Uhaba wa dawa za kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi Kenya wahatarisha maisha

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,280
Wakenya wanaoishi na VVU wanasema maisha yao yapo hatarini juu ya uhaba wa dawa za kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi kutokana na mzozo unaotokota kati ya serikali ya Kenya na Shirika la msaada la Marekani USAID.

Kulinga na wanaharakati kucheleweshwa kwa dawa hiyo ni baada ya serikali ya Kenya kuongeza ushuru kwa misaada huku Shirika hilo la USAID likitilia shaka madai ya rushwa yanayohusishwa na Mamlaka ya Kitaifa ya Vifaa vya Tiba.

Hata hivyo Mamlaka hio imesema imesuluhisha tatizo lililokuwepo na tayari imesambaza dawa za kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi katika kauti 31 kati ya 47 na baada ya siku 5 watakuwa na dawa zinazohitajika za watu milioni 1.4.

Waziri wa Afya Mutahi Kagwe, amesema Shirika la USAID limependekeza kutumia kampuni ya Kimataifa ya Chemonics kununua na kusambaza dawa hizo kwa Wakenya kutokana na ukosefu wa uaminifu na Mamlaka ya Kitaifa ya Vifaa vya Tiba.
 
Wangekuwa wajukuu wa nyerere ,wangesema si watuache tu tufe Hawa mabeberu
 
Ukimwi haulipi tena Kenya. Kitu uviko-19 ndiyo story ya mujini. Uviko-19 imewafanya wajasiliamali watoe kinga toka Urusi.
 
Back
Top Bottom