Uganda Vs Rwanda kimenuka

Uganda Vs Rwanda kimenuka

Kumbuka tz pia ina dili la SGR na Mr slim
Vita ikianza sioni Rwanda ikishinda kwasababu tatu tu.
1. Burundi na yeye atatumia huo mwanya kuvamia Rwanda.
2. Wahutu watambadilika Kagame.
3. Tanzania kwa siri tutamsaidia Uganda kwasababu ya bomba la mafuta.

Sent using my iPhone using jamiiforum app
 
Uganda inawaunga mkono,ma generali waliotoka jeshi LA Rwanda,wanaoishi uhamishoni SA,
Hao ma soldiers,wanataka kumchomoa Kagame ikulu,
Hapo hakuna maelewano tena,mpaka Kagame achomoke.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hao ma General walimuasi pk wapo wangap huko South

Zipi dalili za kuwa wanataka kumchomoa Mr slim ?

Sent using my iPhone using jamiiforum app
 
Hali ni tete katika mahusiano kati ya Rwanda na Uganda.



Ikumbukwe tu nchi zote hizi mbili ni "dola za kijasusi" kutokana na backgrounds za watawala wake (both Kagame na Museveni ni majasusi wabobevu).

Nchi zote mbili ni majirani zetu na wanachama wenzetu kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Sio siri kuwa Jiwe na Kagame ni kama chanda na pete, japo pia uhusiano wa Jiwe na Museveni sio mbaya.

Pengine Rwanda na Uganda zikiingia vitani haitotuathiri kwa lolote lakini what if Kagame akitaka kumtumia Jiwe/kuitumia Tanzania kama PROXY? ("Proxy war" ni vita ambapo nchi zenye uadui zinapigana bila zenyewe kuwepo vitani moja kwa moja. Mfano wa proxy war ni Yemen na Syria ambapo Iran na Saudia technically zipo vitani huku Yemen na Syria zikiwa ndio "proxies").

Lakini pia nchi inaweza kuwa "proxy" katika scenario hii (God forbid)- Rwanda na Uganda zaingia vitani, kisha Burundi ikaiunga mkono Uganda (kwa sababu ya uhasama baina ya Kagame na Nkurunziza) na sie tukaiunga mkono Rwanda (kwa sababu ya uswahiba kati ya "Mtu Mrefu Paulo" na Jiwe)

I hope busara zitatawala kwa wahusika kuepusha vita kati yao.

#FoodForThought

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah....
Vita ikipiganwa itakuwa ngumu sana hii.

Sidhani kama Tanzania inaweza kumuacha Mganda na kumkumbatia Mnyarwanda.
Uganda katika ukanda huu hana rafiki wa kweli ambaye anaweza kukimbia kuomba chumvi mambo yanapokuwa magumu zaidi ya Tanzania, na hili Tanzania inalijua.

Heshima ya Tanzania Uganda ni kubwa sana, hasa kwenye majeshi yao.

Kinachonisikitisha ni mbinu ya kijasusi inayotaka kutumika hapa.

Kwamba Rwanda anataka kumwaga ugali wa Museveni kwa kuipindua dola ya Buganda isiwe ruling class ndani ya Unganda, wakati huo Museveni naye anataka kumwaga mboga kwa kuhakikisha power inahama kutoka kwa watusi kuingia kwa wahutu.
Patamu sana hapo.


Kwa mbaali namuona Nkurunzinza akichekelea mpaka jino la mwisho.
 
Rwanda imewasihi wananchi wake kusitisha ziara na biashara nchini Uganda

_105878613_97f14b6e-5bfb-4f6d-b52d-0606bae92c09.jpg
Haki miliki ya pichaUGANDA MEDIA CENTRE
Serikali ya Rwanda imewasihi wananchi wake kusitisha ziara zao nchini Uganda baada ya kuishtumu nchi hiyo kuwanyanyasa raia wake wanaoishi ama kutembelea nchini humo.
Uganda imeishutumu Rwanda kufunga mipaka baina ya nchi mbili,lakini Rwanda imekanusha na kusema mipaka iko wazi.
Alhamisi iliyopita mamlaka ya mapato ya Rwanda iliamrisha maroli ya mizigo kutotumia tena mpaka wa Gatuna kwa madai ya shughuli za ujenzi wa kituo kimoja cha mpakani 'one stop border' baina yake na Uganda.

Kwa mjibu wa mamlaka ya mapato ya Rwanda malori yaliombwa kutumia mpaka wa pili wa Kagitumba kaskazini mwa Rwanda.
_105878615_8ec82a48-450e-4088-8f7b-4c14507248f9.jpg
Haki miliki ya pichaUGANDA MEDIA CENTRE
Hata hivyo watumiaji wa mipaka hiyo miwili hupendelea njia ya mpaka wa Gatuna kuwa rahisi na fupi kuliko ya mpaka wa Kagitumba.
Nchi mbili zinaendelea kurushiana lawama.
Rwanda inaishutumu Uganda kunyanyasa wanyarwanda wanaoishi ama kufanyia biashara nchini Uganda na pia kuunga mkono makundi ya waasi hususani kundi la Rwanda National Congres linaloongozwa na mkuu wa zamani wa majeshi Jenerali Kayumba Nyamwasa aliyeko uhamishoni nchini Afrika kusini.
Kwa upande mwingine, Uganda inashutumu Rwanda kwa vitendo vya kijasusi kwenye ardhi yake huku ikiwashuku baadhi ya raia wa Rwanda kuhusika na vitendo hivyo.
_105880417_81aa09f8-504e-45f2-a8af-355f079304ed.jpg
Haki miliki ya pichaUGANDA MEDIA CENTRE
Mkwamo wa shughuli katika mpaka wa Rwanda Uganda.
Eneo hilo lina umuhimu mkubwa kibiashara kieneo.
Ni eneo ambalo huruhusu kupita kwa bidhaa kutoka mji mkuu wa Uganda Kampala, au Mombasa pwani ya Kenya.
Wakaazi hapo wanasema ni kama 'ghala kwa biashara kutoka maeneo hayo'.
Akizungumza na BBC, Diwani Abel Bizimana katika eneo la Kisoro anaeleza kwamba, 'Hali haijabadilika. Tunaathirika kama viongozi wa kieneo, kama jumuiya ya wafanyabiashara na wateja pia tunaowahudumia.'
Abel ameeleza kuwa maisha yamebadilika pakubwa.

Kutokana na matatizo ya kibiashara na udhibiti wa watu kutoka na kuingia katika eneo hilo, watu ambao kawaida huja kupokea bidhaa kutoka mjini na wilaya ya Kisoro sasa inaarifiwa hawaji tena, wakiwemo hata waendesha boda boda ambao pia wamesitisha shughuli zao.
Siku mbili kuu za soko katika eneo hilo, Jumatatu na Alhamisi, ambazo hushuhudiwa shughuli nyingi za kibiashara, 'sasa limekuwa kama jangwa', anaeleza diwani Abel.
Usafiri wa mabasi umepungua pakubwa, bidhaa zinaharibika.
Wafanyabiashara wanaobeba mihogo au samaki wanapata hasara katika mpaka kwasababu mali zinaharibika.
'Nilipofika mpakani, nilihisi harufu kali ya samaki waliooza katika eneo hilo' ameongeza Abel.
Wiki iliyopita, msemaji wa serikali ya Uganda Ofwono Opondo ameiomba Rwanda kuruhusu wafanya biashara kuingiza bidhaa ili kuepuka hasara na uhasama zaidi.
Kwa upande wake Waziri wa maswala ya kigeni wa Rwanda, Richard Sezibera amenukuliwa akidai kuwa serikali ya Uganda inawadhulumu raia wa Rwanda wanaoishi Uganda.
 
Hakuna Vita Hapo ila Nkurunziza achunge anaweza kuwa yeye ndie anayepigiwa hesabu Ndefu na Askari wake wanaorudi kutoka kwenye AMISOM wameshapangwa ili kumtoa Nyoka Pangoni Usicheze na Inkhotanyi zikiamua.


Kabisa tuko pamoja pale ni vita vya kijasusi kuna MTU atolewe kafara kwa faida ya M7 na Mr Slim kama walivochapana GOMA na Kivu wakigombea kupora Congo
 
Kabisa tuko pamoja pale ni vita vya kijasusi kuna MTU atolewe kafara kwa faida ya M7 na Mr Slim kama walivochapana GOMA na Kivu wakigombea kupora Congo
Nadhani Kikwete anacheka sana anajua game inavyochezwa ila huyu wa sasa huenda saa hizi anakula mahindi ya kuchoma ya Mo Enterprises Hahahahaa!!
 
Back
Top Bottom