine “.
“ unamaanisha nini kusema kipo chini ya mmiliki mwingine ?”
“ ndio kuna muwekezaji kutoka china anafahamika kwa jina la luang shu , kwa sasa ndio mmilikki halali wa kile kiwanda , na inasemekana alikuwa na nyaraka halali za kukimiliki kiwanda hicho na mahakama ishaidhinisha na anavyo vibali vyote kutoka weizara ya viwanda , mbaya Zaidi ni kwamba anataka kufunga na kudhalisha vifaaa vinavyotumia 5G ndani ya nchi yetu “ aliongea Patrick na mheshimiwa alionyesha dalili za kuwa kwenye mshituko mkubwa sana .
“ hilo swala mbona sina taarifa nalo , linawezekana vipi na huyo mwekezaji ana uhusiano gani na bruno? “
“ kwa taarifa nilizo kuwa nazo kwasasa ni kwamba mmiliki ni mtoto wa waziri wa mambo ya ndani wa china “
Mheshimiwa raisi alijikuta akifuta jasho , kwan swala hilo lilikuwa gumu kweli .
“ Patrick swala hili limenichangaya sana kwa sasa na sina taarifa nalo , nikitoka hapa nitalifatilia kwa umakini mkubwa na nione kipi kifanyike , japo swala hili litakuwa gumu sana kwani kama ulivyosema kwamba kama muwekezaji huyo ni mtoto wa waziri wa china basi swala hili litakuwa gumu , lakini nitaangalia kama nyaraka zao zilikuwa halali “ aliongea na wakati huo walikuwa tayari washafika hospitalini hapo .
“ wote walitoka kwenye gari na moja kwa moja waliongozana mpaka kwenye wodi ya VIP aliolazwa sabi na waliingia na kumkuta akiwa na simu yake na alionekana alikuwa akiperuzi , alivyoona wageni hao aliweka simu yake chini na kukaa na kutoa heshima zake zote kwa muheshimiwa .
“ bwana sabi unaendeleaje “
“ naendelea vizuri mheshimiwa kwa sasa maumivu yamepungua “.
“pole sana , na pia niseme asante kwa kitendo chako cha kishujaa ulichokifanya pale hotelini kwani isingekuwa wewe huenda nikawa marehemu kwa sasa “ .
“ mheshimiwa swala lile halikuwa kubwa sana kwangu , maisha yangu na yako uthamani wake una utofauti, wewe una makujumu makubwa sana ndani ya taifa na ndio maana sikujiuliza mara mbili mbili mara baada ya kuona ile drone ikitaka kukudhuru “ aliongea sabi kwa ujasiri na bwana henry alimuona kijana sabi kama moja ya vijana jasiri sana , maana jaribio la kutoa uhai kwa ajili yake aliona ni jambo ambalo hakujua hata baadhi ya walinzi wake wanaweza kulifanya , kuna kitu alikigundua kutoka kwa sabi , mheshimiwa alimpongeza sana sabi na kisha alimwambia siku atakayopona basi ataitwa ikulu kwa ajili ya mazungumzo na chakula
Raisi alitoka huku akimuacha Patrick na sabi .
“ unajua tukio ulilolifanya limenifanya nishangae , kwanza mpaka sasa najuliza ulifika vipi pale juu ya jukwaa maana ni kitendo cha sekunde tu , ila asante sana rafiki yangu kwa kuniokolea baba yangu maana sijui saivi ningekuwa kwenye hali gani “.
“ hahaha .. usijali bwana Patrick , kuna baadhi ya mambo bado hujayajua kuhusu mimi ila nitakueleza siku tukikaa vizuri na kupata muda “ aliongea sabi , lakini wakati wakiongea aliingia daktari na kumuomba patrick ampishe kwani anataka kufanya kazi yake .
“ sabi nitakuja kukucheki kesho “ alionga Patrick na ksiha alitoka .
“ baada ya kutoka mlango ule ulifungwa kabisa na funguo kwa ndani na kisha jamaa alievalia kidaktari alitabasamu mara baada ya kumuangalia sabi na sabi pia alitabasamu .”
“ nakuona mkubwa ushaanza kutembelewa na wakuu wa nchi “ aliongea bwana yule na kumfanya sabi atabasamu .
Allikuwa ni bwana mmoja hivi mrefu mweusi mwenye mwili wa saizi ya kati, huku makadirio ya umri wake ilikuwa ni kati ya miaka 28 hivi huku masikioni alikuwa ameweka earphone kama ipod
“ mshenzi sana wewe , kwa maumivu nilioyasikia ningejua nisengefata kabisa usharui wako “ aliongea sabi .
“ hahaha .. pole sana , sina muda wa kukaa hapa , boss kanielekeza nikuletee hii flash disk , kama alivyokupa maelekezo, nadhani kazi hio unaijua “.
“suzzane is in the parking lot “( suzzane yupo kwenye parking ya magari ) ilikuwa ni sauti iliosikika upande wa pili kupitia kijispika alichovaa sikioni na hapo hapo aliagana na sabi na kutoka
Wakati hao wanaongea ndani alinekana suzzane eneo la hospitali , na wakati anaingia eneo hilo ndio wakati ambao mheshimiwa alikuwa akitoka na msafara wa magari yake kurudi ikulu .
Suzzane alipaki gari yake vizuri eneo la maegesho na kisha alitoka na kuingia ndani ,alifika mpaka mapokezi na kuelekezwa wodi aliokuwepo sabi , alitembea kwa mwendo wa haraka haraka lakini ile anaingia katika korido ya wodi aliokuwepo sadi alijikuta akipishana na daktari mmoja ambae baada ya kukutanisha macho alitabasamu kisha akapita , suzzane na yeye alitabasamu na kisha kupita , lakini alitembea kama hatua kadhaa kuna jambo lilimtekenya akili yake maana alikuuwa hawaamini tena watu waliokuwa wakimuonesha tabasamu aligeuka na kuangalia nyuma lakini hakumuona yule daktari , kuna hisia zilimcheza ,, alirudi nyuma kwa haraka na kuchungulia kwenye korido nyingine lakini hakuweza kumuona , alijikuta akighairi na kurudi alikotoka kwan kuna jambo alilihisi limetokea katika chumba alicholazwa sabi.
“ sabi kuna daktari kaingia kwenye hiki chumba ?” aliuliza huku akiwa anathema juu juu .
“ ndio kaingia “.
“ kuna dawa kakupa?”
“ hapana kaniuliza tu maendeleo yangu na kisha kanambia atakuja tena kuniangalia siku inayofuata , kwani kuna nini suzzane ?”
“ hakuna kitu , vipi unaendeleaje lakini ?”
“ saivi niko poa kiasi maumivu nayahisi kwa mbali “ aliongea sabi huku akimwangalia suzzane ni kama alikuwa akimsanifu suzzane umbo lake na uzuri wake “. Na hata kwa suzzane alilishitukia hilo na kuona aibu .
“ nitakuja kukucheki mida kuna jambo ngona nikalifatilie “ aliongea suzzane huku akitoka na kukaribia mlango .
“ suzzane “ sabi aliita na kumfanya suzzane ageuke na kumwangalia .
“ you are so beutifull suzzane “ aliongea sabi huku akitabasamu na suzzane alitabasamu kisha alitoka , baada ya kutoka katika chumba cha alicholazwa sabi , moja kwa moja alienda mapokezi .
“ nataka kuonana na anaehusika na camera za hapa hospitalini “ aliongea suzzane huku akitoa kitambulisho chake cha kazi .
“ mdada yule wa pale mapokezi alimwangalia suzzane na kisha alimuelekeza ofisi hio inapo patikana , alienda mpaka upande wa ofisi hio na kisha aligonga na dakika moja alifunguliwa mlango .
“ karibu “ aliongea mwanaume mmoja ambae alionekana muda huo alikuwa kasinzia kwani macho yake yalionekana kuvimba
“ nahitaji kuangalia camera za ulinzi ya wodi ya VIP aliongea suzzane na bwana yule mwenye kipara alimwangalia suzzane kisha alisogelea tarakishi na kuanza kutafuta video hizo .
“ unataka ya muda gani ?”.
“ kwanzia masaa mawili yaliopita “ aliongea na bwana yule sekunde kadhaa alikuwa ashapata video hizo na kuanza kumuonesha suzzane .
Suzzane aliangalia video hizo na alimshuhudia yule daktari akiingia katika chumba cha sabi na hata alipotoka na pia alishudia wakati alivyopishana nae , hakupata jambo la maana , alienda mpaka upande mwingine wa corrido na hapo alimuona mwaume yule akiingia kwenye chumba kimoja na dakika kadhaa alitoka akiwa kavalia suti na kutokomea nje , aliomba irudishwe nyuma na kuikuza na kisha alipiga picha kwa simu yake .
“ angalia camera za nje “ aliongea suzzane ,
Camera zilionesha jamaa yule akiingia kwenye gari aina ya nissani iliokuwa kwenye maegesho tena karibu kabisa na alipopaki gari yake , alinakiri namba za gari ile na kisha alimshukuru muongoza camera na kisha alitoka mpaka nje .
Suzzane mara baada ya kutoka pale alinyoosha moja kwa moja mpaka makao makuu ya TISS , baada ya kuingia kwenye jengo hilo , aliweka kadi yake ya utambulisho na kisha mlango ulifunguka na kwenda moja kwa moja mpaka idara ya mawasiliano(IT ROOM) .
“ suzzane karibu “ aliongea bwana mmoja mrefu kiasi aliekuwa ameshikiria juice mkononi huku akiwa na baadHi ya watu waliokuwa wakionekana walikuwa bize na kila walichokuwa wakifanya huku tarakishi nyingi zikiwa zimezunguka chumba hicho , bwana huyu alikuwa akifahamika kwa jina la stephano sauli , alikuwa ndio mkuu wa kitengo cha IT ndani ya makao makuu hayo .
“ asante Stephan , nina shida ya haraka naomba unisadie “
“ shida gani ?”
“ naomba unisaidie kutambua hii picha , na namba za hili gari mahali lilipo kwa sasa na mmiliki wake “ alingea suzzane na kisha stephano alimwamrisha moja ya kijana aliekuwa akibonyeza keboard kwa haraka na kumwambia afanye hio kazi .
“ tayari nishampata , anaitwa rafeali marko ni mhasibu wa kampuni ya swift motors , inaypatikana mbagala “ aliongea kijana huyu huku akiendelea kutafuta namba za lile gari .
“ gari hio ipo hapo hapo mbagala na mmiliki ni huyo huyo mhasibu “ aliongea kijana huyo , na suzzane aliona ni mchezo ule ule ambao alikuwa akichezewa unaendelea na safari hii hakutaka kucheza ngoma wanayompigia kwani aliwaza jambo lingine kabisa kwenye kichwa chake .
*****
Raisi baada ya kurudi ikulu moja kwa moja alienda ofisini kwake , huku kichwani swala aliloambiwa na Patrick likiwa linazunguka kichwa chake .
Baada ya kukaa tu kwenye kiti aliingia katibu wake na kumjulisha kuwa kimbona alikuwa akitaka kuonana naye , alimwambia amruhusu .
“ mheshimiwa pole sana na yaliokukuta siku ya sherehe , hata mimi jambo hilo lilinifadhaisha sana niliposikia”
“ asante sana kimbona , na umeingia lini nchini ?”.
“ nimeingia jana mheshimiwa baada ya kumaliza mizunguko yangu ya kibiashara , lakini kuna swala ambalo lilinigusa sana na nikaona nije moja kwa moja kuonana na wewe “
“ ni swala gani hilo kimbona?? “
“ ni swala la mali za bwana bruno , kuna taarifa ambayo ni mbaya sana nimeipata “
“ taarifa gani hio “.
“ taarifa iliokuwepo mpaka sasa haijathibitika , lakini taarifa kutoka mahakama ni kwamba mali za bruno nikimanisha asset zake zote ziliuzwa miaka miaka miwili nyuma kwa kampuni ya INNOVA ya Italy “. Aliongea kimbona na kumfanya henry atoe macho kama kabanwa na mlango
“ ndio muheshimiwa swala hilo na mimi limenishitua sana na kwa taarifa za awali ni kwamba washatuma mwanasheria ambae anatarajiwa kutua siku ya kesho asubuhi kwa ajili ya uhalaliswaji wa mali zote kwenda kampuni ya INNOVA yenye makao yake makuu ndani ya jiji la ROME.
“Swala hili vipi U-97 wanalifahamu? “
“ kwasasa sijajua kwani sam na yeye hayupo nchini na nimejaribu kutafuta mawasiliano nae nimekosa kabisa na mheshimiwa ndalu na yeye kashangazwa tu na swala hili .
ITAENDELEA
SEHEMU 23
Taarifa hio ilikuwa mbaya sana kwa raisi na watu wote waliokuwa na malengo na mali za bruno , hata hawakujua ni kipi kinaendelea na ni lini bwana bruno aliuza mali hizo kwa kampuni ya innova , kampuni ambayo ilikuwa ina makao yake makuu ndani ya jiji la rome Italy .
“kimbona swala hili kwa sasa nadhani tusubiri kwanza mwanasheria huyo afike , na nataka atakapo tua tu niongee nae kwanza ili nijue swala hili linakuwaje , kwani mpaka sasa sijui kinacho endelea kwani leo hii alikuja Patrick kulalamika kuhusu moja ya kiwanda cha bruno kilichopo kuasini kuwa tayari mali ya mtoto wa waziri wa mambo ya ndani ya china “.
“ unazungumzia kile kiwanda kwa sasa sio mali ya bruno ?”
“ ndio na hapa ninapo zungumza nishaomba ripoti kamili kutoka mahakamani juu ya kiwanda hicho kilivyo uzwa “.
Kimbona alifuta jasho , hakuelewa mambo hayo yanavyo enda hapa nchini na walikuwa kwenye sintofahamu , kwani kwenye watu ambao walikuwa wakiziangalia mali za bruno ni hao ,japo walitaka kuziingiza ndani ya U-97 lakini waliamini kwamba wao ndio wangekuwa wawekezaji wakuu ndani ya kampuni hizo na hata kwa mashamba hayo pia .
Wakati mazungumzo ya raisi na kimbona yakeindelea aliingia katibu na kumpa mafaili mawili .
“ mkuu hili moja taarifa za sabi , na hili ni kutoka mahakama ya kisutu juu ya shauri za mali za bwana bruno “ aliongea katibu huyo na kumkabidhi kisha akatoka huku raisi akichukua faili hilo la mahakamani kwanza na kulipitia kwa umakini mkubwa , huku kimbona akimwangalia mheshimiwa .
“ hapa kila kitu kinaonesha ni kweli ni mali ya huyu mtoto wa china , kwani inaonekana bruno aliuza kiwanda hichi miezi kadhaaa kabla ya kufariki kwa raisi bendera “ aliongea raisi .
“ mheshimiwa kama hilo swala ni kweli basi kwa sasa hatuna la kufanya , kama kweli mmiliki ni mtoto wa waziri basi swala hili ni gumu kwani hatuwezi kumzuia asifanye biashara zake hapa nchini ukizingatia na ushirikiano tuliojiwekea baina yetu na China lakini pia wanatudai pesa nyingi .
“ kuna swala hapa linanipa wasiwasi sana kuhusu huyu bwana luang shu ambae ndio mtoto wa waziiri wa mambo ya ndani, kwanza hii biashara yake ambao anataka kuianzisha hapa nchini kama itafanikiwa itapeleka moja ya kampuni yangu ya mawasiliano kufa , lakini swala la pili shu liang he ( waziri wa mambo ya ndani ya china ) alikuwa rafiki mkubwa wa bendera na kama unakumbuka alifika kwenye msiba wake akimuwakilisha raisi wake .
“ ndio namkumbuka huyu bwana , lakini hapo wasiwasi wako uko wapi mheshimiwa ?”
“hebu jaribu kuunganisha haya majina bruno , bendera ma shu lianghe , huenda swala la luangshu kufika ndani ya nchi hii kuna ajenda ya siri ambayo siijui na swala hilo ndio linanipa wasiwasi “
“mheshimiwa ngja swala hili nitalifatilia kwa umakini , naomaba kwasababu nimerudi ngoja nitakusaida katika hili na tutaona ni namna gani swala hili tunaweza kulitatua “ aliongea kimbona na kisha aliagana na raisi .
Baada ya kimbona kutoka aligeukia faili la sabi na kuanza kulisoma .
‘ SABI MBONECHE KAZALIWA MWAKA 1986 NI MTOTO WA KWANZA WA BRIGEDIA MBONECHE ALIFARIKI TAREHE KUMI NA MOJA MWEZI WA NANE NCHINI INDIA ALIKOPELEKWA BAADA YA HALI YAKE KUBADILIKA GHAFLA , ANA DEGREE YA COMPUTER SCIENCE KUTOKA CHUO CHA GEORGE TOWN UNIVERSITY , KWA SASA NI MPELELEZI KWA KUJITEGEMEA AKIWA NA MAFUNZO YA KIMAPIGANO KUTOKA CHUO CHA BLACK CAMP CHA THAILLAND .”
Hio ilikuwa ni maelezo yaliokuwa yamewasilishwa ofisini kwa raisi kwani aliomba taarifa iliokuwa ikimuhusu kijana huyu.
Inamaana huyu kijana ni mtoto wa brigedia mboneche “ alijiuliza raisi kwani alikuwa akimfahamu vyema brigedia huyu kwa uchapaji kazi wake kipindi cha uongozi wa bendera na alikuwa ni moja ya marafiki wa karibu sana wa raisi bendera .
******
MIAKA MIWILI NYUMA
IKULU CHAMWINO .
Ilisikuwa ni siku ambayo mheshimiwa bendera alikuwa akiingia ndani ya mkoa huo ambao ulikuwa ndio makao makuu ya nchi akitokea jiji dar es salaam .
Siku hio alikuwa ndani ya uwanja wa ndege wa Dodoma ambapo alikuja kupokelewa na wakuu mbali mbali wa idara ya usalama wa jiji la Dodoma , pia alikuwepo mkuu wa mkoa wa Dodoma , bwana philipo edsoni , huku wakuu wa usalama alikuwepobwana mboneche hassani .
Mheshimiwa raisi mara baada ya kushuka kwenye ndege ya shirika la ATCL alianza kusalimiana na baadhi ya viongozi hao waliokuja kumpokea akipita kwa mmoja mmoja , na alipo mfikia bwana mboneche walisalimiana na kisha alimwambia kuwa alikuwa akimuhitaji ofisni siku inayo fuata na bwana mboncehe kwa ukakamavu alipiga saluti kuitikia wito huo wa mkuu wa nchi .
Siku iliofuata bwana mboneche alifika ikulu chamwino kuonana na mheshimiwa , alikaribisha vizuri na wasaidizi wa raisi na kupelekwa moja kwa moja mpaka ofisini kwake .
“ karibu sana mboneche “ aliongea raisi akimlaki mboneche .
“ unajua sisi tunapokutana kutana nawaza kipindi kile tukiwa pale UDSM tukihangaika na tafiti zetu “ aliongea raisi na kumfanya bwana mboneche kutabasamu kwani ni kweli wawili hao walikuwa wamesoma katika chuo hicho , na tena walikuwa marafiki wa kubwa na walikujja kupoteana baada ya mboneche kujiunga na jeshi na bendera yeye kuingia kwenye siasa “
“ ni kweli muheshimiwa nakumbuka sana kile kipindi , ni moja ya moment ambazo hazifutiki katika kichwa changu ‘ aliongea mboneche huku wakati huo wakiwa wamekaa kwenye sofa za hapo ofisini “.
“ sasa nimekuitia hapa nataka tuongee kirafiki Zaidi na hili ni swala ambalo nahitaji unisaidie kwani pia linaugusa moyo wa taifa hili , na mtu ambae naweza kukuamini kwa sasa ni wewe “ aliognea raisi .
“ ni swala gani hilo muheshimiwa nipo tayari kulisikiliza na kulifanyia kazi “.
“ nadhani unajua nchi yetu kwa sasa juu ya swala la madawa ya kulevya yametoweka kabisa hapa nchini , na hio ni mooja ya misimamo ambayo niliingia nayo na kuitangaza hadharani na kusaidiana na wasaidizi wangu tuliweza kulimaliza swala hili kabisa ndani ya nchi hii “
“ ndio naelewa muheshimiwa na nakupongeza sana kwa hilo, maana taifa lilikuwa likiteketea “
‘ ni kweli , lakini sasa kuna swala Zaidi ya hilo , na nataka unisaidiea kulifanyia kazi swala hilo kwa siri sana “
“ swala gani hilo muheshimiwa ?”.
Aliinuka na kuendea kabati lililokuwa na baadhi yamafaili na kutoka faili moja lililokuwa likisomeka kwa juu U-97 , alirudi nalo na kumkanbidhi mboneche ambae alifungua na kuanza kusoma .
“ U-97 sijawahi kuisikia hio “.
“ ndio huwezi kusikia swala hilo kwani linafanyika kwa siri sana hapa nchini na moja ya shughuli yake kubwa ilikuwa ni kuratibu shughuli za madawa ya kulevya hapa nchini kama ulivyo soma , lakini swala hilo linanitia shaka mpaka sasa , kwani upande wangu na kwa baadhi ya viongozi tunaamini tushauondoa huu umoja ndani ya nchi hii “
“ swala gani hilo linakutia wasiwasi muheshimiwa ?”
“ umeelewa kwanini umoja huo unaitwa U-97 ?”
“ ndio si unamanisha kwamba ni muungano wa nchi 97 ambazo zipo chini ya huu umoja “
“ sasa swala hilo ndio linanipa wasiwasi , kwa utafiti niliokuwa nikifanya kwa kipinfi kirefu nimegundua kuwa umoja huu kama nchi ishajiondoa kwenye umoja huu , basi hata jina linabadilika kama lilikuwa ni U-97 basi lazima liwe U_-96 sijui unanielewa hapo mboneche “
“ ndio nakuelewa muheshimiwa , na mpaka hapa nadhani nishakupata unacho maanisha , unamaanisha kwamba bado jina halijabadilika japo unaamini umoja huu umeutokomeza hapa nchini”.
“ correct , nadhani sasa unaanza kunielewa point yangu na nadhani tutaelewana sasa , kwa utafiti nilio ufanya nchi nzima kwa kushirikiana na idara ya usalama wa taifa , ni kwamba swala la madawa ya kulevya hapa nchini nimeweza kulitokomeza kwa asilimia 80 ,na kwa sheria za umoja huu ni kwamba kama biashara inafanyika chini ya asilimia 20 ndani ya nchi husika , basi umoja huu unakuwa haupo ndani ya nchi hio rasmi , lakini japo ya biashara hio kufanyika kwa asilimia 20 ndani ya nchi ya tanzania ni kwamba bado jina halijabadilika bado umoja huu unaitwa U-97 .
“mheshimiwa mpaka hapo nimekuelewa vyema , lakini swali langu linakuja , kama ni kweli bishara inafanyika kwa asilimia 20 hapa Tanzania na bado jina hili halijabadilika kuwa U-96 unadhani ni kwanini ?”.
“ hilo ndio swala ambalo nataka kulijua bwana mboneche na mtu ambae nimeona anafaa kwa kazi hio ni wewe , kwani naamini kabisa bruno japo namuamini kwa sasa lakini taarifa alioniletea kuhusu U-97 sio sahihi . huenda kukawa na Zaidi ya taarifa hii, kwa hio kwa utashi wako na utaalamu wako naomba swala hili kwa siri sana ulifatilie na unipe majibu ya swali langu “
“ mheshimiwa naahidi kulifanyia swala hili kazi kwa nguvu zangu zote na kukupa majibu ya swali lako “ aliongea mbneche na siku hio waliagana
Kipindi ambacho mboneche anapewa hii kazi ilikuwa ni mwaka mmoja kabla ya uchaguzi wa awamu ya pili Tanzania .
Ilipita Zaidi ya miezi kama sita , kwani mwaka aliopewa kazi hio mboneche ilikuwa ni mwezi wa saba hivyo kufikia mwezi wa kwanza .
Siku hio muheshimiwa raisi akiwa ikulu hapo hapo chamwino alpokea simu kutoka kwa mboneche na kumtaarifu kuwa siku sio nyingi kabla ya uchaguzi atakuwa amekamilisha ripoti hio , kwani kuna maswala mazito alioyapata ambayo yanampelekea kwenye kuujua ukweli .
ITAENDELA
 
SEHEMU 24
Ilipita miezi sita mingine raisi alimpigia simu bwana mboneche kumuulizia maendeleo ya uchunguzi huo , lakini jibu alilopewa ni kwamba bado anaendelea na uchunguzi na huku akimwambia kwamba uchunguzi wake unamtaka kufika nchini Nigeria kwani ndio anakoamini atapata ukweli juu ya U-97 , basi raisi alimtakia safari njema bwana mboneche .

Siku moja kabla ya kuapishwa kwa raisi bendera , akiwa ofisini kwake chamwino hii ni baada ya uchaguzi kupita , alipokea fax ( hii ni nyaraka ambayo ni kama kopi lakini inakuwa halisi na kuna mashine yake baada ya kutumwa huwa inakuwa inachapisha (print )), kwa hio siku hio kwenye muda wa saa mbili ndio muda ambao raisi bendera alipokea ujumbe huo na ulikuwa ukitoka kwa brigedia mboneche , taarifa hio ilimshitua sana rais bendera mpaka kupelekea hali yake kubadilika ghafra , lakini kupitia dawa alizokuwa akitumia aliweza kuituliza hali yake ya mshituko wa moyo , haikujulikana ilikuwa ni nini kilikuwa kwenye hio taarifa .

Basi bwana mboneche alirudi rasmi ncini , miezi miwili hivi , wakati raisi akiwa njiani kutokea Dodoma chamwino kwenda ikulu dar es salaam , alimpigia bwana mboneche simu kumuhitaji ofisini kwake siku iliokuwa ikifuata , siku hio bwana mboneche alikuwa ofisini kwake lugalo brigade na alikubaliana na bwana raisi bendera kukutana.

Ilivyotimia muda wa saa kumi na moja brigedia mboneche alitoka ofisini kwake na kurudi nyumbani kwake , siku hio walipitia kawe kwenda masaki , walipita kawe yote hatimae kuingia haile Selassie road mbele kabisa kabla haujafika mwaya street , mkabala na ubalozi wa Namibia ndipo bwana huyu hali yake ilibadilika kwani alidondoka na kupoteza fahamu hapo hapo, jambo ambalo lilimpa mshituko dereva , alisimamisha na kumuamsha muajiri wake , lakini wapi kwani alikuwa akihema kwa mbali sana na kupumua kwa shida , ilibidi dereva amuwahishe kwenye kituo cha afya cha tindwe medical and health services kwani ndio sehemu alioiona ya karibu .

Baada ya kufika eneo hili madaktari walimpokea brigedia mboneche na kuanza kuhudumiwa , huku dereva akitoa taarifa nyumbani kwa brigedia ambapo dakika chache tu mke wa brigedia aliekuwa presha juu juu alifika .
“ jaffari mzee anaendeleaje “ aliulza mama huyu mara baada ya kumfikia dereva huyu aliekuwa akijulikana kwa jina la jaffari , lakini jaffari hakuwa na majibbu Zaidi ya kusema kuwa hali ya mzee ilibadilika ghafra .

Dakika kadhaa daktari alitoka na kumuita mke wa brigedia na jaffari , walifika ofisini na kuelezwa .
“ hali ya mgonjwa ni mbaya sana na siwezi kusema kitu kwa sasa kwani tumeshindwa kujua kilicho sababisha tatizo lake hivyo mpaka sasa ninavyosema ashaingizwa kwenye gari na anapelekwa muhimbili kwa ajili ya uchunguzi Zaidi ‘ aliongea daktari huyu na kisha walitoka na kweli ile wanatoka gari ya wagonjwa ndio ilikuwa ikitoka getini ikipiga makelele ya ving`ora .

Japo kwa bwana mboneche kuhudumiwa na madaktari bingwa wa hospitali hii , lakini hali yake ilizidi kuwa mbaya taarifa hizi za kuugua kwa ghafra kwa mboneche zilimfikia raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania , na alipo pata habari hizi alipatwa na mshituko na hapo hapo alimpigia mkuui wa hospitali hio bi Sophia na aliambiwa kweli mgonjwa huyo amepokelewa , lakini madaktari wameshauri apelekwe nje ya nchi kwani swala lake mpaka sasa haijabainika chanzo ni nini .

Raisi alikuwa muda huoo bado hajaingia dar es salaam kwani kuna baadhi ya vijiji alikuwa akihutubia , lakini baada ya kupata taarifa hii aliamua moja kwa moja kwenda hospitali ya muhimbili , huko ndiko hali aliomkuta nayo bwana mboneche haikuwa nzuri kabisa kwani bwana huyo alikuwa amepoteza kabisa fahamu .

Mheshimiwa raisi alitoa ndege yake binafsi na vibari kwa ajili ya mboneche kusafirishwa kwenda india na siku hio hio mboneche aliacha ardhi akiambatana na mke wake kwenda india , kwenye hospitali moja iliokuwa ikijulikana kwa jina la ARTEMIS iliokuwa ikipatikana katika jiji la new delh .

Baada ya safari hio ndefu hatimae mboneche alipokelewa katika hospitali hio kwani taarifa zilikuwa zishatumwa na raisi mwenyewe kupitia balozi , madaktari wabobezi walimuhudumia takribani masaa mawili yote ndipo walipotoka na kuonana na mke wa mboneche mama sabi aliekuwa ameambatana na balozi wa Tanzania nchini india bwana davidi ombeni .
“the patient condition is not very good and I would say its just lucky until now , the patient problem is due to polonium 210 poisoning
“ Hali ya mgonjwa sio nzuri mpaka sasa na niseme kwamba ni bahat kwake mpaka kufikia muda huu , tatizo la mgonjwa ni kutokana na sumu aina ya polonium 210.”
Kila mtu alishangaa kwa taarifa hio , ni mama sabi alianza kutoa kilio kwani hakuelewa ni adui gani wa mume wake anaweza kumuua kwa kutumia sumu . aliongea dokta Rajeev dokta huyu ambae alionekana kabisa alikuwa na umri mkubwa katika fani yake hio
“doctor can you tell us more about poison”
“ dokta unaweza kutuambia Zaidi kuhusu hio sumu “ aliuliza davie.
“about this poison it suprises me a lot as its very rare toxin that causes the organs of the body to fail and eventual die “
“ hii sumu imenishangaza sana kwani ni adimu sana kupatikana na inasabisha ogani za mwili kufeli na kumsababishia mtu kifo , ni ngumu sana kuuzwa popote pale “ aliongea dokta
“ sumu hio imeingiaje katika mwili wake ?”
“ kwa uchunguzi tulio ufanya ni kwamba tumefanikiwa kumtoa kijisindano kidog upande wa shingoni ambacho moja kwa moja tumebaini kwamba ndio kilichotumika katika kuingiza sumu hio mwilini “.
“ vipi kuhusu mgonjwa wetu kuna uwezekano wa kupona ?”
“ siwezi kusema chochote kuhusu hilo ila kwasababu yupo hospitalini anaweza kupona “ aliongea na kisha alitoka
Taarifa hizo za sumu zilimfikikia mtoto mkubwa wa dokta mboneche aliekuwa akiitwa sabi mboneche aliekuwa nchini marekani , baada ya kusikia taarifa hio hakujiuliza mara mbili mbili alisafiri mpaka india ambako alipokelewa na mama yake alieanza tu kulia baada ya kumuona mwanae .
Pia taarifa za swala la mboneche kuchomwa na sindano ya sumu lilimfikia raisi , na hata yeye pia alishangaa sana swala hilo hususani sumu iliotumika , kwa akili ya haraka haraka raisi bendera aliona yeye ndie aliemuua mboneche kwa kumuingiza kwenye kazi ambayo ilikuwa ni hatari sana , swala hilo lilimhudhunisha sana raisi bendera .
Siku moja baada ya mnoneche kufikishwa hatimae aliweza kufungua macho , mtu wa kwanza kumuona alikuwa ni mke wake , hakuweza kuongea kabisa , japo hakuwa akitumia oksijeni , alimpa ishara mke wake kwamba anahitaji kuonana na mwanae
Na bi amina bila kuchelewa alikwenda kumuita sabi na mara baada ya kufika mboneche alimpa ishara mke wake kwamba anataka kuongea na mwanae , na bi amina hakukaidi alitoka na kuwapisha, baada ya bi amina kutoka mboneche alimuonesha sabi ishara kwamba ampe peni na karatasi na aliandika maneno
“CALL O712******* AND ID NO 167S0”. TRUST NO ONE
Baada ya bwana mnoneche kuandika maneno hayo alimpa ishara sabi amuite mama yake , na mama sabi alifika na mboneche alimshika mkono mke wake huku machozi ya kiutu uzima yakitoka na dakika kadhaa mbele hali yake ilibadilika , madakttari waliarifiwa na kufika , walijitahidi kadri ya uwezo wao lakini hawakuweza kufanya kitu kwani mboneche alipoteza maisha .
Ikawa msiba mzito kwa familia yake , mama sabi alilia sana kuomboleza kifo cha mme wake akiwemo pia sabi .

Taarifa zilifika nchini Tanzania na taratibu za kusafirisha mwili zilifanyika na mwili hatimae ulipokelewa na watoto wa mboneche na raisi mwenyewe , ilikuwa ni hudhuni kubwa sana ,lakini hauna ambae angeweza kubadilsiha uhalisia kwabi bwana huyo alikuwa tayari ashapoteza maisha .
Siku mbili mbele mwili wa bwana mboneche uliaagwa rasmi jijini dar zoezi hilo likiongozwa na raisi mwenyewe , viongozi mbali mbali walihudhuria katika kumuaga bwana mboneche , baada ya kuagwa hatimae mwili wake ulisafirishwa mpaka kijiji kwao na kuzikwa huku sababu ya kifo cha brigedia huyo kikibaki kuwa siri kwa baadhi ya wanafamilia .
REST IN PIECE DADIII….. ni kauli ya mwisho ya watoto watatu wa bwana mboneche wawili wakiwa wakike na wa kiume alikuwa ni sabi peke yake ambae muda wote alikuwa akitoa machozi.
Wiki moja baada ya msiba ndio siku ambayo sabi alikumbuka kikaratasi alichopewa na baba yake , hakutaka kubaki nyumbani , alimuaga mama yake kwamba anasafiri nje ya nchi na mama yake alimpa Baraka zote , lakini ukweli ni kwamba sabi hakusafiri kwenda nje ya nchi bali alienda kuishi hotelini .
Siku aliofika hotelini ndio siku ambayo alifika ndio siku ambayo alipiga simu ile namba taratibu zile zile zilizokuwepo kwa damiani ndio hizo hizo sabi alipitia kwani alitaja ile namba aliopewa na baba yake dakika kadhaa kabla ya kifo chake , utofauti wa bwana mboneche ni kwamba baada ya kupiga simu yeye alipewa maagizo ya kusafiri mpaka nchini thailland jiji la Bangkok .
Ni kweli kesho yake bila kujiuliza kwani alikuwa akitaka kujua ni kipi baba yake alikuwa akimanisha mpaka kumpa ujumbe ule wa kupiga namba zile , huku akiamnini kabisa mtu aliepiga namba ndio huyo mwenye maelezo aliokuwa akiyataka .
Masaa kumi natano alikuwa tayari ndani ya jiji la Bangkok , mtu aliekuja kumpokea damiani ndio huyo huyo aliekuja kumchukua sabi .
“ welcome thailland sabi “.
“ THANK YOU “

SEE YAH.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom