The Evil Genius
JF-Expert Member
- Mar 21, 2014
- 6,151
- 20,077
Ni jukumu la serekali kuweka mazingira na sera stahili ili kusaidia uwekezaji hasa kwa wazawa kwani sio siri kwamba akipata mzawa sehemu kubwa itabaki hapa.Ni kweli kwamba uwekezaji wa gesi na mafuta ni mkubwa kipesa lakini endapo moja ya masharti ingekuwa ni lazima mwekezaji awe na wazawa ie sehemu ya share zimilikiwe na wazaw hudhani kwamba hilo lingewezekana- wewe ukaweka 100 yako, mimi ya kwangu, yule ya kwake; ingewezekana kabisa na sisi tukawa ni sehemu ya wamiliki.Lakini usisahau pia kama mwekezaji anakuja na pesa na sisi tuna gesi/mafuta, tunategemeana na sio kwamba wao ni bora kuliko sisi!!!
Nakubaliana na wewe mkuu kua ni jambo jema serikali kuboresha mazingira kwa wawekezaji wa ndani,nakubaliana nawe kabisa mkuu.
Hili la gesi hali ni tofauti kidogo mkuu,linahitaji mtaji mkubwa sana kaka. Alafu ni risk sana maana unaweza kuwekeza kwenye kitalu kisha kikawa hakina gesi ya kutosha kwa muda au kisiwe commercial kabisa. Utakua umepata hasara kubwa ya mabilioni ya shilingi kama sio matrilioni.mwenyewe unajua serikali haiwezi kushiriki mchezo wa kubahatisha au kufadhili kwa pesa yake watu wakabahatishe.
Ndio maana serikali inataka mtu aje na mtaji wake yeye mwenyewe,likibuma ime imekula kwake mwenyewe na isishiriki kupoteza mabilioni ya watu masikini.
Kujenga kiwanda cha kuzalisha gesi(plant) unahitaji karibu bajeti ya tanzania. Hata hizo pesa za kuwafadhili tunazitoa wapi maana hata waende kwa mganga wazawa hatuwezi kuvuna gesi mkuu. Mahitaji ya kifedha ni makubwa mkuu hata serikali haiyawezi.