Nteko Vano
JF-Expert Member
- Feb 28, 2012
- 434
- 111
Kambale nao wanafugwa?
Hizi ndio mada za kusaidia na kukwamua jamii. Hongera mleta mada.
Nawapigia hao Kingurwila sasa hivi. Nna eka moja Kibaha si inatosha sana kwa hii kazi?
Bora umegundua mapema kuwa chakula unachowapa hakina virutubisho vinavyohitajika. Ngoja niwaulize wataalamu nitakujuza....
mkuu,
ulipanda mbegu gani? isijekuwa ulipanda dagaa au wajanja walikuingiza mjini ukifikiri umenunua vifaranga wa sato kumbe dagaa. Vipi kuhusu pH ya bwawa na aina ya mbegu uliyoipanda, vinaendana? chakula na aina ya samaki vinamatter, pH, space, usafi wa bwawa, hali ya hewa etc samaki wanakula baadhi ya vegetation na si kila aina ya jani by the way kwa maelezo yako inaonekana ulichukulia ufugaji wa samaki kuwa ni rahisi sana [that's biggest mistake you made]
Asanteni sana wadau, mie pia nina bwawa langu la mita kumi kwa kumi,bwawa hiili nilipandikiza vifaranga 200 miezi sita iliyopita bahati mpaya hao samaki mpaka sasa hawajakuwa wakubwa kufikia saizi kubwa,nilikwenda kwa wataalam wa nyegezi walinipa maelekezo mazuri na sasa mambo yanasonga mbele. Mpaka sasa hawa samaki wametotoa watoto wengi sana kiasi cha kutishia udogo wa bwawa hata hivyo nipo mwishoni namalizia uchimbaji wa bwawa kubwa la mita 35 kwa 30 nadhani mwezi ujao nitapandikiza hao fingerings. Kwa hivi sasa ninacho hitaji ni vitabu vitakavyo nisaidia kuielewa zaidi hii kazi maana mie sijasomea,kama kuna mtu anajua wapi naweza kupata vitabu basi anielekeze au kama kuna mtandao wowote ambapo naweza ku downlod hasa vya kiswahili.
Mkuu kambale wanafugwa, japo changamoto ya kambale ni kuwa ukishawafuga hawawezi kuzaliana kwa njia ya kawaida (natural breeding), hivyo unatakiwa uwazalishe (artificial breeding). Teknolojia yake ni rahisi mno wala haiitaji uwe mtaalamu kinachotakiwa ni mafunzo tu kidogo. Ukiweza watembelee wataalam wa Kingolwira utajifunza mengi hata kwa vitendo.
Hizi ndio mada za kusaidia na kukwamua jamii. Hongera mleta mada.
Nawapigia hao Kingurwila sasa hivi. Nna eka moja Kibaha si inatosha sana kwa hii kazi?
Kambale nao wanafugwa?