Serikali yaruhusu Mabasi ya abiria kusafiri kwa saa 24

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,462
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeruhusu Mabasi ya abiria kufanya usafirishaji wa Saa 24, baaada ya kujiridhisha kiusalama, mwamko wa wananchi, huduma za mawasiliano pamoja na miundombinu ya usafirishaji.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Nchi, Jumanne Sagini wakati anaongea na Baraza la Taifa la Usalama Barabarani na kusema kuwa wamefikia maamuzi hayo baada ya Serikali kuimarisha shughuli za uchumi wa wananchi wake wa maeneo ya mjini na Vijijini.

Akiongeza kuwa wamezingatia maoni ya Wadau mbalimbali wakiwemo Wabunge, wamiliki wa mabasi, madereva wa mabasi, wasafiri, Wafanyabiashara na Wananchi kwa ujumla.

Aidha, Serikali imetoa maagizo kwa wadau wote wa usafirishaji kuzingatia Sheria, Kanuni na utaratibu wa leseni zao.

Pia madereva wametakiwa kuthibitishwa na LATRA, ambayo itatoa ratiba za safari kwa saa 24, TANROADS kuhakikisha ubora wa miundombinu, Serikali za Mitaa kuhakikisha zinasimamia usalama wa abiria kwenye huduma wanazosimamia pamoja na Jeshi la Polisi kusimamia Usalama wa watu na mali zao.
 
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeruhusu Mabasi ya abiria kufanya usafirishaji wa Saa 24, baaada ya kujiridhisha kiusalama, mwamko wa wananchi, huduma za mawasiliano pamoja na miundombinu ya usafirishaji.

simamia usalama wa abiria kwenye huduma wanazosimamia pamoja na Jeshi la Polisi kusimamia Usalama wa watu na mali zao.
Jumanne Sagini Wewe utapanda hayo mabasi ya kutembea usiku?
 
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeruhusu Mabasi ya abiria kufanya usafirishaji wa Saa 24, baaada ya kujiridhisha kiusalama, mwamko wa wananchi, huduma za mawasiliano pamoja na miundombinu ya usafirishaji.
Madereva wa Tz mchana kweupe wanashindwa kufuata mwongozo wa taa za barabarani mpaka awepo askari wa usalama barabarani (trafiki), kweli watafuata sheria za barabarani usiku wa giza, hapa tunajipangia kuongeza takwimu za ajali mbaya za barabarani.
 
Hii nzuri sana kwa kwa jamii inayojali UHAI, UTU na ubinadamu.

Ila kwa akili za madreva wetu ukichanganya na ubovu wa miundombinu na Mabasi tutegemee BOMU la kupoteza ndugu, marafiki, wapendwa wetu au sisi wenyewe!

Kiufupi speed kali ni kifo akuna cha mpango wa Mungu au kurogana.

Mliopewa mamlaka tumieni akili zaidi kuliko hisia
 
Back
Top Bottom