Fainali ni Bayern na Dortmund. Ukiangalia vizuri timu zilizoingia semis hilo halina ubishi. Hilo nilishalisema mapema sana (sio humu JF).Naomba Real tuingie na hawa jamaa final ili wajue kila kubwa ina kubwa yake!
Fainali ni Bayern na Dortmund. Ukiangalia vizuri timu zilizoingia semis hilo halina ubishi. Hilo nilishalisema mapema sana (sio humu JF).Naomba Real tuingie na hawa jamaa final ili wajue kila kubwa ina kubwa yake!
Si uliona kala ya Bayern? Full nyekundu.
EMT acha kunivunja mbavu zaidi, yaani ni umezama kwenye mapenzi ya rangi tu au misukule ya wakina Rage inakusumbua hahahahahahahaPouwa. Vua hicho kitu cha njano vaa the real kala like this.
Hapo lazima Yanga watabakia kuyacheza mayenu kama anavyoyacheza huyo kipa wa Barca. Siyo mchezo.
Fainali ni Bayern na Dortmund. Ukiangalia vizuri timu zilizoingia semis hilo halina ubishi. Hilo nilishalisema mapema sana (sio humu JF).
Keep on dreaming. Bahati mbaya watu wengi mmekuja kuisikia BVB Dortmund ipo semi final. Kwenu ninyi ni timu ambayo haina jina hivyo hamkuifuatilia. Wait and you will see.Sasa kama ulilisemea ndotoni sisi tutagmini vipi? Kwa kuwa mnashindwa kuitofautisha Barca na Madrid basi leo mtamfahamu kwa uzuri tu "The Special One" vurugu za Khedira, Higuain, Ozil, Di Mariamu, Alonso na mtaalam CR7 hatuwezi kutoka bila goli pale, madrid sio timu ya vipasipasi visivyo na tija.
Keep on dreaming. Bahati mbaya watu wengi mmekuja kuisikia BVB Dortmund ipo semi final. Kwenu ninyi ni timu ambayo haina jina hivyo hamkuifuatilia. Wait and you will see.
Messi: I was fit but not '100 per cent'
The Argentine has confessed that he was
rusty after a couple of weeks on the
sidelines after rushing back from a
hamstring injury in time to face PSG in the
quarters...
Masaburi yake...
Keep on dreaming. Bahati mbaya watu wengi mmekuja kuisikia BVB Dortmund ipo semi final. Kwenu ninyi ni timu ambayo haina jina hivyo hamkuifuatilia. Wait and you will see.
Nenda BAKITA au TUKI ukajifunze Kiswahili.Kwa hiyo wewe ndio unaijua sana B.Dortmund? Utasemaje haina jina wakati jina lake umeliandika mwenyewe?
Tupo ulaya huku Mpwa, stress zenu za msimbazi huko huko!
Hii timu mimi niliijua enzi hizo yuko mshambulia mjanja mjanja hivi ana akili nyingi !!!! Akiitwa Chapuisat ! Achaaa !
Hawa jamaa wamewahi kuchukua Champions League !
Nenda BAKITA au TUKI ukajifunze Kiswahili.
Stephanie Chapuisat mtoto wa kiswis huyo...
Umenikatalia kule juu, dakika 4 baade unakuja kukubali kile kile. Au kwa sababu kasema "mzungu". Hii kasumba sijui itaisha lini.Juzi alikua anahojiwa na official Magazine ya UCL, anasema 1997 walivyochukua ndoo ya champions League walikua wametoka kuwaachia Bayern ubingwa wa Bundasliga baada ya kuuchukua back to back na hicho ndicho anachokiona sasa!
... Baada ya kichapo cha 4 - 0
"magazeti ya leo Jumatano yanavyochambua UCL - 2013"
MWANANCHI - Bayern yaisambaratisha Barca:
Bayern Munich inasaka tiketi ya kufuzu kwa fainali ya tatu Ligi ya Mabingwa katika misimu minne iliyopita.
Munich, Ujerumani
Bayern Munich imejisafishia njia ya kucheza fainali ya Ligi ya Mabingwa baada ya kuichapa Barcelona kwa mabao 4-0 katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza, wakati leo Borussia Dortmund wataonyesha kazi na Real Madrid.
Bayern wakiwa kwenye uwanja wao wa Allianz Arena walipata mabao yao kupitia Thomas Muller aliyefunga mabao mawili huku Mario Gomez na Arjen Robben wakifunga bao kila mmoja.
Muller alifungua karamu hiyo ya mabao katika dakika 25 akifunga goli lake kwa kuunganisha mpira wa kichwa uliopigwa na Dante.
Mabingwa hao wa Ujerumani waliendeleza kasi na kufanikiwa kupata bao la pili lililofunga na Gomez akiunganisha kichwa kilichopigwa na Muller katika dakika 47, kabla ya Robben kupachika bao la tatu kwa shuti la chini lililomshinda kipa Victor Valdeskatika dakika 73, wakati
Barca wakiwa hawaamini kinachotokea Muller alipachika baola nne kwa kuunganisha vizuri krosi ya John Alaba.
Leo mabingwa wa kihistoria Real Madrid watakuwa na kibarua kigumu mbele ya Dortmund katika mchezo mwingine unazikutanisha timu za Hispania dhidi ya Ujerumani.Dortmund inajivunia rekodi yake ya kuifunga Real katika hatua ya makundi msimu huu.
CHANZO: MWANANCHI
===
... BBC MICHEZO:
"Bayern yaitandika 4-0 Barcelona"
Mabingwa wa Ujerumani, Bayern Munich wamejiweka katika nafasi nzuri ya kutinga hatua ya fainali ya michuano ya klabu bingwa barani Ulaya baada ya kuitandika Barcelona 4-0 katika mchezo wa kwanzawa nusu fainali nchini Ujerumani.
Mabao mawili ya Thomas Müller, na yale ya Mario Gomez na Arjen Robben yaliizamisha Barcelona ambayo ilikuwa na nyota wake wote wakutegemewa,akiwemo Messi ambaye alikosa michezo kadhaa kabla ya kuanzishwa usiku huu.
Hii imekuwa mara ya kwanza kwa Barcelona kufungwa mabao 4-0 tangu mwaka 1997 walipofungwa na Dynamo Kiev ya Urusi mwaka 1997 kwenye hatua ya robo fainali ya michuano ya klabu bingwa baraniulaya.
Bayern Munich wametoka kutawazwa kuwa mabingwa wa Ujerumani wiki chache zilizopita na iwapo watafanikiwa kuiondosha Barcelona na kutinga hatua ya fainali ya michuano ya klabu bingwa, itakuwa fainali yao ya tatu kushiriki ndani ya miaka minne.
Kocha wa Bayern Munich Jupp Heynckes awali alisema haogopeshwi na urejeo wa Lionel Messi,na katika mchezo huo Messi hakuonekana kuwa katika kiwango chake cha siku zote.
Matokeo haya yanafanya mchezo wa marudiano utakaochezwa wiki ijayo kuwa mgumu kwa Barcelona kwani haijawahi kutokea timu kwenye michuano ya klabu bingwa barani Ulaya kufungwa magoli manne na zaidi katika mchezo wa kwanza kisha kuyarejesha katika mchezo wa marudiano na kufuzu hatua inayofuata.
Baada ya Bayern Munich kuichabanga Barcelona, Jumatano usiku mahasimu wa Barcelona, Real Madrid nao watakuwa na kibarua kikubwa mbele ya Borussia Dortmund kwenye uwanja wa Signal-Iduna-Park,mchezo utakaofanyika majira ya saa nne kasorobo kwa saa Afrika Mashariki.
CHANZO: BBC SWAHILI
by: habari Masai;
"Barcelona yachezea kichapo, yapigwa4-0"
Baryn Munich yaisambaratisha Barcelona.
Leo Borussia Dortmund watapimana nguvu na Real Madrid. Bayern wakiwa kwenye Uwanja wao wa Allianz Arena walifunga mabao hayo kupitia kwa Thomas Muller ambaye alifunga mabao mawili na Mario Gomez na Arjen Robben walifunga bao moja kila mmoja.
Barca wakiwa hawaamini fasta walishutukiwa wakifungwa bao la nne na Muller baada ya kuunganisha vizuri krosi ya John Alaba.
je Pedro,Iniesta,Messi,Xavi,Busquets,Pique,Bartra,Puyol,Valdes,Tello,Thiago,Cuenca,Muniesa,nk achilia mbali kina Fabregas na Alba ambao walikuwa nao La Masia wakaenda nje wakarudi tena,kwani hao si kizazi cha La Masia,au haukulitambua hiloTeam inayotakiwa kujipongeza kuwa hapo ni B.Dortmund peke yake, wako hapo kwa sababu wao ni team bora inayotokana na pure talents na dedication from players, hakuna mchezaji anayeshawishiwa na pesa hapo and they are the only UNBEATEN side left in the competition, wengine wame-buy their way to the semi finals.