Uendeshaji wa Bandari: Wabunge Wataka Rais Samia asirudi nyuma

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
WABUNGE wameishauri serikali kutosikiliza maneno ya watu wa mtandaoni kuhusu ushirikiano wa Serikali za Tanzania na Dubai katika makubaliano ya uwekezaji kwenye bandari zilizopo nchini (IGA) kwa kuwa wanaofanya hivyo hawaitaki nchi mema.

Pia, wameitaka serikali kuharakisha kusaini mikataba inayohusiana na suala hilo, ili bandari iwe sehemu ya kuchangia Pato la Taifa na kuletea maendeleo. Waliyasema hayo jana wakati wanachangia hoja ya Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka 2023/24.

Mbunge wa Jimbo la Ukonga (CCM), Jerry Silaa, alishauri serikali isikubali maneno ya watu wasiotaka iendelee kiuchumi ambao wanapinga uamuzi wake wa kushirikisha sekta binafsi kwenye maendeleo, ikiwamo ushirikiano ilioyongia na Serikali ya Dubai kuhusu uwekezaji kwenye bandari nchini.

Alifafanua kuwa IGA siyo mkataba wa utekelezaji bali ni makubaliano baina ya Serikali ya Tanzania na Dubai kuhusu uwekezaji utakaofanyika kwenye bandari zilizopo katika chi hiyo na kwamba mikataba ya kwenda kutekeleza miradi bado haijaingiwa.

Silaa alisema ushirikiano huo utaongeza ufanisi wa bandari na kufikia malengo ya serikali ya kukuza uchumi wa nchi kwa kuongeza forodha na kuboresha sekta za uchumi ikiwamo kilimo.

"Niombe serikali ikubali ushauri, isikilize wananchi, lakini wakati mwingine isikubali kuyumbishwa na watu wenye nia zao za kuitaka nchi yetu isiendelee kiuchumi, ikubaliane na hoja za msingi za kutetea taifa letu, tuwe na uwekezaji na kushirikisha sekta binafsi katika ameneo ambayo wenzetu wamebobea," alisisitiza.

Kadhalika, alisema serikali haiwezi kupiga hatua bila ushirikiano na sekta binafsi huku akitoa mfano wa moja ya mafanikio ya ushirikishwaji wa sekta hiyo kuwa ni Benki ya NMB ambayo hivi karibuni serikali imevuna gawiwo la Sh. bilioni 45.5 na kodi ya Sh. bilioni 453.

Aidha, Mbunge huyo alishukuru serikali kwa kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati ikiwamo ujenzi wa Bwawa la Kufua Umeme la Julius Nyerere, ambalo utekelezaji wake umefikia asilimia 96, ujenzi wa reli za umeme na adaraja la Kigogo Busisi, mradi wa mwezndo kasi awamu ya tatu, Gongo la mboto-Kariakoo.

Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Pwani (CCM), Subira Mgalu, alishauri serikali kuchukua hatua za haraka kuleta mikataba itakayotokana na IGA ili wawekezaii waje na bandari iwe na nafasi ya kuchangia katika pato la ndani la taifa na serikali ipunguze kukopa.

Kahusu hoja ya kuitwa mbunge mmoja mmoja kupigia kura muswada huo iliyotolewa na mbunge mstaafu Prof. Anna Tibaijuka, alisema hauna mashiko kwa kuwa utaratibu huo unafanyika kwenye kupitisha bajeti ya serikali pekee, masuala mengine ni utaratibu wa kuhojiwa na walishafanya hivyo.

"Lakini nataka nimkumbushe Prof. Tibaijuka alipokuwa waziri 2013 aliwasilisha mpango wa kuifanya Kigamboni kuwa mji wa trilioni 11, haukufanikiwa na tulioupitisha kwa kura za kuhojiwa kwa hiyo aiache serikali inayoongozwa na mwanamama menzie (Rais Samia Suluhu Hassan) ifanye kazi yake," alisema.

Hivi karibuni, Prof. Tibaijuka akihojiwa na chombo kimoja cha habari, alikosoa utaratibu wa kura ya pamoja uliotumiwa na Bunge katika kupitisha Azimio la Bunge kuhusu Mapendekezo ya Kuridhia Makubaliano Kati ya Tanzania na serikali ya Dubai kwenye ushirikiano wa kiuchumi na kijami kwa ajili ya uendelezaji na uboreshaji wa utendaji kazi wa bandari Tanzania.

Aidha, aliwatoa hofu wananchi kuwa bandari haiwezi kuuzwa kwa serikali kugawana idadi ya gati na mwekezaji bali mbinu iliyotumika ni kushirikisha sekta binafsi katika kukuza utendaji kazi wa bandari na kukuza uchumi wa nchi.

Vile vile, alisema bajeti kuu imeonyesha dhamira ya serikali ya kureiesha uuzwaji wa bidhaa nje ya nchi kwa kutenga zaidi ya Sh. bilioni 800 wazalishaji wa mazao, ili kuliletea taifa fedha za kigeni na kukuza uchumi.
Pia, katika mapendekezo ya bajeti ya serikali inatarajia kukusanya Sh. trilioni 44, kati ya hizo Sh. trilioni 31 zitakusanywa kutoka mapato ya ndani na kwamba ni lazima seri-kali ishirikishe sekta binafsi katika uwekezaji.

Aliwataka wananchi kuendelea kutoa na kudai risiti wanapofanya ununuzi ili kuhakikisha kuwa wanalipa kodi na serikali isiendelee kuleta kodi mpya kwa kuwa inategemea pesa hizo kutekeleza miradi ya maendeleo. Mbunge wam Sengerema, Hamis Tabasamu, alimshauri Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, kutokatishwa tamaa na maneno yanayozunguka mitandaoni na mitaani bali kuwa na imani jambo analolifanya litakwenda kuiletea mafanikio nchi.

"Kuna watu ni majemedari wa kupiga kelele kwenye mitandao na kila maeneo, Mheshimiwa Waziri wa Fedha, maneno haya yangekuwa yanatoboa mwili wako leo ungekuwa umejaa viraka na bandeji mwili mzima, kwa hiyo unachotakiwa sasa hivi ni kuwa na ngozi ngumu tu kujenga imani halafu baadaye unatoboa," alisema.

Alimshauri waziri huyo kuwashirikisha wabunge wakati wa uandaaji wa baieti hizo ili watoe ushauri wa vitu muhimu vya kuwapo na kutokuwapo kwa kuwa wao wanajua matatizo ya wananchi ambao wengi wao kukosa pesa ndiyo kunawafanya waitukane serikali kwenye mitandao.​
 
Hao wahuni wanataka Samia asirudi nyuma kuwapa waarabu mikataba ya milele, waitawale ardhi yetu, bandari na anga, kisha pia tuwajulishe waarabu fursa nyingine za kiuchumi zitakazojitokeza.

Huu utumwa wa kifikra unaotawala vichwa vya wabunge wetu kwa sasa, unaenda kuviumiza vizazi vijavyo vya hili taifa.
 
Nitatumia tafsiri ya Mkataba wa IGA kuwajibu hao Wabunge, uhovyo wa huo mkataba, nikiwatahadharisha kuwa tutakutana kwenye majukwaa ya kampeni, kama watasimamishwa na chama chao kugombea.

Maandishi mekundu ni mtazamo wangu kuhusu ubovu wa mkataba huo.

1) UTANGULIZI: JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, iliyowakilishwa ipasavyo na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi (“Tanzania”) na SERIKALI YA DUBAI, iliyowakilishwa ipasavyo na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Bandari, Forodha na Ukanda Huru (“Dubai”)

Tanzania inawakilishwa na Waziri, Dubai inawakilishwa na Mtendaji Mkuu wa Shirika la Bandari

2) SEHEMU YA II: WAJIBU WA JUMLA KIFUNGU CHA 2(1) la LENGO LA MKATABA). Madhumuni ya Mkataba huu ni kuweka mfumo wakisheria wa maeneo ya ushirikiano kwa ajili ya maendeleo, uboreshaji, usimamizi na uendeshaji wa bandari za bahari na maziwa, kanda maalum za kiuchumi, hifadhi za usafirishaji, korido za kibiashara na miundombinu mingine ya kimkakati ya bandari nchini Tanzania. Maeneo ya ushirikiano pia yanajumuisha kujenga uwezo, uhamisho wa ujuzi, utaalam na teknolojia, kuimarisha taasisi za mafunzo na msaada wa utafutaji wa masoko.

Kifungu hicho kina maana nchini hatuna sheria za ushirikiano au uwekezaji, ambayo si kweli

3) KIFUNGU CHA 4: UPEO WA USHIRIKIANO NA VYOMBO VYA UTEKELEZAJI kifungu kidogo cha 4. Serikali ya Dubai inaiteua DPW na Washirika wake kama chombo cha kutekeleza Shughuli za Miradi. 5. DPW na taasisi tanzu zitawajibika kutafuta ufadhili kwa Makampuni ya Miradi husika kwa ajili ya kuendeleza Shughuli za Miradi.

Kifungu hicho kina maana kwamba DPW itakopa na siyo nchi yake itatoa fedha ya miradi ya bandari. Kimsingi DPW itawekeza nchini kibiashara, kwa mgongo wa nchi yake wakati tuna Sheria, Kanuni na Taratibu za uwekezaji.

4) KIFUNGU CHA 5: HAKI ZA KUENDELEZA, KUSIMAMIA AU KUENDESHA, kifungu kidogo cha 1. Nchi Wanachama zinakubali kwamba DPW itakuwa na haki ya kipekee ya kuendeleza, kusimamia na/au kuendesha Miradi kama ilivyoainishwa katika Kiambatisho cha 1 Awamu ya 1, moja kwa moja au kupitia Washirika wake chini
ya Mkataba huu
kama itakavyoainishwa zaidi katika Mikataba ya Mradi husika na HGAs husika.

Mikataba ya HGA itaandaliwa ikizingatia takwa la Kifungu hicho kinachoipa "haki ya kipekee". Hii ina maana Tanzania inafungwa kutokuendeleza maeneo hayo pasipo idhini ya DPW

5. SEHEMU YA IV: MASHARTI YA MWISHO, KIFUNGU CHA 19: MABADILIKO YA UONGOZI WA NCHI Iwapo uongozi wa Nchi Mwanachama utabadilishwa au kurithiwa na uongozi wa awamu nyingine kutokana na majukumu ya mahusiano ya kimataifa ya nchi yote au sehemu ya Eneo lake, uongozi utakaorithi utachukuliwa kuwa mhusika wa Mkataba huu kuanzia tarehe ya mabadiliko au urithi, ikiwa uongozi huo, ndani ya muda ufao kuanzia tarehe hiyo, utaarifu Nchi Mshirika kuhusu nia yake ya kuwa sehemu ya Mkataba huu.

Tanzania ni nchi ya vyama vingi vya siasa vyenye Sera tofauti. Itakuwa ngumu kwa chama kingine cha Siasa kitakapopata ridhaa ya kuongoza nchi.

6) KIFUNGU CHA 23: MUDA NA UTARATIBU WA KUSITISHA MKATABA kifungu kidogo cha 1. Kwa mujibu wa aya ya 2 ya ibara hii ya 23, Mkataba huu utaendelea kutumika hadi pale itakapotokea mojawapo ya yafuatayo: (i) kusitishwa kabisa kwa shughuli zote za mradi; au (ii) kumalizika muda kwa HGA zote na Mikataba yote ya Mradi (pamoja na ya nyongeza yoyote ya muda itakayo fanyika) na utatuzi wa migogoro, ikiwa ipo, kama inavyoelezwa hapo chini.[/COLOR]

Hakuna ubishi kifungu hiki kinaipa DPW muda usio na kikomo wa kuendesha bandari kwani shughuli za bandari ni endelevu
 
Hao wahuni wanataka Samia asirudi nyuma kuwapa waarabu mikataba ya milele, waitawale ardhi yetu, bandari na anga, kisha pia tuwajulishe waarabu fursa nyingine za kiuchumi zitakazojitokeza.

Huu utumwa wa kifikra unaotawala vichwa vya wabunge wetu kwa sasa, unaenda kuviumiza vizazi vijavyo vya hili taifa.
Wanajua wapo walio katika pay roll za wapigaji wanaokwepa kodi kila kukicha hapo bandarini.

Hawa mwisho wao umekaribia, wajipange upya.
 
WABUNGE wameishauri serikali kutosikiliza maneno ya watu wa mtandaoni kuhusu ushirikiano wa Serikali za Tanzania na Dubai katika makubaliano ya uwekezaji kwenye bandari zilizopo nchini (IGA) kwa kuwa wanaofanya hivyo hawaitaki nchi mema.

Pia, wameitaka serikali kuharakisha kusaini mikataba inayohusiana na suala hilo, ili bandari iwe sehemu ya kuchangia Pato la Taifa na kuletea maendeleo. Waliyasema hayo jana wakati wanachangia hoja ya Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka 2023/24.

Mbunge wa Jimbo la Ukonga (CCM), Jerry Silaa, alishauri serikali isikubali maneno ya watu wasiotaka iendelee kiuchumi ambao wanapinga uamuzi wake wa kushirikisha sekta binafsi kwenye maendeleo, ikiwamo ushirikiano ilioyongia na Serikali ya Dubai kuhusu uwekezaji kwenye bandari nchini.

Alifafanua kuwa IGA siyo mkataba wa utekelezaji bali ni makubaliano baina ya Serikali ya Tanzania na Dubai kuhusu uwekezaji utakaofanyika kwenye bandari zilizopo katika chi hiyo na kwamba mikataba ya kwenda kutekeleza miradi bado haijaingiwa.

Silaa alisema ushirikiano huo utaongeza ufanisi wa bandari na kufikia malengo ya serikali ya kukuza uchumi wa nchi kwa kuongeza forodha na kuboresha sekta za uchumi ikiwamo kilimo.

"Niombe serikali ikubali ushauri, isikilize wananchi, lakini wakati mwingine isikubali kuyumbishwa na watu wenye nia zao za kuitaka nchi yetu isiendelee kiuchumi, ikubaliane na hoja za msingi za kutetea taifa letu, tuwe na uwekezaji na kushirikisha sekta binafsi katika ameneo ambayo wenzetu wamebobea," alisisitiza.

Kadhalika, alisema serikali haiwezi kupiga hatua bila ushirikiano na sekta binafsi huku akitoa mfano wa moja ya mafanikio ya ushirikishwaji wa sekta hiyo kuwa ni Benki ya NMB ambayo hivi karibuni serikali imevuna gawiwo la Sh. bilioni 45.5 na kodi ya Sh. bilioni 453.

Aidha, Mbunge huyo alishukuru serikali kwa kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati ikiwamo ujenzi wa Bwawa la Kufua Umeme la Julius Nyerere, ambalo utekelezaji wake umefikia asilimia 96, ujenzi wa reli za umeme na adaraja la Kigogo Busisi, mradi wa mwezndo kasi awamu ya tatu, Gongo la mboto-Kariakoo.

Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Pwani (CCM), Subira Mgalu, alishauri serikali kuchukua hatua za haraka kuleta mikataba itakayotokana na IGA ili wawekezaii waje na bandari iwe na nafasi ya kuchangia katika pato la ndani la taifa na serikali ipunguze kukopa.

Kahusu hoja ya kuitwa mbunge mmoja mmoja kupigia kura muswada huo iliyotolewa na mbunge mstaafu Prof. Anna Tibaijuka, alisema hauna mashiko kwa kuwa utaratibu huo unafanyika kwenye kupitisha bajeti ya serikali pekee, masuala mengine ni utaratibu wa kuhojiwa na walishafanya hivyo.

"Lakini nataka nimkumbushe Prof. Tibaijuka alipokuwa waziri 2013 aliwasilisha mpango wa kuifanya Kigamboni kuwa mji wa trilioni 11, haukufanikiwa na tulioupitisha kwa kura za kuhojiwa kwa hiyo aiache serikali inayoongozwa na mwanamama menzie (Rais Samia Suluhu Hassan) ifanye kazi yake," alisema.

Hivi karibuni, Prof. Tibaijuka akihojiwa na chombo kimoja cha habari, alikosoa utaratibu wa kura ya pamoja uliotumiwa na Bunge katika kupitisha Azimio la Bunge kuhusu Mapendekezo ya Kuridhia Makubaliano Kati ya Tanzania na serikali ya Dubai kwenye ushirikiano wa kiuchumi na kijami kwa ajili ya uendelezaji na uboreshaji wa utendaji kazi wa bandari Tanzania.

Aidha, aliwatoa hofu wananchi kuwa bandari haiwezi kuuzwa kwa serikali kugawana idadi ya gati na mwekezaji bali mbinu iliyotumika ni kushirikisha sekta binafsi katika kukuza utendaji kazi wa bandari na kukuza uchumi wa nchi.

Vile vile, alisema bajeti kuu imeonyesha dhamira ya serikali ya kureiesha uuzwaji wa bidhaa nje ya nchi kwa kutenga zaidi ya Sh. bilioni 800 wazalishaji wa mazao, ili kuliletea taifa fedha za kigeni na kukuza uchumi.
Pia, katika mapendekezo ya bajeti ya serikali inatarajia kukusanya Sh. trilioni 44, kati ya hizo Sh. trilioni 31 zitakusanywa kutoka mapato ya ndani na kwamba ni lazima seri-kali ishirikishe sekta binafsi katika uwekezaji.

Aliwataka wananchi kuendelea kutoa na kudai risiti wanapofanya ununuzi ili kuhakikisha kuwa wanalipa kodi na serikali isiendelee kuleta kodi mpya kwa kuwa inategemea pesa hizo kutekeleza miradi ya maendeleo. Mbunge wam Sengerema, Hamis Tabasamu, alimshauri Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, kutokatishwa tamaa na maneno yanayozunguka mitandaoni na mitaani bali kuwa na imani jambo analolifanya litakwenda kuiletea mafanikio nchi.

"Kuna watu ni majemedari wa kupiga kelele kwenye mitandao na kila maeneo, Mheshimiwa Waziri wa Fedha, maneno haya yangekuwa yanatoboa mwili wako leo ungekuwa umejaa viraka na bandeji mwili mzima, kwa hiyo unachotakiwa sasa hivi ni kuwa na ngozi ngumu tu kujenga imani halafu baadaye unatoboa," alisema.

Alimshauri waziri huyo kuwashirikisha wabunge wakati wa uandaaji wa baieti hizo ili watoe ushauri wa vitu muhimu vya kuwapo na kutokuwapo kwa kuwa wao wanajua matatizo ya wananchi ambao wengi wao kukosa pesa ndiyo kunawafanya waitukane serikali kwenye mitandao.​
ni wabunge wa ccm, wanawawakilisha wanachama wa ccm. ila raia wa vyama vingine wamelikataa na hawautambui huo mkataba. kuna siku utavunjwa tu.
 
Wawakilishi wetu boooora hoyeeee.
Safi sana. Mwaka 2025 uchaguzi ni wa Rais na madiwani tu but bungeni hawa wa sasa wapite unopposed.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom