Sheria na sera hizohizo ndizo zimeliona hilo na zimetutaka tuingie kwenye uwekezaji wa gesi kupitia STAMICO au TPDC wala siyo kuleta ujanja ujanja.
Hili ndilo akina Mengi & Co hawataki kulisikia. Tujiulize sana UZALENDO na UZAWA wa Mzee wetu Mengi ni upi hasa?
-Mzee Mengi aliitesa NBC wakati likiwa ni shirika la UMMA akaharakisha kifo na ubinafsishaji wake wa ajabu. Aliikopa NBC halafu akaipeleka mahakamani.
-Mengi aliwakamua WATANZANIA masikini kabisa kwa mchezo wa kitapeli wa jackpot bingo. Aliangalia ukwepaji rahisi wa kodi kupitia michezo ya kubahatisha akatutafuna kwelikweli.
-Mengi alipoanzisha ITV hakutaka TBC ipewe matangazo ya biashara kwa kisingizio kuwa TBC inaendeshwa kwa kodi zetu. Kimsingi, alitaka TBC1 ife mapema tu.
-Mengi alitaka kuwamaliza kabisa wale vijana wa ZE COMMEDY walipoamua kuondoka EATV.
-Mengi amegombana na kila waziri aliepishana au kugongana naye kwenye maslahi yake binafsi. Wapo akina Lowasa, Masilingi, Shamim Khan, Mramba na sasa Muhongo.
-Mengi aliwahi kutangaza kuwa anakaribia kuuawa na Wahindi wa CTN kwa ajili kugombea kuonyesha kombe la Dunia mwaka 1994.
-Ushiriki wa Mengi kwenye NICOL hadi leo ni utata mtupu.
Mzee wetu Mengi kila anapokwama kwenye madili anatumia vyombo vyake vya habari kuwachafua mawaziri huku akimchekea Rais. Hata ule mradi wake wa mafisadi papa baadae yeye akawa nyangumi ilikuwa ni katika kutafuta huruma ya WATANZANIA.
Uzalendo wa Mengi uko wapi endapo haoni kuwa TPDC na STAMICO zinaweza kusimamia maslahi ya WATANZANIA kwenye uwekezaji mkubwa wa gas na madini?
Angalieni pia na aina ya watu wanaomtetea Mengi. Yapo mashaka na maswali mengi tu juu ya watu hawa lengo hasa ni nini. Ni UKABILA? Ni kuhongwa na kununuliwa tu? Ni nini hasa?