Ugenini kuna kunguni, sijui nifanye nini!

Ugenini kuna kunguni, sijui nifanye nini!

Hivi kweli kuna kitu kunguni ama ni myths tu? Yani siamin
 
Dama rahisi ya kunguni mafuta ya taa ukimwagia tu anakauka kwa wale wanaobana kwenye nyufa za kitanda nunua silinge unavuta mafuta na kuwanyunyiza ila ni zoezi la kila siku kwani mafuta hayaharibu mayai hivo unasubiri wakianguliwa unawa baada ya siku chache hutawaona utalala unono: tahadhari weka mbali mshumaa na kibatari si unajua mafuta tena
 
Hao kunguni n lazima uwahamishie kwako. Kama unataka wasihamie kwako,choma nguo zote ulizoenda nazo na usizingize ndani
upload_2016-10-12_18-41-18.png
 
Dah secondary tulikuwa tunaita mifugo...ilikuwa balaa unakuta mayai kwenye pindo za chupi!!
 
Kesho kanunue dawa ya kupulizia tu na kupulizia chumba kizima
 
Hahaaaa majibu ya watu yamenifanya nicheke kidogo,mimi naona kama unaweza waite wenyeji wako,chagueni siku moja mfanye usafi kwani kunguni ni sababu ya uchafu,
Kuwatangaza humu si busara ila kushiriki nao usafi,dawa ipo madukani.
 
Hahahaha, nimekumbuka nlivomaliza form four nlikua na safari ya kwenda mbeya, enzi hizo ikanolazimu nilale Dodoma.Ugenini nimelala kwa mara ya kwanza naskia vitu vinachoma choma, nkiwasha taa sioni nkizima vinarudi.Kumbe kunguni, nikawaza hapa hapatakucha nliamka nikaenda kumwamsha mwenyeji wangu.Ilibidi wanipe godoro lingine nilale sebleni.
 
Niliwahi kuishi mahali kuna kunguni balaaa

In zaidi ya mateso wakti Wa kulala.

Nilivyorudi home si nikawaleta aiseee

Nyumba nzima walitapakaa hadi kwenye makochi hahahaha


Siku moja home wakaamua kuwafungia kazi.

Walitoa vitu vyotr nje wakavimwagia maji ya moto kwa Siku mbilj mfulilizo na kuwekwa juani

Nyumba nzima illipigwa dawa kwa siku mbili mfululizo

Hadi Leo hakuna na hata kipisi cha kunguni maisha raha kabisa[emoji2]
 
Nashindwa kuelewa hii nyumba niliyofikia hawa wenyeji wangu wanapata vipi usingizi. Kunguni niliowaona baada ya kulinyanyua godoro ni wengi utadhani mchanga umemwagwa hapo kitandani!

Siwapendi kwa usumbufu wao lakini pia unaweza kuaibika mbele za watu unakuta dudu limeshiba halafu linatembea kwenye nguo zako tena shati jeupe. Naona noma hata kumwambia jamaa kwa jinsi anavyokuwa akijipaisha. Wasiwasi wangu nisije nikatoka na mbegu hapa.

Nifanyaje?
Mkuu accomodation kwa hotel ,lodge guest house au mchepuko wa ghafla ghafla inahusu hapo!
Wala usiogope waambie hao mifugo kwako no na hela ya dawa waachie !
Ila wenyeji wako itakuwwa wana asili ya mamba maana kustahmili huko either ngozi ngumu au ina ganzi!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom