Uhusiano ndani miaka 9, ana mimba ya mtu mwingine.

Uhusiano ndani miaka 9, ana mimba ya mtu mwingine.

Nimeajiriwa mwaka jana ndo nilikuwa najinga kumuoa rasmi lakini yametokea hayo tena kapewa mimba na mume wa mtu ambae hawezi kumuoa, nimeumia sana nimeshindwa la kufanya ikitegemea pande zote mbili zilikuwa zikifahamu uhusiano wetu.
 
We kubwa jinga,yani miaka 9 unapiga sound kwa kumgegeda tuuuuuuuuuuuuuuuuu unategemea nini?nyambafu,tena mie ndiye niliyemjaza kenge wewe!

Nafikria kufanya kwa sabab nampenda nahisi nitautesa moyo wangu kwa kumuacha
 
Mwache aenda kwa ampendae, wewe enzi ishaisha
 
Poleee ila muda mwng sana huo....uchumba gn miaka 9.Kutambulisha haikutosha ilibid upige hatua moja mbele zaidi.
 
Afadhali hamkuoana.

Jenga taswira ndo angekuwa mkeo wa ndoa mwenye mimba ya mtu mwingine....
 
Ndg zangu msishangae miaka 9 kwani uchumba wetu ulianza tukiwa kidato cha 2 baada kumaliza kidato cha 4 niliendelea na kidato 5 na 6 na hatimae chuo miaka 3 wakati wote huo nisingeweza kumuoa kwa sbb nilikuwa dependant kwa wazazi wangu.
Form tuu ulikua na miaka mingapi mpaka ukamchumbia?jee wazazi wako walikuruhusu kumchumbia ukiwa form2 mpaka useme uchumba wenu ulianza tangu ukiwa form2??????
 
Nimeajiriwa mwaka jana ndo nilikuwa najinga kumuoa rasmi lakini yametokea hayo tena kapewa mimba na mume wa mtu ambae hawezi kumuoa, nimeumia sana nimeshindwa la kufanya ikitegemea pande zote mbili zilikuwa zikifahamu uhusiano wetu.
Hamishia mashambulizi kwa huyo shoga yake ili utoe machungu.
 
Nimpe sana hongera huyo mchumba wako wa miaka 9. Alishaona wewe si muoaji bali ni wa kumdunda tu sindano bila malengo. Hainiingii akilini eti unakaa na binti wa watu miaka 9 hakuna ndoa!!! Mnazini tu!!! Hakuna mtoto, Imagine hata kama alikuwa 18 ina maana she is 27 anaelekea umri wa utata halafu unaendela bado kumuweka? Atazaa lini? Au alikuwa akipata mimba unamwambia muda bado nenda kwa wataalam wakachoropoe? Ningekuwa wewe the maximum tima I could offer you is 5 years only then nasepa.
 
Form tuu ulikua na miaka mingapi mpaka ukamchumbia?jee wazazi wako walikuruhusu kumchumbia ukiwa form2 mpaka useme uchumba wenu ulianza tangu ukiwa form2??????

Nilikuwa na miaka 18 tulitambulisha nikiwa form 6.
 
Labda alikuwa anatest kama anaweza kupata mtoto

Kukaa na mtu miaka tisa harafu hakuna mimba ni issue nyingine
 
Hahah Mamndenyi...uhusiano wangu na Mary sio wa muda mrefu kwa sababu kama ya huyu jamaa...sisi tulianza mahusiano haya ya kimapenzi mwaka wa mwisho chuoni. so tupo kwenye muda wa kujijenga am sure by next year nitakuwa (ningekuwa) tayari kuoa!!! Na kila mmoja wetu alikuwa akilifahamu hilo...wakubwa zetu ndio waliotufitini!!!
 
Last edited by a moderator:
Mentor pole

Utani wa bisibisi huu

Hata kama ni kuchunguzana hii ya kwenu ya miaka 9 is too much pilipili.

Miaka yote hiyo mmekaa nae hata hukutangaza nia?

Hapo kama ni kumlaumu mwanamke nitamlaumu kidogo tu, ila wewe ndo wakulaumiwa sana.

Mwanamke kaangalia akaona wewe hauna plan yoyote na yeye.

Unawezatuambia "hata ndani ya hiyo miaka 9 hauja nanilihu".
 
Ata kama ndio akabebe mimba ya mtu mwingine siyo fair...

Kaona giza sasa we kila subira ina time limit yake sasa jiulize miaka tisa yote nangojea ndoa tu aaaaaarg this bull shit bora niwapelekee wenye mkojo mkali wafanye kazi.
 
Wewe waeleze ndugu zako ukweli, huyo atalalwa nje tena hata kabla hujamuoa.

Duh ni aibu, unaongea kama hakuna mabinti wengine, mshukuru Mungu amekuepusha na mengi.

Usiwe na wasi utapata mke uliyeandaliwa na Mungu. Muache huyo aende zake tena ushukuru Mungu umejua kabla ya ndoa inaonekana amekuwa analala na wengine wakati mko wote.

Tukio hili ni la kukufumbua macho umjue yeye alivyo kiukweli.

Pole
 
uhusiano (uchumba) miaka tisa?!?!?!?! mhhh

miaka tisa sio mingi hivyo.
Mnaanza uhusiano mkiwa form 1, mkimaliza form 6 na chuo ni miaka kumi hiyo, baada ya kumaliza chuo hapo ndio mnafunga ndoa. Watu wengi tu wameoana kwa mtindo huu.
 
miaka 9 mbona michache tu, kama watu walianza toka shuleni/sekondari ???

Lakini huwa inauma sana mtu wako wa siku nyingi anapokusaliti, tena ni yule uliyekuwa unamuamini sana, unatamani ungeweza kumsamehe lakini vile unakuta kosa ni kubwa unabaki unalia tu mwenyewe!

Ingekuwa amekusaliti, ungeweza piga moyo konde lakini mimba halafu na mtoto, hapo sahau bro' tafuta mwingine hiyo haikupangwa!

Hata mimi si ndio nashangaa. Miaka tisa hadi kumi ndio maximum haswa kwa wale walioanza mahusiano wakiwa form 1, na kusubiri kufunga ndoa baada ya kumaliza chuo.
 
Back
Top Bottom