Ugenini kuna kunguni, sijui nifanye nini!

jmapunda

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2015
Posts
731
Reaction score
2,924
Nashindwa kuelewa hii nyumba niliyofikia hawa wenyeji wangu wanapata vipi usingizi. Kunguni niliowaona baada ya kulinyanyua godoro ni wengi utadhani mchanga umemwagwa hapo kitandani!

Siwapendi kwa usumbufu wao lakini pia unaweza kuaibika mbele za watu unakuta dudu limeshiba halafu linatembea kwenye nguo zako tena shati jeupe. Naona noma hata kumwambia jamaa kwa jinsi anavyokuwa akijipaisha. Wasiwasi wangu nisije nikatoka na mbegu hapa.

Nifanyaje?
 
Nakushauri ghairi huo mwaliko,utabebana na mikunguni hutaamin.
 
Mtaarifu mwenyeji wako anunue/mnunue dawa ya kunguni au mlianike juani hilo godoro.
 
Waite watu wa fumigation ili wawapulizie dawa na kuwaua hao kunguni, utakuwa umemsaidia sana mwenyeji wako lakini pia na wewe utapata nafasi ya kufanya kazi iliyokupeleka huko
 
Nashindwa kuelewa hii nyumba niliyofikia hawa wenyeji wangu wanapata vipi usingizi. Kunguni niliowaona baada ya kulinyanyua godoro ni wengi utadhani mchanga umemwagwa hapo kitandani!
Siwapendi kwa usumbufu wao lakini pia unaweza kuaibika mbele za watu unakuta dudu limeshiba halafu linatembea kwenye nguo zako tena shati jeupe. Naona noma hata kumwambia jamaa kwa jinsi anavyokuwa akijipaisha. Wasiwasi wangu nisije nikatoka na mbegu hapa.
Nifanyaje?
Move out,waachie ''mifugo'' yao..........
 
Kwani hao jamaa hawaoni hao Kunguni au wenyewe hawawadhuru?
 
Napendaga kale kaarufu ka Kunguni nikimbinya na vidole afu apasuke...naweza nusa vidole all day and all night long!

I wish hata perfumes company watengeneze Kunguni essence, au Kunguni fragrance, Kunguni aroma..I'm me!
 
hahahahahaaa pole sana jamaa yangu vumilia kwani uja mshirikisha mtu hata mmoja. ukilala lala na boxer na ukitoka kuoga ussivae chagua boxer moja au nguo moja kwa ajili ya kulalia tu. ukiamka unaivua unavaa safi
 
  • Thanks
Reactions: MC7
Kunguni, mende na panya ndiyo huwa wanatajwa tajwa kuwa wana uwezekano wa kusavaivu ikitokea dunia ikapigwa na jiwe jingine kama lile lililopiga Yucatan Peninsula likaondoka na akina dinosaur. Jamaa wanaweza kuibuka popote anytime. Mahoteli mengi kule US Baby mwaka jana wamehenya kweli kupambana nao.

Uwezekano wako wa kuondoka na mbegu hapo ni asilimia 100. Ukifika tu home loweka kila kitu kwenye maji ya moto (nguo, begi n.k) na uwe makini kuwa unaaangalia godoro mara kwa mara. Bahati nzuri huwa hawaenezi magonjwa mengi otherwise tungekuwa tunaongea mengine.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom