Ina semekana mfubao wa elimu nchi unasababishwa na wanaojiita wasomi wa UDSM kuwa na chuki za kipumbavu na mentality mfuu iliyojengeka vichwani mwao.
Mfano wasomi wa UDSM wamekuwa na tabia ya kuzibia vyuo vingi vilivyo nasababu pia nia ya kua vyuo vikuu mfano DIT, kutokana na kuwa na ma egineer wachache ilikuwa na nia siku nyingi ya kutoa digrii lakini ilipambana na mkono wa uzibe kutoka UDSM isipate wasaha huo mfano wa wazi ni pale kiongozi mwandamizi wa UDSM DR Masua alipoamua kusafiri mpaka ulaya ili kukisiriba chuo hicho kwa wadau ili kisipate hadhi hiyo.
Bado kuna mfano wa Mzumbe kikiandamwa na propaganda za wakuu wa adimizi wa UDSM.
SWALI LA KUJIULIZA!!! kwanini? UDSM ni wahasimu wakubwa wa vyuo vinavyotoa kozi zinazofanana na zile zinazotolewa UDSM.
Na juhudi zao zinapokwama hufanya kila mbinu ili chuo husika kiwe chuo kishiriki chao,habari zinapasha.
Na cha kusikitisha zaidi hawa wahadhiri wamekua mstari wa mbele kukebehi vyuo vingine mfano utasikia ukipata C udsm hii ni A mzumbe, na sivyo hivyo tu wamekua wakienda mbali kulaghai wanafunzi wao na kuwaaminisha vitu vya ajabu ajabu mfano hii digrii ya UDSM ni masters ya ulaya.
Cha ajabu wanafunzi hao nao wamekua wakiamini hayo bila kuhoji mbona hawa ma tutor wetu wengi wamezichukua hizo master ulaya? baada ya ya kuchukua digrii hapa kwanini hawakwenda moja kwa moja DR huko ulaya.habari zilizidi kupasha na kuongeza,
DESA za UDSM ndizo zimeua kabisa elimu ya Tanzania maana zimekuwa zikitoa wanafunzi mabigwa wa desa wasio na skills, chanzo kilipasha.
Na kama mfumo mzima wa elimu Tz kuangaliwa inabidi waanze na UDSM maana inasemekana ni chuo kiliojaa kinyongo, chuki ku-disco watu wenye uwezo kwa sababu za ma-prof binafsi, kupitisha wanafunzi wasio na uwezo kwa uwezo wao wa kuvua chupi.
Ndugu ndugu, chonde chonde, unaporopoka uwe makini. Kwa kuanza nenda kwenye thread moja iliyoandikwa kuhusiana na digrii au Phd feki za Mzumbe then urudi kwenye mada yako.
Mimi sio kwamba nasema hawajawahi kuzuia vyuo vingine visiwe vyuo vikuu but hata kama ni kweli tumewahi kujiuliza ni kwa nini. Na tumewahi kujiuliza maswali yafuatayo:-
- Je, vina wahadhiri wa kutosha wenye elimu inayotambulika na baraza la vyuo vikuu duniani..??
- Je, vina maabara za kutosha kiasi cha kuweza kubeba population size ya University. Manake utambue chuo kikibeba wanafunzi 20, sio University ni College, nenda kwenye standards za vyuo kwa ufafanuzi.
- Je, kina teknolojia ya kutosha kiasi cha kumeet viwango vya kimataifa..??
Mimi nafikiri hayo maswali ni ya msingi sana, then baada ya hapo ndio uanze kuongea. Je, DIT ina Phd ngapi..?? Je, hata huko Mzumbe umeona Phd zao..?? na je hata hizo zilizodaiwa kuwa feki ziko ngapi..??
Huyo binadamu aliyewahi kudai kuwa C ya Mlimani ni A ya mzumbe, mimi namkubalia, sio kwamba ni mdau/mshabiki wa mlimani, no plse. Ukweli ni kuwa, nenda Mzumbe kachukue mitihani ya masomo kama auditing, management accounting, financial accounting and tax. Kisha njoo nayo mlimani na ulinganishe na paper zao, kama ni kipanga, you will obviously detect the difference ya competence ya kimtihani. I have done that, na ndio maana najiamini kuongea hivyo.
Pia nimewahi kuambiwa na wanafunzi hao hao wa Mzumbe jinsi wanavyotungiwa mitihani. Mfano, kuna mwalimu mmoja wa auditing (jina kapuni, ingawa ukifuatilia utamjua), yeye huwa anawapa angles atakazochezea kwenye pepa, na ukichunguza wanafunzi kibao wa Mzumbe wana A kwenye auditing, but walete kwenye soko na tena usiende mbali, walete kwenye mitihani ya NBAA, lazima wale chaka. Sasa kachukue kijana wa mlimani ambaye kapikwa vizuri auditing na mtaalamu anayeitwa Dr. Temu, then uniambie ataifanya nini mitihani ya NBAA.
Swala la uwezo wa wanafunzi wa mlimani hilo napenda kukushauri tusilumbane sana, nenda kwenye big 4 auditing firms watakwambia wanapenda kuchukua wapi wafanyakazi...? Huko kumejaa mlimani tupu, kaangalie kama utakuta vyuo vyako. Mzumbe wameanza kuingia juzi juzi, na wengi wameprove in-efficiency. Kiasi kwamba, moja ya kampuni, jina kapuni, imekiri kutochukua tena vijana wa Mzumbe. Sasa niambie shekhe, huo uwezo unaouongelea ni upi..?? Pia kwenye uwezo, hebu nenda kwenye database ya NBAA kisha uangalie for the past 5 to 10 years, best students (top 3) katika kila somo na if possible overall huwa wanatoka chuo gani. Au kila matokeo ya NBAA yanapotoka, nenda kaangalie kwenye ubao wa kitivo cha biashara mlimani, utakuta tangazo toka bodi ya uhasibu (i.e. NBAA) la kukipongeza chuo kwa "kuendelea kutoa" na sio "kutoa tu" wanafunzi bora wa katika mitihani ya NBAA.
Mimi nafikiri hawa wazee wa Mzumbe, waache kuinvest kwenye kufaulisha, bali wawekeze kwenye kutoa vipaji.
Pia mheshimiwa, ukumbuke kuwa uwezo wa mtu, sio chuo tu, hata kipaji binafsi kinaweza fyatua kitu. So, hata mtu apikwe Havard, anaweza akaja bongo akapigwa bao na mtu mwenye kadiploma cha chuo cha uswazi. Ingawa, je, ni wangapi.?? Manake hizi hazitokei kila siku..!! Watu kama hawa ni wachache kwenye jamii, na ndio maana wataalamu wa viwango duniani, wanasema wanataka mtu anayetoka kwenye chuo kinachotambulika kimataifa, akiwa na mategemeo kuwa vipanga ndio wanaingia humo and not otherwise. Na ndio maana, mlimani kwa sasa, ukiwa na division II hukanyagi na hata I ikiwa ya wasiwasi hunusi majengo ya chuo. Ukikuta hivyo, ni wale ambao Mungu kawapa neema ya kipekee, na huwa ni rare vile vile.
Kwa kipindi cha miaka ya karibuni naweza kukukubalia kuwa mlimani imeshuka, ila haijafikia kiwango hicho unachokifikira au kiwango cha hivyo vyuo vyako. Hii yote ni kutokana na uzembe wa serikali yako ya URT (i.e. United Republic of Tanzania), kwa kuendekeza siasa mpaka kwenye elimu. Kwa sasa wameongeza enrollment kupita kiasi na nahisi hii inachangia hata uwezo wa walimu kumeet mahitaji ya kila mwanafunzi kama ilivyokuwa miaka ya nyuma. Ila hili waheshimiwa wa Mlimani wameshataarifiwa walirekebishe na naamini wameanza kulifanyia kazi.
Kama una maoni, yanakaribishwa, inawezekana una jipya zaidi nisilolijua.