Ufugaji wa Samaki: Pata ushauri, mawazo na michango kuhusu ufugaji samaki. Jifunze changamoto, utaalamu na masoko ya Samaki

Malila

JF-Expert Member
Dec 22, 2007
5,149
4,675
Wana JF

Tanzania imebarikiwa kuwa na vyanzo vya maji ya asili ikiwemo mito, mabwawa, maziwa, bahari, chemchem nk. Kutokana na vyanzo hivi tunapata samaki wa aina mbalimbali wakiwemo perege/sato, kambale, kambamiti (prawns), vibua, changu, kaa n.k.

Samaki ni chanzo cha lishe, kipato na ajira, tunaweza tukatengeneza vito kutokana na lulu wa chaza. Nimejaribu kuzungukia katika soko letu la fery pale nikagundua akina mama na wadau wengi wanafaidika sana na biashara ya samaki nadhani tunawaona mitaani kwetu lakini wanalalamika bei imekuwa juu na upatikanaji wake ni wa shida sana kulingana na msimu.

Nilijaribu kufuatilia kwa undani suala hili kwa wizara husika nikaelezwa ni kweli bei ya samaki iko juu na upatikanaji wake ni mgumu kutokana na samaki wamepungua kwa kiasi kikubwa na wanapungua kwa kasi ya ajabu...Hali hii inatokana na mabadiliko ya hali ya hewa, uharibifu wa mazingira, nguvu kubwa ya uvuvi iliyopo kwa mfano samaki sangara kutoka ziwa victoria wamepungua sana na wanaopatikana kwa sasa ni wadogo. Pia wizara ililazimika kufunga uvuvi wa prawns kwa meli kubwa kubwa kutokana na hali kuwa mbaya. Hata perege wanaopatikana ni wadogo na kwa uchache.

Ili kuokoa suala hili, njia pekee ni kuhamasisha UFUGAJI WA SAMAKI kwa ajili ya kipato, ajira na chakula. Nimevutiwa na suala hili nikaona niwashirikishe wana JF. Nchi za asia china, ufilipino, japan, indonesia fani hii imekuwa sana na wananchi wanajikwamua kiuchumi kutokana na ufugaji wa samaki.

Bado ninafanya ufuatiliaji wa karibu kuhusu suala hili la ufugaji samaki na jinsi tunavyoweza kufaidika nalo. Ninaamini tunaweza kufuga na kupata faida kubwa pia tukatunza mazingira yetu ya asili.

Wakati naendelea kufuatilia suala hili naomba mwenye taarifa basi tushirikiane hapa JF. Nitarudi tena kwa maada hii mara nitakapokusanya taarifa ndani ya siku chache.

Nawasilisha kwa michango yenu.

Nteko Vano Maputo

Penye nia pana njia





 
jambo moja Rahisi sana kwako juu ya mabwawa ya Uvuvi ni kwa wewe kuwasiliana na Idara ya Uvuvi kitengo cha ufugaji viumbe kwenye maji pale Vertinary Temeke, Wizara ya maendeleo ya Uvuvi na Mifugo watakuelimisha vyema maana wao wamesome hayo mambo kwa kina, wanauzoefu wa miaka mingi, watakushauri na mbegu ya kupanda .....kama upo Morogoro nenda kule Kingorwila wanakituo chao pia.

Ha Muji,
 
wazo zuri sana kufuga samaki kibiashara.
Mwaka jana nilianza utafiti jinsi ya kufuga,nashauri uende kunduchi,kuna kitengo cha ufugaji samaki,pia nina rafiki yangu ambaye ni mtaalamu wa samaki,ni PM ntakupa namba yake,na mpange jinsi ya kuonana awe anakupa ushauri.

Fuga samaki wa ziwa victoria-Sato etc kwani wateja ni wengi na pia utakuwa na gharama ya usafiri from kibaha to DAr,
wish u all the best in ur project
 
Kuna wakati nilieleza kuwa nilihudhuria semina ya ufugaji wa samaki kwa kweli nami nilivutiwa sana na waalimu ambao walikuwa wanatoa mada. Kweli kama mtu unataka kufanya biashara ya samaki lazima kweli uwe umedhamiria sana na kuipenda biashara hii (INTEREST).

kwani kama unataka kufuga samaki angalia mazingira yako kama ulivyosema.Umesema kuna maji mengi tu na ninaamini kuwa yanatuama ndio maana ulipochimba wakati wa kiangazi hayakukauka.kwa maana nyingine hapo kwenye eneo lako kuna udongo wa Mfinyanzi ambao unafaa sana kwa kilimo hiki cha samaki.Japo pia unaweza kulijengea vema tu cement na kwa utaalamu bado ukafuga.

Lakini pia unaweza kutengeneza bwawa lako katika vyanzo vya maji vya uhakika kama vijito,chemichemi au mifereji.Pia kwenye udongo unaofaa,eneo lenye mwinuko wa wastani pia lililo karibu na unakoishi kwani bwawa lako linatakiwa kuwa karibu na wewe ili uweze kulilinda na pia kuliangalia kwa namna nyingi kama kulisha chakula n.k pia liwe kwenye eneo lenye miti ili kuleta kivuli.

Hii ni kwa manufaa ya wengine. Kuna umuhimu sana wa kuhudhuria semina hizi zinazotolewa kwani Zinajenga sana na unaendelea kuwasiliana na waalimu wako siku zote.Hawa Africa Upendo Group ndio wanaoendesha semina hizi.kuna njia za kupima udongo kama unafaa.Pia kabla ya kuweka samaki unapaswa kurutubisha bwawa lako vema. yaani liwe na vyakula vya asili vya utosha.unarutubisha kwa kutumia vitu mbalimbali kama mbolea mimea n.k baada ya muda unaweza kupanda vifaranga vyako na kuwapa chakula na mbolea na kuleta ile rangi nzuri ya kijani katika maji na hewa.Samaki anakula vyakula vya kawaida sana ambavyo vinapatikana kirahisi na nikidogo tu bila gharama yoyote kubwa.Hata wadudu bado ni chakula kwao.

samaki hawatakiwi kuwekwa kwenye kina kirefu sana ni kama mita moja tu kwenda chini na inategemea unataka ukubwa gani kama 10 kwa 10 wanaweza kukaa hata samaki elfu kumi hata laki kutegemea na aina ya samaki.Nile-Tilapia ni mbegu nzuri sana kwa biashara hasa ukinzingatia leo kuwa wengi wa wafanya biashara hasa mahotelini wanahitaji gramu 250 ukiwa ndicho kipimo kizuri kwa wateja wengi katika mahotel.utalamu wa kufuga Cat fish au kambale ni tofauti sana kwani wale wanaishi ardhini na huzaana sana wakati wa mvua na mafuriko.Hwazai kabisa kama utawafuga kama hawa samaki wengine.
 
Yaani kambale ni samaki mtamu ajabu Malila umesema.Yaani usipime.

Umenikumbusha pasaka nilienda kwetu toka nimefika hadi naondoka ni supu ya asubuhi chakula cha mchana ama jioni lazima kambale pia awepo pembeni tena ukimpata mwenye mayai yake yaani we acha tu.Tulikula na ndugu zangu hata Nyama haikupata soko sana pasaka hii ni siku ile tu ya jumapili pilau kwa sana.

Ninachozungumzia hapa ni ufungaji wake na maongezeko kuzaliana ndio tatizo.Wanazaa sana na watoto wanatawanyika ama kufa kwa wingi wao lakini bado wanazaa sana.

Cha msingi ni kuwafahamu vema na jinsi ya kuwafunga kutegemeana na Mabwawa uyawekeje ili wazaane
 

Nimetangaza bingo kwa machalii fulani kwamba mtu akiniletea kambale hai hata kama ni mdogo vipi nampa buku tano. Nawatafuta sana hawa samaki. Nimepata sato ila kambale bado. Mategemeo ni makubwa,nikishindwa kuwapata mitaani, nitawafuata mbegani, wapo kule.
 
Shukurani Muanzisha mada, hii mada ni nzuri sana.

Mimi nilitaraji huu wakati hii serikali inaubiri ''kilimo kwanza'' ndio tungekuwa tunapata Makala mbali mbali za kilimo,ufugaji wa wanyama,samaki.lakini wapi TV lao la TBC ni siasa na redio zao zote ni siasa tu ili CCM ishinde. Ukienda kwenye chuo cha kilimo akuna ata sehemu unaweza pata makala za kilimo na ufugaji,yani mambo ayapo kama inavyotakiwa kwa kilimo kwanza.

Mimi nilitarajia wizara ya kilimo itakuwa ata na makala moja kila week kwenye magazeti yote kwa ajili ya kuamasisha na kufundisha watu juu ya kilimo lakini amna same to wizara ya Magufuli amna kitu. Wengine tunapenda kufuga lakini atuna elimu hiyo sasa aka kaela tulikonako kadogo tunaogopa tusijekingiza kwenye ufugaji ikala kwetu.:sick:
 
Mkuu unaendeleaje na samaki kama ulivyoelezea hapo juu. Nimevutiwa sana na moyo wa kushare na wengine vitu vyako.. it is so positive

Nisamehe sana,nilikuwa vijijini kwa muda mrefu kidogo kwa ajili ya mambo yetu haya ya kilimo. Miezi mitatu iliyopita niliweka sato 26 vifaranga,mpaka jana tumerecord sato mmoja kafa,kwa hiyo imenipa nguvu kwamba bwawa langu liko mahali sahihi kabisa kilichobaki ni maboresho,hasa aina ya chakula.

Mwezi juni nilipata Kambale 52,nimewaweka ktk visima vidogo,huku nasubiri bwawa jipya likae sawa,yaani lijijenge kupokea wageni. Kwa mwezi mzima sasa hakuna kambale aliyekufa. Nitakwenda Mbegani/ kunduchi nikachukue shule zaidi ili nifuge kwa wingi. Hapo nitapata mbegu ya kuuza. Mwaka jana kigogo mmoja alikosa mbegu ya kambale,tulitafuta sana bila mafanikio.

Pili,pale Kinguruila gerezani pana mbegu ya samaki inauzwa kwa bei nzuri sana,kifaranga kimoja Tsh 30/ sio 300 kama huku Mkuranga. Contact za mhusika nimepata,kwa aliye tayari aniambie nimpe.

Kwa ujumla ninafurahia kufaulu mtihani wa kwanza,yaani pilot trial niliyofanya.
 
Nimefurahi sana kupata changamoto na wadau katika sekta hii,Kwanza kabisa kuna vitu vya kuzingatia katika utengenezaji wa bwawa.

1.Aina ya Udongo lazima uwe wa Mfinyanzi
2.Maji means uhakika wa maji
3.Sehemu yenye muinuko kidogo
4.Mimea iliyozinguka eneo lako sbb kama kuna miti mingi ndege watakusumbua
5.Njia za mawasiliano means barabara ukizingatia hiyo ni bidhaa inayoharibikia haraka zaidi

BWAWA UNAWEZA KULICHIMBA LENYE UKUBWA TOFAUTITOFAUTI KULINGANA NA UKUBWA WA ENEO HUHUSIKA NA ENEO LAKO LILIVYO,ILA UNASHAURIWA KUCHIMBA BWAWA LENYE UMBO LA MSTATILI

Ni vyema ukamtafuta mtaalamu wa maswala ya uvuvi Makao makuu DSM,NA MIKOANI PIA WAPO WATAALAM WA UVUVI ili uambatane naye kwenye eneo husika sbb vipimo vitabadilika kulingana na eneo.

USHAURI HYUWA NI BURE HAKUNA GHARAMA YOYOTE SSB HILO NI ENEO LAKE LA KAZI
 
Nashukuru kwa msaada wa material hizi, ni lazima tubobee ktk shughuli hizi lakini tukiwa na maarifa na elimu juu ya jambo tunalotaka kubobea nalo. Natumia makala hizi kurekebisha makosa madogo madogo ya kazi ambazo mimi nimefanya tayari na jamaa zangu nitawasaidia wasifanye makosa ( kwa mfano,kujua shughuli za jirani yako ili zisije kukuharibia quality ya samaki nk).

Kabla hatujaingia ktk ujenzi wa bwawa ni vizuri pia utuambie aina ya samaki unaotaka kuwafuga ndugu( Nile perch,Tilapia, kambale, sato, kitoga au blackbassa) Kuna samaki hawataki matope wanataka clear water na wengine wanaweza kuishi ktk tope, pili lazima ujue PH ya hapo unapotaka kujenga bwawa,vinginevyo utajenga na samaki hawatazaliana. Angalia udongo wenyewe kama una capilarity kubwa au la.

Mwisho ni kwamba angalia aina ya samaki unaotaka kuwafuga growthrate yake ikoje na mwisho ni soko la samaki hao. Ukikamilisha utafiti huo rudi tukupe nondo mkuu.
 

Watalaam wapo kibao,ila wanakaa ofisini tu. Wengine wapo pale Temeke ofisi za kilimo,wengine Kunduchi chuoni pale, wengine wapo pale Kinguluira magereza ( hawa hata mbegu wanayo), wengine wapo SUA morogoro.

Mwanzo mgumu si baada ya kupita Chanika kwa mbele kidogo unaingia kushoto unaiacha njia ya kwenda Nzasa? Ni maeneo mazuri sana kwa kilimo. Mimi niko Marogoro/Mfuru mwambao/Msorwa.

Ni vizuri tukiwa na utamaduni wa kutembeleana,unaweza kujifunza zaidi kwa kuona wengine wanafanya nini. Nitakwenda Kinguluira kufuata mbegu ya pelege.
 
Mkuu Malila, hongera sana. Napenda sana mindset yako... najitayarisha, nikiwa tayari nitakutafuta.

Hii nchi ni ya ajabu sana,

week jana nilikwenda ktk kituo cha elimu ya ufugaji samaki Kinguruila sio chuo cha samaki pale SUA, kipo kinguruila. Wapo wataalamu wa kutosha vibaya,elimu bure. Nilitumia muda wa saa sita hivi pale kituoni. Nikanunua na mbegu ya kambale Clarius hybrid. Kituo kina aina mbili tu za vifaranga.sato na kambale. Jamaa ni wakarimu hadi raha.

Ila vifaranga vya Kambale ni haba sana kwa sababu vinasakwa na wengi, mimi nilitaka kununua vyote,wakanikatalia, ikabidi niwaachie kidogo. Vinginevyo ufugaji wa samamki uko vizuri,nilikutana na mkulima mmoja toka Maneromango,yy alinunua vifaranga 500 aina ya sato.
 
Malila

Asante kwa taarifa, Kinguruila kama sikosei ipo Morogoro lakini sikumbuki ni katika barabara ya Iringa au Dodoma. Santo ni aina ya samaki ambaye anakuwa kwa kasi ya ajabu na wanapatikana kwa wingi sana kwenye mto Kilombero.

Kinguluira iko Morogoro barabara ya Dsm, ukishapita Moro junior Seminary kama unakuja DSM toka Moro,kuna kimji kinafuata, unapomaliza kimji kushoto na kulia yanaanza mashamba ya mkonge. Sasa linapoanza shamba la kushoto kwako kuna njia inaingia kushoto na kuna kibao kimeandikwa kituo cha samaki au uliza wale madogo wa pikipiki,kwamba nataka kwenda FAO, ni buku moja kwa pikipiki.

Niliahidi huko nyuma kuwa nitatoa feedback ya jaribio la ufugaji. Nilianza jaribio may 2010, na sasa ni miezi sita imefika. Niliwaweka sato ktk fishpond isiyo na outlet wala inlet. Wamekuwa na kufikia kiwango cha kuliwa na wamezaliana vizuri sana.

Pamoja na kwamba nilipata darasa la kutosha toka Kinguluira,sikubadilisha mazingira ya bwawa lile. Desemba nitakwenda Kinguluira ili nichukue mbegu bora na nifugie ktk mazingira yanayokubalika kitalaam, lakini bwawa lingine nitaendelea kutumia mbegu niliyozalisha pale kwangu ili nione matokeo baada ya miezi sita mingine, hawa ni sato sio Kambale.

Nawatia shime,mwenye nafasi afuge samaki, mbegu zipo nyingi.
 
niliwahi kusikia kwamba unatakiwa kupanda samaki wawili kila mita 1kwa 1mean kwa mita 10 unatakiwa upandikize samaki 20 je mpaka unakuja kuvuna ikiwa utafuata ushauri wa kitaalamu unaweza kuvuna samaki wangapi?

Na je eneo lenye mchanganyiko wa mfinyanzi na kichanga linafaa?
 
je? Bwawa la cement halifai.na je hao samaki wakufugwa wanachukua muda gani mpaka kufaa kuvuliwa?
 
je? Bwawa la cement halifai.na je hao samaki wakufugwa wanachukua muda gani mpaka kufaa kuvuliwa?

Samaki wa biashara mara nyingi hufikia market size ktk kipindi cha miezi sita (sato zaidi). Kimsingi unatakiwa kuangalia ukuaji wa samaki wako kila wakati ili wafikie market size, sato wanaweza kufikia size hiyo bila taabu sana ukilinganisha na kambale, nikipata muda wa kambale nitauweka hapa. Kama unafuga kwa matumizi binafsi,size inayopendeza macho yako ndio nzuri.


Bwawa la saruji unaweza kulitumia kwa kufugia samaki pia,lakini sharti uwaone watalaam ili wawe na wewe kuanzia ktk hatua za ujenzi. Kumbuka virutubisho toka ardhini haviwezi kuwafikia samaki kirahisi kupitia kuta za saruji.
 
Samaki wa biashara mara nyingi hufikia market size ktk kipindi cha miezi sita (sato zaidi). Kimsingi unatakiwa kuangalia ukuaji wa samaki wako kila wakati ili wafikie market size....
Nilishakuwa na plan ya kufuga samaki ila nikawa nashindwa kufahamu costs involved na hata ivo sikuwa vyema kibajeti ingawa shamba la kuweza kufanyia hiyo buisness lipo.

Eneo langu ni shamba la kawaida lakini vilevile lina bonde ambalo maji huwa yanatiririka seasonally hasa masika. huwa nalima mpunga katika bonge hili na wakati wa masika kwa kweli maji huwa yanafurika sana ingawa mvua zinapoisha, kiasi cha maji hupungua na kubakia kama vijisima vidogovidogo.

Swali,..Je naweza kutengeneza fish pond katika eneo la namna hiyo? I mean humohumo bondeni au niweke hiyo fish pond pembeni kidogo ya hilo bonde ingawa slope inakaribia 5%. vilevile eneo hilo hakuna source ingine ya maji zaidi ya hicho kijibonde ambacho ni seasonal ingawa ukichimba unaweza kupata plenty of water kwa chini. Ni feasible kuweza kutumia maji ya ku-pump kutoka ardhini kwa kutumia waterpump?

Naombeni ushauri katika hili,....JF is great.....
 
Nilishakuwa na plan ya kufuga samaki ila nikawa nashindwa kufahamu costs involved na hata ivo sikuwa vyema kibajeti ingawa shamba la kuweza kufanyia hiyo buisness lipo. Eneo langu ni shamba la kawaida lakini vilevile lina bonde ambalo maji huwa yanatiririka seasonally hasa masika. huwa nalima mpunga katika bonge hili na wakati wa masika kwa kweli maji huwa yanafurika sana ingawa mvua zinapoisha, kiasi cha maji hupungua na kubakia kama vijisima vidogovidogo.

Swali,..Je naweza kutengeneza fish pond katika eneo la namna hiyo? I mean humohumo bondeni au niweke hiyo fish pond pembeni kidogo ya hilo bonde ingawa slope inakaribia 5%. vilevile eneo hilo hakuna source ingine ya maji zaidi ya hicho kijibonde ambacho ni seasonal ingawa ukichimba unaweza kupata plenty of water kwa chini.

Ni feasible kuweza kutumia maji ya ku-pump kutoka ardhini kwa kutumia waterpump?

Naombeni ushauri katika hili, JF is great.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…