Ugomvi wa Mengi na Prof. Muhongo nani msuluhishi?

Ileje

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
6,015
2,000
Kuna msuguano mkubwa baina ya Mengi na Muhongo ambao unatishia uchumi wa taifa katika sekta za madini na nishati!

Si serikali wala bunge wanaochukuwa hatua za kuusuluhisha ugomvi huu!

Kutokana na maelezo ya Mbatia katika bunge la bajeti leo ugomvi baina ya watu hawa unahatarisha uwekezaji wa wazawa katika sekta za madini na nishati!

Kwa nini serikali, kwa maana ya Pinda na JK hawachukuwi hatua za kumaliza sintofahahamu hii?!
 
RealMan

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
2,367
1,250
Kumbukumbu inaonyesha michuano yote baina ya Mengi na baadhi ya viongozi huwa droo ama kiongozi wa serikali hupigwa KO.

Alikuweko Masilingi, Malima, Muhongo, yule wa polisi na of coz Manji.......
 
Kamundu

JF-Expert Member
Nov 22, 2006
3,698
2,000
Hakuna ugomvi kwa kuwa mpinanaji ni mengi pekee. Mengi sijajua bado kama anataka kusaidia Watanzania au kujisadia mwenyewe.Kama sera ya umiliki wa vitalu inatakiwa kuruhusiwa basi Watanzania wote waliochukuliwa maeneo yao kwa manufaa ya umma warudishiwe.
 
adobe

JF-Expert Member
May 6, 2009
2,133
2,000
Muhongo ni profesa mwathirika wa ubongo.na ndyo wateule anaowataka Jk. Kwa kuwa mitindio yao ni msukule kwa bwana wake.
 
Mfukua Makaburi

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
3,334
2,000
Mengi anataka kutuibia kwa kisingizio cha uzawa,hana hela ya kuwekeza kenye gesi,anataka apewe kitalu kisha awe dalali,akiuze kwa wawekezaji wengine. Mengi ni mnafiki. Prof Mhongo komaa,nakuombea Mungu akupe nguvu na afya,akulinde..

Imeishaonekana kitaalam hela inayohitajika kwenye uwekezaji mengi hana hata robo,sasa analia nini?anataka matakwa yake binafsi ionekane ni matakwa ya watanzania wote. Mengi kafie mbele,serikalini wanamjua ni mnafiki mkubwa,hana la maana.

Sasa amebaki kuwahonga wabunge wenye njaa kama mbatia wakajiropokee bungeni ili ionekane anaonewa. Watu wenye akili hili wanalijua.
 
kiumbe mzito

Member
Jan 3, 2014
62
95

Toa jina tukujue wewe unaeshangilia watu wa nje tu kuwekeza tz huo ni utumwa wa fikra na ndio utumwa mkubwa zaidi duniani
 
Sipendi Ubepari

JF-Expert Member
Jan 12, 2012
249
0
mengi anataka kutuibia kwa kisingizio cha uzawa,hana hela ya kuwekeza kenye gesi,anataka apewe kitalu kisha awe dalali,akiuze kwa wawekezaji wengine. Mengi ni mnafiki. Prof mhongo komaa,nakuombea mungu akupe nguvu na afya,akulinde..

Imeishaonekana kitaalam hela inayohitajika kwenye uwekezaji mengi hana hata robo,sasa analia nini?anataka matakwa yake binafsi ionekane ni matakwa ya watanzania wote. Mengi kafie mbele,serikalini wanamjua ni mnafiki mkubwa,hana la maana.

Sasa amebaki kuwahonga wabunge wenye njaa kama mbatia wakajiropokee bungeni ili ionekane anaonewa. Watu wenye akili hili wanalijua.

thibitisha pasipo na shaka juu ya mbatia kuhongwa na mengi, VINGINEVYO NA WEWE UNATETEA UDHALIMU WA CCM DHIDI YA WAZAWA WA NCHI HII.
 
Mfukua Makaburi

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
3,334
2,000
Toa jina tukujue wewe unaeshangilia watu wa nje tu kuwekeza tz huo ni utumwa wa fikra na ndio utumwa mkubwa zaidi duniani

ukitaka jina ntakwambia ila uniambie kwa nini unalitaka.

Sio kweli kua natetea wawekezaji wa njee ila penye ukweli lazma tuwe wakweli tuache unafiki. Kama mahitaji/vigezo vya kua mwalimu wa chuo kikuu ni kuanzia digrii ya uzamivu(phd) wewe umemaliza darasa la saba au form 4 hiyo kazi unaitaka wakati vigezo huna ukinyimwa ulaumu,ulie kwamba mzawa unanyimwa fursa??.

Imeonekana kitaalam mahitaji ya kifedha(financial resources) ya uvunaji wa gesi hakuna mtanzania anaweza kukidhi vigezo,sasa wakipewa watafanyaje kuvuna hiyo gesi?. Wanataka,hasa mengi apewe kisha awe dalali,akatafte wawekezaji. Huo utakua ni ujuha kama tunaweza kufanya uwekezaji wa aina hiyo.

Wewe niambie wazawa wakishapewa vitalu hiyo gesi wataivunaje wakati hawana hela? Tusipende kulaumu upuuzi.
 
Unadhani hao wawekezaji wanakuja na hela kwenye mabegi na wao wanakopa ktk kuwekeza kwao.Kwa hiyo unadhani wawekezaji wa ndani hawakopesheki mtanzania uko karne gani hakuna wenye mitaji na hata ukiwa nao ni lazima ukope
 
Mfukua Makaburi

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
3,334
2,000
thibitisha pasipo na shaka juu ya mbatia kuhongwa na mengi, VINGINEVYO NA WEWE UNATETEA UDHALIMU WA CCM DHIDI YA WAZAWA WA NCHI HII.

Wazawa wapi,Mengi ndie wazawa?mbatia hakutakiwa kuropoka,tena halikua swali lake,tena swali halikuhusu gesi,ni chumvi yeye akajiropokea Mengi anaonewa,kwa hiyo anayeitaka gesi ni Mengi na sio wazawa.

Mengi leo hii na wazawa wenzake wanavyojiita(inajulikana mengi anatumia mgongo wa wazawa kutaka ajinufaishe) wakipewa vitalu vya gesi watavifanyaje ili gesi itoke?hawana hela. Mwisho wataenda kutafta wawekezaji nje,na huo udalali ndio haukubaliki. Sio ulilie nyama ya mfupa na meno huna alafu upewe kisha umtafte mwingine aile. HILO JAMBO HALIKUBALIKI.
 
Mfukua Makaburi

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
3,334
2,000
Unadhani hao wawekezaji wanakuja na hela kwenye mabegi na wao wanakopa ktk kuwekeza kwao.Kwa hiyo unadhani wawekezaji wa ndani hawakopesheki mtanzania uko karne gani hakuna wenye mitaji na hata ukiwa nao ni lazima ukope

Mengi aache unafiki wa kutufitinisha....hili jambo la gesi hakuna mzawa ataweza hata kama atakopa. Alafu mengi anajulikana,hakuna benki itakayokua tayari kumkopesha zaidi ya dola mil 100 maana huwa halipi madeni kwani muda wowote anaweza kutangaza kufilisika ili akwepe kulipa deni na akwepe kodi.
 
Elungata

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
36,041
2,000
Hakuna ugomvi kwa kuwa mpinanaji ni mengi pekee. Mengi sijajua bado kama anataka kusaidia Watanzania au kujisadia mwenyewe.Kama sera ya umiliki wa vitalu inatakiwa kuruhusiwa basi Watanzania wote waliochukuliwa maeneo yao kwa manufaa ya umma warudishiwe.
mengi ataanzisha kikundi kama cha Niger delta kule mtwara we acha waendelee kumkenulia meno
 
Swat

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
4,202
2,000
Kama pesa inayotakiwa kuwekeza Mengi anayo,mbona Prof. Muhongo,kashamuambia aende mara moja TPDC akalipie apewe kitalu?. Hii mipasho ya kila siku ya nini. Ukiona mtu anaongea sana hafanyi vitendo,ana lake jambo!
 
FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
71,292
2,000
Mengi ni mtu mmoja mwenye tamaa sana sijapata kuona. Halafu ni mnafik, eti anatumia kibwagizo cha uzawa ili apate sympathy.

Muhongo uzuri wake anampa za uso waziwazi.

Mengi kishakorofishana na kila mtu ambae anaona kwanini huyu kwanini siyo "mimi". Ana ubinafsi, uchoyo na roho mbaya sana. Hata sura yake inaonesha.
 
Elungata

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
36,041
2,000
Halafu mbatia anakubali kufanywa mdomo wa mengi bila hata aibu.
Body language ya mbatia inaonyesha amelipwa kitu ili afikishe message ndo maana hata alipoambiwa kaa chini akalazimisha kumaliza kudeliver message.
Kama watu kama mbatia wanaanza kutumika na matajiri bado hata hawajakamata madaraka,sijui inakuaje iwapo watakamata madaraka.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom