Ufisadi mwingine waibuliwa Bungeni!

Ufisadi mwingine waibuliwa Bungeni!

-Wanatumia pesa zote hizo kwa ajili ya gym ili iweje?
-Sioni hata mmoja anayeenda na mke wake bungeni!
-Sote tunaona wanavyohangaika na vibinti mpaka wanachukuana picha mnato!
-Ahaaaaaaaaa, naona wanahangaika sana na vitambi vyao kuwashughulikia 'wapiga kura' wao hivyo inabidi waingie kwenye msitu wa gym ili wawe fit!
-Tunasubiri kwa hamu kuona 'album' zao mpya wakisalimia wapiga kura wao huku wakionekana kuwa na stamina hatari baada ya kutengeneza gym kwa pesa kibao ambazo ni kodi zetu mimi na wewe huku wenzangu na mimi heshima yetu ndani ya 'master room' ikizidi kushuka kutokana na mihangaiko mikubwa ya mchana kutwa ili kulipa kodi iliyotengeneza gym ya kuwajengea heshima wabunge wetu mbele ya vimada vyao!
NASEMA TENA: NASUBIRI PICHA ZAO WAKIWA NA NGUVU KAMA ZA SIMBA WAKIWASHUGHULIKIA VIMADA WAO. SI GYM BWANA?!
Kabla vumbi la ufisadi wa bilion 200 halijatua, ufisadi mwingine wa kutisha umeibuliwa tena bungeni. Ufisadi huu unahusisha matumizi ya Tsh bilion 2.8 kwa kisingizio cha ujenzi wa gym ya bunge inayodaiwa kugharimu kiasi hicho cha fedha.

Licha ya kwamba gym hiyo ni white elephant, haiwezekani gym moja tu igharimu fedha nyingi kiasi hicho. Watanzania wenzangu, hivi ni lini serikali hii 'sikivu' ya CCM itaacha kutafuna fedha za wanananchi? Wakati wanafunzi wanasomea chini ya miti na kuketi sakafuni au juu ya matofali, serikali hii isiyokuwa na khaya inawezaje kutafuna fedha za umma kiasi hiki? Fedha hizi kama zingeelekezwa kwenye ujenzi wa madawati, madarasa, maabara ya shule za kata au nyumba za walimu, haya matatizo yangebaki historia. Lakini kwa kuwa serikali ni 'sikivu', wakaona njia sahihi ni kufisidi fedha za umma kwa kutumia kisingizio cha kujenga gym!

Yaani hawa walafi waibe fedha za umma watengeneze vitambi halafu watumie tena fedha za umma kupunguza vitambi hivyo? Marvelous!!
 
Kama nyumba ya kuishi inagharimu zaidi ya Bilioni mbili, je kuhusu gym yenye vifaa vya kisasa kibao?

Kwa hiyo unataka kusema kwamba wizi mmoja huhalarisha wizi mwingine? kwamba wizi kwenye ujenzi wa nyumba uhalarishi wizi kwenye ujenzi wa gym? Are you serious? What message do you want to convey to the public?
 
kweli mkuu, nyumba ya gavana wa benki kuu ilipigwa rangi mpya kwa thamani ya billioni 2.8 na kina msalani wanaoishi kwenye mabanda sombetini wakashangilia kwelikweli kuwa ni halali kabisa kiasi hicho kutokomea kwa ukarabati mdogo tu kama huo, kweli ccm ni wachawi haswa! Kuweza kuwaloga watanzania wengi ukawakandamiza na kuwaibia, kuwapora, kuwapiga, , kuwaua na kuwadhalilisha jinsi unavyotaka ba bado wakakuabudu kunahitaji miujiza.

ili mradi mnaendelea kuuabudu mwenge,akili zenu zitaendelea kuwa butu.

Uchawi ule ule aliotambikiwa mwl.nyerere ili mahakama za kikoloni ziwe bubu ni uchawi ule ule uliobebwa kwenye mwenge mwendelee kumulikwa ili macho na masikio yenu yaone na yasikie lakini yasifahamu.

Mwenge huo mwenge mbio mbio!
 
Last edited by a moderator:
Kama nyumba ya kuishi inagharimu zaidi ya Bilioni mbili, je kuhusu gym yenye vifaa vya kisasa kibao?

We mpuuzi huna haya,
Unakubali Bunge liwe na Gym, 2 Bil ingeweza kununua madawati kiasi gani? au kwa sababu watoto wrnu wanasoma UK, basi hamjui kama kuna hizo shida?
 
We mpuuzi huna haya,
Unakubali Bunge liwe na Gym, 2 Bil ingeweza kununua madawati kiasi gani? au kwa sababu watoto wrnu wanasoma UK, basi hamjui kama kuna hizo shida?

bavicha kwa matusi hamjambo, yani huwezi kuchangia bila matusi
 
Tatizo linaanzia kwa Watz wenyewe, mngekuwa serious hawa wabunge wenu wala wasingekuwa wanawachezea namna hiyo!!!!

Sent from my iPhone using JamiiForums app

Uko sahihi kabisa! Serikali yetu siku zote ina msaidizi wake ambaye ni JESHI LA POLISI ambalo huagizwa kumtandika yule atakaye hoji! Ila na wao serikali sasa waone aibu! Bilioni 2. kadhaa nikwa ajili ya kujenga chumba cha kupashia misuli wabunge na alhali kadhalika kupitisha tu bajeti ya kujenga vidispensary vinavyo gharimu vimilioni 10 hawataki?? MUNGU sasa ingilia kati!
 
Kabla vumbi la ufisadi wa bilion 200 halijatua, ufisadi mwingine wa kutisha umeibuliwa tena bungeni. Ufisadi huu unahusisha matumizi ya Tsh bilion 2.8 kwa kisingizio cha ujenzi wa gym ya bunge inayodaiwa kugharimu kiasi hicho cha fedha.

Licha ya kwamba gym hiyo ni white elephant, haiwezekani gym moja tu igharimu fedha nyingi kiasi hicho. Watanzania wenzangu, hivi ni lini serikali hii 'sikivu' ya CCM itaacha kutafuna fedha za wanananchi? Wakati wanafunzi wanasomea chini ya miti na kuketi sakafuni au juu ya matofali, serikali hii isiyokuwa na khaya inawezaje kutafuna fedha za umma kiasi hiki? Fedha hizi kama zingeelekezwa kwenye ujenzi wa madawati, madarasa, maabara ya shule za kata au nyumba za walimu, haya matatizo yangebaki historia. Lakini kwa kuwa serikali ni 'sikivu', wakaona njia sahihi ni kufisidi fedha za umma kwa kutumia kisingizio cha kujenga gym!

Yaani hawa walafi waibe fedha za umma watengeneze vitambi halafu watumie tena fedha za umma kupunguza vitambi hivyo? Marvelous!!

Ufs.

Ritiz, Malichela Nape, njoo mjibu hizi hoja
 
GYM ya nini wakati mavitambi yao hayapungui?

Mis-Allocation of resources
 
Maana kuna mambo mengine hupatikana Tanzania tu. Wabunge wanataka gym wajenge six packs.Wakina Komba wanavituko sana.
 
Kama nyumba ya kuishi inagharimu zaidi ya Bilioni mbili, je kuhusu gym yenye vifaa vya kisasa kibao?

Lakini tuwe siriasi jamani, gym ya nini bungeni? Vitambi vinaletwa na tabia zao, kupenda kula na kunywa! I expect hata kuviondoa viwe ni initiative yao wenyewe and so mfuko wao! Yaani unatumia fedha za walipa kodi hivi... halafu tunasifia "na vifaa vya kisasa kibao..." seriously?
 
Cc Wtz ni wangese kishezi mm Nina uhakika hata zichotwe billions of money hakuna atakayepaza sauti .jee sisi tunaojiita wana Jf a.k.a G T hata siku moja kwa nn tusikutane na kuangalia ni vipi tutaikomboa nchi yetu .Ni mtazamo turn.

Upo sahihi mwana, nasisi hapa Jf hatuna tofauti na hao tunaowapigia kelele. Kama sisi ndio ilitakiwa kua chanzo cha mabadiliko badala yake sisi ndio tumekua reporters sasa sijui tunawahamasisha watu wa vijijini. Sijui tulilogwa na nani.
 
Yaani kula ovyo wale wao...kuota vitambi wapate wao...halafu wajenge gym ya kupunguza miili walioinenepesa kwa pesa yetu tena kwa ufisadi. Hii haikubaliki...nitawafuata huko huko na' AK-47'!
 
Kweli mkuu, nyumba ya gavana wa benki kuu ilipigwa rangi mpya kwa thamani ya billioni 2.8 na kina MSALANI wanaoishi kwenye mabanda sombetini wakashangilia kwelikweli kuwa ni halali kabisa kiasi hicho kutokomea kwa ukarabati mdogo tu kama huo, kweli ccm ni wachawi haswa! Kuweza kuwaloga watanzania wengi ukawakandamiza na kuwaibia, kuwapora, kuwapiga, , kuwaua na kuwadhalilisha jinsi unavyotaka ba bado wakakuabudu kunahitaji miujiza.

Ndio hivyo, mkuu. Yaani pesa za umma zinapigwa hivi na kutuumiza wananchi kwa ujumla wetu bila kujali jinsia, kanda, kabila au vyama vya siasa, lakini utakuta kuna baadhi ya misukule kama Ritz, lusungo, Simiyu Yetu, MSALANI na wajinga wengine kibao wanasapoti! Kweli watanzania tumerogwa na aliyeturoga kafa--angekuwa hai angelikwisha kutionea huruma na kutuzindua. Nawapongeza baadhi ya wanalumumba kama vile Nyani Ngabu na FaizaFoxy kwa kujitambua na kuanza kutetea rasilimali za taifa. Ipo siku nji hii itakuja kuingia vitani kwa sababu ya watawala wake kuendekeza ufisadi. Tuombe Mungu tusifike huko.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom