Ufafanuzi wa Mch. Gwajima Kuhusu Mkenya wa Dr. Ulimboka

Ritz amechoka kutetea uovu hatimaye sasa amefahamu kwamba lengo la wapenda haki si Chadema kutawala wala CCM kutawala bali tunahitaji Equal rights & Justice for all. That's it.
 
Last edited by a moderator:
Takukuru wanafanya kazi, DPP mwenye dhamana ya kushitaki watuhumiwa ndio kazuiwa. Waambie wabunge watunge sheria na waanzishe mahakama maalum ya kesi za rushwa kama ilivyo kesi za kazi na ardhi hlf waruhusu takukuru kushitaki bila kupitisha kwa DPP uone moto utakavyowaka!

Hoseah ashawaambia kupitia weekleaks!, msimuonee
Kwenye Kuisafisha Richmond DPP alihusika vipi? Hii ni Taasisi ya Kupamba Rushwa basi... Haina kazi nyingine, tusimsingizie DPP
 
Mkuu Mnyakatari, hapa umewahi kuelezea wasiwasi wangu juu ya upangwaji wa hii habari na tarehe za matukio.
1. Jumapili pekee ya karibu na tukio ni Jumapili ya tarehe 1/7/2012 na wala sio tarehe 26/6 kama Mchungaji anavyosema.
2. Lakini juzi tarehe 13/7, Kova alituambia kuwa tukio la huyu Joshua kujipeleka kanisani lilitokea tarehe 29/6 (yaani Ijumaa).

Mimi simezi maneno ya Kova wala ya Mchungaji - Wote wajipange upya, hata kama ni uongo, basi watupe uongo wa kweli na sio uongo wa kiuongouongo.
Sidhani kama tarehe ni ishu kubwa kwa kuwa mchungaji amesema kanisa lilitangulia kulaani tukio la kuteswa kwa Dr Uli. Pia makanisa ya kipentekoste huwa yana ibada nyingi za katikati ya wiki, cha muhimu hapa ieleweke huyu mtu alienda kanisani baada ya tukio la kutekwa Uli. Akina Kova walikiri mbele ya walinzi wa kanisa kuwa jamaa ni kichaa wasihangaike naye hivyo Kova amelitangazia taifa huku anajua mazingira yanayomzunguka huyo GunStar ni utata mtupu. Kova ni janga la kidunia
 
Last edited by a moderator:
Kwenye Kuisafisha Richmond DPP alihusika vipi? Hii ni Taasisi ya Kupamba Rushwa basi... Haina kazi nyingine, tusimsingizie DPP
Honga ngoshi!.....wamanya wasambaa wanasema ukitandika mvyedi na ugoshe mvyedi. Tutafika hagoshowa ndima za kibahau, pumbavu kabisa.
 
Last edited by a moderator:
Hebu tuwekane sawa jamani, Dr Ulimboka si alitekwa usiku wa kuamkia tar 27 June 2012?
 
Wana mi nimeshikwa na butwaa, nashangaa tu users gunia ila mpaka sasa sijaelewa kitu..........Mwanakijiji nakuona hapa naomba uniungie ungie
 
Hili si tabasamu,
kakenua meno tu,
macho yake yamekosa nuru,
yako empty mpaka rohoni.

may God rest his soul in peace


Kamanda+Ahmed+Msangi+alietaka+kumuua+Dr+Ulimboka_thumb%5B2%5D.jpg

AMEN
 
Afadhari kuku umbo lake dogo.

Kiusahihi kabisa Watanzania tuna roho dhaifu kama ya nyumbu.


Mkuu DALLAI LAMA,


Tume huru ni wazo zuri sana, lakini sidhani kuna mob psychology katika Tanzania yenye uwezo wa kushikiza hilo hadi litimie. Watanzania ni waoga kuku ana nafuu. Of course mimi pia ni mtanzania. Kwa hiyo sijajitenga na hiyo lawama.
 
polisi
-tume imeundwa
-ulimboka akahojiwa
-tume ikaanza uchunguzi
-mwezi july gangster amejisalimisha
-tume imekamilisha uchunguzi na kutoa report [gangster na silencer wahusika]

GWAJIMA
-mtuhumiwa alikamatwa kabla ya tume ya uchunguzi kuundwa
-gangster alijitokeza june
-

Najaribu kuunganisa hizi facts kwa bahati mbaya sana haziunganishiki

USHAURI
- serikali ikae kimya kuhusu swala la ulimboka kwakuwa watanzania ni watu wa matukio na wakikaa mwezi mmoja watasahau kabisa hili swala
``

Gwajima kashaita Press Conference kusema haya? Kama alivofanya Kova SULEIMAN ambako kimsingi ilikuwa ni kupaka matope kanisa lake? Nadhani aite press kwa faida ya wale ambao pia hawafiki kanisani kwake
 
1. Sidhani kama tarehe ni ishu kubwa kwa kuwa mchungaji amesema kanisa lilitangulia kulaani tukio la kuteswa kwa Dr Uli. 2. Pia makanisa ya kipentekoste huwa yana ibada nyingi za katikati ya wiki, cha muhimu hapa ieleweke huyu mtu alienda kanisani baada ya tukio la kutekwa Uli. Akina Kova walikiri mbele ya walinzi wa kanisa kuwa jamaa ni kichaa wasihangaike naye hivyo Kova amelitangazia taifa huku anajua mazingira yanayomzunguka huyo GunStar ni utata mtupu. Kova ni janga la kidunia
@Ulokolokwitanga Mkuu, angalia hili dondoo hapa chini, na urejee kuangalia hizo red&blue:
  • Baada ya ibada ya jpili alikuja mtu ambaye yupo kama kichaa akasema anataka amwone Mch Kiongozi. Walinzi walimkatalia kwa vile hawakumwelewa. Mtu huyo akasema anataka kumweleza mchungaji kuhusu wao kumteka Dr Ulimboka.
  • · Walinzi baada ya kuona huyu ni mhalifu ambaye labda ametumwa au alikuwa na nia ya kufanya uhalifu wakapeleka polisi. Jambo hili liibuka tarehe 26.6 na wala si juzi. Baada ya kumpeleka polisi wakamwacha pale na hawakufuatilia tena
Huwezi kusema suala la tarehe sio ishue kwa sababu tarehe haziambatani na matukio. Kumbuka kuwa Ulimboka alitekwa usiku wa tarehe 26.6 usiku, siku ambayo kwa mujibu wa Mchungaji mwenyewe, Joshua alikwenda kanisani. Hii inaonesha kuwa Joshua alikwenda kanisani kabla ya tukio, isipokuwa tu Mchungaji apange upya hizo tarehe ilo ziendane na tukio. Huoni hapa panatosha kutoamini kinachosemwa?
 
Uwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii Kova kaumbuka kumbe mtu mwenyewe mwehu halafu tukio lilitokea kanisani tangu tarehe 26.06.2012 loooooooh aibu yao.
 
Bajameni mnataka kuniambia huyu KOVU wetu na intelejensia yake hawajagundua kuwa wana pata confession kwa chizi? au ndio wanambambikia kesi halafu watangaze kuwa ni mgonjwa tunampeleka ulaya kutibiwa(kuishi)? na pengine si chizi bali ni mtu wao anapozi kama chizi from kenya kwa sababu wakisema yule ni mbonde chizi, wandengereko watasema mbonde wetu si chizi tena ni askari mtiifu! fikiri!
 
``

Gwajima kashaita Press Conference kusema haya? Kama alivofanya Kova SULEIMAN ambako kimsingi ilikuwa ni kupaka matope kanisa lake? Nadhani aite press kwa faida ya wale ambao pia hawafiki kanisani kwake
Hakuna Press Conference inayoizidi hii JF. hapa vyombo vyote vya habari tayari News room zao wako kwenye hii thread, wewe subiri magazeti ya kesho upate salamu ndio utaijuwa vizuri kama ulikuwa huijui JF.
 
Maafisa wote wa Polisi wenye cheo cha kamishna nawaomba muitishe kikao cha dharura, aitwe ACP Msangi mbele yenu atoe maelezo yake. Pia aitwe kamanda Kova atoe maelezo yake kuhusiana na huyo 'kichaa' kutoka kenya.

Baada ya hapo mtoe taarifa kwa umma kupitia msemaji wa jeshi la polisi ili kurudisha imani kwa wananchi. Endapo itathibitika kuna mchezo mchafu, kova na msangi wasimamishwe kazi mara moja kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yao.

Atoe maelezo kwa kutekeleza maelekezo yao? He!
 
Back
Top Bottom