Ufisadi mwingine waibuliwa Bungeni!

Ufisadi mwingine waibuliwa Bungeni!

Gym nani apige chuma?

Said Mkumba na Maji Marefu,Nkamia,Mwigulu wanataka vifua kwani bungeni kuna Ulinzi wa mabaunsa?
 
Mkuu, huu ukoo wa panya unaudhi sana, mpaka wanahamasisha vita! Ipo siku watanzania tutakuja kuingia msituni (ule aliopo Kapteni Komba) tupambane na hawa panya mpaka kieleweke.
naunga mkono hoja. inawezekana kabisa kuutoa huu ukoo wa panya ni kwa kuingia msituni.
 
Well said, Mystery.
Sifa kubwa ya kuwa mwana CCM ni "uhamnazo".

Sifa moja kubwa ya vyama vyote vya siasa vilivyoleta uhuru ni kwamba, wakati wa kutafuta uhuru, vyama hivi vilivutia wasomi wengi na vijana wengi wenye uwezo mkubwa (kwa wakati ule) wa kutambua mambo. Vyama hivyo hivyo kwa sasa hivi havina kabisa uwezo kwa sababu vijana wote wanaojiunga navyo ni wale ambao uwezo wao ni mdogo ktk mambo mengi: kufikiri, kutambua mema na mabaya, kupanga mikakati mizuri, n.k

Hilo ndo tatizo la CCM ya hapa kwetu.
 
Siku zote nasema "Wajinga ndo waliwao" Sidhani kama kuna jamii ya watu wapumbavu na wajinga kama ya watanzania.
Huko vijijini wakitaka Maji wanaambiwa wachange na mijitu inachekelea tu!! Halafu tunahubiriwa Uzalendo!!!
 
Mnaipenda sana Ccm, ngoja iwaonyeshe inavyofanya kazi na kutumia ipasavyo kodi zetu.
 
Du kungoja niende nikajiandikishe nianze tizi....kwani ni wabunge tu ndio wanaruhusiwa kufanya tizi hapo? Nahisi kuna chai lunch na dinner kabisa baada ya tizi free of charge.....plus full body massage.....na ka red wine....
 
Kweli mkuu, nyumba ya gavana wa benki kuu ilipigwa rangi mpya kwa thamani ya billioni 2.8 na kina MSALANI wanaoishi kwenye mabanda sombetini wakashangilia kwelikweli kuwa ni halali kabisa kiasi hicho kutokomea kwa ukarabati mdogo tu kama huo, kweli ccm ni wachawi haswa! Kuweza kuwaloga watanzania wengi ukawakandamiza na kuwaibia, kuwapora, kuwapiga, , kuwaua na kuwadhalilisha jinsi unavyotaka ba bado wakakuabudu kunahitaji miujiza.

Lakini mkuu haya tunayataka sisi wenyewe,(mimi na wewe) ingekuwa haya yanatokea halafu mi na wewe tunatimua kivumbi pale Posta mpya cha Kama siku 3 hivi, kuchoma moto gari za serikali na uharibifu mwingineo kushinikiza walaji wa Mali ya umma wawajibishwe unadhani haya yangetokea? Tena sio kufanya hivyo mara moja, uwe mtindo wa Mzalendo kupinga kwa nguvu zote pindi anaposikia Mali ya umma inafujwa.Naamini hakuna serikalini ambae angekuwa na mawazo ya kufuja Mali za uma. Lkn tunabariki tu, shughuli ipo kwa hakika.
 
Last edited by a moderator:
Lakini mkuu haya tunayataka sisi wenyewe,(mimi na wewe) ingekuwa haya yanatokea halafu mi na wewe tunatimua kivumbi pale Posta mpya cha Kama siku 3 hivi, kuchoma moto gari za serikali na uharibifu mwingineo kushinikiza walaji wa Mali ya umma wawajibishwe unadhani haya yangetokea? Tena sio kufanya hivyo mara moja, uwe mtindo wa Mzalendo kupinga kwa nguvu zote pindi anaposikia Mali ya umma inafujwa.Naamini hakuna serikalini ambae angekuwa na mawazo ya kufuja Mali za uma. Lkn tunabariki tu, shughuli ipo kwa hakika.

Mkuu, mtaji wa CCM katika nchi hii ni UPUMBAVU wa watanzania. Mtu anaona akipewa ubwabwa sahani moja na kuuza kura yake, atakuwa amefaidi sana wakati atateseka kwa miaka 5 bila maji, elimu, barabara, huduma za afya, nk

View attachment 165251
 
Kabla vumbi la ufisadi wa bilion 200 halijatua, ufisadi mwingine wa kutisha umeibuliwa tena bungeni. Ufisadi huu unahusisha matumizi ya Tsh bilion 2.8 kwa kisingizio cha ujenzi wa gym ya bunge inayodaiwa kugharimu kiasi hicho cha fedha.

Licha ya kwamba gym hiyo ni white elephant, haiwezekani gym moja tu igharimu fedha nyingi kiasi hicho. Watanzania wenzangu, hivi ni lini serikali hii 'sikivu' ya CCM itaacha kutafuna fedha za wanananchi? Wakati wanafunzi wanasomea chini ya miti na kuketi sakafuni au juu ya matofali, serikali hii isiyokuwa na khaya inawezaje kutafuna fedha za umma kiasi hiki? Fedha hizi kama zingeelekezwa kwenye ujenzi wa madawati, madarasa, maabara ya shule za kata au nyumba za walimu, haya matatizo yangebaki historia. Lakini kwa kuwa serikali ni 'sikivu', wakaona njia sahihi ni kufisidi fedha za umma kwa kutumia kisingizio cha kujenga gym!

Yaani hawa walafi waibe fedha za umma watengeneze vitambi halafu watumie tena fedha za umma kupunguza vitambi hivyo? Marvelous!!
Kabla hatujaanza kuchangia hebu tupe BOQ ya jengo hilo ( BILLS OF QUANTITES).
 
The so called Amani imetufanya wajinga wa kulalamika tu
 
Kabla hatujaanza kuchangia hebu tupe BOQ ya jengo hilo ( BILLS OF QUANTITES).

Ukishajua BOQ ndipo matumizi sahihi ya fedha za yatazingatiwa na serikali yako ya CCM? Nimesema kwamba hili gym ni white elephant labda hujanisoma vizuri. Hata kama lingejengwa gym la Tsh 10,000 haya ni matumizi ya kipumbavu ya fedha za walalahoi. Gym bungeni la nini? Kuna wabunge wanaishi mle bungeni kwamba wawe wanalitumia kila siku? Wabunge wanazo fedha za kutosha kulipia kwenye magym ya binafsi. Hilo gym bora lingejengwa hapa uwanaja wa fisi ili walalahoi tusiokuwa na fedha za kulipia kwenye magym binafsi tulitumie. Get me?
 
Kama nyumba ya kuishi inagharimu zaidi ya Bilioni mbili, je kuhusu gym yenye vifaa vya kisasa kibao?

Hivi mkuu kila kitu kinachohusu serikali yetu kikikosolewa wewe lazima utetee? Mbona uzalendo wako unatia mashaka? Yapo mambo sio ushabiki wa vyama bali ni hali halisi ya nchi yetu na lazima yakemewe kwa manufaa ya nchi na raia wake.
Sasa wewe unapo yashabikia na kutetea unatutia mashaka kuwa huipendi nchi yako.


Sent from my iPad using JamiiForums
 
Back
Top Bottom