Watanzania sijui mmelogwa?Lini mtakuwa wajanja kama majirani zenu?Mimi bado ninamtetea Mengi na hoja yake ya Wazawa wamiliki vitalu vya gesi na mafuta,Najua Watanzania wengi hawana uwezo wa kumiliki hivyo vitalu hivyo ushauri wangu ungekuwa hivi;Ianzishwe kampuni ya umma ambayo itamilikiwa na Watanzania mbalimbali kupitia ununuzi wa hisa kisha hiyo kampuni iingie kwenye umiliki wa vitalu vya gesi na mafuta;Wafanyabiashara wakubwa wazawa wa nchii waunganishe nguvu kwa kuunda kampuni moja itakayojihusisha na gesi na mafuta;Na serikali iwadhamini/iwafadhili Wazawa katika kumiliki vitalu na hatimaye kuchimba mafuta na gesi.Tunajua kuwa Watanzania wengi hawana uwezo wa kuchimba mafuta na gesi hivyo watalazimika kuingia ubia na makampuni ya nje yenye kujihusisha na shughuli za uchimbaji mafuta na gesi.Hapa Wazawa watamiliki vitalu wakati Wageni watamiliki teknolojia na biashara itafanyika.Hata hili nalo ni gumu kufanyika isipokuwa kuwapa Wageni umiliki wa rasilimali zetu kwa 100%?
TPDC wamepewa jukumu hilo na wazawa wote wameambiwa waende huko, sasa sijui kwa nini baadahi ya wazawa wenzetu wanataka wapewe vitalu vya kwao peke yao.