Ufisadi kwenye uteuzi wa Nehemia Mchechu?

Ufisadi kwenye uteuzi wa Nehemia Mchechu?

Mimi namfahamu huyu na kwa kweli CV yake ni nzito, ni mtu msafi na mchapa kazi na uteuzi haukuwa na mizengwe isipokuwa wale waliokosa kazi hii ndyiyo wanataka kila mtu aamini kuwa kulikuwa na mizengwe.
Nimefuatilia kwenye source muhimu ndani ya E&Y na hii ndo hadithi kamili. Jamaa aliomba hiyo kazi na ni kati ya watu 26 waliokuwa shortlisted na E&Y kuwa wanafaa kwa kazi hiyo. Lakini badala yake E&Y walisaili majina kumi na moja tu kati ya 26 na baada ya waiziri kutoridhika na mapendekezo alichagua kampuni nyingine iliyofanya usaili kwenye majina yaleyale ishirini na sita na mshikaji aliwapiga watu mbali vibaya sana. Na ukweli uko wazi hakuna aliyekuwa na CV inayokaribiana na yake na jamma ana track record nzuri kwa yale aliyofanya akiwa stanchart kwa miaka mitano kwenye nafasi za juu na pia CBA akiwa CEO kwa miaka mine. Hizi ni kelele za kukosa kazi na tunataka tuambiwe ni nani anajihisi alikuwa bora kuliko yeye katika wale 26 na tujadili. Mimi nilikuwa ni mmojawapo wa waliokuwa kwenye mchakato na nilipojua kuwa jamaa yupo kwenye mchuano nilijua basi nipo nje ya game. Na mwisho Bodi waliajiri E&Y iliwaweze kumshauri waziri na kisheria waziri na wajibu ndiye mwenye wa kuteua na si lazima afuate mapendekezo.
Pia nimefuatili pale CBA kujua jamaa alianza kazi na uhusiano wake na hizo EPA, jamaa alijiunga na CBA mwaka 2006 na EPA ilipita mwaka 2004 sasa uhusiano na ufisadi uko wapi. Jamani inabidi watu tufanye utafiti kabla ya kuandika andika na kuchangia habari zisizo na utafiti wala kichwa!
Huyu jamaa ni mtu wa Tanga na sasa hayo mambo ya kusini yanatoka wapi na tatizo liko wapi if he is a perfomer?
GT wewe unasema unamfahamu huyu jamaa na rafiki yako, hebu tuambie credentials zako na achievement zako ili tuweze kukuchambua na kukujua, vipi uwe na rafiki halafu unajificha na kutuletea habari hapa au na wewe ulikuwa kwenye mchakato huo na ukakosa hiyo kazi.
Jamaa anaheshimika na resource nzuri na kwenye CV nimeona yuko kwenye Bodi nafikiri kwasababu ya ubora wake, huyu jamaa ni Board member Ardhi University Real Estate School, pia ni Bodi Member na mwenyekiti wa Audit Committee wa Tumaini University (TURDACO), Ni mwenyekiti wa Bodi wa Rightway Schools, Ni Board Member na mwenyekiti wa Audit Committee wa PTF, Ni Board member wa CEOrt, CEO roundtable of Tanzania, kwa uchache tu! GT hivi kwakuleta hoja hii inasaidia vipi watanzania leo?
Wakichagua wazee malalamiko, vijana malalamiko, wakiletwa watu waliotoka nje ya system ilikuleta ufanisi wao malalamiko, wakichaguliwa wa ndani mnasema ni walewale, wakija wakenya mnalalamika, mghana mnalalamika, wahindi mnalalamika n.k. hivi watanzania tunataka lipi. Serikali taratibu imeanza kuvutia watu wa private sector basi tuwaunge mkono maana na wewe watakufikia as long as your competent.
Mchechu kachape kazi tunakuaminia kijana acha hawa watu wenye njaa zao wanaoshinda kujadili watu na matukio!!!!!


Mkuu karibu sana jamvini hapa. Inaonekana umekuja rasmi kujibu mapigo. Karibu. Hii ina maana JF inasomwa na mawe yanafika mbali kuliko tunavyoona.

I say it again, hakuna mwenye shida na Muungwana Nehemia. Kama umeona wengi humu hata kwenye ile thread nyingine they have faithfully acknowledged his significant achievements kote alikopita. Kwamba alikuwa anafaaa kwenye hiyo nafasi aliyopewa, ni wale waliomfanyia usaili na kuchambua credentials zake wanaoweza kutwambia hili. Na hapa hakuna anaye-question hilo. Maana sisi hatukuwemo kwenye chumba cha interview (kama alifanyiwa anyway!)

Naomba nikukumbushe, hapa hatuongelei duka la mhindi, tunaongelea shirika linalo exist kwa JASHO LA WALIPA KODI wa nchi hii.

Unajua katika maisha yangu yooote ya shule na kwingineko, nilifundishwa kuheshimu na kuthamini KODI. Sasa hoja si kwamba Nehemia is a performer siyo issue hapa......swala ni kwamba...how was he ideantified as an ideal candidate suitable for the post?

Wakuu, lets be real, hapa I personally, sina chuki na yeyote. I always believe that Merit should be the defining element ya mafanikio ya mtu yeyote. Mimi nakuwa VERY BITTER maana naamini watu kama sisi watoto wa wakulima tusio na God father popote..kama huu mtindo ukibarikiwa na akina Chiligati..tutakuwa wapagazi kwenye nchi yetu, ingawa vyetu tumevitafuta kwa jasho mpaka hapa tulipo. We need merit jamani. Tuache kuspin au kuteteana. Its our country. Its our future!

Your argument kwamba E & Y wali muacha....kati ya watu 26..inazidi kuleta maswali mengi zaidi. I believe A & Y ni kampuni yenye heshima zake ambayo imefanya kazi kwa miaka mingi...kama kweli walimuacha hata shortling hakuwemo. Trust me, A & Y wana sababu za MSINGI si hivi hivi.

Mkuu hii ngoma bado mbichi. Mengi tutayajua na watu wataaibika. Trust me. Remember we live in the era of google and facebook...shauri yako!

Masanja
 
MM, come on grow up men, what is so difficult about getting the right person on this case, when you judge that this person is bad what process do you foloow in your mind? Let us encourage this guy on the difficult task that is lying ahead, na akiweza tutaweza kupiga kelele nyingi kama vijana!

my previous statement was not singularly applied to Mchechu's situation.. I was trying to point to another reality that we can not just agree because the end result is good then the process doesn't matter then we should have the process at all.

Mara zote mimi si muumini wa ujana au wa uzee, siyo muumini wa CVs au mlolongoo wa digree (Wanigeria wengi wanazo kama wabongo vile vile). Mimi ni muumini wa uwezo wa mtu. Naamini kabisa kuwa uongozi mara zote ni uwezo; siyo jina, siyo fedha, siyo kabila, siyo dini wala siyo rangi.

Hoja zilizotolewa hapa kubwa ni kwamba (according to GT):

a. Mchechu aliteuliwa bila kuonesha interest (umetupa upande ambao GT hakutupa kuwa kweli aliomba, I'm giving you the benefit of the doubt)
b. Waziri katika kufanya uteuzi hakufuata mapendekezo ya E&Y (japo hadi sasa sijasikia jina lililopendekezwa ni lipi na likakataliwa - njia pekee ya kupima CV kwa CV ni kujua wale wengine ni kina nani)
c. Kwamba Sheria haikufuatwa (nimetoa changamoto huko nyuma mtu anioneshe sheria gani haikufuatwa hakuna aliyefanya hivyo).

Sasa, sisi wengine hapa tumeshazoea mtandao huu na nimejifunza through experience not to be harsh and in a rush to pass judgement. Napenda sana kusoma pande zote mbili na zaidi kwani ni katika kusikiliza pande zote ndipo naweza kufikia karibu zaidi na ukweli.

Simjui Mchechu zaidi ya kumsoma magazetini na kusema kweli nimemjua binafsi zaidi kwa mjadala wa siku hizi chache. Ndio maana me being me ningependa kumpa nafasi ya kufanya mahojiano nami na kusikiliza upande wake yeye mwenyewe. Sipendi sana kuamini nukuu za magazeti au maneno ya 'rafiki anayemjua kwa ukaribu'.

So far, barring any information that would portray Mchechu in a negative light I believe all the questions that have been raised so far can be fully answered by telling the whole side of the story. Ndio maana hapo nyuma (if you go back several pages) nilisema kuwa natumaini Mchechu hatoumizwa na haya yanayosemwa humu kwani it comes with the territory na ashukuru kwa sababu badala ya kutokujua yanayosemwa juu yake anapata nafasi ya kuyajua na kama kuna mambo ambayo anayitaji kuyabadilisha au kujisahihisha anapata nafasi ya kufanya hivyo.

Ni sehemu ya kuwa kiongozi.
 
Masanja; watu hawana data, mimi nimepata habari za ndani, application zaidi ya 100 na shortlisted ni 26 tu ambao walikidhi vigezo na jamaa alikuwa ndani ya lisit, na hii ni habari ya kutoka ndani na usisahau na mimi niligombea hicho kinyang'anyiro. lakini kushiriki kwangu kulinifanya niwe karibu na huo mchakato mzima na hvyo kama watu tunatoka nje ya msitari kupotosha hoja lazima tuzungumze. The process was right, kama jamaa alikuwa pia ni prefered candidate then its well. Lakini tunapaswa kuelewa ni nani mwenye madaraka ya kuteua before complining about the process, the whole process is made to help to the appointing officer to reach a good decision, and if in the decision maker the process was right then there shouldnt be a complain. If you want to practise the decision making go and run the show, but you cant expect to be making the decisions while your just a spectator!!!!!! Huu ni ukweli ambao unapaswa kukubalika hata kama unamaumivu.

This country is behind because of peoples inability to make decision and not the appointment process. Dubai inapendeza na kukua kwa kasi, uliambiwa Makhtoom ana hizo process au anapick the best brains?
 
Mimi namfahamu huyu na kwa kweli CV yake ni nzito

Duh! Ndugu wewe umejiunga leo tu na umekuja in full force kwenye mada hii. Things that make you go hhmmmm....!!

Anyway, kwa vile unamfahamu huyo jamaa, tuwekee basi hiyo CV yake nzito na sisi tuisome....
 
MM, well written na kweli nakubaliana na wewe kwa hoja zako ambazo ninazinukuu tena hapa chini!!

Hoja zilizotolewa hapa kubwa ni kwamba (according to GT):

a. Mchechu aliteuliwa bila kuonesha interest (umetupa upande ambao GT hakutupa kuwa kweli aliomba, I'm giving you the benefit of the doubt)
b. Waziri katika kufanya uteuzi hakufuata mapendekezo ya E&Y (japo hadi sasa sijasikia jina lililopendekezwa ni lipi na likakataliwa - njia pekee ya kupima CV kwa CV ni kujua wale wengine ni kina nani)
c. Kwamba Sheria haikufuatwa (nimetoa changamoto huko nyuma mtu anioneshe sheria gani haikufuatwa hakuna aliyefanya hivyo).



My hats off MM, na sasa watu wajadili kama kuna majibu yenye data ya hoja hizo na mimi nimetoa data zangu, Otherwise tupumzike na JF itafanya kazi kufuatilia kama kijana huyu atafanya mageuzi kusaidia nchi hii na hii ndiyo kiu ya watanzania kuona mabadiliko ya vitendo!!
 
Nyani mtoto, mambo yanapopindishwa kwa makusudi bila tija kwa taifa basi daima tutaingia tu.
He who knows not and knows not that he knows not is a fool; shun him.
He who knows not and knows that he knows not is a child; teach him
He who knows and knows not that he knows is asleep; wake him
He who knows and knows that he knows is wise; follow him
 
MM, well written na kweli nakubaliana na wewe kwa hoja zako ambazo ninazinukuu tena hapa chini!!

Hoja zilizotolewa hapa kubwa ni kwamba (according to GT):

a. Mchechu aliteuliwa bila kuonesha interest (umetupa upande ambao GT hakutupa kuwa kweli aliomba, I'm giving you the benefit of the doubt)
b. Waziri katika kufanya uteuzi hakufuata mapendekezo ya E&Y (japo hadi sasa sijasikia jina lililopendekezwa ni lipi na likakataliwa - njia pekee ya kupima CV kwa CV ni kujua wale wengine ni kina nani)
c. Kwamba Sheria haikufuatwa (nimetoa changamoto huko nyuma mtu anioneshe sheria gani haikufuatwa hakuna aliyefanya hivyo).


My hats off MM, na sasa watu wajadili kama kuna majibu yenye data ya hoja hizo na mimi nimetoa data zangu, Otherwise tupumzike na JF itafanya kazi kufuatilia kama kijana huyu atafanya mageuzi kusaidia nchi hii na hii ndiyo kiu ya watanzania kuona mabadiliko ya vitendo!!

Hivi katika yooote uliyoeleza humu umetoa data? shule gani uliyosoma waliyokueleza kuwa data huwa zinatolewa kama ulivyoweka?

Kumbuka kuwa watu hawana tatizo na Nehemia, watu wana matatizo na utaratibu uliotumika.
Tafuta data hizi

1. Kwa nini mchakato wa awali wa E&Y ulikataliwa? kweli akina Chiligati hawakuwapa vigezo vinavyotakiwa E&Y, au unataka kusema E&Y walifanya kazi bila terms wala direction?? YOU MUST BE KIDDING!
2. Kampuni gani ilifanya mchakato wa pili?
3. Zabuni ya hii kampun ya pili ilitangazwa gazeti gani?
4. Tangazo la nafasi hii ililitoka kwenye chombo kipi cha habari?
5. Majina ya hao watu 26 ni akina nani?

Ukimaliza hayo maswali tafuta na tuhakikishie uhusiano wa huyu jamaa na EPA, alipokuwa CBA,

nakuuliza haya mwasalikwa sababu uko jikoni

Pakua mtu wangu tunakusubiri, leta data na sio siasa.

Sisi tuna judge humu kulingana na ni vipi mashirika ya umma yanatakiwa kupata wafanyakazi, we are based on democracy that we are claiming have and not 'familiocracy or 'kujuanocracy''

sorry nimesahau, karibu jamvini!
 
Yaani wewe hujaona majibu, lazima ni kilaza kweli,

1) Jamaa aliaply
2)alikuwa shorlisted
3)alifanyiwa interview

umeambiwa mwaka aliojiunga CBA ambao hauhusiani na EPA, sasa unataka data gani. Na kazi imekwenda na mimi walau nilikuwa kwenye mchakato wa kupata kazi. Sasa machozi yako ya mamba ni ya nini? Ahaa vilaza kweli mnatabu!!!!!!!!!!
 
Waberoya, by the way who told you there's a democracy in job applications and who are the voters? and who was supposed to be a voter and a NEC in this process? Huu sasa ni ukilaza wa hali ya juu and I will not argue with you again!!!!!
 
Ever since I heard about Roberto Calvi,the famous banker's story with his his holy money banking, the stories about bankers have been interesting and fascinating. Kama mambo yanayosemwa yana ukweli, basi bank zetu zinafuata mfumo ule ule wa bank ya Roberto Calvi, bank Ambosino.Nisichojua ni kama na wao wanacheza na hela takatifu kama alivyokuwa anacheza nazo bwana yule
 
Yaani wewe hujaona majibu, lazima ni kilaza kweli,

1) Jamaa aliaply
2)alikuwa shorlisted
3)alifanyiwa interview

umeambiwa mwaka aliojiunga CBA ambao hauhusiani na EPA, sasa unataka data gani. Na kazi imekwenda na mimi walau nilikuwa kwenye mchakato wa kupata kazi. Sasa machozi yako ya mamba ni ya nini? Ahaa vilaza kweli mnatabu!!!!!!!!!![/QUOTE]!!!!!

Waberoya, by the way who told you there's a democracy in job applications and who are the voters? and who was supposed to be a voter and a NEC in this process? Huu sasa ni ukilaza wa hali ya juu and I will not argue with you again!!!!!


Mr.Tafakari vizuri, asante kwa majibu yako mazuri sana:

Mr.TV, kwanza naomba nikupe highlight ya mission yetu hapa maana tusije tukawa kwenye pande mbili za dunia. tunaongelea kitu kimoja.

Hakuna mtu ndani ya JF ambye ana question hili swala la kwa sababu zake binafsi, akiwepo huyo mtu , basi lazima aweke HOJA au maswali ambayo yanaleta common sense kwa kila mtu. GT ameuliza na majibu ndiyo dawa yake!

Kabla ya thread hii, kulikuwa na thread ya kumpongeza Nehemia, na katika waliompongeza nilikuwemo, kabla ya swala la mchakato ulivyokuwa halijaingilia hii maada. Hii ndio JF, na ninaamini unaifahamu vizuri wewe sio mgeni humu!

Kujibu hoja tuko tofauti wewe mwenzetu unatafakari vizuri, mimi kilaza kama unavyosema, so naomba kwa busara zako zinazotokana kutafakari vizuri ujibu maswali ya mtu kulingana na alivyouliza , usiende nyuma ya pazia. Maswali kama " hivi GT hili swali lina faida gani kwa mtanzania?" kilaza, machozi ya mamba , leta CV yako! n.k ni defence mechanisms ambazo zina rise tena question mark nyingi kuwa mgeni huyu vipi? mbona haukunisema nina machozi ya mamba nilipomsifia same guy kwenye thread ile nyingine?

Kumbuka na ninafurahi kama sauti nzito ya JF inaweza kuwaamsha watu huko waliko wakaja kujitetea humu, hakuna furaha ambayo unatuletea wana JF kuwa kumbe maada zetu na maswali yetu yanawanyima watu usingizi! JF siyo JK, siyo mahakama, siyo bunge, siyo polisi, but yet we can shake authorities na kuweka hali tete katika mawazo ya watu. Kwa hiyo ujue JF we have nothing than questioning!! my dear.Hakuna anayemfahamu Nehemia na humu kila mtu ana kazi yake! hata angekuja aliyekosa kazi angetoa sababu za upuuzi still tungemuuliza tu

So relax man, defence yako na kutoa maneno unayoona yana irritate, siyo kuwa unazima mto, ndio kwanza unawasha na watu wanaweza kujiuliza is this man Nehemia? au ana uhusianio na Nehemia?(Yes kama umeandika mimi kilaza ambalo ni neno sio zuri si mimi naweza nikasema wewe Nehemia ambalo ni zuri wala sio tusi?), what gives you audacity of using those langauge just in the very first day ya kuwa member wa JF?!

Nashukuru na nimefurahi kujua kuwa kwako wewe definition ya democracy lazima iendane na vote!!! Lakini nimefurahi zaidi kukiri kuwa kupatikana kwa kazi kwenye mashirika ya umma siyo lazima democrasia!

Kama kilaza niliuliza maswali yel machache na simply kwa sababu ya kuwa umesema uko jikoni, na si vinginevyo, huwa tunatabia ya kuweka wazi vitu haopa mkuu, ndio maana nataka hayo uliyoyasikia jikoni uyamwage hapa.

Kumbuka swala la kwamba anayehoji hili swala anaona wivu au analia machozi ya mamba umelisema wewe! na kwa sababu wewe aidha ni mzoefu humu (sitaki kuamini hilo) au mgeni humu , kumbuka tangu JF ianzishwe tumewapa watu SIFA, TUMESHAURI, TUMEONYA, na kukosoa, wa kwanz katika hao si NEHEMIA, Nehemia anakuwa mfano mzuri wa mtu aliyesifiwa sana na JF, na mpaka sasa hivi hakuna aliyemponda(unless uonyeshe nani kafanya hivyo) tena Nehemia hana matatizo, we are only questioning procedures my dear, procedure that is our business here! hii defence haitamsaidia Nehemia, kwa sababu kama ungeidharau JF basi wala usingejiandikisha humu leo!

Mr. TV, JK kasemwa humu, tulitaka nafasi ya JK? au tunatoka machozi ya mamba? same as EL, RA, n.k?? au unaturuhusu tuwaseme akina Kikwete ila ikifika kwa Nehemia ndiyo iwe sisi vilaza, machozi ya mamba, tukupe CV zetu n.k?

1. Matangazo ya kazi yalitoka kwenye chombo gani cha habari?

2. Kampuni ya pili iliyofanya mchakato ni ipi?

3. Zabuni ya hii kampuni ya pili ilitangazwa gazeti gani?
4. Tangazo la nafasi hii ililitoka kwenye chombo kipi cha habari?
5. Majina ya hao watu 26 ni akina nani? na walikuwa shortlisted kwenye chombo kipi cha habari kama ilivyo kawaida kwa nafasi za serikalini?

Ukijibu haya maswali mkuu sio utakuwa umetusaidia tuachane na threa dhi tuende kwenye maada zingine , kunamamukwa mengi humu, kwa sababu wewe ni mgeni nakukumbusha tu kuna jokes, dini, mapenzi, photo, kote huko tunahitaji kwenda baada ya kupata majibu mazuri kutoka kwako.

Ukiona hutaweza kujibu haya maswali nakuomba chondechonde dharau kabisa hii post huku ukijisemea kwa sauti , KILAZA HUYU!

Umesema ulikuwa kwenye mchakato, weka wazi kila kitu mkuu! sijaelewa hiyo ( "mimi" kwenye post yako ina maana gani??)

cheers

Waberoya
 
ma Grads wa East Anglia mna mambo!!

hivi kuna ubaya gani ukanyamaza tuu au basi tuu unataka kuongeza stats humu?
 
Ohh btw

Tangazo la awali lilipotolewa lilitaka mwombaji awe ma sifa kem kem

tangazo la pili likatolewa bila ufafanuzi...kwa nini lile la kwanza halikufaa...sifa zikapunguzwa infact wakasema kuwa wanataka awe na normal degree tuu

sasa jiulizeni yote ilikuwa ni kwa manufaa ya nani?

nishaitafuta ile thread weee lakini wapi! infact gazeti la MTZ walicopy that data from JF ndiopo wakaenda kumvaa Chiligati!!
 
umeambiwa mwaka aliojiunga CBA ambao hauhusiani na EPA, sasa unataka data gani. Na kazi imekwenda na mimi walau nilikuwa kwenye mchakato wa kupata kazi. Sasa machozi yako ya mamba ni ya nini? Ahaa vilaza kweli mnatabu!!!!!!!!!!

TV.. EPA haikuishia 2004.. akaunti ya EPA ilikuwa wazi na inafanya kazi up to late 2006. Mwaka ulioangaliwa na uchunguzi wa E&Y ni kati ya 2005/2006.. hawakuangalia 2004/2005 au kabla ya hapo..
 
Ohh btw

Tangazo la awali lilipotolewa lilitaka mwombaji awe ma sifa kem kem

NI sifa zipi hizo GT.. unaanzisha maswali mengine.. mwaga data zote ili tulikabili hili jambo kwa utimilifu wake wote.

tangazo la pili likatolewa bila ufafanuzi...kwa nini lile la kwanza halikufaa...sifa zikapunguzwa infact wakasema kuwa wanataka awe na normal degree tuu

What is a "normal degree" in contrast to "abnormal degree"? tunaomba hivyo vigezo vilivyotofautiana katika tangazo la kwanza na hilo la pili.

sasa jiulizeni yote ilikuwa ni kwa manufaa ya nani?

Hili swali twaweza kulijibu vizuri baada ya kupata all the information.

nishaitafuta ile thread weee lakini wapi! infact gazeti la MTZ walicopy that data from JF ndiopo wakaenda kumvaa Chiligati!!

I remember baadhi ya maswali niliyouliza kule bado ninayauliza.
 
Mambo anayo yafanya Mzee Luhanjo atakapo staafu baadae watanzania watamwadabisha kwa namna yoyote. Yanajulikama muda si mrefu atastaafu na ataulizwa
 
Kule kwetu huwa tunasema hivi: Ukifanya kitu kwa kukurupuka maana yake hujatulia, hujatafakari, hujatafiti, hujachambua na ukajijaza hisia na kupitisha maamuzi ambayo mara nyingi hayana msingi wa kuyafanya yahimili ukweli na hali halisi inapokuwa bayana. Hii ndiyo maana ya kukurupuka. Nilisema " He is the Right Person for the Job" watu wakakurupuka na kuacha hoja na kuanza kushanishambulia. Kwa kumalizia kule China huwa tunasema hivi: "One needn't devour the whole chicken to know the flavour of the bird"
 
Mimi namfahamu huyu na kwa kweli CV yake ni nzito, ni mtu msafi na mchapa kazi na uteuzi haukuwa na mizengwe isipokuwa wale waliokosa kazi hii ndyiyo wanataka kila mtu aamini kuwa kulikuwa na mizengwe.
Nimefuatilia kwenye source muhimu ndani ya E&Y na hii ndo hadithi kamili. Jamaa aliomba hiyo kazi na ni kati ya watu 26 waliokuwa shortlisted na E&Y kuwa wanafaa kwa kazi hiyo. Lakini badala yake E&Y walisaili majina kumi na moja tu kati ya 26 na baada ya waiziri kutoridhika na mapendekezo alichagua kampuni nyingine iliyofanya usaili kwenye majina yaleyale ishirini na sita na mshikaji aliwapiga watu mbali vibaya sana. Na ukweli uko wazi hakuna aliyekuwa na CV inayokaribiana na yake na jamma ana track record nzuri kwa yale aliyofanya akiwa stanchart kwa miaka mitano kwenye nafasi za juu na pia CBA akiwa CEO kwa miaka mine. Hizi ni kelele za kukosa kazi na tunataka tuambiwe ni nani anajihisi alikuwa bora kuliko yeye katika wale 26 na tujadili. Mimi nilikuwa ni mmojawapo wa waliokuwa kwenye mchakato na nilipojua kuwa jamaa yupo kwenye mchuano nilijua basi nipo nje ya game. Na mwisho Bodi waliajiri E&Y iliwaweze kumshauri waziri na kisheria waziri na wajibu ndiye mwenye wa kuteua na si lazima afuate mapendekezo.
Pia nimefuatili pale CBA kujua jamaa alianza kazi na uhusiano wake na hizo EPA, jamaa alijiunga na CBA mwaka 2006 na EPA ilipita mwaka 2004 sasa uhusiano na ufisadi uko wapi. Jamani inabidi watu tufanye utafiti kabla ya kuandika andika na kuchangia habari zisizo na utafiti wala kichwa!
Huyu jamaa ni mtu wa Tanga na sasa hayo mambo ya kusini yanatoka wapi na tatizo liko wapi if he is a perfomer?
GT wewe unasema unamfahamu huyu jamaa na rafiki yako, hebu tuambie credentials zako na achievement zako ili tuweze kukuchambua na kukujua, vipi uwe na rafiki halafu unajificha na kutuletea habari hapa au na wewe ulikuwa kwenye mchakato huo na ukakosa hiyo kazi.
Jamaa anaheshimika na resource nzuri na kwenye CV nimeona yuko kwenye Bodi nafikiri kwasababu ya ubora wake, huyu jamaa ni Board member Ardhi University Real Estate School, pia ni Bodi Member na mwenyekiti wa Audit Committee wa Tumaini University (TURDACO), Ni mwenyekiti wa Bodi wa Rightway Schools, Ni Board Member na mwenyekiti wa Audit Committee wa PTF, Ni Board member wa CEOrt, CEO roundtable of Tanzania, kwa uchache tu! GT hivi kwakuleta hoja hii inasaidia vipi watanzania leo?
Wakichagua wazee malalamiko, vijana malalamiko, wakiletwa watu waliotoka nje ya system ilikuleta ufanisi wao malalamiko, wakichaguliwa wa ndani mnasema ni walewale, wakija wakenya mnalalamika, mghana mnalalamika, wahindi mnalalamika n.k. hivi watanzania tunataka lipi. Serikali taratibu imeanza kuvutia watu wa private sector basi tuwaunge mkono maana na wewe watakufikia as long as your competent.
Mchechu kachape kazi tunakuaminia kijana acha hawa watu wenye njaa zao wanaoshinda kujadili watu na matukio!!!!!

Tafakari vizuri ndugu yangu
mimi nina maswali kadhaa yanatokana na highlights nilizoziweka hapo juu kwenye post yako

1: Katika hayo majina kumi na moja kutoka E&Y, jina la Mchechu lilikuwemo?

2: Hujatuweka wazi Huyo Waziri hakuridhika na nini Kutoka E&Y, au kwa sababu mchechu Hakuwepo kwenye Short listed?

3: Kwa mtazamo wako na kwa maelezo yako ni kuwa wewe pamoja na huyo Waziri mnaamini kwa asilimia kubwa kuwa E&Y wako biased?

4: Kama E&Y wanaaaminika na Serikali kuwa ni reliable Recruiter wewe huoni hicho kitendo cha Waziri kuwaingilia kwenye maamuzi yao ni kuwashushia heshima hao jamaa kuwa wako Unfair

5: nina Uhakika hao jamaa wa E&Y walishalipwa fedha za watanzania kwa hiyo kazi, ina maana Waziri anaamua kutumia fedha za walipa kodi kama apendavyo kwa kuitafuta kampuni nyingine ifanye kazi amabayo imeshalipiwa na kufanywa na kampuni nyingine? UNAWEZA KUTUPA NI KIASI GANI CHA WALIPA KODI KILITUMIKA KUYALIPA HAYA MAKAMPUNI KWENYE HUU MCHAKATO WA KUMWEKA MCHECHU MADARAKANI?

6: Sasa huyo Waziri aliridhika nini na Mchechu kuwa anafaa?, wewe uoni kuwa kuna HILA, GILBA, UBINAFSI, UPENDELEO kwenye huu mchakato.

7: kama hiyo kampuni ya pili ilikuwa kwenye kugombea tenda na E&Y na wakashindwa, hivi huwezi kuwa na wasiwasi kwamba, hiyo kazi waliyopewa walipewa na masharti ya nani na nani ndio waingie kwenye final na mwisho MCHECHU achukue?

NDUGU YANGU "TAFAKARI VIZURI" KAMA JAMAA WENGI WALIVYOSEMA HAPO AWALI, WANAMUAMINI NA KUMJUA KUWA NI MCHAPA KAZI, LAKINI TATIZO LIKO KWENYE MCHAKATO MZIMA WA KUMWEKA HAPO, HIVI KWELI UNASHINDWA KUPAMBANUA HIYO INFLUANCE YA WAZIRI KWENYE HII ISSUE
 
Mojawapo ya vitu ambavyo hutokea mara nyingi ni kuwa kama kuna mtu wanamtaka basi wanamuambia na wewe omba.. the rest is the classic "formalities"..
 
Kule kwetu huwa tunasema hivi: Ukifanya kitu kwa kukurupuka maana yake hujatulia, hujatafakari, hujatafiti, hujachambua na ukajijaza hisia na kupitisha maamuzi ambayo mara nyingi hayana msingi wa kuyafanya yahimili ukweli na hali halisi inapokuwa bayana. Hii ndiyo maana ya kukurupuka. Nilisema " He is the Right Person for the Job" watu wakakurupuka na kuacha hoja na kuanza kushanishambulia. Kwa kumalizia kule China huwa tunasema hivi: "One needn't devour the whole chicken to know the flavour of the bird"

Safi Sun Tzu, ila hapa huwa hatufanyi maamuzi, sio bunge ili wala chombo cha serikali, na ndiyo maana wanaokuja humu kwa defence, kutetea, huwa tunashtuka.

Katika process za kutafiti huwa kuna kuuliza na kuchambua, na mwanzisha thread ameuliza, soma tena title.

Halafu huwa watu hawaoni aibu humu, huwa hatushindani kama wengine mnavyotaka ionekane, huwa tunauliza maswali yakijibiwa huwa tunaangalia ustaarabu mwingine. JF inatisha mpaka watu wanaona tunafanya maamuzi bwana!Sisi ni kama madaktari mgonjwa akija anaachekiwa akiwa hana tatizo sitajilaumu kwa nini nilimpima, wala sitamlaumu mgonjwa kwa nini ulikuja hospitali! You ahve to know this forums by now buddy!

Kumbuka pia ni taifa hili la Tanzania na kwa kuuliza huku huku watu wamefichua uovu ambao haujapata kusikika katika nchi hii! watu wana experience Mr. Sun Tzu, wala hwana tatizo na Nehemia.

Mr. Tafakari vizuri kaja humu na kusema alikuwa mmoja wa watu waliouwa shortlisted, hajatueleza tangazo lilitoka kwenye chombo gani cha habari , au kwa njia ya sms?, hajasema alisailiwa na kampuni gani!!

Please wakubwa tunajadili procedures na sio kuwa hafai! nini kisichoeleweka hapa??

Nasisitiza watu hawana shida na bwana mdogo Nehemia, watu wana demand procedures ambazo tangu mwanzo zinawalakini! kama tuna uwezo wa kuwapata watu kwa head hunting, why tunawalipa fedha watu watufanyie mchakato? after all head hunting kwenye public sectors haitakiwi! hii kwa tusio wachina tunacopy hwa watu wanasemaje;

If liberty and equality, as is thought by some, are chiefly to be found in democracy, they will be best attained when all persons alike share in the government to the utmost.-Aristole

When great changes occur in history, when great principles are involved, as a rule the majority are wrong. The minority are right.-Eugene V.Debs

It is not the fact of liberty but the way in which liberty is exercised that ultimately determines whether liberty itself survives.-Dorothy Thompson

There's a world of difference between truth and facts. Facts can obscure the truth-Maya Angelou


Don't confuse facts with reality-Robert D. Ballard
 
Back
Top Bottom