tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 23,246
- 21,029
Kabla vumbi la ufisadi wa bilion 200 halijatua, ufisadi mwingine wa kutisha umeibuliwa tena bungeni. Ufisadi huu unahusisha matumizi ya Tsh bilion 2.8 kwa kisingizio cha ujenzi wa gym ya bunge inayodaiwa kugharimu kiasi hicho cha fedha.
Licha ya kwamba gym hiyo ni white elephant, haiwezekani gym moja tu igharimu fedha nyingi kiasi hicho. Watanzania wenzangu, hivi ni lini serikali hii 'sikivu' ya CCM itaacha kutafuna fedha za wanananchi? Wakati wanafunzi wanasomea chini ya miti na kuketi sakafuni au juu ya matofali, serikali hii isiyokuwa na khaya inawezaje kutafuna fedha za umma kiasi hiki? Fedha hizi kama zingeelekezwa kwenye ujenzi wa madawati, madarasa, maabara ya shule za kata au nyumba za walimu, haya matatizo yangebaki historia. Lakini kwa kuwa serikali ni 'sikivu', wakaona njia sahihi ni kufisidi fedha za umma kwa kutumia kisingizio cha kujenga gym!
Yaani hawa walafi waibe fedha za umma watengeneze vitambi halafu watumie tena fedha za umma kupunguza vitambi hivyo? Marvelous!!