Uhuru Kenyatta jirani mwema, atupenda Watanzania, amkubali sana JPM. Asisitiza upendo, umoja na ushirikiano kati Wakenya na Watanzania tujenge EAC 1

Kenyans ni alama kamili ya ubeberu, beberu akikuona umenuna yeye anakuchekea, akikuona umefurahi yeye ananuna, wanaenda kwa timing ili wakwapue kwa maslahi yao nyangau hawa
Ahsante sana na ndio maana hapo juu nimesema kwa mara nyingine Uhuru nimemuogopa zaidi!
 
Kwahiyo unaona Kenya wanafanya Jambo jema kwa Tanzania
Hapa ndio hua najiuliza sana, hivi inamaana hapa EAC ni Tanzania tu ndio wanapaswa kutunza diplomasia?

Yani kwamba sisi ndio tuwe wanyonge tu wa kulamba watu miguu na kujishusha kwenye kila jambo kisa diplomasia?

Yani wenzetu watufanyie upuuzi kwa makusudi kabisa Ila sisi tusijibu tukae kimya au tukawabembeleze kisa sisi ni wana diplomasia?
 
Leo nimekudharau sana jamaa yangu.

Yaani kuturuhusu kuingia Kenya bila ya Passport wewe umeona cha maana sana hujagundua kama huo ni mtego?Unadhani Watanzania watapata fursa gani ya kazi kule Kenya?

Hapo alitaka na sisi tuwaruhusu waingie bila ya passport waje wakamate nafasi za kazi kwetu kawaulize Rwanda kinachoendelea kwa sasa.

Kiufupi baada ya kuwakatalia ardhi yetu kuingizwa katika itifaki ya EAC wamekuja na mbinu nyingi za kutaka kuwa wengi upande wetu.

Kibali cha kufanya kazi Kenya kinatolewa bure kwa Watanzania sasa kaulizie ni Watanzania wangapi wame quality kupata hicho kibali?
 
Ni kweli na Tz sio adui wa Kenya isipo kua awamu hi hatuna sere ya kimataifa inayojulikana( foreign policy) tumejikuta kwenye counter reaction tena ya kishamba inayo onyesha kwamba viongozi wetu hawana exprience ya dipulomasia na PR..........ila Kenya na Tz kila mtu anategemea mwenzie sana na watakua majirani siku zote hamna haja ya kuzozana

Tutamkumbuka Balozi A. Mahiga!
RIP
 
Uhuru hana shida,tatizo Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu kwa sasa!View attachment 1524535
Ila wao kuzuia raia wetu wasiende kwao ndio wanaakili timamu Ila sisi wendawazimu tulitakiwa tukubali turuhusu ndege na raia kutoka kwao waje tena kwa Uhuru kabisa wafanye mambo yao kisha warudi kwao Ila sisi kuonekana huko ni haramu kabisaa?

Tungefanya hivo ndio tusingekuwa kichwa Cha mwendawazimu?
 
Naunga mkono hoja, kwa maoni yangu Tanzania tume overreact, kulikuwa hakuna sababu, siyo jinsi ambavyo watu matured wanavyopaswa kutatua matatizo, inanikumbusha ex girlfriend wangu, ilikuwa nikikosea kidogo tu hata kama tumepishana kidogo sana hiyo revenge yake unaweza kujiua, alikuwa immature.
Very interesting!!
====
Lakini ,je. kama kulikuwa na fununu kuwa huyu jirani alikuwa anaanda kubwa zaidi ya kuzuia ndege zetu, napo tulitakiwa kukaa kimya!? Sidhani kama jirani mwema alitakiwa kutingisha kiberiti kuona kama kimejaa! Alitakiwa, huyo jirani ajue kwa upya ule wa ganda la kiberiti kunauwezekano kimejaa hivyo aendelee kuandaa tambi za jiko.
 
Hapa ndio hua najiuliza sana, hivi inamaana hapa EAC ni Tanzania tu ndio wanapaswa kutunza diplomasia?

Yani kwamba sisi ndio tuwe wanyonge tu wa kulamba watu miguu na kujishusha kwenye kila jambo kisa diplomasia?

Yani wenzetu watufanyie upuuzi kwa makusudi kabisa Ila sisi tusijibu tukae kimya au tukawabembeleze kisa sisi ni wana diplomasia?
Asante mkuu, hili pia nlikua najiuliza maana hvi visa vya Wakenya hua ni vingi sana ukichunguza katika historia ya hzi nchi 2. Mi nadhani in future hawatakua wakituletea ujinga bali watafanya maamuzi ya kujitambua watakapokua wanadili na sisi
 
Kuongea na kutenda ni vitu viwili tofauti, Kenyatta hutenda tofauti na anachoongea,nenda Kenya ndugu na kitambulisho tu cha taifa pitia namanga ukipita unipigie simu hapo usitoke nije nihakiki, unaongelea Kenya ipi ya kuingia kiholela?
 
Leo nimekudharau sana jamaa yangu.

Yaani kuturuhusu kuingia Kenya bila ya Passport wewe umeona cha maana sana hujagundua kama huo ni mtego?Unadhani Watanzania watapata fursa gani ya kazi kule Kenya?

Hapo alitaka na sisi tuwaruhusu waingie bila ya passport waje wakamate nafasi za kazi kwetu kawaulize Rwanda kinachoendelea kwa sasa.

Kiufupi baada ya kuwakatalia ardhi yetu kuingizwa katika itifaki ya EAC wamekuja na mbinu nyingi za kutaka kuwa wengi upande wetu.

Kibali cha kufanya kazi Kenya kinatolewa bure kwa Watanzania sasa kaulizie ni Watanzania wangapi wame quality kupata hicho kibali?
Kinacost almost 1.5m kama sikosei.
 
Kuongea na kutenda ni vitu viwili tofauti, Kenyatta hutenda tofauti na anachoongea,nenda Kenya ndugu na kitambulisho tu cha taifa pitia namanga ukipita unipigie simu hapo usitoke nije nihakiki, unaongelea Kenya ipi ya kuingia kiholela?
hua tunatumia temporary passport mkuu, mara ya mwisho nmetumia mwaka jana september
 
Back
Top Bottom