Mzee wa Twitter
JF-Expert Member
- Nov 5, 2023
- 1,283
- 2,043
Watanganyika nawasabahi.Majuzi kumefanyika HARAMBEE ya kukusanya Fedha kwa ajili ya Timu ya Taifa iliokwishaenda IVORY COAST kushiriki Michezo ya CAF.
Katika HARAMBEE hiyo jumla ya Sh.Bil.3.7 zilikusanywa.Nampongeza sana Mh.Rais Waziri Mkuu Waziri mwenye dhamana na michezo Naibu waziri Tff na Kamati ya hamasa na wote waliochangia.
Binafsi nilikuwa najiuliza je ni wakati sahihi kwa kufanya HARAMBEE wakati Timu iliyobakiza siku 3 ianze Michuano?Je HARAMBEE ilikuwa ya kuisaidia Timu ya Taifa kupata Fedha kwa ajili ya nini?
Najua Fedha zilikuwa zinahitajika sana kwa Timu ya Taifa lakini HARAMBEE ilipaswa ifanyike Miezi 3 kabla ya Mashindano ili hizo Fedha zingetumika kuisaidia Timu kuweka kambi BORA NDANI na NJE ya Nchi,kucheza Mechi kadhaa za Majaribio na Timu kubwa kimpira ili kupata Uzoefu na mbinu mbalimbali za Michezo mikubwa kama hiyo na pia Fedha hizo zingetumika kama POSHO na Motisha kwa Wachezaji wa Timu ya Taifa kipindi chote cha Mashindano ili WACHEZE VIZURI.
Bahati mbaya sana hiyo HARAMBEE haikufanyiki kipindi hicho imekuja kufanyika siku 3 kabla ya Mashindano na ni ukweli usiopingika TIMU ya TAIFA imekusanywa kwa muda mfupi imecheza mechi 2 za Mazoezi imecheza na Timu ya Taifa ya Zanzibar timu isiyo na cha kujifunza na kutoka nayo sare,imecheza na Timu ya Taifa ya Misri na kufungwa Goli 2-0 baada ya Mechi hizo 2 Timu haijacheza Mechi zozote na Tayari Timu imekwishaenda Ivory Coast tayari kwa Mashindano.Najiuliza je Timu ya Taifa kwanini haikuwekwa KAMBINI Mapema na kwa Muda wa kutosha?
Je hizi mechi 2 za Majaribio ni MAZOEZI TOSHA kwa Timu inayokwenda Kupambana na Timu za Mataifa makubwa zenye Wachezaji wakubwa wanaocheza Kwenye VILABU vikubwa ULAYA na Uzoefu mkubwa wa Haya Mashindano?
Je Timu yetu ikishindwa kufanya Vizuri na HARAMBEE ya BIL.3.7 tumefanya siku 3 kabla ya Mashindano NANI ALAUMIWE?
Viongozi wetu tuache SIASA kwenye Michezo tena Mikubwa kama hiyo iwapo tunataka USHINDI
.Mashindano haya ni MAKUBWA na MAGUMU sana Timu nyingi zimejiaandaa pakubwa kwa muda mrefu na zinecheza Michezo mingi ya MAJARIBIO TOFAUTI na TANZANIA.
Binafsi ukweli useme VIONGOZI wetu wa Michezo Serikali na TFF TIMU yetu ya TAIFA Haijaandaliwa KIMASHINDANO bali KUSHIRIKI Tusitarajia Makubwa na Maajabu kwa Timu yetu ya TAIFA ktk MASHINDANO HAYA.
Sent from my SM-A145R using JamiiForums mobile app