Uganda Vs Rwanda kimenuka

Uganda Vs Rwanda kimenuka

Hali ni tete katika mahusiano kati ya Rwanda na Uganda.



Ikumbukwe tu nchi zote hizi mbili ni "dola za kijasusi" kutokana na backgrounds za watawala wake (both Kagame na Museveni ni majasusi wabobevu).

Nchi zote mbili ni majirani zetu na wanachama wenzetu kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Sio siri kuwa Jiwe na Kagame ni kama chanda na pete, japo pia uhusiano wa Jiwe na Museveni sio mbaya.

Pengine Rwanda na Uganda zikiingia vitani haitotuathiri kwa lolote lakini what if Kagame akitaka kumtumia Jiwe/kuitumia Tanzania kama PROXY? ("Proxy war" ni vita ambapo nchi zenye uadui zinapigana bila zenyewe kuwepo vitani moja kwa moja. Mfano wa proxy war ni Yemen na Syria ambapo Iran na Saudia technically zipo vitani huku Yemen na Syria zikiwa ndio "proxies").

Lakini pia nchi inaweza kuwa "proxy" katika scenario hii (God forbid)- Rwanda na Uganda zaingia vitani, kisha Burundi ikaiunga mkono Uganda (kwa sababu ya uhasama baina ya Kagame na Nkurunziza) na sie tukaiunga mkono Rwanda (kwa sababu ya uswahiba kati ya "Mtu Mrefu Paulo" na Jiwe)

Kijasusi, tayari Rwanda na Uganda wapo vitani. Vita ya kijasusi. Na "kwa vile Dar imesheheni majasusi wa mataifa mbalimbali kama ilivyo Brussels, Ubelgiji (soma zaidi hapo chini)" basi nayo technically ni sehemu ya vita hiyo.



I hope busara zitatawala kwa wahusika kuepusha vita kati yao.

#FoodForThought

Sent using Jamii Forums mobile app


Very true Mungu aepushie mbali tatizo hili. Rwanda kwanini walikuwa wanateka Uganda na kurudisha Rwanda? Kwanini PK anaamini Museveni anamsaidia Gen. Kayumba?
Sisi tuwe neutral. Kuna faida nyingi kuliko hasara.
 
Wakianza kuzichapa mimi nitaenda kupigana kumsaidia museveni maana simpendi mwizi kagame hata kama magufuli atamsaidia kagame
 
Dah....
Vita ikipiganwa itakuwa ngumu sana hii.

Sidhani kama Tanzania inaweza kumuacha Mganda na kumkumbatia Mnyarwanda.
Uganda katika ukanda huu hana rafiki wa kweli ambaye anaweza kukimbia kuomba chumvi mambo yanapokuwa magumu zaidi ya Tanzania, na hili Tanzania inalijua.

Heshima ya Tanzania Uganda ni kubwa sana, hasa kwenye majeshi yao.

Kinachonisikitisha ni mbinu ya kijasusi inayotaka kutumika hapa.

Kwamba Rwanda anataka kumwaga ugali wa Museveni kwa kuipindua dola ya Buganda isiwe ruling class ndani ya Unganda, wakati huo Museveni naye anataka kumwaga mboga kwa kuhakikisha power inahama kutoka kwa watusi kuingia kwa wahutu.
Patamu sana hapo.


Kwa mbaali namuona Nkurunzinza akichekelea mpaka jino la mwisho.
Jiwe ataweza kusuluhisha huu ugomvi? Au atamtuma Mkapa ambaye tayari mgogoro mdogo wa Burundi umemshinda?
 
Hili jambo sio jepesi kama vile tunavyolijadili humu, na ukizisoma baadhi ya comments hapo juu unaona kabisa kuna tofauti kubwa ya uwezo wa wachangiaji kwenye mambo ya diplomasia na mahusiano.

Kwanza mtambue hili, sasa hivi watu wanafanya kazi chini chini kuhakikisha hii hali haiendelei.. majasusi wanapanda ndege au tayari wapo Kigali na Kampala kusaidia kuhakikisha hakuna vita. Pili kwa kuwa ni Kenya na Tanzania peke yao ndio stable countries katika ukanda huu, ujue tu kuwa wataubeba huu mzigo wa mashauriano.

Vita ya Uganda na Rwanda HAINA FAIDA YOYOTE KWETU, zaidi sana ni HASARA. Kwanza kukiwa na vita hamna Biashara, bandari zetu na miradi yetu ya miundombinu kwa kiasi kikubwa inategemea sana amani na maendeleo ya biashara katika hizo nchi. Pili wakimbizi, ukiwa unachekelea Ug na Rw kupigana utambue kuwa ni Tanzania ndio itapokea wakimbizi wengi, tegemeeni uhalifu na ujambazi pia kuongezeka... Tatu wao wakiwa hawana amani na sisi pia hatuna amani, hujui ni bomu gani litakosewa likaja kutua Tanzania, ni lazima tutumie rasilimali zetu kulinda mipaka hivyo pesa za miundombinu, hospitali zitaenda kulinda mpaka.. na mengine mengi, bila kusahau masuala ya uhamiaji haramu n.k

So weka mihemko pembeni, ombeni hili jambo lisitokee, vita sio kitu cha kufurahia, sio jambo la kuchekelea.. vita ni damu na hasara, hakuna faida ya vita... uwe unampenda Magufuli au humpendi, ombea sana nchi yako na hekima ya viongozi wetu ili hili jambo liweze kuepukika..

Nahisi pia hili linaweza kuwa ni sababu ya reshuffle ya Foreign Ministry.
 
Back
Top Bottom