Camilo_Cienfuegos
JF-Expert Member
- Sep 9, 2011
- 11,378
- 15,384
Hali ni tete katika mahusiano kati ya Rwanda na Uganda.
Ikumbukwe tu nchi zote hizi mbili ni "dola za kijasusi" kutokana na backgrounds za watawala wake (both Kagame na Museveni ni majasusi wabobevu).
Nchi zote mbili ni majirani zetu na wanachama wenzetu kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Sio siri kuwa Jiwe na Kagame ni kama chanda na pete, japo pia uhusiano wa Jiwe na Museveni sio mbaya.
Pengine Rwanda na Uganda zikiingia vitani haitotuathiri kwa lolote lakini what if Kagame akitaka kumtumia Jiwe/kuitumia Tanzania kama PROXY? ("Proxy war" ni vita ambapo nchi zenye uadui zinapigana bila zenyewe kuwepo vitani moja kwa moja. Mfano wa proxy war ni Yemen na Syria ambapo Iran na Saudia technically zipo vitani huku Yemen na Syria zikiwa ndio "proxies").
Lakini pia nchi inaweza kuwa "proxy" katika scenario hii (God forbid)- Rwanda na Uganda zaingia vitani, kisha Burundi ikaiunga mkono Uganda (kwa sababu ya uhasama baina ya Kagame na Nkurunziza) na sie tukaiunga mkono Rwanda (kwa sababu ya uswahiba kati ya "Mtu Mrefu Paulo" na Jiwe)
Kijasusi, tayari Rwanda na Uganda wapo vitani. Vita ya kijasusi. Na "kwa vile Dar imesheheni majasusi wa mataifa mbalimbali kama ilivyo Brussels, Ubelgiji (soma zaidi hapo chini)" basi nayo technically ni sehemu ya vita hiyo.
I hope busara zitatawala kwa wahusika kuepusha vita kati yao.
#FoodForThought
Sent using Jamii Forums mobile app
Childish analysis

