Tujadili Wabunge wanaoshindwa kutimiza ahadi zao majimboni

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
876
4,101
Moja ya jimbo linalotabiriwa kwenda upinzani ni jimbo la Kawe, hata hivyo tunayo miaka miwili mbele. Naamini yapo maoni yanayoweza kumwonyesha Mbunge husika alipokosea then aboreshe.

Mchungaji Gwajima amepeleka bonanza na mchezo wa rede Kawe, amejenga madaraja na kufanya jogging zakutosha akiwa na vijana wa kawe.

Pamoja na haya yote, juzi niliomba tufahamu majimbo yanayokwenda upinzani tume ikiwa ya haki. Kawe wakasema wana jambo lao 2025. Tusiwakatalie ila tuwaulize Mch. Gwajima amekosea wapi? Tusaidieni kumfanyia tathimini ya wazi may be tutaona akirekebisha alipokosea.

Karibuni mliopo huko Kawe mtuambie mzee wa Kolomije kawakosea nini?
 
Atarudi kwa kishindo,usiwe na wasiwasi,wapiga kura unaowaona,hawana maamuzi ya kumuondoa,nikimaanisha kura zao ni bosheni tu.

Kama ulikua nje ya nchi na haujawahi kushuhudia maigizo ya uchaguzi Tanzania,uliza mtu ambaye amekuwa hapa nchini katika vipindi vyote vya uchaguzi, atakwambia.

Ondoa shaka ndugu yangu,tume tu,mwenyekiti wake huteuliwa na mwenyekiti wa chama tawala,utangazaji matokeo,kuna wateule wa mwenyekiti wa chama tawala, ndiyo watakaohusika kuyatangaza,kutokana na maelekezo ya chama tawala.

Kuwa na amani ndugu,Gwajima njia nyeupe,anarudi mjengoni.
 
Hivi kuchagua mbunge kwa vigezo vya upinzani au ccm ina msaada gani kwa jimbo husika?
 
Moja ya jimbo linalotabiriwa kwenda upinzani ni jimbo la Kawe, hata hivyo tunayo miaka miwili mbele. Naamini yapo maoni yanayoweza kumwonyesha Mbunge husika alipokosea then aboreshe.

Mchungaji Gwajima amepeleka bonanza na mchezo wa rede Kawe, amejenga madaraja na kufanya jogging zakutosha akiwa na vijana wa kawe.

Pamoja na haya yote, juzi niliomba tufahamu majimbo yanayokwenda upinzani tume ikiwa ya haki. Kawe wakasema wana jambo lao 2025. Tusiwakatalie ila tuwaulize Mch. Gwajima amekosea wapi? Tusaidieni kumfanyia tathimini ya wazi may be tutaona akirekebisha alipokosea.

Karibuni mliopo huko Kawe mtuambie mzee wa Kolomije kawakosea nini?
Wabunge karibia wote hawastahili kurejea bungeni labda wachache kama akina mpina, wengine wote hakuna walichofanya tulitarajia kuwaon kwenye suala la DPW, mswada wa mafao, mswada wa sheria ya uchaguzi, report ya CAG,lkn wao ni kimyaaa.
 
Ukisema sema hivyo uwe na hoja ya msingi moja kati ya majimbo yalifanya vizuri Kwa mda mfupi ni kawe Gwajima amefanya mengi ikiwa na kujenga vituo vya afya, barabaran, vivuko vya waenda Kwa miguu ikiwemo baadhi ya maeneo yaliyoshindikana na yaliyokuwa na kero za mda mrefu Kwa wakazi wa maeneo hayo mf. Tegeta machinjioni, kivuko Cha mto ndumbwi nk CCM Jimbo la kawe wamefanya mengi tunaweza kusema Gwajima anaupiga mwingi
 
Mbunge hajengi miundombinu, acha kuleta upotoshaji wa kijinga. Kazi za mbunge ni:
  1. Muwakalishi wa wananchi wa Jimbo lake bungeni.
  2. Kuisimamia na kuishauri serekali bungeni.
  3. Kutunga na kupifisha Sheria.
Huu utapeli kuwa mbunge anaweza kujenga miundombinu Jimboni kwake, utapeli huo wanafanyiwa wale wajinga wanaoshabikia kiongozi aliyekuja na GXR, kisha anashuka na kupanda punda, au lory.
 
Kwani Uncle Gwaji kakosana na mwenyekiti au wanec. Maana hao ndio wanaweza wakaamua kama anaukosa ubunge au la.
 
Wabunge wa hii nchi ni zaidi ya mashetani
Wameumiza wazee wetu kwenye kikokotoo ile mbaya ,yaan mzee wa watu kafanya kazi miaka 34 analiwa million 40 kweli jaman!!
Ajabu wenyew miaka mitano tu wanakunja 240m.
Kama kweli mungu yupo Hawa jamaa wataenda kuungua vibaya mno,Mimi sijawah shtuka nikisikia kigogo wa ccm kapatwa na lolote baya ndio kwanza inakua furaha moyon mwangu.
 
Mbunge hajengi miundombinu, acha kuleta upotoshaji wa kijinga. Kazi za mbunge ni:
  1. Muwakalishi wa wananchi wa Jimbo lake bungeni.
  2. Kuisimamia na kuishauri serekali bungeni.
  3. Kutunga na kupifisha Sheria.
Huu utapeli kuwa mbunge anaweza kujenga miundombinu Jimboni kwake, utapeli huo wanafanyiwa wale wajinga wanaoshabikia kiongozi aliyekuja na GXR, kisha anashuka na kupanda punda, au lory.
Inamaana hauelewi hata unacho zungumza hayo yote unayoyazungumza yamefanyika au la! hawakilishi wananchi kawe bungeni ??? Miundo mbinu ipi unaisemea ww zaidi ya barabara zilizo jengwa bunju, mabwe pande , kawe na mitalo iliyojengwa msasani unapotoa hoja uwe na evidence za kutosha umesahau hospital zilizojengwa mbweni, Kawe, chini ya mbunge Gwajima hoja zako hazina mashiko
 
Ukisema sema hivyo uwe na hoja ya msingi moja kati ya majimbo yalifanya vizuri Kwa mda mfupi ni kawe Gwajima amefanya mengi ikiwa na kujenga vituo vya afya, barabaran, vivuko vya waenda Kwa miguu ikiwemo baadhi ya maeneo yaliyoshindikana na yaliyokuwa na kero za mda mrefu Kwa wakazi wa maeneo hayo mf. Tegeta machinjioni, kivuko Cha mto ndumbwi nk CCM Jimbo la kawe wamefanya mengi tunaweza kusema Gwajima anaupiga mwingi

Naunga mkono hoja yako kiongozi moja kati ya majimbo tata ambayo yalishikiliwa kwa muda mrefu na chama pinzani bila kuwa na maendeleo yoyote ni jimbo la kawe, mbali na hivyo tuliona matatatizo mengi ja mapungufu mengi kipundi cha ambayo yako wazi, lakini kwa sasa kati ya majimbo yanayofanya vizuri na ambayo ushindi wake upo dhahiri basi ni jimbo la kawe ,

Hii inatokana na kiongozi alieko kwa wakati huu kwanini kipindi kile hatukuwa na maendeleo chanya kwenye jimbo letu kwasababu kiongozi alikuwa hawajibiki ipasavyo lakini sio kwa kiongozi wa sasa Mh Gwajima

Mbali na hivyo Mh josephat Gwajima amefanya mambo kadha wa kadha kwenye jimbo la kawe na kwa muda mfupi haya ni baadhi mambo machache kati ya mengi

1 . Ametanua mitaro
2. Amejenga vivuko ( madaraja)
3 . Amechonga barabara kadha wa kadha na nyingine kuwa katika kiwango cha lami
4. Ameanzisha michezo ambayo imekuwa chanzo cha ajira kwa vijana
5. Amesaidia wahanga walioathirika na mafuriko

Na mengine mengine, ni mpaka uwe unamatatizo ya macho usione alichofanya kiongozi Gwajima au uwe na chuki isioya msingi ambayo itakuzuia kutokuona mambo kengi mazuri alioyafanya kwa mtazamo huu Jimbo la Kawe ni kati ya Majimbo yatakayo shinda kwa kishondo na Gwajima atarudi tena mjengoni kupiga kazi huyu baba anaupiga mwingi

Naunga mkono hojaa
 
Ukisema sema hivyo uwe na hoja ya msingi moja kati ya majimbo yalifanya vizuri Kwa mda mfupi ni kawe Gwajima amefanya mengi ikiwa na kujenga vituo vya afya, barabaran, vivuko vya waenda Kwa miguu ikiwemo baadhi ya maeneo yaliyoshindikana na yaliyokuwa na kero za mda mrefu Kwa wakazi wa maeneo hayo mf. Tegeta machinjioni, kivuko Cha mto ndumbwi nk CCM Jimbo la kawe wamefanya mengi tunaweza kusema Gwajima anaupiga mwingi
Naunga mkono hoja kiongozi, kati ya majimbo ambayo tangu uchaguzi wa 2020 yamekenda kwa kasi kubwa ya kimendeleo, utakuwa huna jicho la kisiasa kama usipoongelea jimbo la kawe. Kawe ni kati ya majibo ambayo yameonyesha maajabu na mapinduzi makubwa katika uwanja wa kisiasa.

kama utakuwa na kumbukumbu nzuri jimbo la kwe lilikuwa na matatizo sugu lilipokuwa linamilikiwa na upizani mf. barabara mbovu, mafuriko katika maeneo mbali mbali. lakini pia wanachi kutokusikilizwa baadhi ya changamoto zao walizokuwa wakipitia, Sasa tangu Mh Gwajima aingie mzigoni mabadiliko chanya tumeyaona.

Gwajima ni kati ya viongozi wachache kambao huutoa muda wake mwingi sana akuzungukia jimbo lake na kusikiliza kero na changamoto wanazopitia wananchi wake kitu ambacho kwa siasa zetu za bongo hii kitu sijaionaga aisee, lakini pia amejenga madaraja ya watembea kwa miguu pale mto ndumbwi, machinjioni kule tegeta daaah hiki chuma jamani kinakosaje MITANO TENA aisee,

cheki mwamba alivyoweza kuconect vijana wa jimbo zima kwa michezo kama mtu anahisi kuunganinisha vijana wa jimbo zima kwa michezo ni mdebwedo na yeye aanzishe tumuone, Kifupi Askofu GWAJIMA ameweza. na kumpongeza mtu anapofanya vizuri ni uzalendo
 
Atarudi kwa kishindo,usiwe na wasiwasi,wapiga kura unaowaona,hawana maamuzi ya kumuondoa,nikimaanisha kura zao ni bosheni tu.

Kama ulikua nje ya nchi na haujawahi kushuhudia maigizo ya uchaguzi Tanzania,uliza mtu ambaye amekuwa hapa nchini katika vipindi vyote vya uchaguzi, atakwambia.

Ondoa shaka ndugu yangu,tume tu,mwenyekiti wake huteuliwa na mwenyekiti wa chama tawala,utangazaji matokeo,kuna wateule wa mwenyekiti wa chama tawala, ndiyo watakaohusika kuyatangaza,kutokana na maelekezo ya chama tawala.

Kuwa na amani ndugu,Gwajima njia nyeupe,anarudi mjengoni.
Mnaosema kuwa Gwajima njia nyeupe kurudi bungeni kwa kuanzisha michezo ya Rede huko Kawe mnamlisha upepo na mnataka kumlia hela zake tu!
Gwajima hajatimiza ahadi zake za uongo za kuwapeleka wanakawe ulaya kujifunza uvuvi wa baharini; Gwajima hajashuhulikia mafuriko wakati wa mvua yanayosababishwa na matajiri kuziba barabara sehemu za Jangwani beach.
Gwajima aliahidi kutengeneza mifereji kwenye barabara ya kutoka Nyaishozi kwenda ndani kule Nyamachabezi., barabara hii haipitiki wakati wa mvua.
Bila kuyafanyia kazi malalamiko haya Gwajima ataliwa hela hao madalali wa uchaguzi na bungeni harudi tena!
Gwajima lazima atambue kuwa Rede na jogging kwa vijana wenye njaa/ kukosa ajira kutawapa hasira vijana kuwa unawafanya wajinga na hivyo kukunyima kura! Kawe wanajitambua!
 
Mkuu bado unaaminigi kua wananchi huchagua kiongozi wao kwenye sanduku la kura?
Pole sana,muhimu ni CCM wakupitishe,the rest is known.
 
Wabunge karibia wote hawastahili kurejea bungeni labda wachache kama akina mpina, wengine wote hakuna walichofanya tulitarajia kuwaon kwenye suala la DPW, mswada wa mafao, mswada wa sheria ya uchaguzi, report ya CAG,lkn wao ni kimyaaa.
Shida yetu watanzania tunapienda kwenye chaguzi za wabunge tunatanguliza vyama kwanza. Unajikuta kama una support chama fulani basi utampigia kura mgombea wa chama chako bila kujali uwezo wake na kupelekea kuwa na wabunge wasio na uwezo wa kuchambua na kujenga hoja!
 
Mkuu bado unaaminigi kua wananchi huchagua kiongozi wao kwenye sanduku la kura?
Pole sana,muhimu ni CCM wakupitishe,the rest is known.
Hiyo ilikuwa enzi ya Jiwe! Gwajima na wenzie waliobebwa na Jiwe hawarudi tena bungeni!!
Kawe hawataki kusikia jina la Gwajima, hizo Rede zake na jogging anapoteza fedha tu!
Chawa wake wamshauri aende Ubungo lilipo kanisa lake, huku Kawe ameisha poteza.
 
Back
Top Bottom