Uingereza nao wafuata Tanzania na nchi zingine abiria wote watakaotua UK kutakiwa kujiweka karantini kwa gharama zao wenyewe kwa siku 14

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,939
20,400
1590155824175.png


Waziri wa mambo ya ndani wa Uingereza Priti Patel

Serikali nchini Uingeeza leo jioni inatarajia kutangaza kuwa abiria wote wa kimataifa ambao watatua kwenye viwanja vya ndege vya nchi hiyo watatakiwa kujiweka wenyewe karantini kwa gharama zao wenyewe.

Pia abiria hao watatakiwa kutoa taarifa zao binafsi zikiwemo anuani za barua pepe na namba za simu ili kuweza kufuatiliwa huko walokojifungia kwenye ama hoteli au nyumba za wageni maarufu kama B&B.

Uamuzi huu ambao unapingwa na baadhi ya wabunge kwamba umekuja huku ukiwa umechelewa unatarajiwa kutangazwa leo jioni na waziri wa mambo ya ndani wa nchi hiyo Priti Patel.

Zaidi ya miezi miwili ilopita nchi mbalimbali duniani khasa barani Afrika ziliweka utaratibu huu wa kuhakikisha abiria wote wa kimataifa wanajiweka wenyewe karantini Tanzania ikiwemo

Nchini Tanzania abiria wote (nikiwemo mimi mwenyewe) walitakiwa kujitafutia utaratibu wa kujiweka karantini na wengi walitafuta hoteli mbalimbali kwa ajili hiyo

Had leo mchana idadi ya watu walokufa kwa ugonjwa wa COVID -19 nchini Uingereza walikuwa wamefikia 36,393.

Utaratibu huo mpya utawahusu abiria wote wa ndege, njia za reli na usafiri wa majini

Abiria atakapowasili nchini humo atajaza fomu maalum akiweka anuani ya nyumba anapoishi au sehemu atakapofikia na namba za simu.

Tofauti iliyopo kwa nchi hii ambayo ni ya sita duniani kwa uchumi mkubwa, na Tanzania ni kwamba kama abiria huyo atakuwa hana pa kufikia basi serikali itagharamia malazi ya abiria huyo kwa wiki hizo mbili, jambo ambalo litakuwa ni nadra kutokea.

Maofisa wa karantini watakuwa wakitembelea kufanya ukaguzi katika sehemu hizo na endapo mtu atavunja masharti ya karantini basi atatozwa faini ya pauni zisizopungua 1000.

Serikali nchin humo itakuwa ikipitia utaratibu huo kila baada ya wiki tatu.
 
Noma sana!!! Hao abiria wanatoka wapi au anga ndo limefunguliwa?

Mashirika mengi yameanza kurusha ndege Emirates na zile ndege za bajeti ndogo.

Kama wasafiri kutoka London kwenda Estonia usafiri upo na watakiwa kuvaa barakoa.

Ila taratibu hizi zikitangazwa leo jioni basi karantini itaanza mara moja jioni hii hii.
 
KLM kwenda Amsterdam ipo pamoja na other airlines, connection ya bongo hiyo kutoka UK. Emirates naona nao wako njiani .... …….. pamoja na Turkish Airlines. The sky will be open very soon for everyone. Sema hivi sasa bado hazijai kutokana na bei, maana airlines wamekuwa wamepigwa sana na Covid-19.
 
Back
Top Bottom