Uhuru Kenyatta jirani mwema, atupenda Watanzania, amkubali sana JPM. Asisitiza upendo, umoja na ushirikiano kati Wakenya na Watanzania tujenge EAC 1

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,504
113,618
Wanabodi,

Kila nipatapo fursa, huwa ninaandika kitu kupitia safu yangu ya "Kwa Maslahi ya Taifa" zenye kuhimiza patriotism kwa Watanzania kuwa wazalendo kwa taifa letu, kwa kutanguliza mbele maslahi ya taifa.

Pia niliwahi kusisitiza humu kuwa unaweza kuchagua marafiki lakini huwezi kuchagua majirani, ili uishi vema kwa raha na amani na majirani, ni lazima uwe na upendo kwa jirani yako hata kama unamuhisi hakupendi, wewe mpende tuu na muishi kwa ujirani mwema na jirani yako, na hata kukitokea sintofahamu yoyote baina yako na jirani yako, katika kutafuta suluhisho la simtofahamu hiyo, utangulize kwanza upendo na kuutatua mgogoro wowote na jirani yako kwa kutanguliza njia za kidiplomasia kwanza, diplomacy, zikishindikana ndipo tuje kwenye tit for tat ambayo nayo pia ni diplomacy ya kanuni ya reciprocity.

Kwavile amri kuu ni upendo, mpend jirani yako kama unavyojipenda wewe na umtendee vile unapenda kutenda, na hata ikitokea jirani akaghafilika, akikupiga kofi la shavu lako la mkono wa kushoto, kama una upendo, usimrudishie, bali utamgeuzia na shavu la mkono wa kuume na sio kumrudishia.

Hoja hii ni kufuatia hiki kinachoendelea sasa kati yetu na jirani yetu kuhusiana na yatokanayo na COVID-19 kulikopelekea back biting, kunyoosheana vidole na tit for tat.

Nimenote baadhi ya comments za baadhi yetu sio comments za upendo na ujirani mwema, zenye nia ya kutafuta suluhisho la amani na kidiplomasia bali ni comments zenye hatred na fuelling the situation instead of resolving.

Sasa kwa vile sisi waandishi wa habari, huwa tunauwezo wa kuona ndani ya moyo wa mtu, na huwa tunapata access ya kuzungumza na marais wa nchi mbalimbali na katika kuzungumza huko, huweza kuusoma moyo mtu, na mimi niliwahi kupata access ya kuzungumza face to face na Rais Uhuru Kenyatta, hivyo...

Naomba kuchukua fursa hii kuwasisitiza Watanzania wenzangu kuwa nimeusoma moyo wa Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya, anaupendo na Watanzania. Kenya ni jirani mwema. Rais Uhuru Kenyatta, anatupenda Watanzania na ndie yeye alianza kufungua mipaka yake kwa Watanzania sio tu kuingia Kenya bila viza, bali hata bila passport, kitambulisho tu cha taifa zinatosha, tena hadi aka joke mko huru kuwaoa wanawake wao!

Hebu msikilize kwa makini Uhuru Kenyatta anasema nini hapa, je unajua anayezungumziwa ni nani?
Msikilize.



Huyo anayezungumziwa hapo, sii mwingine, bali ni Dr. John Pombe Joseph Magufuli kufuatia track record yake kwenye ujenzi wa taifa letu.

Rais Uhuru Kenyatta amesisitiza upendo, Umoja, mshikamano na ushirikiano kati ya Wakenya na Watanzania katika kujenga Jumuiya moja ya Africa Mashariki.

Pia amethibitisha anampenda Magufuli na anamkubali sana, kwa track record ya kuijenga Tanzania na kuna kitu rais Uhuru Kenyatta ametusisitiza dish Watanzania tukifanye hapo mwezi October, naomba nisikiseme hapa ila kama kuna mwenye
masikio na asikie!.

Namalizia kwa kuwasisitiza Watanzania wenzangu, despite all the odds, bado tuwe na upendo kwa majirani wetu wote, leo kwako, kesho kwangu, tutumie njia za kidiplomasia kwanza katika kutafuta ufumbuzi wa sintofahamu yoyote, ofcourse kwa kutanguliza mbele Tanzania kwanza na maslahi ya taifa, upendo kwa majirani, upendo kwa wote, tutakuwa na amani, na tutabarikiwa sana!

Nawatakia Jumapili njema

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali
 
Pascal Mayalla,

Ni kweli na Tz sio adui wa Kenya isipo kua awamu hi hatuna sere ya kimataifa inayojulikana( foreign policy) tumejikuta kwenye counter reaction tena ya kishamba inayo onyesha kwamba viongozi wetu hawana exprience ya dipulomasia na PR, ila Kenya na Tz kila mtu anategemea mwenzie sana na watakua majirani siku zote hamna haja ya kuzozana
 
Ingawaje Watu, hususani Wafuasi wa JPM na CCM wanashangilia kwa tambo na majigambo ya kuamini wamemtia adabu Kenyatta, kwa upande wangu, na kwa mara nyingine nimemuogopa zaidi Kenyatta!

Wakati wa Mkapa (RIP), Tanzania tuliiwekea vikwazo Burundi! Yaani tunaiwekea vikwazo nchi inayotumia bandari yako! Nilipata kusema hapa, ingekuwa KE, katu wasingekubali upuuzi ule ambao TZ tuliufanya!
 
Tunampamba tu Magufuli lakini kusema ukweli jamaa hatoshi, hana management na leadership skills.

Ataishia tu kuteua na kutumbua watu lakini shida inaanzia juu kabisa ya pyramid.
Wewe akili ,macho na masikio yako yapo kwenye uteuzi na kutengua, vingine vya muhimu zaidi huvioni, huvisiki, wala kuvifikiria, basi utakuwa Bwana au Bibi hamnazo.
 
Naunga mkono hoja, kwa maoni yangu Tanzania tume overreact, kulikuwa hakuna sababu, siyo jinsi ambavyo watu matured wanavyopaswa kutatua matatizo, inanikumbusha ex girlfriend wangu, ilikuwa nikikosea kidogo tu hata kama tumepishana kidogo sana hiyo revenge yake unaweza kujiua, alikuwa immature, ...
 
Back
Top Bottom