Uhusiano ndani miaka 9, ana mimba ya mtu mwingine.

Uhusiano ndani miaka 9, ana mimba ya mtu mwingine.

Molembe

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2012
Posts
9,933
Reaction score
11,865
Nina mchumba ambaye nimedumu nae kwa muda wa miaka 9 lakini sasa ana mimba ya jamaa mwingine stori kamili nimeipata toka kwa rafiki yake nimembana amekubali na kuniomba msamaha nimeshindwa la kufanya na tayari tulishatambulishana kwa wazazi.
 
Piga chini, tafuta hela, mwache akawe mama na we tafuta kitu kingine KIKALI
 
Nina mchumba ambaye nimedumu nae kwa muda wa miaka 9 lakini sasa ana mimba ya jamaa mwingine stori kamili nimeipata toka kwa rafiki yake nimembana amekubali na kuniomba msamaha nimeshindwa la kufanya na tayari tulishatambulishana kwa wazazi.
huyo hakuwa mchumba wako, alikuwa mchumba wenu, sema jamaako mweingine amebahatika kuwa wa kwanza kuweka mimba, wakati uko naye, wewe ulijua uko peke yako, kumbe mwenzio alikuwa anachuma pande zote mbili. anakula kwako na kwa jamaa. ameamua amzawadie jamaa mimba, pole sana.
 
Uchumba kwa muda wa miaka 9, halafu unalalamika kuwa ana mimba ya mtu mwingine. Jiulize kwanza kwa nini miaka 9 yote hana mimba wala mtoto wako. Huyo keshaona kuwa wewe sio mwoaji, ila unavuta tu utamu, kajilengesha kwa mwoaji.
 
Mmedumu miaka 9, mlikuwa shule ama tayari uraini. Kama shule I can try to understand labda mlianza mahusiano mkiwa form 1 kama uraiani duh mvumilivu huyo dada...mie ningeibeba na miaka 5 tu na wala nisingekuomba radhi.
 
Nina mchumba ambaye nimedumu nae kwa muda wa miaka 9 lakini sasa ana mimba ya jamaa mwingine stori kamili nimeipata toka kwa rafiki yake nimembana amekubali na kuniomba msamaha nimeshindwa la kufanya na tayari tulishatambulishana kwa wazazi.

nawe ulizidi acha iwe hivyo,. Miaka 9 yote unamsubirisha mwenzio kwan ye nani avumilie muda wote huo? au ndo kusema ulitaka harusi kama ya mjukuu wa malkia eliza bet eeeh? Hayo ndo matokeo jipange tena mkuu!
 
Na bado!! Kama ujajipanga kimaisha achana kbs na masuala ya mapenzi la sivyo utakuja kujinyonga. Miaka 9 umekaa unambwela mbwela, kuoa uoi na mimba hutii? Tena kajiangalie maana unaweza ukawa hauna uwezo wa kumpa mimba mwanamke. Kwa taarifa yako jamaa ana miezi mi2 tu kitu tayari. Kalaghabao!!
 
Nina mchumba ambaye nimedumu nae kwa muda wa miaka 9 lakini sasa ana mimba ya jamaa mwingine stori kamili nimeipata toka kwa rafiki yake nimembana amekubali na kuniomba msamaha nimeshindwa la kufanya na tayari tulishatambulishana kwa wazazi.
Lakini na wewe bwana ulifanya mzaha sana. Uchumba gani sasa huo wa miezi 108!!!
 
miaka 9 mbona michache tu, kama watu walianza toka shuleni/sekondari ???

Lakini huwa inauma sana mtu wako wa siku nyingi anapokusaliti, tena ni yule uliyekuwa unamuamini sana, unatamani ungeweza kumsamehe lakini vile unakuta kosa ni kubwa unabaki unalia tu mwenyewe!

Ingekuwa amekusaliti, ungeweza piga moyo konde lakini mimba halafu na mtoto, hapo sahau bro' tafuta mwingine hiyo haikupangwa!
 
Ni fundisho kwa wanaume wengine wa tabia yako. Unamuweka miaka 9 yote hiyo, mwisho wa siku unachukua mke mwingine. Yamewakuta wengi ndiyo maana mwenzako kaamua kupewa mimba na mtu mwingine.
 
Shetani amemzidi nguvu baada ya kuvutana nae kwa miaka 9.uchumba gani miaka 9? Au ulidhani enzi za kina Nuhu wanaoa wakiwa na miaka 100?
 
Hata kama ni kuchunguzana hii ya kwenu ya miaka 9 is too much pilipili.

Miaka yote hiyo mmekaa nae hata hukutangaza nia?

Hapo kama ni kumlaumu mwanamke nitamlaumu kidogo tu, ila wewe ndo wakulaumiwa sana.

Mwanamke kaangalia akaona wewe hauna plan yoyote na yeye.

Unawezatuambia "hata ndani ya hiyo miaka 9 hauja nanilihu".
 
Yawezekana hajawahi sikia neno NITAKUOA kutoka kwako ndo maana kabeba mimba ya mtu mwingine,miaka 9!
 
copy; Mentor

Hata kama ni kuchunguzana hii ya kwenu ya miaka 9 is too much pilipili.

Miaka yote hiyo mmekaa nae hata hukutangaza nia?

Hapo kama ni kumlaumu mwanamke nitamlaumu kidogo tu, ila wewe ndo wakulaumiwa sana.

Mwanamke kaangalia akaona wewe hauna plan yoyote na yeye.

Unawezatuambia "hata ndani ya hiyo miaka 9 hauja nanilihu".
 
Last edited by a moderator:
Nina mchumba ambaye nimedumu nae kwa muda wa miaka 9 lakini sasa ana mimba ya jamaa mwingine stori kamili nimeipata toka kwa rafiki yake nimembana amekubali na kuniomba msamaha nimeshindwa la kufanya na tayari tulishatambulishana kwa wazazi.

Sasa miaka yote tisa ulikuwa unafanya nini hasa,ndo maana tunawashauri vijana kuwa uhusiano mzuri usizidi mwaka
 
Back
Top Bottom